DHAMANA (22)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"Khaa! Kumbe tupo hapa kwa ajili ya kumuangalia firauni huyo, sina muda huo muache afe maana huyo ni zaidi ya shetani" Ally aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Mzee Buruhan na akajikuta akimtazama mzee Mahmud akionekana kutoelewa kafanya nini, Ally alinyanyuka ili aondoke lakini mzee Mahmud alimuita akamuomba aketi akakaa chini.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Ally tambua undugu ni kovu na halifutiki usifanye hivyo, najua unaumia kwa kile alichokifanya kaka yako lakini kumbuka ndugu ni ndugu tu" Mzee Mahmud aliongea kwa ustarabu wa hali ya juu akitegemea ataeleweka na Ally lakini haikuwa hivyo.
"Baba zangu mngejua alichokifanya huyo firauni mnayekuja kumuangalua wala msingethubutu kukaa hapa, na sijui hata ni kwasababu gani nilikuwa nikimpenda kwa kipindi chote hicho nahisi aliniroga yule maana miale ya mkufu wake sielewi hata imemifanyaje wakati nilikuwa nikimchukia" Ally aliongea huku akionesha kumchukia kaka yake.
"Ally unaongea nini wewe?" Mzee Buruhan aliuliza akionekana kushangaza na maneno anayoyaongea mwanae.
"Mzee mwenzangu kama nilivyokuambia hili tatizo linajulikana ila huyu hatakiwi kulisema na akilisema atakuwa kiziwi kama mwanzo muache huyo Shafii aeleze kila kitu. Unajua..." Mzee Mahmud aliongea maneno yaliyomfanya Mzee Mahmud atulie kimya na alishindwa kumalizia kauli yake baada ya mke wa Hamis kurudi akiwa amebeba chombo cha chakula kwenye mfuko wake.
"Vipi mgonjwa jamani tayari ameshaamka?" Mke wa Hamis aliongea baada tu ya kuwasili na alimuonesha Ally tabasamu kisha akampa mkono akampa mkono ili amsalimie akijua kuwa Ally hawezi kuongea.
Ally hakuupokea mkono wa Mke wa Hamis zaidi ya kusonya kwa nguvu kisha akanyanyuka akasema, "shetani jike mkubwa wewe".
Ally alinyanyuka kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akaelekea mahali akimuacha wazee wake na mke wa Hamis wakimshangaa sana, mke wa Hamis alipotaka kumfuata nje Mzee Buruhan alimshika akamzuia.
"Salma mama naomba unisikilize kwa umakini, achana na Ally kwa sasa kaa hapo usubiri muda wa kumuona mgoniwa akizinduka tukamuone" Mzew Buruhan alimuambia Salma mke wa Hamis.
"Lakini Ally kapatwa na nini wazee wangu kwani alikuwa hawezi kuongea na kusikia ila sasa hivi anaongea na kusikia ila amekuwa kama akili haziko sawa hadi ananisonya mimi" Salma aliongea huku akishangazwa na hali ya Ally yule aliyekuwa anamsikiliza na kumtii na kumuheshimu ameamua kuonesha dharau.
"Hebu mama kuwa muelewa achana na habari za Ally sasa hivi, tufikirie kuhusu mgonjwa tu" Mzee Mahmud aliongea kwa msisitizo huku akionekana kutopendezwa na maneno ya Salma.
"Sawa baba zangu nimewaelewa" Salma alijibu kwa shingo upande ili tu asiwaudhi wazee ambao anawaheshimu.
****
Wakati Ally akifunguliwa na kuanza kumuoneshea dharau upande wa himaya ya Majichungu Zalabain ndiyo alikuwa amerejea muda huo na aliamua kupitia chumbani walipo mama yake na dada yake ili awaone kutokana na upendo alionao kwao, alibisha hodi kwa adabu ingawa alitambua hata akiingia muda huo asingewakuta wakiwa bila stara. Alipokaribishwa aliingia kwa adabu na akaenda hadi walipokuwa wamekaa kitandani na akawasalimia, halafu naye akaketi kitandani jirani yao.
"Mwanangu kila nikikutazama namuona baba yako kwa jinsi wote mlivyokuwa na sura zilizofanana, haya niambie unatoka wapi?" Bi Farida aliongea kisha akamuuliza Zalabain.
"Nilikuwa Tanga kwenye hospitali ya SBN nilienda kuongea na mzee Mahmud" Zalabain alimuambia mama yake.
"Mh! Huyo mzee huko hospitalini anafanya nini?" Bi Farida aliuliza.
"Amekuja kumuangalia mumeo amelazwa" Zalabain alimuambia mama yake.
"Jamadin sina mume kama huyo mimi tena sitaki kumsikia ukimtaja, mume aliyetakiwa kunioa mimi ni Faimu tu na sijui ilitokea nini mpaka nikamkana na nikamsababishia matatizo makubwa sana akahama kijijini akiwaacha jamaa zake. Nampenda Faimu na natamani nimuone hata leo ili nimuombe msamaha maana yeye ndiyo kila kitu kwangu" Bibi Farida aliongea na mwishowe akalia kutokana na kujutia aliyoyafanya ya hapa zamani, Zalabain ilimbidi amkumbatie mama yake ambembeleze kutokana na upendo alionao kwake.
"Samahani mama kwa kukupa taarifa smbayo hutaki kuisikia, sipendi uhuzunike nakupenda sana" Zalabain alimuambia mama yake baada ya kunyamaza.
"Nakupenda pia mwanangu" Bi Farida alisema huku akitabasamu kwa mbali, waliendelea kuongea maongezi mengine kwa furaha wakiachana na suala ambalo lilionekana kutomfurahisha kabisa Bi Farida.
****
Baada ya masaa mawili Shafii aliamka kutoka usingizini akiwa yupo vizuri kiafya kuliko awali, hali yake iliendelea kutengemaa na ilipofika muda wa alasiri aliruhusiwa na daktari na alirudi nyumbani akiwa ameongozana ns wote waliokuja kumuona hospitali kasoro Ally tu ambaye hakurudi tangu aondoke pale hospitali. Shafii alipelekwa moja kwa moja chumbani kwake na akaachwa apumzike na kisha wazee wake wakakaa sebuleni hadi ilipoingia jioni ndiyo mzee Buruhan na mzee Mahmud waliingia chumbani kwa Shafii wakamkuta akiwa ameamka ameegemea mito kitandani kwake, Shafii alipoona ujio wa wazee wale alihisi kuna jambo ila alikaa kimya ili apate uhakika wa wasiwasi wake.
"Shafii" Mzee Buruhan alimuita
"Naam Baba" Shafii aliitikia
"unajua kama wewe ndiyo nguzo kuu kati ya nguzo zangu nne zilizobakia?" Mzee Buruhan alimuuliza
"nafahamu hilo baba" Shafii alijibu.
"Hussein hatunaye, Hamid hatunaye, Hassan ni mdogo kwako, Falzal ni mdogo kwako na Ally pia ni mdogo kwako. Wewe pekee ndiyo mkubwa ndiyo kiongozi wao ingawa wote wana maisha yao na hata wanajisomesha wakitaka kujiendeleza kielimu. Nadhani unatambua hilo" Mzee Buruhan alisema.
"Ndiyo baba natambua hilo" Shafii alijibu.
"Sasa basi inapotokea tatizo lenye kuhitaji kuelezewa ili lisizidi zaidi inabidi lielezewe mwanangu ikiwa utakaa kimya haitasaidia chochote" Mzee Buruhan aliongea.
"Baba sijakuelewa unachomaanisha" Shafii aliongea.
"Shafii najua unatambua suala la upotevu wa mke wako na hata mwanao linalokufanya uwe na matatizo kila kukicha, sasa mwanangu ukilificha itakusaidia nini ikiwa unalifahamu chanzo chake. Kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua mwanangu, mwanangu ni bora uitoe aibu mbele ya daktari ili utibiwe kuliko kuficha tatizo halafu ufe na ugonjwa. Ongea chanzo cha haya ni nini?" Mzee Buruhan alimsihi mwanae.
"Baba kusema ukweli sijui wala sitambui suala hili linasababishwa na nini?" Shafii alikataa.
"Shafii vuta kumbukumbu zako vizuri umefanya nini mpaka yote haya yatokee au hutaki familia yako uione tena ikiwa na upendo" Mzee Buruhan alizidi kumsihi.
"Baba napenda sana familia niione tena ikiwa ina upendo lakini sikukumbuki chochote kilichosababisha haya ninayofanyiwa" Shafii alikana kabisa juu ya suala hilo.
"Jirani na mashine ya kusaga unga kule Mpirani miaka ishirini na moja iliyopita unakumbuka kilitokea nini pale kwenye nyumba yako uliyokuwa unaishi baada ya wewe kuhama tena ilikuwa majira ya saa sita usiku?" Mzee Mahmud aliongea kwa mara ya kwanza na kumfanya Shafii ashtuke kwa jambo alilotajiwa, lilikuwa ni jambo ambalo alishalisahau kabisa katika ubongo wake na sasa alikumbushwa na mzee huyu ambaye ni mganga mtaalam.
"Shafiii unakumbuka nini hiyo siku" Mzee Buruhan naye aliunganisha maelezo ya rafiki yake ingawa hakuyaelewa kabisa, maneno ya mzee Mahmud yalimfanya anyamaze ghafla huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
"Shafii si nakuuliza" Mzes Buruhan aliongea huku akimtikisa bega baada ya kuona yupo kimya, Shafii alikurupuka baada ya kutikiswa bega kama alikuwa yupo katika usingizi mzito.
"Ha..hapana si....sikumbuki chochote" Shafii aliongea kwa kubabaika baada ya kuhisi moja ya jambo baya alilolifanya linakaribia kugundulika.
"Una uhakika?" Mzee Mahmud aliuliza.
"ndiyo baba zangu nina uhakika wa kile ninachokiongea" Shafii alijikaza akajibu kwa kujiamini.
"mzee mwenzangu sisi twende tukanywe kahawa si unaona muda huu na kiubaridi cha kipupwe kimeanza, Shafii kama hujui juu ya hilo basi inakupasa utambue kuwa maisha ya mkeo na binti yako yapo kwenye kinywa chako kueleza unachojua na ukikaa kimya jua kinachofuata ni kama kilichowapata wadogo zako ia utambue umebaki peke yako" Mzee Mahmud huku akiwa tayari amesimama na Mzee Buruhan naye akasimama, wote kwa pamoja walianza kutembea kuelekea ulipo mlango ili waondoke lakini sauti ya Shafii ikiwaita iliwafanya wasimame na kugeuka wakamtazama.
"Nipo tayari kuwaambia kilichotokea wazee wangu naomba mnisaidie" Shafii aliongea baada ya kuona maji yamemfika shingoni na maneno ya mzee Mahmud ndiyo kabisa yalimfanya akubali. Mzee Mahmud alimtazama Shafii kwa tabasamu hafifu halafu akamuambia, "kesho muda kama huu pale ulipokuwa unaishi kule mpirani ndiyo kutakupa ahueni ya tatizo lakokwa familia yako"
Mzee Mahmud aliposema maneno hayo alitoka humo ndani bila hata kumuangalia Shafii kwa mara nyingine, Mzee Buruhan naye alifuata akiwa nyuma yake.
****
Maneno ya Ally baada tu ya kupewa mkono na Salma yalimfanya Salma karibia siku nzima akiwa anajifikiria kwani Ally alikuwa amepatwa na nini mpaka awe vile, ilipofika jioni aliamua kutoka na kwenda kumtafuta Ally bila ya kumueleza mtu ili aongee naye tu kwani Ally alikuwa ni mmoja kati ya wanaume aliokuwa anawapenda na kipindi cha nyuma alipokuwa msichana alishajaribu kujivika ujasiri na kumueleza Ally yaliyo moyoni mwake lakini aliishia kukataliwa baada ya Ally kuwa anamuheshimu sana Hamis ambaye alikuwa na mahusiano na Salma kabla hajamuoa.
Baada ya mpango ambao ndiyo chanzo cha balaa lote lililowakumba watoto wa mzee Buruhan, Ally alifungwa akili na akawa anasikiliza wote waliofanya mpango ule bila hata kuwapinga na alifungwa akili baada ya kuujua mpango huo akawa amekasirishwa nao. Baada ya kufungwa akili ndipo Salma alipompata Ally kutokana na yeye pia ni mmoja kati ya watu walioshiriki huo mpango, alimtumia Ally vyovyote atakavyo baada ya Ally kutopinga kauli yake. Sasa akili ya Ally ilipofunguliwa na Mzee Mahmud na Salma kujibiwa vile alijikuta roho ikimuuma akijua Ally amepatwa na tatizo hivyo aliamua kumtafuta. Hakukujua kama Ally wa leo siyo wa jana alichokuwa anakijali yeye ni penzi lake haramu alilolianzisha kwa Ally hata alipokuwa yupo ndani ya ndoa.
Tamaa za kutamani kingine wakati akiwa tayari ana kingine mkononi ndiyo zilimfanya Salma afanye jambo hilo ambalo lilipelekea afiche siri nzito sana ambayo laiti ingaligundulika mapema basi angekuwa ameleta matatizo makubwa sana kwa Hamis na Ally.
Juhudi za Salma kumtafuta Ally ziliendelea kwa usiku huo akiwa yupo ndani ya gari yake na hatimaye alimkuta akiwa amekaa kwenye matairi yaliyochimbiwa katika uwanja wa mpira uliopo mkabala na shule ya sekondari ya Usagara, Salma alimfuata hadi hapo akaegesha gari pembeni kisha akashuka akaenda kumkumbatia Ally akitegemea atapokelewa lakini alijikuta akisukumwa hadi akaanguka chini akaumia.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni