Notifications
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…

DHAMANA (24)

Jina: DHAMANA

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
TULIPOISHIA...
Baada ya kijana yule kuondoka Ally aliendelea kukaa hapo akikumbuka mambo mbalimbali kipindi akiishi ndani ya nyumba hiyo kabla hajahama, mambo mengine ya furaha na upendo na alivyokuwa akiishi na shemeji yake ambaye alimjali yalimpa tabasamu kila akiyakumbuka ila alipokumbuka wema aliofanyiwa na kaka yake alijikuta anasonya tu kwani hakuupenda hata kidogo huo wema wake na wala hadi muda hakuona umuhimu wake.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"Shetani katumia ushetani kunifanikishia malengo yangu, hadi sasa sioni umuhimu wa mimi kufikia haya malengo ikiwa kuna mwenzangu kateseka kwasababu ya huyo shetani. Kakimbia kwao kwasababu ya huyo shetani. Shetani huyu kanisaidia ili na mimi anitumbukize katika ushetani"Ally aliongea kwa hasira kisha akanyanyuka akasema, "namchukia maana bila yeye mimi nisingetumiwa kama mtumwa wa ngono na yule malaya aliyekubuhu kwa umalaya tangu yupo kigori. aaargh! Nawachukiaaa!" Ally aliongea kwa hasira kisha akapiga ngumi ukutani na kupelekea sehemu ya plasta iliyowekwa juu ya ukuta wa udongo wa nyumba hiyo uanguke.

Chuki za waziwazi kwa kaka yake ndiyo zilikuwa zimeutawala moyo wake na hakumpenda kama ilivyokuwa akimpenda hapo awali, hakuona umuhimu wa yeye kumuita kaka wakati kafanya mambo yasiyopendeza kwa mwanadamu yoyote mwenye moyo wa kibinadamu na siyo wa kama aliokuwa nao kaka yake. Alitokea kuwachukia ndugu zake wote walioshiriki mpango ule hakuona faida ya kuwa na ndugu kama wao katika dunia hii, aliona ni bora angekuwa na undugu na jiwe kuliko kuwa na undugu na hao aliowaheshu kama kaka zake lakini hakuona ustahiki wao wa heshima hiyo aliyowapa.

Majira ya magharibi katika eneo hilo alilokuwepo Ally paliiingia ugeni mwingine ambao haukutia mguu katika eneo hilo kwa miaka kadhaa tangu walipoondoka, ugeni huo ulikuwa ni msafara wa magari mawili ya kifahari yenye thamani kubwa sana nchini Tanzania kwa kipindi chote. Magari hayo yalikatisha katika majani baada ya barabara ya kuingia eneo hilo kuwa imeota majani kila sehemu. Ally aliposikia mingurumo ya gari hiyo wala hakujishughulisha kwenda kuangalia zaidi ya kutulia vilevile sehemu ya dirishani ya sebule hiyo alipokaa katika eneo ambalo dirisha limetolewa, aliposikia hatua za mtu akiingia hapo ndani yeye alielekeza machp mlangoni tu na hadi mtu huyo anaingia tayari alikuwa ameshamuona na ni mtu kati ya watu anaowaheshimu akiwa amebeba mikeka inayotengenezwa kwa ukindu maarufu kama majamvi kwa wakazi wa jiji la Tanga

"Ally kumbe huku" Sauti ya mtu huyo ilimsemesha na hapo Ally akainuka akamfuata.

"ndiyo baba nipo huku, shikamoo" Ally alimuamkia baba yake baada tu ya kumjibu swali alilouliza.

"marhaba tumekutafuta sana mchana wa leo ili uje huku maana kuna jambo muhimu sana" Mzee Buruhan alisema.

"sawa baba nipo tayari hakuna kilichoharibika" Ally aliongea huku akimpokea baba yake majamvi.

"yatandike hapo chini kwa ajili ya wageni watakaokuja maana mzee Mahmud kasema kuna ugeni utafika hapa kwa ajili ya jambo hili tuliloitiwa hapa.

"sawa baba" Ally alitii amri akaanza kuyatandika majamvi chini kama alivyoambiwa na baada ya muda akawa amemaliza.

"vizuri sasa tumsubiri mzee mwenzangu anakuja sasa hivi na nimeambiwa nisiwaruhusu ndugu zako kuingia mpaka yeye afike" Msee Buruhan aliongea huku akienda kuketi dirishani alipokuwa ameketi Ally awali, Ally naye aliungana naye kwenda kukaa alipokuwa awali.

Baada ya dakika tano mlio wa pikipiki ulisikika nje ya nyumba hiyo ikija na kisha baada ya dakika moja ikaondoka, muda huo huo mzee Mahmud alionekana akiingia mlangoni akiwa amebeba taa nne kubwa za kuchaji baada ya pikipiki hiyo kuondoka.

"vipi kila kitu tayari?" Mzee Mahmud aliuliza.

"ndiyo kila kitu tayari mzee mwenzangu" Mzee Mahmud alijibu.

"vizuri basi, Ally hujambo mwanangu" Mzee Buruhan alipongeza kisha akamjulia hali Ally.

"Sijambo baba shikamoo" Ally alijibu kisha akamsalimia.

"Marhaba mwanangu vizuri kwa kuwepo hapa, ngoja nianze kazi" Mzee Buruhan aliongea kisha akaanza kutamka maneno yasiyoeleweka akawa anazunguka eneo zima lenye mikeka halafu akafanya hivyo kwenye kila pembe ya ukuta hadi akamaliza sehemu zote na alipomaliza kufanya hivyo aliwasha taa alizokuja nazo akazitundika ukutani kwenye kila kona.

"Sasa hao wanaweza kuingia wakae upande wa kushoto na uwaambie wasiongee mpaka niwaambie mimi, Ally kaa pembeni yangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akakaa chini, mzee Buruhan alitoka nje na baada ya muda akarejea akiwa pamoja na Shafii,Salma, Hamida na Jamal.

Shafii aliongozwa na Jamal hadi eneo wanalotakiwa wakae na alishushwa kwenye kiti akakalishwa kitako, baada ya wote kukaa chini kwenye jamvi waligeuka wakawa wanamtazama mzee Mahmud kujua kinachofuata.

"Bado ugeni mmoja uingie, wageni karibuni" Mzee Mahmud aliongea huku akitazama mlangoni na kupelekea watu wote watazame mlangoni, ugeni ulioingia hapo ulikuwa ni watu wanaowajua ambapo wengine walishtuka baada ya kuuona ugeni huo ambao haukueleweka umefika hapo kwa usafiri gani kwani walionekana tu wapo mlangoni.

Wa kwanza kuonekana mbele ya macho yao alikuwa ni Zalabain akiwa amevaa joho jeusi na kofia nyupe ambaye alitambulika kwa Ally na Shafii pamoja na mzee Mahmud, Ally alimtambua Zalabain kama Fahmi aliyekuwa naye hapo hadi muda wa adhuhuri na hakumfahamu kwa vingine kabisa. Shafii alimtambua huyo mtu kama mbaya wake baada ya kuiona sura yake siku aliyokufa mganga Sauti ya radi na alimkimbia, alipomuona alishtuka sana alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie asionekane eneo hilo kwani alishuhudia ukatili wa Zalabain hivyo alimuogopa. Wageni wengine walioingia eneo hilo walikuwa ni Bi Farida na Zayina wakiwa wamevaa nguo za thamani kubwa walizopata wakiwa katika ulimwengu wa majini, Shafii alipowaona alijikuta akijawa na furaha akataka kutamka neno ila ishara ya baba yake ikimkataza kutozungumza ikamfanya atulie.

"Karibu Zalabain mwana Zaif mjukuu wa Zulain mfalme wa himaya ya majini ya Majichungu, karibu uketi upande ule wa pili ukiwa na wageni wenzako" Mzee Mahmud alisema huku akitabasamu na kusababisha Zalabain atabasamu pia, Zalabain na mama yake pamoja na dada yake walienda kukaa mwingine kabisa pembeni ya upande aliopo Shafii.

"Sasa basi nimewaita hapa ili tuweze kutatua tatizo ambalo lingemsababishia mzee mwenzangu hapa asibakiwe na hata muhomili mmoja ndani ya dunia hii, utatuzi wa tatizo hilo utaanza kuonekana tu ikiwa ukweli wote utakuwa utakuwa hadharani" Mzee Mahmud alisema kisha akamwangalia Shafii akamwambia, "Shafii napenda uanze kuongea ukweli kuanzia unaanza kumpenda Bi Farida na ulivyompata hadi ukamuoa, tafadhali narudia tena tafadhali ukweli ni muhimu katika kila kitu".

Baada ya mzee Mahmud kumaliza kuongea alimpisha Shafii ili aeleze ukweli wake wote, Shafii naye hakuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli wote juu ya suala hilo ili apate nafuu ya matatizo yake kwa jinsi anavyoamini na kwa jinsi alivyoambiwa na mzee Mahmud. Shafii alianza kwa kusafisha koo lake kisha akasimulia, "Kwanza napenda nitangulize msamaha kwa hichi nitakachokusimulia ikiwa kitakuwa kimemkwaza yoyote kwani si kizuri, nilikuwa ni mtoto mtiifu sana kwa wazazi wangu kwa kipindi ambacho bado sikuwa nimepevuka kutokana na malezi ya kimaadili aliyonilea baba yangu kwa kipindi hicho.

Ndiyo muda huo huo mke wangu mama Zayina alikuwa angali binti mdogo hata kuvunja ungo bado ingawa alikuwa akitajwa ni mmoja kati ya mabinti wenye uzuri ambao haukuwahi kutokea katika kijiji chetu cha Bwagamacho Baada ya Farida kuanza kupevuka ndipo uzuri huo wa umbo na kila kitu ulianza kuonekana na kipindi hicho na ndiyo wavulana wa rika langu wakaanza kumfuata lakini waliambulia kukataliwa na binti huyo na hata wengine walishtakiwa kwa wazazi wao baada kumtongoza, jambo hilo lilinitisha na kunifanya nishindwe kwenda kumuambia kwa kuhofia ukali wa baba yangu kama akijua.

Nilimpenda sana tena sana lakini nilihofia kupigwa sana na baba yangu kama nilivyoshuhudia wenzangu wakifanyiwa hivyo na baba zao baada tu ya mashtaka kuletwa nyumbani juu ya kumtongoza Farida. Baada ya miaka miwili kupita ndipo nilipoanza kupata ujasiri wa kumtongoza ingawa nilikuwa nina uoga kwa mbali, kutongoza kwangu kuligonga mwamba na hata nilipomueleza rafiki yangu kipenzi Hamis ambaye ni kaka yake juu ya suala hilo aliniambia yupo tayari kumsaidia ikiwa tu na yeye nitamsaidia kufanikisha jambo analolitaka.

"Jambo gani wataka nikusaidie Bonoeza" Nilimuuliza Hamis.kwa kutia jina la utani ambalo hakuwa analipenda kabisa kwa kipindi hicho.

"Shafii waanza sasa nimesema hilo jina silitaki nitaacha kusaidia nikamjaze sumu dada yangu umkose" Hamis alinijia juu baada ya kumtajia hilo jina.

"Hamis nisamehe rafiki yangu niambie shida yako sasa" Nilimuomba radhi na nikawa tayari kuisikiliza hiyo shida yake kwani ndiye rafiki yangu wa shida na raha.

"rafiki yangu hii ni aibu sana hasa kwa vijana wa rika langu na nimeificha ila kwakuwa wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu nimeamua nikueleze ili unisaidie na wewe nikusaidie, kiufupi nampenda sana Salma yule mtoto mzee Rajabu ila mdomo wangu ni mzito kutamka neno hili kwake na ninabaki nikiungua ndani kwa ndani tu" Hamis alinieleza tatizo lake ambalo nilikuwa nipo tayari kumsaidia tu ili nipate moyo wa dada yake kipenzi, tatizo lake lilikuwa ni dogo tu kwani hata Salma alikuwa akimpenda vilevile na ishara zote niliziona ila tu wote hawakuwa na ujasiri huo.

Nilimsaidia hadi akampata Salma na mimi akaanza harakati za kunisaidia lakini hazikuzaa matunda kabisa kwani msimamo wa Farida bado ulikuwa ni uleule na hata alipomtumia Salma katika suala hilo ilikuwa vilevile na yeye alizidi kunipa moyo kuwa nitampata ingawa nilianza kukata tamaa juu ya suala hilo. Niliendelea kumbembeleza Farida lakini sikuchoka kwani niliamini yeye alikuwa akinipenda mimi pia na kama angekuwa hanipendi basi angelikuwa amenishitaki siku nyingi nyumbani kwetu juu ya kumsumbua kwangu lakini hakufanya hivyo, hakika sikutambua kama kaanza kukomaa kiakili na jambo kama hilo hakuwa na haja tena kulisema kwani ingeonekana ni akili za kitoto.

Niliendelea kujipa moyo nikijua ipo siku nitampata na sikutambua kama mawazo yangu ni sawa na kuchemsha mawe nikitegemea yatachemke kutokana na upendo mzito nilionao kwake, sikutambua kama najipa matumaini hayawezekani kutokea hivihivi kama kubadilika kwa majira ya mwaka kutoka kiangazi hadi vuli. Nilichojali ni kupata jibu sikujali itachukua muda gani hadi niwe naye, niliendelea kusumbuka katika kumueleza kila siku lakini niliambulia patupu na nikawa natembea na matumaini ya kumpata tu kichwani mwangu.

Matumaini yangu yaliishi katika moyo wangu lakini baadaye yalikufa baada ya muda wa miezi kadhaa tu na nikajikuta nikiumia moyoni, kufa kwa matumaini yangu kulikuwa ni baada ya kuingia kikwazo katika kumpata Farida...

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
58 Dhamana Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni