KIJIJINI KWA BIBI (26)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mkuu wa polisi akalainika, akatoka nje, kisha akawatafuta askari watatu aliowaamini, akawapa bunduki, kila mmoja risasi thelathini, kisha akawapa yule Babu kama dira ya safari yao,
"Mwanangu unanipa askari watatu!? hivi unamchukuliaje yule kijana?" Babu wa monchwari aliongea huku anasikitika,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Wana bunduki hao, kwa hiyo usiwe na shaka, watafanikisha tu hiyo misheni" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama Babu wa monchwari,
"Ujue awa wanaenda kupambana na dubwana, sio mtu wa kawaida, sasa unapowapeleka watatu tu itakuwa unafeli" Babu wa monchwari aliongea kwa sauti tulivu,
"Lakini si uliniambia ni kijana tu wa kawaida?" Mkuu wa polisi alimuuliza Babu wa monchwari,
"Ni kijana wa kawaida, ila anabadilika na kuwa likitu moja la ajabu sana, linatisha hakuna mfano" Babu wa monchwari alijibu,
"Nitakuongezea askari wawili wengine wawili" Mkuu wa polisi aliongea na kuagiza askari wengine wawili wenye silaha na walipofika, Mkuu wa polisi aliwapa maelekezo.
Baada ya hapo, mkuu wa polisi aliwaruhusu kuondoka, kisha akarudi ofisini kwake, akachukua simu yake ya kiganjani, akabonyeza namba anazojua yeye, inaonekana hakupata majibu anayoyataka, akarudia tena na tena kuipiga ile simu lakini ilionekana inaita muda mrefu mpaka inakatika bila kupokelewa,
"minja nae ana matatizo sana, anajijua yeye ni mtu muhimu, alafu hapokei simu", Mkuu wa polisi alijiongelesha na nafsi yake huku akiiweka simu yake mezani.
Hiyo siku sajenti Minja aliamka mapema, na katika ratiba zake, zilionesha ofisini kwao anaitajika mchana wa saa sita, wazo alilolipata ni kwenda nyumbani kwa Babu wa mochwari, maana tokea wameachana pale kwa sheikh hajajua Babu ana hali gani.
Ilipofika saa nne, Sajenti Minja alijipakia kwenye gari na kwenda nyumbani kwa Babu wa monchwari.
Hakupata tabu sana kufika kwa maana alishawahi kufika hapo Siku za nyuma.
"leo sijisikii hata hamu ya kupika, ila nitaenda kula kwa dada, ningewajulisha ila simu nimeiacha kwenye chaji", Sajenti Minja alijisemea peke yake, wakati gari yake inapaki mbele ya kajumba kamoja kaudongo, akatelemka kutoka katika gari, na kwenda kugonga katika mlango wa kale kajumba, akatoka mtoto mdogo wa kike, mwenye umri kati ya miaka kati ya miaka kumi na mbili na kumi na nne,
"karibu, shikamoo", yule mtoto akamsalimia Sajenti Minja,
"marahabaa, Babu yako nimemkuta?",Sajenti Minja alimuuliza yule mtoto,
"yupi, yule anaefanya kazi hospitali?", kale kabinti nako kalimuhoji Sajenti Minja,
"ndio huyo huyo", Sajenti Minja akajibu kwa kifupi,
"yule ni baba yangu na sio babu yangu kama unavyodhani", kale kabinti kalimtaharifu sajenti Minja,
"alah, we ni mtoto wake wa ngapi?", Sajenti Minja alimuuliza yule binti,
"wa tisa", yule binti akajibu,
"kwani nyie mmezaliwa wangapi?", akakatupia swali jingine, inavyoonekana kalimvutia katika kupangua maswali,
"kumi na nne, ila watatu wamefariki", kale kabinti kalijibu,
"oooh, haya, baba yuko wapi?",Minja akarudi katika topic iliompeleka pale,
"ameenda polisi", yule binti akajibu jibu lilomshtua kidogo Sajenti Minja,
"polisi?!",Sajenti Minja akauliza kwa mshangao,
"ndio, nilimsikia anamwambia mama kuwa, eti anaenda kutoa taharifa za mnyonya damu",yule binti aliendelea kupasua moyo wa Sajenti Minja bila kufahamu,
"ha!, sasa si kuharibiana uko!", Sajenti Minja aliongea bila matarajio yake,
"kwani nini kaka?", yule binti akamuuliza Sajenti Minja huku akiwa na wasiwasi,
"hakuna, shika hii kanunue soda", Sajenti Minja aliongea katika hali ya kuchanganyikiwa huku akimpa yule binti noti ya shilingi elfu mbili (2000).
Sajenti Minja akapanda gari, kisha akaliondoa gari kwa mwendo wa kasi sana,
"ngoja nikawape taharifa kule kwa dada, kisha tujue cha kufanya", Sajenti Minja aliongea kwa sauti ya chini ambayo ilijawa na kitetemeshi kutokana na habari mbaya alizozipokea muda mfupi uliopita.
Alitumia dakika kumi na tano mpaka kufika jirani na mtaa wa wakina kayoza, kulikuwa kuna kona kama tatu, ndio afike katika nyumba ya dada yake.
Kona ya kwanza aliikata vizuri huku akiwa katika mwendo ule ule wa kasi, kwenye kona ya pili ndo kulikuwa na shughuli, gari ya polisi ambayo alikuwemo Babu wa monchwari na askari nayo ilikua katika spidi ya juu, ndio ya mwisho, nao walibakia mita chache waifikie nyumba ya mama kayoza, ile kukata kona tu, ili gari lishike barabara ya nyumba ya wakina kayoza, na Sajenti Minja nae ndio alikuwa anaingia katika hiyo hiyo barabara inayoelekea kwa dada yake, basi kikasikika kishindo kikubwa sana ambacho hakikuwai kutokea pale mtaani, ni gari ya polisi iliivaa gari ya Sajenti Minja kwa ubavuni, ilikuwa ni ajali ya kutisha sana.
Ni damu pekee ndizo zilionekana vizuri katika eneo lile na gari ya Sajenti Minja ilibondeka vibaya sana, haswa upande wa dereva. Hakuna mtu aliyeweza kuiangalia Mara mbili gari ya Sajenti Minja na hakuna mtu aliyekuwa na akili timamu aliyedhani katika ile ajali kuna mtu yupo hai….
..eneo lote liligubikwa na harufu ya damu, watu wakaanza kujisogeza mmoja mmoja, dakika mbili tu zilitosha kujaza watu eneo la tukio.
Wasamalia wema wakatoa taharifa polisi baada ya kugundua kuwa gari moja lilikuwa na polisi.
Kwa jinsi hali ilivyoonekana, ilikuwa vigumu kujua kama watu waliohusika katika ajali ni wazima, ilionesha wote wamekufa. Kwenye gari ndogo ambayo ndani alikuwepo Sajenti Minja peke yake, yeye aliganda pale pale huku damu zikimtoka puani na mdomoni, wakati katika gari ya polisi, dereva, babu wa mochwari na askari mmoja aliekuwepo mbele, wote walitokea kupitia kioo cha mbele na kuangukia juu ya gari la Sajenti Minja, wote watatu walikuwa wamepoteza maisha, na nyuma ya gari, hakukuwa na dalili yoyote iliyoonesha bado kuna mtu ana hati miliki ya pumzi yake, wote walikuwa wamepoteza uhai.
Baada ya dakika kadhaa, gari ya polisi ilifika huku ikiongozana na ambulance ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa polisi alishtuka sana baada ya kugundua kuwa lile gari dogo ni la Sajenti Minja, aliakikisha kila jambo linafanyika haraka.
Madaktari waliofika pale waligundua kuwa yule aliyekuwepo katika gari dogo ni mzima, baada ya kumpima na kugundua kuwa mapigo yake ya moyo yanapiga kwa mbali sana.
Wakamwekea mashine ya kusukuma hewa safi (oxygen) puani kwake, pamoja na dripu, kisha gari ya hospitali ikaondoka kwa kasi sana, huku ikipiga king'ora kumuwahisha hospitali majeruhi.
Kisha gari ya polisi nayo iliubeba mwili wa Babu wa monchwari na wale askari waliopoteza maisha na kuwapeleka monchwari kuwahifadhi.
Masikini Babu wa monchwari, toka kulinda maiti mpaka kulindwa kama maiti.
Ndivyo dunia ilivyo, kifo chake kilifanya aukose utajiri aliokuwa anaenda kuupata Siku chache zijazo. Kifo chake kimeacha majonzi kwa ndugu, marafiki na familia yake. Na zaidi kifo chake kimeacha tabu sana kwa watu waliokuwa wanamtegemea.
Alazwe pema peponi babu wa monchwari.
Mama kayoza na wanae walikuwa wanaongea maongezi yao ya kawaida pale nyumbani, ghafla wakasikia kishindo kikubwa sana,
"mh!, na huku kuna kambi ya jeshi karibu nini?", Kayoza alimuuliza mama yake,
"hakuna, ila iko kishindo inaweza kuwa tairi la gari limepasuka", mama Kayoza alijibu,
"Sio tairi ya gari hilo mama, mlio wa tairi naujua" Omary alimbishia Mama Kayoza na kisha Omari peke yake ndio aliamua kwenda nje kuangalia kilichotea.
Baada ya kusikia kelele za watu, nae alitoka tu mlangoni akamuuliza mtu mmoja aliekuwa anapita pale nje, akamjibu kuwa kuna ajali, baada ya kuridhika na jibu, Omari akarudi ndani.
"vipi, umeshaangalia?",Kayoza akamuuliza Omari,
"yah, ni ajali imetokea pale kwenye kona", Omari akamjibu,
"mtu kagongwa nini?", Kayoza akaendelea kudadisi,
"mimi sijafika, ila kwa kile kishindo, itakuwa gari imeikuta gari pale", Omari alijibu,
"madereva wa siku hizi hovyo kabisa, enzi zetu hizi ajali zilikuwa ni nadra sana", mama Kayoza aliongea kwa manung'uniko,
"mama ile kona mbaya sana", Kayoza aliongea kuwatetea madereva wa siku hizi,
"hata kama", mama Kayoza alishikilia msimamo wake,
"Wewe mama hushangai Sikh hizi magari yapo chungu mzima lakini ajali ni chache sana?" Kayoza aliendelea kuwatetea madereva wa kisasa,
"Zamani magari yalikuwa machache ndio, ila miundombinu ilikuwa mibovu na ajali zilikuwa chache pia" Mama Kayoza aliongea,
"Mimi nafikiri madereva wa Siku hizi ndio chanzo cha ajali nyingi, kwanza hata leseni zenyewe hawasomei, ila wanazipata kiujanja ujanja tu kwa kununua kwa rushwa" Omary aliongea kwa kumuunga mkono Mama Kayoza,
"Bora wewe mwanangu umeongea, hili likayoza bishi sana, kama marehemu Baba yake vile" Mama Kayoza aliongea,
"Basi yaishe, maana mmeamua kunichangia sasa" Kayoza aliamua kumaliza mada,
"Sio yaishe tu, kwanza kubali madereva wa sasa si madereva ila washika usukani tu" Mama Kayoza aliongea kwa utani,
"Sawa, kwa hiyo hata Mjomba Minja ni mshika usukani tu?" Kayoza aliuliza huku akicheka,
"Sasa yule udereva ni Nazi yake?, yule ni polisi bwana" Mama Kayoza alimjibu mwanaye,
"Tunapozungumzia madereva tunajumuisha wote, wanaobeba abiria na wanaoendesha magari yako binafsi" Kayoza aliamua kuipa nguvu point yake,
"Haya sawa umeshinda, maana unachotaka ni kubishana tu na mimi sitaki" Mama Kayoza aliongea,
Na katika kipindi hicho hicho kuna mtu alikuwa akigonga hodi mlangoni, kwa hiyo hodi iliyokuwa inapigwa ndio iliwakatisha maongezi yao,
"pita, mlango uko wazi", Mama Kayoza aliongea kwa sauti ili mgonga hodi amsikie,
"hodi tena, jamani salama hapa?", Kijana mmoja ambae anakaa nyumba ya pili kutoka pale, aliwasalimia huku akionekana mwenye wasiwasi,
"kumbe ni wewe Tino, sisi wazima, we hujambo?", mama Kayoza akamuuliza yule kijana,
"jambo ninalo mama yangu", yule kijana alijibu,
"haya tuambie hilo jambo sasa", mama Kayoza aliongea kwa sauti ya ucheshi,
"yule bro polisi, white white hivi, anaekujaga hapa amepata ajali pale kona", Yule kijana alitoa taharifa iliyowapa mshtuko wote waliopo pale,
"ah!, kagonga mtu", Omari aliuliza huku akisahau kuwa yeye ndiye aliyesema kile kishindo sio cha kugongwa mtu, ila ni magari yamegongana,
"gari yake imegongana uso kwa uso na gari ya polisi", Yule kijana aliendelea kuelezea alichokiona,
"ile gari ya polisi wote wamekufa, ila yule bro kabebwa hajielewi, sijui hata kama atafika hospitali", Yule kijana alipigilia msumari wa mwisho katika maumivu ya mama kayoza na wanae, kisha akawaaga, ila hakujibiwa kutokana na hali iliyokuwepo.
"Mama sasa tunafanyaje?" Kayoza aliuliza kwa sauti tulivu,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni