MAMA MWENYE NYUMBA (62)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA MBILI
Aliongea Rose akisimamisha gari nje ya jingo la benk ya wananchi na kushuka akiwa na note book yake ile aliyo kuwa nayo safarini, pamoja na karamu akawafwata polisi walio kuwa wanalinda benk hileSASA ENDELEA...
Edgar akawaona wale polisi wakimpigia salute Rose, naye akaitikia kwa kupiga salute, kisha akaona wanaongea maneno flani flani huku Rose akiyaandika kwenye ile note book yake, baada ya hapo akamwona askari mmoja akiiga salute na Rose akaitikia kisha Rose akarudi kwenye gari, “hongera sana yani unaonekana mdogo, alafu unacheo kikubwa sana” alosema Edgar akijaribu kuzigusa nyota za Rose kwenye mabega yake, huku gari likiondoka na kuendelea na safari zao “ongera wewe kwa kumpagawisha afisa wa polisi” aliongea Rose wote wakacheka
Sophia akiwa njiani akitokea Tumbi hospital akielekea nyumbani kwake mbezi kwa msuguri, na sasa alikuwa mitaa ya Kiluvya gogoni wengi wanapenda kupaita njia panada ya kawawa, Sophia aliona kabisa akili zake zinaanza kuvurugika, kutokana na mambo yanayo mkabiri, ukiachilia kutomwona mwanaume aliempa mimba, kwa muda wa siku zaidi ya nne, pia aliwaza juu ya kuchangia mwanamume na mama yake, huku bado baba yake akiwa hospital, japo alikuwa amesha pata nafuu, namama yake ameomba aruhuiwe akajiuguze nyumbani, lakini baba yake angeendelea kutembelea magongo kwa muda wote wa maisha yake, kitokana na mfupa wa mguu wake kuvunjika mala kadhaa, lamwisho lililo msumbua ni Suzane Rafiki yake wa muda mrefu kutembea na baba yake pengine na kusababisha matatizo yote haya
“Yaani leo silali naenda kwake, japo nimwone Edgar, najuwa atakuwa amemficha ndani anamwogopa mzee Mashaka” aliwaza Sophia huku akipandisha daraja la kwa bi mtumwa, na kuingia nja panda ya shule, atuwa chache mbele akaingia kibamba ccm na kukata kona kushoto, kisha akapaki gari kwenye ile bar, ambayo walisha wai ukaa na Suzane na Edgar, kisha akashuka na kwenda kukaa kwenye moja ya meza, zilizopo ndani ya hile bar, wazo lake likiwa ni kunywa bia kadhaa zakutolea uoga ndipo aende kwa Suzane, dakika chache baadae alikua amesha hudumuwa na kuanza kukandamiza bia, akiwa ajafikisha atanusu ya bia akasikia sauti ya kike ikimsalimia, “shikamoo dada Sophi,” Sophia aliitambua sauti ya Joyce mala moja, akatabasamu akijuwa kuwa ameha mpata Edgar wake, baba kijacho ........
Sophia akageuza shingo kumtazama Joyce, “hooo marahaba mdogo wangu za kupoteana,” aliongea Sophia akimtazama Joyce na tabasamu aliachia, “yani umepotea dada sophi, vipi tena leo hupo mtaani kwetu” aliongea Joyce akivuta kiti na kukaa, “nime amua kuwa tembelea sija mwona Sizie mda refu, nimeona leo nije ni mwone” aliongea Sophia huku akimtazama Joyce usoni, lakini akastuka kuona Joyce akionyesha kushangaa, “inamaana haja kuaga?” aliuliza Joyce kwa mshangao, Sophia naye akashangaa, “kuniaga kwani ameenda wapi?” aliuliza Sophia huku akijiweka sawa kuksikiliza Joyce, na Joyce bila kinyongo akamza kumsimulia kuwa, Suzan ame ama kikazi na kuelekea Songea yeye na mpenzi wake Edgar
“Na pengine kesho kuna mtu amweza akaamia, maana ile nyumba ameipangishia benk ya wananchi” alimalizia Joyce, na kumfanya Sophia aonekane kuchanganyikiwa, “huyu mshenzi kumbe alikuwa na mipango yake kichwani, hahahahaha, Suzane kweli kichwa” alisema Sophia na kumalizia kwa kicheko, akimwacha Joyce akiwa ame duwaa “huyu naye vipi, mbona simwelewi” aliwaza Joyce kwa mapicha picha ya Sophia, “usi shangae mdogo wangu hayo ni maisha tu, asa unapo mpenda mtu ambae anapedwa na mwingine” aliongea Sophia na kuikamata chupa ya bia akaiweka mdomoni na kuigugumia kwa fujo kisha akiweka chini ikiwa tupu, akainuka, “ok! my tutaonana” alisema Sophia na kuondoka zake, Joyce alimshuhudia Sophia akiingia ndani ya gari lake na kuondoka kwa fujo nusu akanyage meza za wamama wauza samaki, “makubwa kumbe tulikuwa wengi” alijisemea Joyce nakuinuka zake
Suzane na Sline walikaa pale kwa mzee haule huku wakijadiriana kuhusu sakata la Edgar kumtandika shemeji yake, “ sasa huyu shemeji yake atakuwa wapi?” aliuliza mzee Haule, “polis wamesema yupo hospital ya mkoa,” aalijibu Suzane au mama mwenye nyumba wa Edgar, wakati huku sebuleni wakiendelea na majadiriano, huku chumbaninako mke wabwana kazole aliendelea kutumiana sms na wadogo zake wakina mama semeni, wakipanga mipango ya kuendesha kesi, pamoja na kuwa julisha kuwa mchumba wa Edgar amekuja, “tena anajifanya ana fedha nyingi sana” nao wadogo zake waki mshauri kudai fidia pamoja na kumchaji fedha za matubabu na kumtibu mume wake, pia walipanga kesho yake wakutane, lakini muda wote hawakujuwa bwana Kazole yupo wapi
Bwana kazole alikuwa Hospital, amelala kwenye kitanda ndani ya hodi moja ya wanaume, huku pembeni yake ame kaa bwana kalolo akimtazama jamaa yake ambae alisha anza kupata nafuu, usizani huyu bwana kalolo alikuwa hapa bule bule, “sasa ndio muda wa kumfilisi mzee haule yani nikusingizia ghalama kibao na hasara alizo ziingiza mwanae, yeye si alijifanya mjanja kunilipa fedha za shamba mapema, bwana Kalolo aliwaza huku akitoa simu yake na kutazama muda, niile simu aliyo uziwa na bwana Kazole miezi michache iliyo pita, “mh! hisjeuwa na hii alikwapua huyu mshenzi” aliwaza mzee huyu akiwa amesha tazama muda kisha akairudisha simu mfukoni, saa tatu usiku ndio muda ambao bwana Kalolo aliaga na kuelekea nyumbni kwake
Rose ni mschana mrembo sana ambae alikuwa na miaka miwili tu! kazini, baada ya kumaliza mafuzo ya uafisa pale chang’ombe dar es salaam akapangiwa Songea, kwenda kufanyia kazi namaelekezo yakiwa kwamba Rose na wenzake kumi natano waliopangiwa huko mwanamke akiwa peke yake, wapangiwe vijijini, ambako kulikuwa na askari wengi wenye vyeo vya chini kuanzia sajenti na koplo au constebo, kiukweli kitendo cha kupangiwa Songea tu! ilikuwa adhabu kwake sasa apangiwe tena vijijini, Rose akaiona kazi kuwa ngumu, lakini alipo fika pale Songea na kulipoti kwa afisa utawala wa polisi mkoa, na kukutana afisa utawala afande Mgige Chacha , walipo ripoti hapo mkoani, wakaambiwa wasubiri baadae kusomewa post zao
Huku Rose akaambiwa asubiri humo humo ofisini asitoke wakati wenzie wanatoka, baada ya kubaki na kusubiri alicho bakiziwa, ndipo yule afisa wangazi za juu za kiutawala polisi mkoa akamwuliza Rose, “hupo tayari kwenda vijijini ukafubae mtoto mzuri” hapo Rose akauona msaada una kuja lakini, ulikuwa unakuja kwa mambo mazito zaidi, “hapana afande, naomba uni saidie nibaki ata hapa mjini” aliongea Rose kwa sauti flani ya kuliamsha dudu, “ok! najuwa wewe ni kijana tena msomi, unajuwa kumsoma mtu sasa tukutane Nyumbani Lodge tukaongee vizuri, wewe ni wa hapa hapa mjini” alionge kamanda MAGIGE CHACHA
“Sipajuwi hapo nyumbani lodge,” aliongea Rose huku akaijuwa kabisa kuwa anaitiwa kwenda kupewa dudu na siyo kingine, “ok! andika namba yako ya simu hapa, nitakupigia jioni” aliongea Magige akimkabidhi peni na karatasi Rose, hivyo ndiyo Rose alivyo bakia mjini Songea na kuwa mpenzi wa bwana Magige mkuu wake wakazi, mwanzo Rose alizani itakuwa ni mala moja ja tu! kisha kila mmoja angeshika hamsini zake, lakini alishangaa maze huyu mkubwa kiumri akimng’ang’ania mazima na kumfanya ndie nyumba ndogo yake, maana alikuwa ana famila ya mke na watoto wa tano, huku Rose akilingana na mtoto wa pili wa mzee Chacha, kuna jambo lili mpa wakati mgumu sana Rose, maana aikuwai kutokea siku atamoja mzee Magige akamkoleza kiasi cha yeye kuona kuwa amefanya mapenzi, zaidi mzee huyu alikuwa akifika pale nyumbani kwake aliko mpangishia na kumvamia, wangetumia dakika mbili au pengine ange jitaidi ata tatu alafu alafu ange mwaga mzigo game lime kwisha
Hapo Rose ange baki na utamu wake, kiukweli mzee Magige hakuitendea haki fedha nyngi aliyo ighalimia kwa penzi la huyu mwanamke, maana licha ya kumpangia nyumba na kumweke a kila kitu ndani, pia alimnunulia gari Toyota harrier na kumfungulia duka la vipodozi maeneo ya soko kuu, eti akifika kitandani anapapasa kama kuku “hivi kwaniini anani ng’ang’ania kama mambo hayawezi” aliwaza Rose sikumoja, akiwa hajuwi kuwa yule boss wake hyo ndiyo ilikuwa tabia yake, kila anapoamia mwanamke mrembo mkoa hule lazima ammiliki atakwa mwezi mmoja ndiyo amwache na wengine waendelee, lakini kwa rose aliganda na sasa alikuwa anfunga naye mwaka, mmoja kati ya wanawake waliowai kutembea na kufaidi fedha za mzee huyu, ni WP Anifah, ambae aliachwa na Magige baada ya ujio wa Rose
Japo baadae Anifah ali pata mume na kuolewa, lakini bado alikuwa anaumia sana kwa kukosa huma ya mzee huyu ambae alikuwa aionei huruma fedha yak, labda kwasababu alikuwa anazipataa kwa njia hisiyo alali, tena ukichukulia ata kitumbua chenywe ukitafuna kwa kichovu sana na akisha kula leo ange kaa atawiki mbili ange ombatena malamoja na asinge tumia ata dakika tatu kula kitumua dudu inge cheuwa na kulala mazima, “henheee amekwisha” alisema Aifah dakika chacehe baada ya Rose kuondoa gari lake akiwa ame mchukuwa mahabusu anaye julikana kama Edgar, huku akiacha maagizo kuwa maelezo ya mahabusu huyo yafutwe
Kilicho mfanya Anifah ajuwe kuwa Edgar ana afande wake Rose ni watu wano fahamiana na wanahuusiano wa kimapenzi, ni pale Rose alipo kataa kuwa sikiliza wale wanawake waliokuja kumtaazama Edgar mmoja wao akisema ni mchumba wake, ndio maana akamwambia Edgar kuwa “haya baba kumbe unakula na wakubwa” japo Edgar akuelewa lakini yule dada alikuwa anamaanisha, ile gari linaondoka tu! polisi Anifah aka chukuwa simu yake na kutuma sms kwa mpenzi wake wa zamani, kamanda Magige Chacha,‘haya sasa, mrembo wako huyoooo anaenda kuliwa, we lala tu!’
Sms hiyo ilimkuta mzee Magige akiwa metulia sebuleni kwake sambamba na mke wake, macho kwenye TV, magige alijikuta kajasho kakimchuruzika baada ya kuisoma ile sms toka kwa WP Anifah, mpenzi wake wa zamani, akamjibu haraka sana ‘mbona sikuelewi, au umeanza utani?’ alipo ituma sms hiyo akaanza kutafuta majina kwenye phone book yake akalipata jina la dereva wake wa kazini aitwae koplo Said, akaipiga ile ndamba yasimu, ikaita kidogo kisha ikapokelewa, hapo akasikika afande magige akiongea na huyo dereva wake, na kutoa maagizo “hupo wapi Said... ok! fanya haraka chukuwa gari mfwatilie Afisa wa zamu... kisha niambie yupo wapi .... maana nasikia anataka kufanya mambo tofauti na maadili ya kazi.. fanya haraka sana” alisema bwana Magige akiwa na uakika kabisa mke wake hato elewa kitu, huku ana fungua sms nyingine toka kwa Anifah
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA SITINI NA TATU
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni