DHAMANA (5)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Muda ambao ajali ya pili ya moto inatokea kwa upande mwingine mkoa wa Tanga katika sehemu ya jiji kulikuwa kuna kikao kizito cha viongozi waiuu wa kampuni ya Extoplus wakiongozwa na mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa kampuni hiyo bwana Hamid Buruhan, kikao hicho kilikuwa kinajadili mambo mbalimbali kwa ajili ya kukuza kampuni hiyo.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Mambo mbalimbali ya kimaendeleo yalikuwa yakijadiliwa kuhusu kukuza kampuni ikiwemo suala la kuongeza nyumba za kupangisha katika sehemu zote zenye maendeleo duni ambazo watumishi wa umma hupelekwa ili wapate makazi bora kama waliyoyaacha mjini. Mojawapo ya kutekezwa mpango huo ulikuwa umeshaanza katika kijiji cha Duga na ulitegemea kuendelezwa katika sehemu zingine za Tanga nzima, mameneja hawa wakuu walikuwa, mkurugenzi, pamoja na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo walionekana wana ari ya kuwa na kampuni kubwa yenye maendeleo katika kila kona ya nchi na hata nchi nyingine.
"Hadi kufikia mwaka 2020 mpango wetu huu utatufikisha mahala tulipojiwekea kufika katika nyanja za kimaendeleo. Extoplus kwa maendeleo" Hamid alihitisha kisha kikao hicho na hapo kikao kikawa kimefikia mwisho kwa siku hiyo, alipeana mikono na wafanyakazi wake wakuu huku akibadilishana nao mawazo kwani walikuwa pia ni marafiki zake. Walionekana na furaha sana wala hawakutambua kama kuna kuzungumkuti kimetokea kinachohusu kampuni yao, walikuwa na furaha sana kutokana na kiasi kikubwa cha fedha wanachokiingiza kutokana miradi yao na hata uzuri wa maisha wanayoishi.
"GRIIIIII! GRIIIIIIII!" Mlio wa simu ya mezani isiyo na waya ulisikika ukilia ambayo ilikatisha maongezi na Hamid akaipokea kisha akasema, "halloo!".
"kuna tatizo gani wewe Gasper hebu eleza vizuri nikuelewe" Hamid aliongea
"etii! Unase.."Hamid alisema kwa mshangao sana akionekana ameshtushwa sana na taarifa aliyopewa na hata maneno aliyoyataka kuyasema hakuyasema kabisa kwani nguvu zote zilimuishia kutokana na taarifa hiyo na akaanguka kama gunia la chumvi akiwa tayari ameiachia simu. Wenzake walipomfikia na kumtazama mapigo yake ya moyo walikuta yanapiga kwa mbali na ikawalazimu wote kwa pamoja wambebe kumuwahisha katika zahanati ya kampuni hiyo iliyopo ghorofa ya pili ya kampuni hiyo, walifanikiwa kufika salama na wakamuingiza kwenye wodi akaanza kuhudumiwa kwa haraka sana.
Mameneja wakuu wote walikaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa ili wasubiri majibu ya daktari pamoja na wauguzi ambao walikuwa wanashughulika katika kumtibu mkuu wao wa Kampuni, baada ya kupita dakika kumi na tano tangu waanze kusubiri kaimu mwenyekiti mtendaji wa kampuni na hiyo na rafiki wa karibu wa Hamid anayeitwa Hisan Shelukindo alinyanyuka kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akasema, "jamani mimi nimesahau simu katika chumba cha mkutano floor ya nane wacha niifuate nitarejea maana ni muhimu kuwa nayo kwa ajili ya kupokea taarifa muhimu".
Hisan aliposema hivyo wenzake waliitikia kwa kutikisa vichwa kisha akaondoka hadi nje ya mlango wa kuingilia katika zahanati, akitokea kwenye korido kisha akatembea hadi zilipo lifti za jengo la kampuni yao. Alibonyeza kitufe kilichokuwa kipo jirani na lifti kisha akasubiri kwa muda mfupi ambapo lifti ilifunguka akaingia akabonyeza kitufe namba nane, milango ya lifti ilijifunga na lifti ikaanza kupanda kuelekea juu hadi ghorofa ya nane, lifti ilifunguka kisha Hisan akashuka akatembea hadi kwenye mlango wa chumba cha mkutano akaufungua. Alikutana na giza kutokana na taa ya humo kuzimwa na chumba chenyewe huwa hakipitishi mwanga hata mchana kutokana kuwa na vioo visivyoruhusu mwanga kupita.
"Mmh! Hizi taa za humu kazizima nani tena" Hisan ajisemea huku akiwasha taa na ilipowaka alirudishia mlango wa chumba hicho cha mkutano kisha akatembea kuelekea mezani alipoiacha simu yake, akiwa yupo katikati ya umbali uliopo kati ya meza na mlango taa za humo ndani zilizima tena na giza likarudi kama ilivyokuwa awali kabla hajawasha taa.
"Shit! Hawa vijana wa chumba cha kuongozea umeme wanafanya upuuzi gani, inamaana wameachia umeme wa Tanesko ndiyo ufanye kazi" Hisan alijisemea kisha akageuka ili aende kufungua mlango ili hata mwangaza wa madirisha yaliyopo kwenye ngazi yamuongoze kuifuata simu yake, alipopiga hatua moja taa zikawaka ten akaghairi kwenda kufungua mlango akarudi kuchukua simu yake. Alianza kutembea kuelekea kwenye meza na alipofika akaichukua simu yake halafu akaanza kuelekea mlango ili atoke nje, alitembea kwa hatua kubwa hadi mlangoni akanyonga kitasa kuufungua lakini haukufunguka na ilionekana ulikuwa umefungwa kwa nje. Hisan alijikuta akiachia tusi zito sana kutokana na kitendo hicho, aligeuka nyuma akaangalia chini akaiona simu iliyoangangushwa na Hamid alipopoteza fahamu.
Wazo la kuiokota ndiyo lilimjia kichwani mwake na akalitaka kulitekeleza tu kwani hakukuwa na njia nyingine itakayomuwezesha yeye kupata msaada kutoka nje, alipoanza kupiga hatua ili aifuate taa zilizimika tena kisha kofi zito lilitua shavuni mwake lililompeleka hadi chini. Taa zilipowaka hakuona mtu yoyote ndani ya chumba hicho ingawa maumivu ya kofi alilopigwa alikuwa anayasikia, aliposimama miguu yake yote ilizolewa yote kama anapigwa mtama na akajikuta ameenda kusalimiana na sakafu yenye marumaru katika chumba hicho. Taa za chumba hicho zilizima tena safari kipigo kizito kikawa kinamshukia Hisan bila hata kumuona huyo anayempiga, taa zilipowaka tena Hisan hakuwa anaweza hata kuinuka na alikuwa akitokwa na damu usoni sehemu nyingine za mwili wake na mbele yake kulikuwa kuna mtoto wa miaka takribani saba akiwa amekasirika san ambaye sura yake haikuwa ngeni sana kwa Hisan.
"Jamadin" Hisan aliita kwa uoga na macho yake yakawa yakimtazama yule mtoto.
"nipe" Yule mtoto alisema kwa sauti nzito iliyojaa kitetemeshi.
"nikupe nini?!" Hisan aliuliza kwa uoga.
"narudia kwa mara ya mwisho nimesema nipe" Yule mtoto aliongea kwa hasira akaanza kumfuata Hisan
"nikupe nini?!" Hisan aliongea akiwa anatetemeka akijiburuta kusogea nyuma kwa makalio yake, Yule mtoto alizidi kumsogelea na alipomkaribia alipotea kimaajabu akamuacha Hisan akiwa anashangaa lakini mshangao wake haukudumu kwani alijikuta akishikwa kichwa chake kwa nguvu kutokea upande wa nyuma. Kichwa chake kiliminywa kwa nguvu hadi kikapasuka na akawa ameingia katika orodha ya wasio na uhai waliowahi kuwa hai.
****
Gari ya waliyopanda James na wenzake pamoja na Asp John ilikuwa ilienda kilomita kadhaa kutoka pale bwaga macho kwenye ajali wakaikuta ile gari aina ya Landcruiser prado iliyotumiwa na wakina James kuja nayo ikiwa ipo pembeni na mwenzao akiwa yupo pembeni akiwa ameegemea. Gari ya polisi waliyopanda kina James ilienda kuegeshwa mbele ya gari hiyo na kisha wote kwa pamoja wakashuka wakamfuata mwenzao wakiwa na Asp John.
"Vipi Tom gari mbovu nini?" Gasper alimuuliza yule mwenzao waliyemuachia gari arudi nalo kule Duga kwenye sherehe ya kampuni.
"aisee hii gari kuiendesha ni kujitakia kifo bora mlivyokuja tuondoke wote mimi siigusi tena na kazi kwenye hii kampuni naacha" Tom aliongea huku akiwafuata.
"kuna nini kijana?" Asp John alimuuliza.
" jamani baada ya kuniachia hii gari nimeendesha vizuri ila nilipo fika hapo nyuma nikiwa kwenye mwendo mkali naanza kusikia sauti ya bosi mkuu ikivuma kama mwangwi masikioni mwangu ikisema nataka damu ya vijana wangu kumi. Nikiwa najifikiria juu ya eneo inapotoka sauti hiyo si ndiyo nikashudia kioo cha mbele chote kikiwa kimejaa damu hadi nikawa sioni kabisa ingawa nilijitahidi kusimamisha gari nikafanikiwa na hapo damu hizo zikawa zimetoweka mara moja na kioo kikawa kawaida kama ilivyokuwa awali. Nimeshuka ndani ya gari na sina hamu nalo tena" Tom aliongea akiwa anahema sana kwa uoga, wenzake wote waliposikia kilichomkuta ndiyo walizidi kuingiwa na hofu kasoro tu Asp John alionekana yupo kawaida tu.
"nyie hebu wacheni uoga wenu, wewe hebu nipe hizo funguo za gari hiyo niendeshe mimi na nyinyi pandeni hiyo ya polisi tuondoke" Asp John aliwaambia akionekana hana hofu kabisa.
"Afande utakufa usipande" James aliongea.
"kwani wewe ndiyo utakuwa hufi, kama leo ndiyo nitatakiwa nife nitakufa tu hata nisipoendesha hili gari, hebu nipe ufunguo sasa"Asp John aliongea na Tom akampatia ufunguo wa gari.
"mambo si hayo bwana sio kuleta uoga wa kike wakati nyinyi ni wanaume" Asp John aliongea akiwa anaelekea kwenye gari ya kampuni ya Extoplus baada ya kukabidhiwa ufunguo na Tom, aliufikia mlango wa gari hiyo akaufungua akawa anaingia ndani ya gari.
"leo sihitaji damu ya askari jasusi nataka ya hawa hapo mbele sasa ukijipendekeza tu katika jambo lisilo kuhusu utasalimiana na kaburi" Sauti ya mwangwi ilivuma kwenye masikio ya Asp John lakini akaipuuzia na kuamua kuingia ndani ya gari kisha akaiwasha gari hiyo, alinyonga ufunguo na gari ikawaka kisha ikazima. Alinyonga tena ufunguo safari hii gari ikatikisika sehemu ya injini kisha moto mkubwa ukawaka ukawa unakuja kwa kasi mithili ya moto wa nyikani kwenye katika upande aliopo Asp John.
"Ha! Ha! Ha! Ha! Si mbishi wewe ngoja nikuchome kama kuni" Sauti yenye kuvuma iliendelea kusikika masikioni mwa Asp John na hapo akaona hatar ipo mbele yake na akaamua kujirusha nje akaangukia upande wa pili barabara sehemu yenye majani, moto uliokuwa unawaka ndani ya gari haukuonekana na wala gari halikuonesha kama linalipuka. Asp John alijinyanyua kutoka pale alipojirusha akaenda hadi pale alipowaacha vijana wa kampuni ya Extoplus akawaambia, "pandeni kwenye gari tuondoke".
"Afande kulikoni mbona umejirusha nje baada ya gari kuwaka si ulisema unaliendesha" Tom alimuambia Asp John kwa kejeli kutokana na tabia yake ya kudharau mambo anayoambiwa.
"kaa kimya na upande kwenye gari na mwenzako tuondoke" Asp John aliongea huku akipanda kwenye gari la polisi aliyokuja nayo, vijana wa Extoplus nao wakapanda na safari ikaendelea na muda huo ndiyo Gasper alimpigia simu msichana wa mapokezi makao makuu aliyemuunganisha simu na mkuu wao Hamid akamueleza tukio zima.
Baada ya dakika kumi na tano walikuwa tayari wameshafika Duga maforoni na wakielekea moja kwa moja hadi kwenye soko kuu la Duga maforoni wakashukia upande huo kutokana na upande wa pili kwenye eneo la tukio kutokuwa na nafasi, walivuka barabara wote kwa pamoja wakaupita uwanja wa mpira wakakuta umati wa watu ukiwa umezunguka nyumba hizo bado zilikuwa zinateketea na moto huo ulishindikana kuzimwa na kikosi cha zima moto kilichofika hapo kwani magari yao yalitumia maji hadi yakaisha lakini moto haukuzimika hata kidogo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni