MY EVA (21)
Zephiline F Ezekiel
2 min read
JINA: MY EVA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Ghafla maaskari police walikuja pale kambin...wakamkamata victor na kwenda nae...SASA ENDELEA..
Rachel akiwa chumban anamuuguza mwanae...alikuja mtu na kuwapa habar za kukamatwa kwa victor.Ameyataka mwenyewe victor... Yaan dunia hii unaweza ukaish na mashetan ndan ukazan ni watu...alisema rachel... Maskin eva wa watu nlikua namfanyia unyama bure tu...yaan najuta kwakwel...alisema rachel.
Sasa si unaona mama..eva wa watu mmempakazia mabaya hadi watu wanamuuona muuaji...alisema Danny.
Nisamehe mwanangu...naona hata aib kumwangalia eva...baba yako alinidanganya kwao eva ni wachawi wakubwa na ndo waliwaua wazaz wa eva..na mm bila kufkir nikaziunga mkono njama zake...najiona mjinga sasa...alisema rachel
Habar zilimfikia kazmoto...alishtuka sana.
Zam yangu inakaribia sasa...alisema kazmoto.
Kwahyo unachukua hatua gani?...aliulza maria.
Sitafanya lolote,sitaenda popote...nitasubiri tu ..nastahil hukum kwa niliyoyafanya.
Kwa mbali maria alimuonea huruma mtu aliekua akimchukia sana
Maria,najua itakua ngum kwako kuyasahau nliyokutendea lakin naomba kama ikiwezekana unisamehe.
Lakin ulikua na sababu gani ya kumuua kaka yangu?...
Ni hiv maria...
Ile kazmoto anataka kueleza waliingia maaskaria na yeye akakamatwa pia...
Wakiwa sero, victor na kazmoto walikua wanajadili..
Sasa kwahyo tunafanyaje kazmoto?.
Mimi sifanyi kitu.. lolote litakalonikuta sawa tu..
Hiv wewe kazmoto una akili kweli....yaan ufungwe hivihivi??....utafungwa mwenyewe mimi simo..
Danny utanisamehe kukuacha hapa mgonjwa....naenda police nimeitwa...si unajua tukio lilitokea kwangu...alisema eva
Haya eva alisema Danny wakaagana na eva akaondoka....
Eva alienda kituo cha police kama alivyoitwa na kesi ilishughulikiwa....kwa kua victor alikua na pesa alihonga kesi ikaishia juujuu...
Skendo nyingne iliibuliwa na wanaomchukia eva wakishirikiana na victor na wapambe wa victor kwamba eti eva alimsingizia victor ili apate kulipwa maana ameshaishiwa siku hizi.....
Eva aliumia sana.. Lakini hakukata tamaa...alikusudia kufungua kesi mahakamani...
Usiogope eva... We fungua kesi ipo siku yataisha...alisema miriam
Danny alipoina skendo ile aliumia sana...aliamua kufuata eva kumfarij..
Eva...usiwaze...kila gum lina mwisho...mungu atakusaidia eva...
Asante danny.....nashukuru sana danny wangu.
Alifungua kessi chini ya usimamizi wa jaj massawe baba yake miriam ambae alimtaftia mwanasheria mzoefu
Victor alikua nyumban kwake anaangalia tv....mara alikuja mtu akamletea barua ya wito mahakaman...
Victor alicheka sana..
Huyu eva anajisumbua bure tu....hawezi kushinda kessi maana kwanza sio mzoefu...sijui nani huyo anaemdanganya kua atanishinda...hahaaa.
Alicheka sana..
Mda wote danny na mama yake walikua wanavunga kama hawamsikii....
Usiku victor alienda kwa hakim ili ampe hongo...lakin aligonga mwamba maana hakim alikua ashaambiwa kilakitu na jaji massawe...
Utanisamehe tu victor... Siwez kuifanya kaz yako..alisema hakimu
Victor alikasirika sana.... Tumaini lake lilibaki kwa mwanasheria wake...
********
Siku ya kesi ilifika....wote walienda mahakamani...
Victor alisomewa mashtaka yake na aliyakana yote..hakukubali hata moja...
Eva alileta ushahidi wake ule wa barua iliyokua na stamp na tarehe ya siku baada ya mauaji ...mwanasheria wake alipinga vikali akidai ni ushahid wa kutunga...
Waliambiwa warud siku nyingne ya kurud ili kuendelea na kes..
Eva alitoka amenyong'onyea....akakutana na miriam nje aliekua anamsubiria..
Kesi imeendaje...aliuliza miriam.
Eva alieleza kila kitu kwa miriam....
Mmh pole eva ila tutashinda tu.....
Mimi nawaza tutatoa wapi ushahid mwingne...alisema eva.
Mmh sijui tutaoa wapi...akidakia miriam
Mmh nikishindwa hii kesi nitakua nimeisha...watu watanisakama kama kipind amekufa jamira
Mara ghafla sim ya eva iliita..alikua ni kazmoto
Usijali eva mimi ninaushahid wote...usijali siku hiyo ntakua shahidi wako....alisema kazmoto..
Mmh kweli?....ni ushahid gani? Aliulza eva
Utajua yote siku hiyo ila wewe jua umeshashinda kesi...
Sawa ntashukuru sana...eva alifurahi...wote walifurahi...
Kazmoto aliamua kujitolea kumuokoa eva hata kama atagungwa maana alishajutia kwa aliyoyafanya nyuma.....
Alienda akamwambia maria ambae alimhuzunikia sana lakin hakukua na jins.hiyo ndo ilikua njia pekee ya kumuokoa evanmaaba eva akishindwa kesai mambo yatakua magum kwake
Siku ya kesi iliwadia tena...wote walihuzuria...eva alikua na wasiwasi maana kazmoto alichelewa...lakin victor alikua akichekelea maana alijua hakuna ushahid eva anao tena...
mara ghafla kazmoto aliingia na kukaa kama shahidi wa eva.victor alishtuka kumuona kazmoto...
Kazmoto!!!... Alillopoka victor kwa nguvu bila kujali yupo mahakamani
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni