MAMA MWENYE NYUMBA (37)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
Akapiga simu kwa Suzan kumjulisha kuwa anakaribi a pale ofisini, “hoo jamani Edgar nimetoka, njoo hapa tulipo kula sikuile, kwenye ile bar”SASA ENDELEA...
Suzan akiwa na Monica mfanyakazi mpya wale kazini kwao, alikuwa amefika pale Full dose dakika chache zilizo pita, akipishana na gari la mama Sophia, japo akuwa nalo makini sana kutokana na yeye kuwa kwenye gari lake na walipishana mbali mbali wakizuiwa na magari mengine yaliyo kuwa kwenye foleni, leo aliondoka na gari tofauti na siku zote akiwa na lengo la kuondoke pale kwenda nyumbani ukizingatia ni nusu siku kwa wafanya kazi wa benk hivyo mala kumaliza kula mda utakuwa umekwisha, sasa wakati anatoka Monica akaomba lifti, nayeye alikuwa na safari ya kwenda kwenye lunch, kiukweli tokea Monica aingie nakuanza kazi pale benk kwenye kitengo cha keshia
Watu wengi sana walimtolea macho kutokana na uzuri wake uliopambwa kwa uzuei wa sura pia rangi yake ya chocret,kwenye umbo ndio balaha, alikuwa mrefu alafu ame jazia hips wa na makalio wastan, kuanzia wateja adi wafanya kazi wenzake, walimsumbua kila siku wakitaka kuonja kitumbua cha mrembo Monica, lakini kutokana na umakini aliokuwa nao, monica aliishia kuwa piga chini, maana alijuwa kuwa akiwaendea kwa kupa ataishia pabaya, licha ya ahadi na offer mbali mbali lakini alifumba macho nakuwa piga chini, “nani huyo shemeji,?”aliuliza Monica wakati wana msubiri mhudumu kuja kuwasikiliza, “hapana ni mdogo wangu mtoto wa mama mdogo” alijibu Suzan ambae mpaka leo alikuwa anaficha mausiano yake na Edgar, kuepusha balaha litakalo weza kutokea endapo mzee Mashaka na Edgar wange gunduana, japo mzee mashaka kwa zaidi ya miezi mitatu akuwai tena kuingiza dudu kwenye kitumbua cha Suzan, aliishia kupigwa kalenda kwa sababu mbali mbali
“Ok! kumbe unakaa na ndugu yako?”aliuliza Moica huku mhudumu alikuwa amesha wafikia, wakamwagiza chakula na vinywaji huu Suzan akitoa oda ya chakula cha Edgar pia, wakiwa wana subiri chakula huku wakiendelea kuongea mawili matatu, ambapo sasa walikuwa wanaongelea maswala yakazi, mala Monica akatuka, “mungu wangu, nina balaha gani mimi na huyu mtu?” kauli hiyo ili mstua sana Suzan akauliza, “vipi kuna mtu una ugovi nae?” kiukweli Suzan ni mwoga sana wa ugomvi, “hapana ni huyu kijana anaekuja, namwonaga mala nyingi sana pale benk” aliongea Monica akionyesha upande ambao watu wanaingilia pale full dose, Suzan akatazama lakini aliona watu wengi tu, wakiingia na kutoka macho yake yakakutana na macho ya mpenzi wake Edgar amba elikuwa anaangalia huku nahuku kumtafuta, akujuwa Monica anamaananisha niyupi kati ya wale
“Yupi mbona wapo wengi?” aliuliza Suzan kwa kunong’ona huku macho yake bado yapo kule mlango wakuingilia, Monica akiwa bado ame tazama pembeni akimaanisha ataki kutazama kule mlangoni, akasema “mwangalie yule alie vaa tisheri nyekundu na jinsi, huyo mrefu” hapo Suzan akagunduwa kuwa mlengwa ni Edgar, moyo wake ukastuka, akiwaza lazima Edgar amemtongoza huyu mdada, maana alijuwa jinsi yule binti alivyo mrembo, na alifahamu jinsi wanaume walivyo shindaniana kumpata yule dada, lakini akajizuwia kuhamaki akauliza, “kwani ame kufanya nini” hapo Monica aligeuza uso na kutazama upande alipo mwona Edgar akamwona kwa mbali akija upande wao, akageuza tena sura yake, “yani sijuwi kwanini, nimetokea kumpenda sana huyu kijana, ila sijawai kuwa nae karibu, yani sijuwi nifanyaje kuna wakati najisikia ata nimfwate nika mwambie, yani bola atanisinge mwona huyu kaka”
Kusikia hivyo Suzan alihisi mkojo una taka kumtoka. kwa mstuko, akamtazama yule dada usoni ndo “Edgar huyu” Suzan akajikuta amelopoka kwa kifupi, “kumbe ata wewe una mfahamu huyu kaka?” aliuliza yule dada Monica huku akimtazama Edgar ambae bado alikuwa mbali akijaupande walipo waohuku macho amewakazia wao, kisha akamtazama Suzan, “ndiyo si nime toka kuongea nae kwenye simu sasa hivi,” aliongea suzan wakati huo, muhudumu awa vinywaji alikuwa anaweka vinywaji mezani, “weee, usini ambie, kumbe huyu ni mdogo wako, yani una kaka mzuri sana” aliongea kwa kunong’ona Monica maana Edgar alisha karibia, hapo wote wakapoteze maongezi yale, “karibu Eddy, vipi mbona kama hauko sawa kuna usalama kweli?” aliongea Suzan akimkaribisha Edgar ambae alivuta kiti na kukaa upande mmoja na Suzan nawote wawili wakitazamana na Monica, uso kwa uso, “hooo nipo freshi tu sema sijuwoi kwanini, namejikuta nanyongea ghafla” aliongea Edgar akiinua macho yake kuwatazama wahudumu wawili wa chakula ambao walipeba tray mbili kubwa za vyakula vya watu watatu, wale wahudumu wakaweka mezani na kuwa karibisha, kisha hao wakaondoka zao
“Naitwa Monica, nazani unifahamu ni rafiki wa dada yako” walistuliwa na sauti ya Monica iliyo mfanya Edgar akumbuke kuwa toka alipo mwona Suzan alimwona akiwa na mwenzie, kwaupande wa Suzan alijikuta akitoa kicheko kidogo cha mguno, “samahani mwaya kwa kusahau kuku tambulisha, Edgar huyu ni rafiki yangu anaitwa Monica ni mgeni pale kazini kwetu,” alitambulisha Suzan akishindwa atambulisheje kwa upande wa Edgar, maana aliona kuendelea kuficha italeta masala baadae, “ok! nashukuru kumfahamu” aliongea Edgar na wote wakaanza kula kila mmoja na chakula chake, ilikuwa ni kimya kimya ikionyesha wazi Edgar kuna jambo lina mkwaza, lakini muda wote Suzan alifwatilia macho ya Monic ambayo mala nyingi alikuwa akiibia kumtazama Edgar
“Edgar karibu kwetu kimara, siku moja moja week end” alivunja ukimya Monica, “unataka akatwe mapanga huko” alidakia Suzan, “haaa! dada Suzie mapanga yatoke wapi, Edgar husi msikilize huyo wala hakuna wakukukata mapanga” Edgar aliishia kucheka bila kuongea kitu, “au una mwogopa wifi yetu?” aliuliza Monica baada ya kuona hapakuwa na jibu toka kwa Edgar, ikawa kicheko tena safari hii alisaidiwa na Suzan, “haya mama atakuja kukutembelea”alisema Suzan akiondoa ngoma juani, lakini japo ilikuwa ni kuzuga kwa Monica ilikuwa kama nafasi muhimu kwake, aliachia tabasamu moja matata, huku akiinua macho yake kumtazama Edgar ambapo wakati huo Edgar anaye aliinua yakwake kumtazama mwanamke huyu anaebembeleza kutembelewa, macho yao yakakutana, Suzan alishuhudia tukio hilo, maana alimwona Monica akitazama chini kwa aibu huku akitabasamu, kimahaba flani hivi, “mh! huyu mshenzi nini, aje tu! hivi hivi nanguo zako” aliwaza Suzan “utakuja lini Edgar,” aliuliza Monica akishindwa kabisa kumtazama Edgar usoni, “atakuambia suzan
Walikaa pale kwa muda wa nusu saa wakipata chakula, walipo maliza suzan ambae aliona mahali pale ni pachungu, aliwashauri wanzake wampeleke Monica ofisini, kisha wao waondoke zao kuelekea nyumbani, kweli walifanya hivyo wakaelekea kwenye gari lao, wakiwa wana elekea kwenye gari mala mzee Mashaka naye akawa anaingia na gari lake NISSAN SAFARI, akasimama nakuwafwata wakina Suzan ambao walikuwa wamesha fungua milango ya gari tayari kuingia, “ingieni tu ngoja nisalimiane na huyu mzee,”alisema Suzan akiwaacha Edgar na Monica wakiingia kwenye gari wakati monica akiingia siti ya mbele Edgar alikaa siti ya nyuma, yeye akapiga atua kumwai mzee Mashaka asiogee sana kwenye gari “niambie baba naona sisi tunatoka nwewe unaingia” alisma Suzan huku akiachia tabasamu, “nikweli tumekuwa tukipishana sana maali hapa, alafu mpezi unazidi kupendeza sikuizi” aliongea mzee Mashaka, akimaanisha anacho kiongea
“Si una nipendezesha wewe mwenyewe baba angu” aliongea Suzan, alafu wote wakacheka na kugongeana mikono, “alafu nina mda mrefu sijaonja kitu, tatizo tumekuwa busy sana, leo nitakuja usiku unipe mambo” alisema mzee Mashaka, hapo Suzan akawaza jibu la haraka sana “Hata mimi nina hamu kweli kweli, sema leo nita chelewa kwenda nyumbani ya ni ivi unavyo tuona tuna enda kimara kwa yule dada, kuna inshu flani hivi ya huyu mdogo wangu” alidanganya Suzan na mzee Mashaka akaafiki, “ok poa, basi tutawasiliana kesho” hapo wakaagana kisha Suzan akarudi haraka haraka kwenye gari, masiwasi wake Edgar na Monica wasije wakatongozana, akawakuta wakiwa kimya, kila mmoja akiwa busy n simu yake, hapo akajuwa kuwa wamesha peana namba za simu na sasa wana chat, “samahani Eddy naomba simu yako mala moja” alionga Suzan akinyoosha mkono kwa Edgar nakupokonya simu, “haaa! umenivurugia gemu langu”alilala mika Edgar, Suzan akuyajali malalamiko ya Edgar, akaitazama simu ile, akaona Edgar alikuwa anacheza game nasiyo kuchat kama alivyowaza, akazuga kuangalia muda kisha aka mrudishia simu yake Edgar, “kumbe saa tisa, ngoja tuwai” aliongea Suzan akiwasha gari nakuondoka
Ulikuwa umepita mda mrefu huu siku hiyo bwana Kazole alikuwa na mchepuko wake akipiga pombe mwembeni pub, akiwa ajaamini kama kweli mke wake ameshindwa kupata chochote kwa wazee wake, alisha jaribu kuvizia mala kadhaa kama angeweza kufanya kama alivyo fanya mwanzo, lakini ilikuwa ngumu maana sikuizi mzee haule alikuwa na nywea pombe nyumbani kwake sanasana alikuwa akimwalika rafiki yake mzee Ngonyani pale nyumbani kwake, na kilicho muumiza zaidi nijinsi mzee huyo alivyozidi kupata mafanikio, hapo bwana kazole alizidi kuumiza kichwa kwamba atafanyaje ili apilia pate kwa mzee huyu, kiukweli alikikuta akimchukia mzee wawatu bila sababu yoyote, kwa upande wa mkewake bado alikuwa ana jiuliza niwapi aliopo pata fehda za kuanzisha mambo yote yale
Baada ya kuchunguza kwa mda mrefu ndipo siku moja akiwa anatoka kwenye vikoba, huku mawazo yakimlikita sababu sikuile hakuwa nafedha ya malejesho, mume wake alimnyima, akimtolea maneno ya kashfa “siumeamua kukubari uongo wa baba yako, sasa utajuwa mwenyewe kwakwenda kuchukuwa fedha ya vikoba” aliongtea hayo bwana kazole akisahau uwa fedha hiyo ni kati ya fedha aliyo itumia kufanyia starehe zake, alitembea kwa mguu miguu iliyo jaa vumbi nakajasho kanamtoka, “lakini huyu baba kwanini ana tufanyia hivi, siatupatie wenzie hizo ela” alisema dada yake Edgar kwa uchungu mkubwa, wakati anakatiza mbele ya bar moja kubwa ya mwembeni, “njoo uchuku epesa yako we mwanamke, kisha njoo na bia nyingin kama tulivyo” akaisikia sauti moja iliyo penya masikioni mwake, na aliitambua vyema kabisa hiyo sauti, ni sauti ya mume wake, mke wa bwana kazole alijikuta akishikwa na hamu ya kuchungulia mle ndani ilikuakikisha kama kweli sauti ile ni ya mume wake.... akasogea karibu na maua, ambayo yalikuwa yame mtenga nisha na kumzuwia asiweze kumwona vizuri, huyo alie zani ni mume wake
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni