KIJIJINI KWA BIBI (22)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"jamani mbona unanifanyia hivyo, au kwa kuwa nimekwambia
nakupenda?" Binti Mchungaji alilalamika kwa huruma.
"sikia binti, hapa unapoteza muda wako bure, kiukweli kabisa mi
siwezi kukubalia ombi lako" Kayoza aliongea kwa ujasili kwa maana
aliona bora amueleze ukweli tu kuliko kumpotezea muda,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Binti
Mchungaji alijishusha sana, alafu akajenga chuki kali sana kwa
Kayoza.
"Kwanini umeamua kufanya hivyo? au kwa kuwa nimeamua kukueleza
hisia zangu?" Binti Mchungaji aliongea huku machozi yanamtoka,
"Nimefanya hivi kwa sababu nakupenda na najipenda pia" Kayoza
aliongea kwa sauti ya chini kisha akaondoka kumfuata Omary,
"anajiona mzuri kumbe hana lolote, ni shetani tu ananyonya damu za
watu, na kesho nitaitoa taharifa polisi ili nipate yale mapesa
waliyotangaza" Binti Mchungaji aliongea kimoyo moyo huku akiwa
anarudi kanisani na hasira kibao zikiwa zimemtawala.
"kaka umeniangusha" Omari aliongea huku akitabasamu
"achana nae, mtoto wa mchungaji alafu anaendekeza ukicheche" Kayoza
alijibu.
"Ila mpaka mwanamke akuambie maneno nayo, ujue anakupenda kweli"
Omary alimwambia Kayoza,
"Akampende baba yake na mama yake, mimi sina taimu nae" Kayoza
alijibu kijeuri,
"Sawa bwana, kufanya hivyo umemuepusha na kifo",Omary aliongea,
"Sijamuepusha, sema nimemsogezea mbele kifo kwa maana kifo
hakiepukiki" Kayoza aliongea wakati wanafika eneo la nyumbani kwao.
*""""
Ilipofika alfajili, Sajenti Minja aliondoka kanisani na kuelekea
moja kwa moja nyumbani kwake kupumzika, kwa kuwa alichelewa sana
kulala alijikuta anautandika usingizi mzito.
Mida ya saa nne akakurupuka kitandani kwake, ni kawaida yake
kujisachi anapoamka, hasa pale anapolala na nguo alizotoka kutembea
nazo,
alipojisachi, akakuta hana kitambulisho cha ofisini,
"mh, kitakuwa wapi, ila ngoja nikakicheki kwa dada kule na nidoee
chai kabisa" sajenti Minja alijiongelesha peke yake.
Akaenda kuoga na kujisafisha kinywa kisha akajiandaa ili aende kwa
Dada yake.
Akatoka nje akawasha gari, akaondoka
Binti wa mchungaji aliamka ana hasira sana siku hiyo, aliamka saa
tatu, ila mpaka saa nne alikuwa ameshawapiga makofi wadogo zake
wawili kutokana na hasira alizonazo. Tena aliwapiga kwa makosa
madogo madogo tu yasiyo na msingi.
Binti Mchungaji alipomaliza kazi zake, akaenda kuoga, kisha akanywa
chai, akavaa viwalo vyake vilivyompendeza, akamuaga mama yake kuwa
anaenda kununua nguo.
"leo ndio mwisho wake, anaringa kama hana dhambi!" Binti Mchungaji
aliongea kimoyo moyo wakati akitoka ndani ya geti la nyumba yao na
kuishika barabara iendayo sehemu kilipo kituo kikubwa cha polisi
cha mkoa,
"nikifika pale polisi namueleza askari yeyote, hata wasiponipa hela
sawa, nataka tu nimkomeshe" Binti Mchungaji aliendelea
kujiongelesha Mwenyewe, mara akasikia gari inapiga breki miguuni
kwake, alishtuka na kuruka pembeni mpwa barabara, maana alikuwa na
mawazo kiasi kwamba hakujua kama anatembea katikati ya barabara,
"punguza mawazo dada, mbona we bado mdogo tu" yule dereva wa ile
gari alimwambia binti wa mchungaji.
"samahani kaka yangu" binti wa mchungaji alijitetea.
Kisha yule dereva wa gari akashuka ili kuiangalia gari yake iko
salama, maana breki aliyoipiga ilikuwa Kali sana.
"aha! Kumbe polisi!" Binti Mchungaji alijikuta anahamaki baada ya
kumuona yule dereva wa ile gari amevaa gwanda za polisi.
"ee, kwani vipi?" yule polisi aliuliza huku akimuangalia Binti wa
Mchungaji,
"kuna habari njema nataka kukwambia" Binti Mchungaji alisema huku
furaha yake ikionekana dhahiri machoni pake,
"habari gani hiyo?" yule polisi akamuuliza huku akiwa na shauku ya
kutaka kujua,
Yule binti akageuka nyuma kuangalia kama kuna mtu anakuja,
aliporidhka kuwa hakuna mtu, akasema,
"yule kijana anayenyonya damu za watu anakaa palee" Binti Mchungaji
akasema huku akiionyeshea nyumba ya Mama kayoza ambayo ilikuwa
inaonekana kwa mbali kidogo.
"Una uhakika binti?" Askari aliuliza huku akiwa ahamini
anachoambiwa,
"Twende unipeleke" askari aliongea huku akimfungulia Mlango binti
Mchungaji ambayo aliingia kwenye gari kwa madaha kwa maana
alishaimaliza kazi aliyokusudia kuifanya….
Binti Mchungaji akaingia ndani ya gari na kukaa siti ya mbele,
"Wewe umejuaje kuwa huyo kijana ndiye mnyonya damu?" Askari
aliuliza huku akimuangalia Binti Mchungaji machoni,
"We hutakiwi kuniuliza, unachotakiwa ni kwenda kumkamata" Binti
Mchungaji aliongea,
"Akikataa kuwa sio yeye unafikiri tutafanyaje, inatakiwa uniambie
umejuaje kuwa ndiye yeye ili ninapoenda kumkamata niwe na ushahidi"
Askari aliuliza,
"Ameshawahi kuja kanisani kwetu ili tumuombee ili apone na ahachane
na hayo mambo ya kuua kwa kunyonya damu" Binti Mchungaji alijibu,
"Kumbe hata yeye hapendi we kunyonya damu na kuua?" Askari aliuliza
huku akimtazama,
"Itakuwa hapendi, na ndio maana alikuja kanisani kuombewa" Binti
Mchungaji alijibu,
"Sasa kama hata yeye hapendi kuua kuna haja gani ya kumkamata na
wakati anaonekana ni mtu mwema?" Askari aliuliza,
"Wewe kaka ni hakimu au askari? Maana unauliza tu badala ya kwenda
kumkamata mtuhumiwa, au unaogopa kunyonywa damu?" Binti Mchungaji
aliuliza kwa hasira,
"Samahani, naomba nikuulize swali la mwisho kabla sijaenda
kumkamata" Askari alitoa ombi,
"Sitaki swali, kama hauendi niambie nishuke, mbona askari mpo wengi
tu, nitaenda kuwaambia Askari wengine" Binti Mchungaji aliongea kwa
jeuri huku akiangalia pembeni,
"Naomba uniruhusu tu nikuulize hill swali, baada ya hapo
sitokuuliza tena" Askari aliongea kwa upole,
"Na liwe la mwisho kweli, haya uliza" Binti Mchungaji aliongea kwa
mbwembwe,
"Je huyo mnyonya damu angekua ndugu yako ungetoa taharifa polisi?"
Askari aliuliza huku akiwasha gari,
"Inategemea na undugu wenyewe, kama ni wa mbali namchomea tu" Binti
Mchungaji aliongea huku akifurahi gari kuwashwa kwa maana alipata
uhakika wa kutimiza malengo yake,
"Angekuwa mtoto wa Dada yako au wa kaka yako je?" Askari aliuliza
huku akiliondoa gari,
"Huo ni undugu wa karibu kabisa, siwezi kwenda kumsemea polisi
kamwe" Binti Mchungaji aliongea huku akijitengeneza nywele vizuri,
akiwa bado anajiweka vzuri alishangaa yule askari akisimamisha gari
na kumpiga Kofi zito la usoni,
"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akiwa
amejishika uso, ila yule Askari hakumjibu, akamuongeza jingine la
uso tena pale pale alipopapiga mwanzo,
"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akisikilizia
maumivu,
"Hiyo tabia yako ndio imekuponza" Askari aliongea huku akitabasamu,
"Tabia gani jamani" Binti Mchungaji alilamika huku akiwa amejishika
shavu,
"Umbea, sio kila kitu kinatolewa taharifa" Askari aliongea huku
akimuongezea kofi na kisha akafungua mlango wa gari ili yule
msichana ashuke.
Binti akatelemka haraka haraka na yule Askari akaiondoa gari kwa
spidi ya juu.
Gari la yule askari lilipopotea, yule binti mchungaji nae
akahairisha safari yake,
"akha mwenzangu, huyu mmoja tu nimekutana nae njiani kanipiga vibao
namna hii, je nikienda huko polisi si wataniua kabisa?" yule binti
wa mchungaji aliongea huku akiwa ameshika njia ya kwenda kwao.
Sajenti Minja aliingia kwa Dada yake asubuhi na kuwakuta wakiwa
wamekaa,
"Hivi huyu Mchungaji wenu ana binti mkubwa?" Sajenti Minja aliuliza
baada ya salamu,
"Anae binti mkubwa kabisa, kwani vipi?" Mama Kayoza aliuliza,
"Aisee yule sio mtu mzuri kwetu, so nimekutana nae hapo njiani
akanisimamisha na kuanza kunipa habari za Kayoza" Sajenti Minja
aliongea,
"Eeeh, makubwa, amekwambiaje?" Mama Kayoza aliuliza,.
"Ooh Mara mnyonya damu namjua, alikuja kanisa kwetu na kuombewa,
ooh Mara sijui nini, yaani inaonekana anamjua vzuri Kayoza" Sajenti
Minja aliongea,
"Ikawaje sasa?" Mama Kayoza akauliza,
"Aisee nimemuwasha mabanzi, sijui hata kama atarudia tena kusema"
Sajenti Minja aliongea huku akicheka,
"Usiseme hivyo, anaweza kwenda kituoni yule, maana ameshaonekana
sio mtu mzuri" Mama Kayoza aliongea,
" hata akienda atakuwa hana Maelezo ya kutosha" Sajenti Minja
aliongea kwa dharau,
"Tatizo lako wewe ni mpuuzi" Mama Kayoza aliongea kwa hasira baada
ya kumuona Sajento Minja ana dharau
"Sasa Dada mbona unanitukana tena?" Sajenti Minja aliuliza,.
"Mpuuzi sio tusi, mtu anayepuuza jambo ndio huitwa mpuuzi" Mama
Kayoza alimjibu ndugu yake,
"Sijapuuza hill jambo, mimi bado namfuatilia huyo binti ila sidhani
kama ataenda kutoa taharifa polisi" Sajenti Minja aliongea,
"Haya bwana" Mama Kayoza aliongea kinyonge,
"Jana niliangusha kitambulisho changu, alafu hata sijui
nilipokiangushia" Sajenti Minja aliamua kubadilisha mada,
"Kipo ndani, ulikiangushia hapa" Mama Kayoza alijibu,
"Afadhali, maana nilishapatwa na wasiwasi wa kukipoteza" Sajenti
Minja aliongea.
Baada ya kukichukua kitambulisho chake aliaga na kwenda moja kwa
moja hospitali kwa ajili ya kwenda kumuona Msaidizi wa Mganga.
Alifika mapema na moja kwa moja akaenda kumjulia hali Msaidizi wa
Mganga, baada ya kumjulia hali mgonjwa wake, Sajenti Minja
alifarijika kumuona mgonjwa wake amepata nguvu na anatembea kama
kawaida.
Bila kupoteza muda, sajenti Minja akamtafuta daktari, kisha akapewa
ruhusa ya kuondoka na mgonjwa wake, akamchukua hadi nyumbani kwake.
Kisha akampa taharifa mkuu wa polisi kuwa yule msaidizi wa mganga
ametoka hospitali na anakaa nae nyumbani kwake, mkuu akafurahi
kusikia hivyo.
Kayoza na Omari walijua sababu kubwa ya binti wa mchungaji kutaka
kwenda polisi ni kutokana na kukataliwa na Kayoza kuwa mpenzi wake,
Omari akaamua amchukue yeye, ikawa kila siku ni lazima aende kwa
mchungaji, tena gia aliyokuwa anaenda nayo ni kununua maziwa,
taratibu mazoea yakaanza hadi wakazoeana kabisa, mwisho kabisa
Omari akamtongoza binti wa mchungaji, bila iyana alikubaliwa kwa
roho safi, na sasa Omary na Binti Mchungaji wakawa Wapenzi rasmi.
Siku moja mkuu wa polisi alikuwa anafungua mlango wa ofisini kwake,
ndio akawaona askari watatu wakiwa wameongozana na babu aliyefungwa
pingu. Alikuwa ni yule Babu wa monchwari, akawaita, kisha akaingia
ofisini, wale askari na yule babu nao wakaingia,
"hii kesi ya huyu mzee mbona mnaiendesha pole pole sana". Mkuu wa
polisi aliwauliza wale askari.
"ushaidi ndio unatuchelesha mkuu" Askari mmoja alijibu
"niambieni katika uchunguzi wenu mmefikia wapi" Mkuu wa Polisi
akawatupia swali jingine,
"hakuna mwanga wowote tuliopata" yule askari akamjibu tena mkuu wa polisi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni