DHAMANA (21)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alifika hadi sehemu iliyokuwa na matanki ya maji ambapo kama maji yakijaa na kumwagika basi hujulikana wa eneo hilo kulowana hasa bustani ya maua ambayo imezunguka eneo lenye matanki ya maji, cha ajabu eneo hili lilikuwa kavu kabisa hakuna dalili ya kumwagika maji.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Akiwa anashangaa hali hiyo alisikia sauti ya mjomba wake akipiga yowe la maumivu huko ndani na ikamlazimu kukimbia kuelekea chumbani kwa mjomba wake (muda huo Shafii anapiga yowe la maumivu ndiyo muda ambao Bi Farida alizirai kule kwemye himaya ya majini baada ya kutapika vitu visivyoeleweka).
Jamali alipofika chumbani kwa mjomba wake alimkuta akiwa ameanguka chini akiwa amekaukiwa na sauti, alimuinua na kumuweka kitandani ambapo Shafii alionesha ishara ya kutaka maji kwenye bilauri yaliyppo humo chumbani mwake mezani na ikamlazimu Jamali amletee maji upesi. Shafii alikunywa maji yote kwenye bilauri ndiyo akaweka kuongea na neno la kwanza kulitamka ni jina la mkewe, alipoona hamuoni mkewe alimuuliza Jamali mahali alipo shangazi yake. Jamali alimueleza kila kitu juu ya kutoonekana kwa shangazi na maajabu aliyoyaona, hali hiyo ilimshtua sana Shafii akabaki amechanganyikiwa.
"mpigie baba yako muambie aje hapa sasa hivi" Shafii alimuambia Jamali huku akimuonesha simu ilipo, Jamali alienda kupiga namba ya baba yake lakini haikuwa inapatikana na alijaribu zaidi ya mara nne lakini jibu ni lilelile.
"Haipatikani"Alimuambia mjomba wake
"He...hebu mpigie na Hassan usipompata piga nyumbani kwenu umuulizie baba yako" Shafii aliongea akionekana amepagawa kabisa, Jamali alupiga namba ya Hassani ila matokeo yalikuwa yaleyale na ikamlazimu apige nyumbani kwao amuulizie baba yake.
"Anko nyumbani wanasema hajarudi tangu alipoondoka na anko Hassani"Jamali alimuambia Shafii huku akionekana kuchanganywa na haliya mjomba wake.
"Etii?!" Shafii aliuliza kwa nguvu halafu akazirai papo hapo kutokana na taarifa anazoambiwa, hali hiyo ilimchanganya Jamali na ikambidi awaamshe wafanyakazi wote wa nyumba hiyo na jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanywa mara moja.
****
Shafii alikuja kuzinduka siku iliyofuata akajikuta akiwa yupo hospitalini amelazwa akiwa ametundikiwa dripu ambayo ilikuwa inakaribia kuisha, alipoangaza pembeni aliwakuta Mzee Buruhan, Mzee Mahmud na Mama Jamali mke wa Hamis wakiwa wamezunguka kitanda chake.
"Faridaaa!" Shafii aliita jina la mke wake kwa nguvu huku akijaribu kuinuka kitandani
"Shafii hebu tulia kwanza utasababisha matatizo mengine tu" Mzee Buruhan alimuambia huku akimzuia asifanye fujo.
"Mama Zayina, Zayina mpo wapi?" Shafii alipiga kelele zaidi na ikabidi daktari aitwe mara moja ili kumtuliza, Mzee Buruhan na Mzee Mahmuf walimshikilia Shafii hadi daktari alipokuja akamchoma sindano ya usingizi ndiyo ikawa ahueni.
Baada ya Shafii kulala mzee Buruhan na mzee Mahmud walitoka pamoja na mke wa Hamis wakaenda kuka kwenye madawati ya kusubiria wagonjwa, baada ya muda mke wa Hamis aliondoka kwenda kufuata chakula kwa ajili ya mgonjwa akawaacha wazee hao peke yako.
"Kama nilivyokuambia mzee mwenzangu kuhusu huyu mwanao, awe mkweli ujue tatizo alilonalo ndiyo nitakubali kumsaidia" Mzee Mahmud aliongea.
"Mzee mwenzangu tatizo kila kukicha una misemo ambayo imejaa vitendawili vitupu hebu niweke wazi walau kidogo nipate fununu ya jambo linalomsumbua mwanangu" Mzee Buruhan alimlalamikia rafiki yake kutokana na kauli zake zilizo jaa mafumbo.
"mzee mwenzangu hiyo kinyume na utaratibu wa taaluma yangu siwezi kusema hata kama nalitambua tatizo hili, huwa sina tabia ya kukuficha kitu ila kwa hili wacha nikuambie ukweli tu nitakuwa nimekiuka masharti ya utalaamu wangu wa uganga ikiwa nitalisema suala hili pasipo muhusika mwenyewe kufungua kinywa chake na kuliongelea. Utanisamehe kwa hilo" Mzee Mahmud aliongea huku akimshika bega mzee Buruhan ambaye alionekana kuwa njia panda kutokana na matatizo yaliyomkumba mwanae
"mzee mwenzangu hakuna hata njia nyingine ya kunisaidia niweze pata fununu kidogo ya hili suala?" Mzee Buruhan aliuliza huku akiwa ameinamisha uso wake chini akionekana amekata tamaa kabisa ya suala hilo.
"Siku zote mwanamke atakaye mtoto lazima akubali kuvua nguo ya ndani ili alichokificha kionekane na hawezi kupata mtoto ikiwa atakataa kuivua hiyo nguo. Ndiyo hivyo hivyo mwanao akubali alilolificha moyoni mwake lifumbuke la si hivyo hataweza kupata msaada katika hilo, cha kukusaidia akiamka muambie umebaki peke yako ukitaka usipoteze vyote awe muwazi kwangu na kwako. Naenda msalani mara moja mzee mwenzangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akajiinua kivivu kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akawa anaelekea chooni, mzee Buruhan alimtazama tu akiwa anatamani sana ajue jambo lililopo ndani ya kichwa chake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Mzee Mahmud aliipopotea katika upeo wa macho yake aliinua kichwa juu akiweka ishara ya kuomba dua halafu akatikisa kichwa kuonesha anasikitishwa, hakuwa na jambo jingine alilomuomba Mungu zaidi ya kumshtakia tu juu ya balaa lililomkuta mwanae na kumfanya awe na matatizo tu katika mwaka huo ambapo miaka mingine yote aliishi kwa amani na furaha pamoja na familia yake lakini sasa furaha hiyo imetoweka katika maisha yake. Laiti angelijua kwamba alikuwa anashtaki mtuhumiwa kuwa ameonewa wala asingelifanya hivyo lakini kwakuwa hakujaliwa uwezo wa kulibaini kwani alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu, hakutambua kama jereha la mwanae ni la kujitakia hivyo halihitaji pole hata kidogo.
Mzee Mahmud alipofika kwenye mlango wa msalani baada ya kuondoka pale kwenye dawati alihisi hali isiyokuwa ya kawaida katika mwili wake lakini aliipuzia na kuingia humo msalani, alipoingia ndani alipitiliza sehemu za kujisaidia haja ndogo akawa anaelekea sehemu maalum ya yenye vyoo ndani ambayo hutumiwa na wale wanaohitaji kumaliza haja zao kwa siri tu. Alipofika hilo eneo alifuata mlango wa moja wa vyoo akashika kitasa ili aufungue lakini alisita baada ya kusikia upepo mzito ukivuma kwa ghafla ambao ulitaka hata kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni lakini aliuzuia, upepo huo ulipotulia Mzee Mahmud alionekana kukerwa nao kwa kitendo cha kutaka kumuadhiri ambapo aligeuka nyuma akionekana kuwa na hasira za waziwazi juui ya tukio hilo.
"Adabu gani hizo ewe mwanajini wataka kuniadhiri kwa hizo nguvu zako ulizojaliwa?" Mzee Buruhan alilalamika baada ya kumuona yule aliyetaka kumuadhiri kwa kutaka kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni alikuwa yupo mbele yake baada ya kugeuka nyuma, alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa amefumbata mikono kifuani mwake.
"Samahani mzee wangu kwa hilo" Zalabain aliomba radhi.
"sema una shida gani" Mzee Buruhan aliongea huku akiuweka msuli aliojifunga kiunoni vizuri.
"nimekuja kukuambia tu mimi ndiye ninayemtesa Shafii na huwezi kuharibu kazi yangu kwa kujaribu kumsaidia" Zalabain aliongea kwa msisitizo.
"Ndiyo nimeshakutambua tangu unajitokeza pia sipo kwa ajili ya kumsaidia dhalim kama yule bali nipo kwa ajili ya kumsaidia Buruhan ili asiondokewe na nguzo zake zote, kiufupi ni hivi nazuia usimuue yule mziwanda wake asiye na hatia" Mzee Mahmud alimuambia huku akijiamini halafu akameza mate kidogo kisha akaendelea, "Shafii ni haki yake kwa alichokifanya ila Ally hana hatia yoyote na usimuingize katika orodha hiyo, pia ningependa mumponyeshe sikio lske na taya lake ambayo mumjeruhi kutokana na kujaribu kuleta kile kitakachoyafanya majini ya marehemu Hamis yafanye kazi. Ukumbuke pia yeye anachukia ulilofanyiwa ila mali yako anayoimiliki Shafii ndiyo inamfanya ashindwe kufanya jambo lolote, usihukumu yule asiye na hatia kama ni ufalme utapewa pasipo yeye kupoteza uhai wake".
"unasema nini wewe?" Zalabain alimuuliza Mzee Mahmud
"kama ulivyosikia ewe mwana wa jini, ukumbuke mimi nilikataa kutengeneza uchawi kama uliomtapisha mama yako jana kwasababu najua siyo haki kufanya hivyo, pia niligoma kufanya dawa ya kumuua baba yako ili mama yako awe chini ya mwingine kwasababu najua haikuwa haki. Pia utambue nakuambia usimuue Ally kwasababu najua utakuwa hutendi haki ewe mwanajini kamuuulize ibin Zultash atakueleza, mwisho kabisa nakuambia hivi upotee sasa hivi kuna mtu anaingia humu msalani sasa hivi asije akaniona naongea peke yangu kama kichaa wakati nina akili zangu timamu"
Mzee Buruhan aliongea kisha akageuka nyuma akaingia chooni bila kujali kama Zalabain ameondoka au yupo, baada ya kumaliza haja zake alitoka hakumkuta Zalabain na akarudi kule alipokuwa yupo awali. Alimkuta mzee Buruhan yupo na Ally wakiongea na iilonekana Ally alikuwa kapona kabisa tatizo la kuvunjika taya na sikio kwani hakuwa mwenye kuweza kuzungumza wala kusikia, lakini hapo alikuwa akizungumza na kusikia vizuri kabisa.
Mzee Mahmud alimuonesha ishara ya kumsalimia Ally kama ilivyokuwa akifanyiwa kwa kutoweza kusikia vizuri lakini.
"Mzee mwenzangu anaongea huyu na kusikia sasa hivi usimsabahi kama vile unamsabahi bubu" Mzee Buruhan alimuambia rafiki yake.
"Yapaswa tumshukuru Mungu basi mzee wangu maana huu muujiza tosha" Mzee Mahmud aliongea akionekana kufurahishwa na suala hilo.
"Alhamdililah" Ally na baba yake waliitikia kwa pamoja.
Mzee Mahmud alibaki kutabasamu tu kila alipomuangalia Ally kwa kufurahishwa na usikivu alionao Zalabain baada ya kufanya kile alichomuambia, tabasamu lake lilifanya Mzee Buruhan na Ally nao watabasamu wakijua kafurahishwa na hali ya Ally kutengemaa.
"Ally hebu sogea karibu" Mzee Mahmud alimuambia Ally huku akimtazama kwa umakini, Ally alimsogelea Mzee Mahmud pasipo kujua ni kipi alichokuwa anataka kufanyiwa kwani alimzoea sana mzee Mahmud na alimchukulia kama baba yake tu. Alipomsogelea Mzee Mahmud aliambiwa achuchumae mbele yake naye akatii amri kama alivyoambiwa, mzee Mahmud alimshika kichwani na akamtamka maneno yasiyoeleweka na kusababisha Ally ashtuke halafu aangalie mazingira ya hapo yalivyo halafu akaenda kukaa kwenye dawati pembeni ya baba yake alipokaa awali.
"Baba hivi hapa tupo kwa ajili gani?" Ally aliuliza tu baada ya kukaa pembeni ya baba yake akionekana kutotambua yupo hapo kwa ajili gani.
"Kha! We Ally maswali gani hayo hutambui kama tupo hapa kumuangalia kaka yako kalazwa tangu jana" Mzee Buruhan alimuambia Ally akionekana kutoelewa kitu alichofanyiwa na mzee Mahmud hadi akasahau yupo pale kwa lengo gani wakati alipoingia tu aliulizia hali ya kaka yake.
"Khaa! Kumbe tupo hapa kwa ajili ya kumuangalia firauni huyo, sina muda huo muache afe maana huyo ni zaidi ya shetani" Ally aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Mzee Buruhan na akajikuta akimtazama mzee Mahmud akionekana kutoelewa kafanya nini, Ally alinyanyuka ili aondoke lakini mzee Mahmud alimuita akamuomba aketi akakaa chini.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni