SIKUACHI BABY (5)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Juma Hiza
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Siku hiyo nilifanya kazi mpaka muda wa saa tano za usiku, nilipitia katika moja ya mgahawa niliyouzoea, nikala nilipomaliza nilirudi ghetto. Nilipofika nikaenda kuoga na baada ya kumaliza nikajilaza kitandani, muda huo Samira alikuwa tayari amenitumia ujumbe mfupi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
“Naweza kukupigia Metu?” alinitumia.
“Ndiyo kama hutojali,” nilimjibu kisha akaweza kunipigia, nikapokea.
“Hallo Metu vipi uko salama?” aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Una uhakika?” aliniuliza tena kwa sauti iliyokuwa na utulivu wa hali ya juu.
“Ndiyo kwani vipi?” nilimjibu kisha nikamuuliza.
“Hapana unajua leo jioni nilikuona haupo sawa ndiyo maana nimekuuliza hivyo,” aliniambia.
“Samira,” nilimuita.
“Abee,” akaitika.
“Upo na nani hapo?”
“Niko peke yangu kwanini umeniuliza hivyo?”
“Hapana nahisi hiki ninachokwenda kukueleza nitakuvunjia heshima ila utanisamehe,” nilimwambia kisha nikavuta pumzi ndefu na kuziachia.
“Wewe niambie usiogope lolote,” aliniambia.
“Samira,” nilimuita tena kisha nikanyamaza kwa muda.
“Abee Metu niambie basi,” aliniambia, wakati huo nilikuwa nikijipanga kumwambia yale yaliyokuwa yananisibu moyoni na sababu kubwa alikuwa ni yeye.
“Najitahidi kukaa nacho moyoni, nisikiseme lakini kuna muda nashindwa, nahisi nahitajika kukisema ila nitakisemea wapi wakati mazingira sio rafiki na licha ya mazingira muhusika mwenyewe anaonekana kutokuwa sawa na mimi,” nilimwambia maneno ya kuuzunguka mmbuyu.
“Sasa unavyoendelea kuzunguka na kunifumba unadhani nitafahamu ni nini kinachokusumbua?” aliniuliza.
“Samira wewe ni mtu mzima najua una akili ya kufikiria baya na zuri. Sitaki kuamini kuwa lugha ya Kiswahili imekutupa mkono na wenda asili yako ni ya Ughaibuni. Sitaki kuamini hilo kabisa,” nilimwambia huku nikiamini bado hajang’amua lolote nililokuwa namaanisha.
“Metusela hutaki kuniambia au?” aliniuliza kwa sautiya kukata tamaa, alitamani kusikia kile kilichokuwa kikinisumbua lakini kwa muda ule ni kama vile nilikuwa namficha.
“Samira nimetokea kukupenda halafu hata sielewi hisia hizi zimetokea wapi yani nashindwa kuelezea,” nilimwambia huku nikiwa nimejikaza mwili mzima, nilihisi baada ya kumwambia maneno hayo labda angeweza kunitukana nikajipanga kuyakoga matusi kisawasawa.
Nilimsikia akivuta pumzi ndefu na kuziachia, akabaki kuwa kimya cha muda wa sekunde kadhaa, nikahisi labda atakuwa amekata simu, nikaitazama bado alikuwa hewani.
“Samira,” nilimuita.
“Niambie.”
“Mbona umekaa kimya tena huongei?”
“Hapana Metu hivi nikuulize kitu.”
“Yeah! niulize.”
“Hivi umefikiria nini mpaka ukaniambia hivyo.”
“Hakuna nilichokifikiria zaidi ya mapenzi ya dhati niliyokuwa nayo kwako, nimejikuta nikitamani kuwa na wewe, uwe mwanamke wangu wa maisha na nitakupenda siku zote za uhai wa maisha yangu.”
“Metusela.”
“Naam!”
“Sidhani kama itawezekana.”
“Kwanini?”
“Mimi na wewe ni kama dada na kaka halafu isitoshe nina mpenzi wangu japo siishi naye lakini nampenda sitaki kumuumiza.”
“Nahisi nimekukosea nisamehe sana.”
“Usijali Metusela nafahamu kila kitu kuhusu mapenzi, naelewa jinsi hisia zinavyomuingia mtu kwa haraka. Wala hujanikosea, najua ni hisia zimekutuma uniambie hivyo, unastahili kuniambia lolote ila kwa wakati huu umechelewa mimi nina mpenzi wangu tayari.”
“Mpenzi wako ni yupi?”
“Mbona umeniuliza hivyo au unataka kumfahamu?”
“Ndiyo lakini kama itawezekana maana tangu nilipokufahamu sijawahi kukuona ukiwa na mwanaume labda wa kuniambia kila siku mdomoni.”
“Kwa sasa hayupo nchini amesafiri yupo Marekani kikazi.”
“Anafanya kazi gani?”
“Mbona unataka umfahamu sana wewe elewa kuwa yupo kikazi.”
“Sawa nimekuelewa Samira basi acha nilale, nahisi sipo sawa kabisa.”
“Una nini?”
“Nahisi homa halafu natetemeka.”
“Umemeza dawa?”
“Hapana.’
“Kwanini?”
“Sijanunua mpaka kesho Mungu akipenda.”
“Metu ujue unahatari wewe yani unaumwa halafu hununui dawa kweli?”
“Ningefanya nini wakati Muda wote niliutumia kwa ajili yako.”
“Kwa ajili yangu?”
“Ndiyo ila usijali nitakuwa sawa, acha nilale pia nikutakie usiku mwema,” nilimwambia kisha nikakata simu.
Licha ya maumivu niliyoyapata ghafla! baada ya Samira kuniambia alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa nchini Marekani lakini sikutaka kuamini kama kweli nilimkosa, niliona kushindwa kumfuata kesho yake kwa ajili ya kumpeleka kazini kama ilivyokuwa kawaida yangu, niliutumia uongo wa kuumwa homa ili siku inayofuata nisiende kumchukua. Niliona haya kukutana naye.
Nikamkumbuka Sesilia ambaye ni siku chache zilipita tangu nilipomtukana na kumpa maumivu makali ya mapenzi, nilimkosea sana na kwa kitendo kile kilichokuwa kimenitokea cha kushindwa kumpata Samira nikaanza kumkumbuka.
Akili ikaniambia nichukue simu kisha nimuandikie ujumbe mfupi wa kumuomba msamaha lakini nilishindwa kufanya hivyo. Ni kama vile kulikuwa kuna nafsi inakuja na kuniambia ‘aliyepita amepita mtazame mwingine.’ Nikaghairi na sikutaka kuishika simu tena nikaamua kulala.
****
Niliamka asubuhi ya siku nyingine, nikakutana na ujumbe wa Samira aliyoniandikia kuwa siku hiyo nipumzike, nisiende kumchukua kutokana na kuumwa kwangu, hakuacha kunikumbusha katika ujumbe huohuo aliyonitumia kuwa nisisahau kwenda hospitali kupima kujua ni nini kilichokuwa kikinisumbua. Nilitabasamu baada ya kuusoma ujumbe wake aliyoumalizia na maneno ASUBUHI NJEMA.
Nilishindwa kuelewa kulikuwa kuna kitu gani kilichokuwa kikiendelea, ghafla! Samira alitokea kuwa mtu wa kunijali sana kitendo ambacho sikukitegemea kabisa.
“Unatumia usafiri gani?” nilimtumia ujumbe wa kumuuliza.
“Nitachukua bajaji usijali.”
“Leo unapanda bajaji?”
“Ndiyo sina jinsi itabidi nipande, sitaki nikusumbue Metu unaumwa.”
“Lakini sijazidiwa.”
“Hata kama lakini inabidi upumzike Metu.”
“Sawa.”
“Jioni nikirudi nitakuja kukusalimia ili nijue kama kweli umeenda hospitali na dawa unionyeshe.”
“Sawa karibu,” nilimjibu.
Sikutaka kuumiza kichwa juu ya vipimo na dawa za kumzugia Samira, nilichoamua kukifanya nilimpigia simu rafiki yangu ambaye alikuwa ni daktari, nilimueleza shida yangu na aliahidi kunisaidia.
Nilipomaliza kuweka mambo sawa nilienda kufanya kazi yangu ya bodaboda huku nikiwa makini kutazama muda ambao Samira alikuwa akitoka kazini.
Ilipofika majira ya saa tisa nilirudi nyumbani kwangu, sikupika wala kuandaa chochote zaidi ya kufikiria jinsi ya kumdanganya pindi atakapokuja kuniona. Nikajilaza kitandani.
Baada ya kupita lisaa limoja ghafla! nilisikia mtu akibisha hodi, nilitabasamu baada ya kuisikia sauti ya Samira.
“Karibu,” nilisema kisha nikaenda kufungua mlango.
Nilipoufungua mlango nilikutana na Samira ambaye alionekana kuwa na wasiwasi, aliponitazama akatabasamu.
“Nilihisi labda nimechanganya chumba,” aliniambia kisha akacheka kidogo.
“Usingeweza kupotea,” nilimwambia kisha nikamkaribisha ndani. Akaingia lakini alionekana kuwa muoga kiasi, hakukuwa na kochi, kabati wala kitu chochote cha kukalia zaidi ya ndoo mbili za maji, kitanda, vyombo baadhi vya kupikia pamoja na lundo la nguo chafu zilizokuwa zimezaa chini huku nyingine zilizokuwa safi zikiwa katika mpangilio mbovu.
Alisimama kwa muda wa sekunde kadhaa baada ya kuingia ndani, alionekana kushangazwa na muonekano wa chumba changu ambacho kilionekana kukosa matunzo. Kwa jinsi alivyokuwa akishangaa ni sawasawa na mtu ambaye alikuja na kuniambia yani muonekano wangu na chumba changu vilikuwa ni vitu viwili tofauti.
“Nini?” nilimuuliza baada ya kumuona amebaki ameduwaa.
“Hakuna kitu,” alinijibu kisha akaendelea kuzubaa huku akiwa haelewi ni wapi alitakiwa kwenda kukaa.
“Karibu pita uje ukae hapa,” nilimwambia kisha nikampa ishara ya kukaa kitandani, akazidi kuonekana kusita. Wasiwasi wake ulijidhihirisha wazi kupitia uso wake ambao haukuwa na chunusi hata moja, alionekana kuwa mrembo mno.
Nilifahamu alikuwa akihofia tukio ambalo lingeweza kutokea muda wowote endapo angekubali kukaa kitandani, hata hivyo sikutaka kuwa sawa na mawazo yake, sikutaka kufanya jambo lolote zaidi ya kuzungumza naye pamoja na lengo lake kubwa lililokuwa limemleta.
Unajua ukitaka kumteka kimapenzi msichana ambaye moyo wake upo kwa mwanaume mwingine inabidi utumie akili nyingi sana, usikurupuke katika kufanya maamuzi na hicho nilichokuwa nikikifanya kwa Samira.
Hatimaye aliweza kukaa kitandani huku ule wasiwasi wake ukiwa bado haujamuondoka, hakuzungumza lolote alibaki kuwa kimya huku akiendelea kukishangaa chumba changu ambacho kilionekana kuwa hovyo.
“Enhee! Vipi huko kazini kazi zinaendaje?” nilimuuliza huku nikitabasamu wakati huo nilikuwa nimekaa pembeni yake.
“Zinaenda vizuri tu,” alinijibu kwa sauti ya chini iliyosheheni kila rangi ya aibu.
“Mbona sasa umechelewa hivyo au ulipitia nyumbani kwanza?” nilimuuliza.
“Hapana nimetoka kazini nikasema nikupitie kwanza nijue unaendeleaje.”
“Umetumia usafiri gani?”
“Nimepanda daladala.”
“Kumbe foleni.”
“Ndiyo leo kulikuwa na foleni sana.”
“Sawa mimi naendelea vizuri kama unavyoniona.”
“Umeenda hospitali?”
“Ndiyo.”
“Wamekuambiaje?”
“Nimekutwa nina malaria ila wameshanipa dawa.”
“Dawa gani?”
“Mseto.”
“Sawa vizuri ila inabidi uzingatie kumeza dawa kwa wakati na kula chakula cha kutosha ili uwe sawa.”
“Mbona nazingatia,” nilimwambia.
Kwa muda ambao niliendelea kuzungumza na Samira nilijikuta nikianza kuingiwa na pepo la ngono, nilipomtazama nilihisi kama kuna mtu anayenisukuma na kunishawishi nimlazimishe Samira kufanya naye mapenzi hata kwa nguvu.
Sikutaka hisia ziendelee kuniongoza, niliendelea kupambana na hali hiyo huku nikijitahidi kujiweka sawa na kujisahaulisha na mawazo hayo lakini kuna muda nilianza kushindwa, mtarimbo wangu ulikuwa tayari umeshasimama.
“Metu mimi sikai nimekuja kukuona mara moja acha niende nyumbani kwangu nikaendelee na ratiba nyingine,” aliniambia kisha akasimama tayari kwa kuondoka, nilishindwa kusimama kutokana na hali niliyokuwa nayo, nikabaki nikimtazama huku nikiwa nimekaa pale kitandani.
“Mbona mapema sana?” nilimuuliza.
“Hapana acha nikaendelee na ratiba nyingine za nyumbani siunajua mimi ni muajira hivyo lazima niwahi kujiandaa na majukumu ya kesho ila nimefurahi kukuona uko salama.”
“Sawa lakini umesahau kukagua vitu vyako.”
“Vitu gani?”
“Dawa pamoja na majibu ya daktari.”
“Usijali nakuamini ila zingatia uzimalize ili upone,” aliniambia kisha akaniaga na kuondoka zake.
Kiukweli sikutaka kuamini kama kweli nilijizuia kiasi kile mpaka Samira akaweza kuondoka bila kufanya naye lolote. Hii haikuwa desturi yangu katika kumbukumbu za wasichana ambao waliingia ndani ya chumba changu hakuwepo mmoja wao ambaye aliweza kutoka salama, wote niliwarubuni na mwisho wa siku wakajikuta nimefanya nao mapenzi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni