Vita vya Mapenzi (16)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA KUMI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mkabala na Hospital kubwa ya Dr Nyango Bango kubwa lililosomeka ‘KWA MZEE ANDOGA’, Lilikua likiunadi mgahawa mkubwa wa kupatia chakula pamoja na vinywaji, watu wengi hujumuika maeneo yale kupata chakula safi.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Kwa nyuma ya mgahawa huo palikua na Bustani kubwa iliyotengenezwa vizuri sana kwa ajili ya wateja kupata vinywaji huku wakiburudishwa na upepo mwanana utokanao na miti kadhaa iliyapandwa kuizunguka bustani hiyo huku harufu ya maua ikizipendezesha pua zao. Suhail na Sharifa walikua wameketi katika kona kabisa ya bustani ile baada ya kutoka kupata sindano, Sharifa hakua na furaha kabisa na hata Suhail nae alijilazimisha tu kua katika hali ya furaha lakini haikutoka moyoni
“Sharifa nadhani jana ulifikia kuchukua maamuzi yale bila kutaka kunielewa lakini kama ungenisikiliza kwa kina wala tusingefikia kule kote”
“Hauwezi kutaka kunifanyia unyama ule wewe Suhail, angalia sasa Wazee wameshaanza kujadili suala hili la Ndoa, na jana tu walikua wakijadiliana halafu wewe ulete mambo ya aibu kweli?”
“Sawa, sasa wewe pamoja na hayo tuliyojadiliana unashauri tufanyaje?”
“Hakuna cha kushauri chochote hapa, Ndoa kama kawaida halafu hayo mengine sijui ya ubovu yatajuliakana baadae, ila Ndoa ni lazima”
“Na vipi kama nitaendelea kua mbovu ndani ya ndoa hata kama tutahangaika huku na kule, utaweza kuvumilia kweli?”
“Ndio nitaweza, halafu kwanini ufikirie kutokupona tu? Nakwambia we utakua na Ajenda ya siri, sio bure” Mjadala ulichukua muda mrefu huku Suhail akionesha kukubali kishingo upande tu lakini ndani ya moyo wake alijua dhahir kua hayo ndio makubaliano yake na Shekhia. Baada ya kuhitimisha mjadala, Suhail akamchukulia Teksi Sharifa impeleke kwao japo haikua mbali sana tokea hapo walipokua
*****
“Nimetokea kwa Bwana Kusekwa, amesema amekwishaongea na binti yake na ameridhia kuliwahisha jambo hili, hivyo tumeazimia kua Ndoa hii Ifanyike wiki mbili zijazo,” Mzee Kusekwa alikua akiongea na mkewe Sebuleni kwao
“Mimi sina tatizo ila kwa muda huo mlioafikiana naona kama hautatosha kufanya maandalizi yote.. yaani kuwaalika watu, kuandaa maakuli, Mahari, nk yote hayo yanahitaji pesa na muda..”
“Hatuhitaji harusi kubwa sana bali ni ndogo tu ya kupendeza, gharama za kawaida hazitamshinda Suhail kulipa” Wakiwa katika mazungumzo ndipo na Suhail nae akarejea
“Enhee bora umefika wakati muafaka, kuna jambo hapa linakuhusu,” Mzee Kusekwa alimdaka mwanae bila hata kusalimiana, akamsogezea kiti kisha akaanza kumpa maelezo aliyokua akimwambia mkewe, Suhail alikua kimya akimsikiliza baba yake na kwakua tayari alikwisha yamaliza na Shekhia sasa hakua na hofu sana zaidi ya kuafiki tu, na hata aina ya harusi kwamba itakua ni ndogo tu ilimfurahisha pia, hakutaka harusi ya Gumzo, Baada ya Baba yake kumaliza kuongea nae akaweka lake
“Lakini Baba..”
“Lakini nini wewe, mbona unataka kunikwaza tena” Mzee Kusekwa alimkatisha mwanae akihisi kua anataka kuweka kipingamizi, lakini akazuliwa na mkewe
“Mwache basi nae atoe maoni yake, usimpelekepeke tu. Hebu sema Suhail”
“Kwa kua mmeazimia zoezi hili lifanyike baada ya wiki mbili mimi nimeafiki ila siwezi kukaa huku siku zote hizo huku, kumbukeni nimewaambia kua mimi kwa sasa nimeajiriwa, ninasimamia Biashara za watu” Suala lile likawa zito sana japo Mzee Kusekwa hakuafiki kabisa akiamini kua Suhail akiondoka tu pengine angeibuka na kisingizio kikubwa cha kutokuja tena siku hiyo ya Harusi, ikawa ni malumbano mule ndani lakini kwa uzito wa hoja aliyoitoa Suhail ikawa hakuna budi kuikubali tu.
*****
Siku mbili baadae Suhail aliondoka na kurejea Dar kuangalia miradi yake na kuwaacha watu wa nyumbani kwao wakianza pilikapilika za maandalizi ya harusi ikiwa ni pamoja na kuwaalika majirani zao, pia Suhail aliacha amekwishalipa mahari na akawaachia wazazi wake pesa za matumizi muhimu. Kwa upande wa Mzee Fungameza hapakua na maandalizi makubwa, Ukizingatia tofauti ya kiimani baina yake na binti yake hivyo hakua na uwelewa mkubwa wa harusi za dini nyingine zinavyokua hivyo mambo mengi alimruhusu Mzee Kusekwa ayasimamie.
Siku ziliyoyoma kuelea katika Ndoa ambayo kwa Suhail aliamini ni ndogo sana lakini huko Tabora ilipokelewa kwa Shangwe ya hali ya juu, marafiki zake wengi kwa jinsi wanavyompenda waliisubiri kwa hamu huku jamaa na majirani wa pande zote mbili kwa Mzee Kusekwa na Fungameza nao wakiipokea kwa aina yake kutokana na ukweli kwamba wazee hawa ni wacheshi na wanakubalika sana kila mmoja kwa namna yake na kwakua wao pia hujitolea sana kushiriki katika Shughuli za wenzao hivyo fadhila ilikua ikilipwa sasa.
Harusi ilipangwa kufanyika siku ya Ijumaa saa tatu asubuhi, Sharifa aliendelea kutawa huku akiisubiri siku hiyo kwa hamu. Na Suhail nae aliendelea na shughuli zake huko jijini Dar es Salaam huku akiahidi kua angewasili Tabora kwa usafiri wa Ndege siku moja kabla ya harusi, yaani siku ya Alkhamisi
*****
Siku ya alkhamisi ikiwa imesalia siku moja kufika siku ya harusi Suhail alikua ameshajiandaa kwa safari ya kuelekea Tabora, ilikua ni saa tisa alasiri akiwa na mabegi yake mikononi alikua akiagana na mkewe wa mwanzo Bi Shekhia Bint Sufian. Hapakua na mazungumzo mengi kwani masuala walikwisha zungumza na wakakubaliana kwamba Shekhia atabaki pale Mbezi na Sharifa ataenda kukaa Ilala. Lakini gubu la Shekhia lilafanya mjadala uanze kumea upya
“Usije ukafikiri mimi ni mpumbavu kukubali ufunge ndoa na huyo Sharifa, nimeamua tu kukunusuru na matatizo ya kwenu huko Sasa wewe ujitie tu hamnazo hakyamungu utajuta kunifahamu,” Shekhia alikua akiongea na Suhail kwa mkwara mzito
“Usijali mke wangu, nakupenda sana kuliko hata unavyojipenda wewe mwenyewe, huyu namuoa tu kwa kuwaridhisha wazazi” Suhail alijibu kwa utulivu na ulaghai mkubwa huku akiwa tayari amekwishapendeza kwa ajili ya safari, na mabegi yake yakiwa miguuni pake
“Ila nakusisitiza tena kua ‘Tendo’ ni marufuku, usithubutu..”
‘Itawezekania wapi,’ Suhail alijibu kimoyomoyo huku akijua kua anaiingia hatari kubwa sana, Sasa wakiwa katikati ya Mazungumzo ndipo ghafla Pete ya Suhail ikawasha mwanga mwekundu huku ikimtetemesha kidoleni kwa nguvu mfano wa simu iliyowekewa huduma ya ‘Vibration’, hali ile iliwashitua sana, mara Pete ile ikaanza kupiga mbinja kwa sauti kali, Wakaangaliana huku kila mmoja akitetemeka hasa kuona hali ile ya hatari, ilikua ni taarifa ya wito kutoka kwa Mzee Sufiani Shamhurish akihitajia msaada wa ‘Khatam Budha’, bila Shaka amevamiwa na amezidiwa nguvu na Maadui zake kutoka katika himaya ya Budha.
Shekhia akaanza kulia kwa sauti huku akitetemeka kwa woga, Suhail nae akawa hajui afanyeje. Haraka akayatupa chini mabegi yake aliyokua ameyaweka tayari kwa ajili ya kutoka kuelekea ‘Airpot’ Kisha akaitumbulia macho pete ile mpaka nae macho yake yakaanza kubadilika yakawa kama ya Paka aliejeruhiwa, akaona mambo yote yanayojiri kwa Mzee Shamhurish, ilikua ni hali ya hatari Baba mkwe wake alikua anashambuliwa vibaya katika Jengo moja kubwa sana lilotawaliwa na ukimya katika mji mmoja huko Yemeni.
Aliwashuhudia Wanaume watatu wenye asili ya ki-asia wakiwa wamemuangusha chini Mzee Sufiani huku wawili wakihitaji kumuua lakini mmoja wao alikua akikataa wasifanye hivyo mpaka Mzee Sufiani atakapowaeleza mahali ilipo Pete yao(Khatam Budha), Wakaanza kumpa kibano cha hatari jinni mwenzao. Suhail alioogopa sana ukizingatia tangu akabidhiwe Pete ile hakawahi kupambana na jinni yoyote Yule hivyo ile ilikua ni mpambano wake wa kwanza, Hofu ilimvaa kiasi cha kuanza kusahau namna ya matumizi katika mashambulizi. Akajipa moyo kisha haraka akaiamuru Pete ile ikamchukua kwa kasi na kumpeleka Eneo la tukio huku akimuacha Shekhia akitokwa tu na machozi
*****
Wakati Suhail akiwa njiani kuelekea Yemeni kumnusuru Baba Mkwe wake hali ilikua ya kipekee huko Tabora ambapo ilikua imesalia siku moja tu tu kufika siku ya Ndoa. Shamrashamra na maandalizi ya Ndoa vilizidi kupamba moto, Ilikua ni Ndoa ndogo tu lakini ya kipekee, Ndoa ambayo kwa Suhail aliamini ni ndogo sana lakini huko Tabora ilipokelewa kwa Shangwe ya hali ya juu, marafiki zake wengi kwa jinsi wanavyompenda waliisubiri kwa hamu huku jamaa na majirani wa pande zote mbili kwa Mzee Kusekwa na Fungameza nao wakiipokea kwa aina yake kutokana na ukweli kwamba wazee hawa ni wacheshi na wanakubalika sana kila mmoja kwa namna yake na kwakua wao pia hujitolea sana kushiriki katika Shughuli za wenzao hivyo fadhila ilikua ikilipwa sasa.
Lakini hofu ilianza kutanda baada ya kuona muda ukizidi kuyoyoma na hakuna taarifa zozote za Suhail kuwasili mkoani, Wazazi na majirani walianza kuulizana juu ya ukimya wa Bwana Harusi mtarajiwa, mbaya zaidi Simu yake kila ilipopigwa iliita bila kupokelewa.
Muda ukazidi kupotea, Giza likapiga hodi kuashiria siku inakwish hatimae matumaini ya kumuona Suhail yakafifia, Hofu ikazizima.
*****
Maandishi makubwa yaliyofifia na kupoteza ile rangi yake ya asili yaliyosomeka
‘AL- JAMHURIYYAH AL-YAMANIYYAH.
MAT’ HAF’ yalilinadi jengo moja kubwa na chakavu lililokua likionesha kila dalili ya kuhamwa na kutelekezwa kwa kipindi kirefu. Kama ambavyo maandishi hayo yanavyojieleza kua hilo ni Jumba la Makumbusho lililo chini ya Jamhuri ya Yemen. Jumba hilo lililopo katika kisiwa cha Socotra Nchini Yemen lilihamwa miaka mingi iliyopita na Shughuli zake kuhamishiwa katika Jengo jingine lililopo katika mji mku wa SANA’A Nchini humo.
Kutokana na hali ya Upweke ya Jumba hilo la zamani la makumbusho ikiwa ni pamoja na kukosa ulinzi wala usimamizi hivyo uovu mwingi umekua ni sehemu ya maisha ya ndani ya Jumba hilo pweke ambalo si vibaya kama utaliita ‘Pagara’ kwa jinsi lilivyoharibika na kuachilizwa huku miti mingi ikiota kwa nje ikilizunguuka jumba hilo.
Mzee Sufian Shamhurish nae hatimae akawa ni miongoni mwa wahanga waliowahi kufanyiwa unyama na Udhalimu mkubwa ndani ya Jumba hilo, Alikua akiteswa vikali humo ndani alipoingizwa msobemsobe baada ya kukamatwa ghafla kwa kushtikizwa alipokua akitembeatembea maeneo aliyokua akiishi, waliomkamata ni Makomandoo watatu wa Kijini kutoka katika Himaya ya Budha ambapo waliagizwa kufanya msako mkali na kuhakikisha wanamtia nguvuni Mzee Sufiani kisha Wamnyang’anye Pete yao(Khatam Budha) kabla ya Kumfikisha Budha akiwa hai au akiwa Maiti.
Mzee Sufian hakua na ujanja tena kwani Nguvu zake pekee za kijini hazikua na uwezo wa kufua dafu kwa Makomandoo wale watatu wa Kijini waliokua wakimporomoshea Kipigo na mateso ya nguvu ili aseme ilipo Pete(Khatam Budha) hivyo tegemeo lake Pekee ni Silaha takatifu iliyopo kidoleni kwa Mkwewe, Suhail Kusekwa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni