MTAA WA TATU (43)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA TATU
Mariam akiwa amesimama huku kajikunyata sababu ya baridi akashtukia kazungukwa na kikundi cha
mijibaba mziki mnene wakiwa wametinga mijacketi myeusi
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Mariam hofu kidogo ikamshika sema
akajiamini kama wataitaji kumfanyia vitendo vya kishenzi atapambana ghafla akapuliziwa kitu kama
paphumu bibiye akayumba na kuanza kuona maluweluwe akajitahidi kijizuia lakini hakuweza kuona
vizuri akakunja ngumi huku akirudi nyuma mmoja kati ya wale vijana akamfumua ngumi moja tu ya
tumbo mpaka hapo hakuwa na ujanja tena akacheuwa nyongo ukizingatia kule jela hakula kitu tokea
asubuhi “Nigger embu mbebe huyo malaya twen’zetuni vijana, basi bibiye akabebwa na kuanza
kuondoka nae wakati wanapiga hatua mbili tatu ghafla kuna pikipiki ikaja kwa kasi na kupaki mbele yao
“wee mtoto wa malaya towa huo uchafu wako wanaume tupite’’
“iwapo mtaweza kumuachia huyo binti naweza kuwaacha muende mukiwa wazima lakini kama mkikaidi
amri juwa la kesho hamtoweza kuliona’’,,,
“hahaha Nigger umemsikia huyu shoga anavyoongea kudadeki zake kwanza hii pikipiki naitaka’’
Kumbe hawakumjuwa ehee, kitendo cha kusogea kwa mmoja wao karibu na pikipiki akajikuta akirushwa hewani na kwenda kutuwa barabarani
Kama vile mzigo wa kuni puhuu
Damu zikaanza kumchuruzika.
“Heyiii Nigger
Wote kwa pamoja wakatamka hivyo na kwenda kumvamia bwana mkubwa"...
Mwanaume nae akajampu na kuruka juu kwa kuiyacha ile pikipiki
Akatuwa kwa nyuma yao huku majambazi yale wakikumba ile pikipiki.
Nao wakageuka kwa kutizama nyuma, hakuwa yule tena hapo yupo kivingine
yeye ndio akawafata na kuingia katikati akasema
“hakika mtajuta baada kufika kuzimu"
Akazunguka na kutembeza nyembe kwa kila mmoja nyembe zilikuwa zile siraha zake aina ya mundu.
Majambazi watatu double wakaenda chini
huku wawili kati yao wakibaki kushikwa na taharuki, wakaona isiwe shida kumbe
hiki kiumbe ni hatari tupu,
Wakaanza kukimbia wakati huo bibiye
Mariam yupo chini hajitambui kabisa.
Sema Ninja short hakutaka kuwaacha maharamia wale kwa kuogopa huwenda watakuja kusimulia,
Ikabidi awakimbize majambazi wale walikimbia kufika mbele kidogo mwanaume kawatokea,
“tusamehe brother, hatukujuwa kama ni wewe please
Tusamehe tupo tayari kufanya chochote juu yako ili mradi tuweze kuokoka,
(SEASON ONE TULIISHIA PALE STEVEN YUPO KWA MGANGA AKIITAJI KUONYESHWA NI NANI KAMUUWA MDOGO WAKE, MGANGA AKAANGALIA HAKUWEZA KUONA KITU ZAIDI YA KIVULI TU CHOMBEZEKA NAYO SASA)
“Kivipi mzee mpaka unasema nimeingia njia sio nini shida? Nini tatizo?"
Steven akamuuliza Mganga akiwa anaikodolea macho ile TV ya asiri,
“sikia nikwambie kitu kijana huyu mtu si wakawaida kama unavyofikilia wewe hiki ni kiumbe cha hatari sana
Wewe huwoni mpaka mambo yangu yote yameshindwa kufanya kazi, haijawai kutokea hii, hata siku moja"
Mganga aliongea huku kijasho kikimtoka
“kama umeshindwa kazi sema
sio kuanza kumfagilia huyo bwege mitunguri yako ime eksipaya tu, huna lolote
Steven akatamka hivyo huku akinyanyuka kujiandaa kuondoka kuonyesha jinsi gani kachukia
Baada mganga kumfagilia
Hafidhi,
“Steven tafadhali embu kaa chini usianze kunitusi hivi mambo yako mangapi
Nimeweza kuyafanya,
nitakugeuza kuku sasa hivi ohoo"....
Mganga aliongea kwa hasira
Steven mwenyewe akakaa chini.
“kwakuwa huyu kijana kashindwa kuonekana itabidi nimtumie Majini yaende kuifanya hii kazi, au unaonaje hapo?"
“sawa Mzee mimi nakuaminia wewe sina kimbilio jingine zaidi yako.
Maana huyu mshenzi kanipa pigo maumivu yasiowezekana kupowa leo wala kesho
Kaniulia mdogo wangu"..
Steven machozi yakaanza kumtoka
“Ha!ha!ha!"....
Mganga akaanza kucheka na kusema
“kijana usitake kunichekesha sana tambuwa kitu kimoja kuna msemo unasema
Akunyimae mbaazi kakupunguzia mishuzi.
Akuanzae kukuchokoza wewe mmalize, kama pigo wewe ndio umeanza kumpa baada kumuuwa kipenzi chake.
Kama ikatokea tukimuacha atazidi kufanya mauwaji kwa watu wako wa karibu!"
“dahaa sasa Mzee mi shida yangu kubwa ni picha yake na sehemu ambayo naweza kumpata naitaji nimuuwe kwa mikono yangu mimi mwenyewe"
Steven akakunja ngumi na kubana meno kwa hasira,
“biringe bayoyo,,,,biringe bayoyo,,,,tunamuomba Dada Asia aingie kati tumuone maringo yake bingilibingili mpaka chini!!!
Ni sauti nzuri za watoto wakike wakiimba na kucheza Asubuhi ile ndizo zilizoweza kumuamsha Hafidhi kutoka kitandani, basi akajinyanyuwa kwa uchovu huku akijinyoosha akalisogela dirisha na kuipandisha panzia kwa juu na kuangali kwa nnje.
Akaweza kukiona kikundi cha watoto wakicheza na kuimba akabaki kutabasamu tu, na kukumbuka mbaali
kipindi yupo mtoto akicheza na watoto wenzake
“kioo kioo alikivunja nani...."wamwisho akamatwe atiwe gerezani"....
“Hafidhi"
“naamu Azizi unasemaje?"
“embu jitemee mate tumboni"
“kwanini nijitemee mate tumboni?"
“wee umuoni yule Albino kapita hapa kama hukufanya hivyo nawe utakuwa kama yule,
Basi Hafidhi akaifunuwa T-shirt yake na kujitemea mate asije akawa Zeruzeru.
Yote yalikuwa mawazo yake wakati akiwa kasimama pale dirishani.
Akatabasamu na kurudi tena kitandani akakaa kama dakika tano hivi, kisha akaanza kupiga pushapu huku
Akifanya na mazoezi mengine kulainisha viungo, kijasho kilimtoka
Akaichukuwa ndoo ya maji na kutoka nayo nnje, kama ujuavyo vyoo vya uswazi ndio hali aliyokutana nayo
Bwana mkubwa ni foreni
“hivi huyu Meja anakunya kokoto au maana muda wote huo"...
“itakuwa anatafuta sehemu ya kutaga tu maana tokea aingie ni nusu saa hii"...
“wee Meja embu toka humo chooni pumbavu zako,
Ikabidi sister duu mmoja akapaza sauti kwa hasira,
Ndipo Meja akatoka huku kajishika
tumbo
“wee kaka embu ingia basi ukaoge"
ilikuwa ajabu mwenye zamu yake akimpisha Hafidhi nae hakuwa na jinsi zaidi ya kushkuru
Akaingia kwenda kuoga
“mmh! Mijitu mingine bwana kujifanya kimbelembele kama vile shipa"
Kuna mama mmoja wakikubwa akaongea hivyo,
“haikuhusu bibi wewe, ndio nishampa zamu yangu na akitoka tu naingia Mimi!"
“unasemaje wee Malaya yani umpishe yule boya kisha uingie wewe jiangalie nitakunasa makofi ohooo"...
Ilikuwa kauli ya jamaa mmoja akimchana live na kumtishia yule sister duu kuhusu kitendo chake cha
kumpisha Hafidhi aingie chooni arafu aseme akitoka eti ataingia yeye tena, binti ikabidi awe mpole tu
maana huyo kijana si mtu mzuri mbele ya jamii kwanza anasifika kwa tabia yake ya ukorofi kukutia
chongo au kukuchana na kiwembe kwake ni kitu cha kawaida tu, baada kupita kama dakika moja hivi
Mwanaume akatoka chooni na kusimama mlangoni,
“wee boya embu pisha hapo yani umepewa lift unataka kupiga na honi wee vipi’’ jamaa akaongea hivyo
huku akimpushi Hafidhi ajabu mwenzake hata hakuyumba wala kusogea zaidi ya kupepesuka yeye, si
akapandisha mori wa kimasai “wee!!! Bwege nini nakwambia nipishe puhuu akayumba na kudondoka
chini wakati anaongea kwa jaziba akapigwa ngumi ya uso moja tu kisha mwanaume akashuka kutoka juu
ya ngazi za choo huku yule jamaa nae akijiweka sawa si akarusha ngumi mbili tatu mwanaume kama
kawaida yakeakapanch na kumdaka mkono akafanya kuunyongorota hivi basi hizo kelele alizozitoa
jamaa shida tupu “jamani nakufa!!! Mkono wangu huku mamuweee’’,,,, kisha akamchota zinga la
mtama yani ilikuwa kama vile baba anamchapa mwanae wakati ugomvi wa yule jamaa ukiendelea kila
mmoja alikuwa bize kushuhudia mtanange huo
Jinsi mbabe akifinywa
Hakika kila mmoja akatamani hata kucheka lakini hawakufanya hivyo zaidi ya kuishia kuzomea tu
“hillooo leo umepatikana pigana sasa"..
Nae akajibu kwa kusema
“nyie mabwege si mnanicheka sio sasa nikitoka hapa mtaona yalaa!!!
Akazidi kupiga kelele kwa maumivu.
Baada mwanaume kuona kumbe jamaa mwenyewe hana lolote
Akaamuwa kuachana nae na kuingia zake ndani
“huyu boya tu mamaye zake si anajifanya mjanja ehee subiri ataona
Kudadeki zake atahama huu mtaa bila kupenda
Bwege tu, jamaa akazidi kupayuka na kutukana matusi wakati huo
Hafidhi akatoka ndani na kusepa zake,
“Fatuma shogaangu umemuona yule mkaka kwanza yuko smart!
Kingine inaonekana hapendi dharau"...
“nimemuona sema nini
Ngozi boy sikuzote hakubari kushindwa mi nahisi yule kijana anaweza kuvamiwa na kikundi cha watoto wambwa"...
“yani hapo ndio nina wasiwasi si kidogo kama ikitokea yule
Handsome akavamiwa sijui itakuwaje ukizingatia yeye ni mgeni hana
Kampani hata yamtu mmoja"
Walikuwa ni mabinti wawili wakiongelea swala zima la tukio hilo"
Kifo cha bibiye Yusra kiliweza kuwaasili
Wenzake kwa kiasi kikubwa tu si Vivian wala
Mariam wote wakabaki kuhudhunika na kuwa na mawazo mazito juu ya swala hilo.
Hata utendaji wa kazi haukuwa na maana juu yao,
Taarifa za kifo cha mke wa muheshimiwa Raisi ziliweza kuwashtuwa wengi
hasa mataifa mengine
na kusema ni uzembe wa jeshi la polisi kutokuwa makini katika kitengo kizima cha ulinzi
Wakati vyombo vya habari waliweza kuriport tukio zima jinsi
Mke wa muheshimiwa alivyotekwa na kuanza kuongea ukweli yeye ni nani
sasa kwaajili ya kutaka kuficha siri
ndio watuhumiwa wengine wakaamuwa kumuuwa,
sema huu ni mwanzo tu serikali itahakikisha washukiwa wote wakiingia kwenye mikono ya Dora,
Wakati muheshimiwa Raisi kilio chake kikubwa ni kuhusu yule Ninja yani alitamani akutane nae aweze kumuhoji mawili matatu
sema ni kitu kisichowezekana,
“halloo baby uko wapi kwa sasa?"
Vivian akauliza swali baada kumpigia simu
kipenzi chake upande wapili sauti ikasikika ikimjibu
“nipo mitaa ya Tandika hapa nimekuja kuchukuwa nguo, ghafla kuna jamaa akapita na kuikwapua ile simu,
Hafidhi kile kitendo hakuweza kukitegemea Aisee akaona akizubaa simu itapotea
Akaanza kumkimbiza kimya kimya hakuna cha kelele za mwizi wala
nini. Yule kibaka alionekana ni mwenyeji wa mitaa hiyo hakuweza kufahamu kama
Kanunuwa chumvi akijuwa sukari
Nyeupe kimbembe akaimimina kwenye sufuria ya shukhuri pasipo kuonja akagawa chai unafikilia nini kilitokea hapo,
ilikuwa mkimbize mkimbize
Mpaka Temeke mikoroshini
Jamaa kila akikimbia na kutizama nyuma mtu huyu hapa akaingia maeneo ya makaburi na kusimama si kuna masela wake walikuwa wakicheza kamari
Akajiamini yule jamaa hawezi kufika
“wee Chidy vipi mwamba mbona tunashtuana umekinukisha nini? Huko utokako?"
“nikinukishe wapi kuna bwege mmoja nimemchukulia hiki kimeo kule Tandika sokoni sasa kila nikila kona naye yupo."
Baada kusema vile wenzake wakacheka kwa dharau na kusema
“ha!ha!ha! Achaga uboya wewe inamaana huyo jamaa alikuwa apigi kelele za mwizi au?"
Wakati wanaongea wote wakashtuka upepo ukivuma
maeneo hayo na kubaki kuulizana".......
Kila mmoja akashtuka na kujiuliza huo upepo unatokea wapi mbona upo kasi kwa kiasi kikubwa
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni