RANIA (32)
Zephiline F Ezekiel
3 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Baba mwanao yamenikuta makubwa...nimenusurika kifo baba..Tharia ni watu wabaya sana..alisema Mars.Wamekutenda nini?..aliuliza Mfalme kwa hamaki....
SASA ENDELEA..
Baba...nchi ya Tharia ina mambo mengi sana ya ajabu...baada ya Mfalme na mwanae Fasha kujua kua mimi nimeyafahamu wakataka kuniua...alisema Mars.Mfalme alishituka sana.
Yapi hayo mambo?.. Aliuliza mfalme.
Ni mambo tu ya ukatili na mauaji wanayoyafanya kwa watu wasio na hatia.. Wameshawaua wengi hata watoto wa viongozi wa nchi na ndio maana wanahofia yasijulikane usije ukatokea uasi... alisema Mars.
Yaani yeyote atakaejua tofauti na mfalme na mwanae basi anauawa..hata malikia suya na Mganga kwa saaa hawapo ikulu walitoroka kwa kuogopa kufa kwakua walikua wameshajua siri...Alisema Mars.
Mfalme alishangaa sana kusikia vile na alipatwa na hasira sana.hakuwaza hata kidogo kua mwanae ni mwongo.
Baba...mimi siwezi kurudi huko tena...kwanza sasahivi Mfalme anampango wa kuishambulia nchi yetu na anapanga kunitumia mimi kama mateka ili wewe ukose nguvu.. Alisema Mars
Mfalme alikasirika kusikia hivyo... Alikasirika haswa...
Mars alipoona hivyo alifurahi maana ndio maana alikua mpango wake.
Huku suya na Mganga walikua wakiendelea na mipango.
Malikia hata sasa watu wanne katika wale tuliowatuma wamfuatilie Fasha na wenzie hawajarudi.. Fasha atakua amewaateka....alisema Mganga.
Ni kweli... Nina wasiwasi mkubwa kua watatoboa siri zetu nyingi... Alisema malikia.
Ni kweli kabisa... Sasa tunafanya nini?..aliuliza Mganga.
Kwanza tuma watu wamfuatiie Mars kama anakwenda kweli tuliko mtuma...Vilevile kama kuna wapelezi wa Fasha wanamfuata tuwadhibiti...alisema Suya.
Kingine ni kuwatafuta hao aliowateka Fasha walipo na kuwaua ili wasiendelee kutoa siri zaidi...alisema malkia
Suya na Mganga waliagiza watu kumfuatilia Mars kama ameenda kweli na Vilevile walikua wakifuatili kama kuna watu wanamfuata.
Baada ya hapo suya aliandika barua ndeefu sana kusikia ili aipeleke Lazi..hio yote iikua katika kukamilisha mpango wake.
Baada ya kuindika alwapatia vijana wawili anaowaamini sana ii waipeleke Lazi.
Huku Dom alikua akishangaa sana siku hiyo maana alikua hamwoni Rania.. Alijiuliza maswali mengi hakupata jibu.
Aliamua kwenda kumwona Fasha..alipofika alimuuliza kama anajua Rania alipo.
Kaka...sijui nianzie wapi kusema... Lakini kiufupi Rania ameenda Lazi.. Alisema Fasha.
Lazi?.. Kufanya nini?..aliuliza Dom.
Fasha alimweleza kuhusu taarifa aliyoileta Namadi kuhusu Kuondoka kwa Mars.
Rania amesema hatokuaga maana anajua huwezi kukubali aende.. Alisema Fasha.
Ni hatari sana Rania kwenda...kumbuka una mateka wa Suya.. Na ni lazima ametuma watu kumlinda Mars afike salama kwa kuhofia wewe utamfuatilia.. Alisema Dom.
Ni kweli... Tumefanya maamuzi ya kukurupuka sana..alisema Fasha.
Mimi nitaenda huko...alisema Dom.
Hata wewe kwenda haitoshi...ngoja tuongee na mfalme atupatie vikosi vyake vya siri maana jeshi ka nchi haliwezi hii kazi kwa kua liko chini ya msaliti.. Alisema Fasha.
Sawa... Basi na iwe haraka.. Alisema Dom.
Fasha haraka alikwenda kwa Mfalme na kumweleza hali halisi juu ya kupotea kwa Mars na kua alitoroka usiku na kwenda kwa suya
Mfalme alishituka na kushangaa sana.
Sasa huko Mars ameenda kufanya nini?. Aliuliza Mfalme kwa mshangao.
Sijajua ila bila shaka huu utakua mpango wa Suya kupata msaada kutoka kwa Mfalme wa Lazi.. Alisema Fasha.
Fasha.. Wewe unahisi suya na Mganga wanampango wa kupindua utawala huu?..aliuliza Mfalme.
Kwa asilimia zote nina hakika na hilo.... Inavyosemekana anamajeshi ya siri hata ikitokea kama hatapata msaada wa bakanga mkuu wa majeshi.
Sasa tunafanya nini?..aliuliza Mfalme..
Nataka vikosi vya siri...vielekee Lazi Alisema Fasha.
Huwezi kwenda Lazi kwa siri maana wewe ni mwanamfalme la sivyo utatafsiriwa kama mvamizi...alisema mfalme.
Sitakwenda mimi...ataenda mwingine... Atakwenda Dom Alisema Fasha.
Fasha hakutaka kutaja habari za Rania kwenda huko kwa huo muda maana alihofia mfalme atamchukuliaje hasa baada ya kujua uhalisia wake.aliona bora asubiri atamwambia baadae.
Mfalme alitoa ruhusa na vikosi vililetwa na omandi na Fasha alikabidhiwa ambae pia alimkabidhi Dom.
Bila kuchelewa Dom na watu wake walianza kuelekea Lazi wakijifanya kama kundi la wafanya biashara ili wasitambulike.
Fasha alibakia pale kupambana na yatakayotokea huku Tharia.
Namadi alipomwona Mars akiondoka alileta taarifa ndiyo lakini hakuzileta siku hiyohiyo..kwahiyo Mars aliwatangulia kufika muda wa siku kama moja na nusu hivi.
Wakiwa njiani kuelekea Lazi wale wapambe wa Suya Na Mganga nao walikua wanakuja...
Walipofika sehemu moja Rania alimwambia Namadi wabadili uelekeo wapite njia nyingine licha ya kua njia hiyo ilikua ndefu kuzidi ya mwanzo.
Kwanini?.. Aliuliza Rania.
Bila shaka suya atakua ametuma watu kumfuatilia Mars kwa nyuma...sina hakika ila nahisi..alisema Rania.
Njia pekee wanayoijua wao ni hii aliyopita Mars.. Huku vichochoroni bila shaka hawajui kama ni njia ya ziada.. Alisema Rania.
Walikubaliana waondoke njia ile na wapite njia nyingine.
Walipokatiza walipumzika kidogo wale na chakula na waendelee na safari.
Wakiwa wamepumzika mara wapambe wawili Suya walipita kwa kasi na kuwaacha Rania na na Namadi nyuma.
Rania na Namadi walijificha huku wakiangalia kama kua wengine wamekuja.
Mbona ni wawili tu?..aliuliza Rania.
Ona..wengine hawa huko ila wanakuja kama kwa tahadhari..alisema Namadi baada ya kuwaona baadhi ya wapambe wa Suya wengine wengi.
Sasa hawa wawili watakua wameenda kufanya nini..aliuliza Rania.
Haraka tuondoke twende Lazi.. Haya mambo sio ya kawaida.
Waliondoka kwa kasi ya ajabu ingawa walikua wamepita njia ndefu.
Wale wapambe wawili walikua wameagizwa kupeleka barua kwa Mfalme wa Lazi na barua hiyo ilitoka kwa suya.
Walifika mapema kidogo kuzidi Rania na Namadi.
Mars aliwapokea wageni wale maana alijua watakuja...walimkabidhi barua ile ili aje ampe Mfalme baadae..baada ya hapo watu wale waliondoka.
Baada ya Mfalme kukutana ba Mars, Mars alimpatia barua ile na kusema kua umetoka kwa malikia suya.
Mfalme alifungua barua ile ba kuisoma yoote....alionekana kukubaliana na yaliyoandikwa pale ingawa sina hakika sana😊.
Wale wapambe walipotoka tu tayari Rania na Namadi walikua wameshafika....NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni