MTAA WA TATU (45)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
“Ossss,,,,ahaaaa,,,hapooooo,,,,uwiiiii,,ingizaaa,,,yoooote,,,,mmmmm,,, Mwanaume akaweza kutambuwa
kuwa mlinzi kwa wakati huo hayupo getini yupo kwenye chumba kingine akifanya mapenzi na House girl,
wakati akiendelea kusikilizia nae akahisi kusimamiwa na kiumbe nyuma yake
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Kupitia macho yakeakakitizama kwanza kivuli na kugunduwa kuwa kiumbe kilichopo nyuma yake si binadamu maana kina
mapembe na mkia basi akaona kile kiumbe kikijiandaa kumpiga sijui kofi au ngumi ile anarusha
mkono tu Hafidhi akachumpa na kuinama kwa chini mkono ukapita na kwenda kutuwa ukutani ukuta
wenyewe ukaweka alama ya mkono wa yule kiumbe.
Hakika alikuwa na gadhabu si mchezo, akageuka na kumuona Hafidhi akikimbia nae akaruka juu na
kumfata kwa speed wakati Hafidhi kwenye akili yake akijiuliza hiki kiumbe kimetokea wapi mbona kama
anataka kuniuwa.
“Ibnuwasi’’ “naam mama, “embu hamka mwanangu angalia kule kwenye TV jinsi mwanao
anavyokimbizwa na Makata, basi Ibnuwasi akatupa macho yake kuangalia TV hiyo spesho kwaajili ya
kufatilia maisha ya Hafidhi sijui hata akifanya mapenzi na wanawake wao wanaona au vipi.
“Pumbavu zake huyu Makata nahisi anijui vizuri wacha nikamuonyeshe kazi pumbavu zake’’,, Ibnuwasi
alitamka hivyo akijiandaa kuondoka lakini mama yake akamzuia kwa kumwambia embu tulia kwanza
umuone mjukuu wangu akimchezesha gwaride huyo Makata, Tukija maeneo ya kitimutimu Hafidhi
akazidi kumkimbia Makata na kumpeleka kule ambako wale wauwaji wengine wameingia, majambazi
nao wakiwa hawana hili wala lile wakashtuka baada kukiona kiumbe cha ajabu kikija mbele yao, na
kujikuta wakizikoki silaha zao na kuachia risasi mfurulizo kwenye mwili wa Yule kiumbe mpaka hapo
hakukuwa na siri tena wenye nyumba nao wakashtuka mlinzi na house girl wakaingia uvungu wa
kitanda, Bwana Peter Ally ndio baba mwenye nyumba hiyo baada kusikia milindimo ya risasi ndani ya
nyumba yake akapiga simu polisi wakati kituo cha polisi Osterbey washasikia kila kitu na wapo njiani kuja
eneo la tukio, Hafidhi baada kuona kawachomesha wale majambazi kwa yule kiumbe nae hakuwa na
budi kuondoka haraka ndani ya eneo hilo, basi akachumpa na kuruka juu ya ukuta na kutokezea upande
mwingine na kusepa zake. Kimbembe kikabaki kwa Majambazi na yule jini, Kwanza walijuta kummiminia
Risasi ilikuwa kama vile kutwanga maji kwenye kitu risasi zote zilizoweza kukita mwilini mwake kiumbe
hata hakijafa wala kutokwa na damu, Zaidi ya kubaki matobo kama vile driri imetobowa ndani ya mwili
wake. Jambazi mmoja akashikwa na kuchanwa chanwa tumboni utumbo na mabandama kule, mwingine
akashikwa na kuanza kunyonywa damu hakika Makata alikuwa anatisha, majambazi wengine wakaona
ehee tutakuja kufa kizembe maana tukisema tuzubae hiki kiumbe hakifai kabisa, kila mmoja akatimua
mbio si wakapitia getini na kujikuta risasi zikituwa maungoni mwao kwani polisi walikuwa washafika
kitambo tu na kutega targert yani wakitokeza tu, hakuna kuuliza ni kuwapiga shaba ndivyo ilivyokuwa.
Kwa upande wa Makata baada kugunduwa kuwa mlegwa wake kamkimbia akapiga mahesabu na kuona
kumbe hayupo mbali akatoka ndani ya nyumba hiyo kwa kupaa juu, polisi hawakuweza kuamini aisee
baada kukiona kiumbe hicho wakabaki kukodowa macho wasijuwe nini cha kufanya, kitu kama vile Popo
bawa, yupo angani
“ebwana hiki kitu sijawai kukiona tokea kuzaliwa kwangu, zaidi ya kuona
Movie tu.
“usiseme hujawai kukiona kiumbe kama kile tokea uzaliwe, si ndio ushakiona hapa au vipi!"
Afande mmoja akamuweka sawa mwenzie juu ya kauli yake kuwa haiko
sawa. Wakati katika mitaa ya Namanga kulikuwa na kitimtimu
Baina ya Makata na Hafidhi, wakikimbizana
Mwanaume akiwa juu ya pikipiki akizidi kuchanja mbuga wakati
Makata akiwa juu ya anga akimtemea cheche za moto, mpaka wanaingia maeneo ya Dry
Mwanaume hakuweza kufikiwa akazidi kuchanja mbuga, na kutokezea Mikocheni
(B) sijui kwanini kampeleka maeneo hayo
anajuwa yeye mwenyewe,
Kiumbe kiliunguruma njia nzima sauti yake kama mlio wa baruti
Tena usiku huo iliweza kupenya kwenye ngome za masikio ya watu wengi na kuwafanya waamke kutoka usingizini
“Mume wangu embu hamka bwana unasikia milio ya mabomu hayo,
Mwanaume baada kusikia mabomu akakurupuka na kutoka zake nnje mbio,
Sauti ya kiumbe kile iliweza kusambaa ndani ya jiji la Dar es salaam nzima,
Hafidhi baada kuona kamkimbia vya kutosha akaona sasa inatosha wacha apambane tu kama kumkimbia atamkimbia mpaka wapi
Akaingia kwenye Viwanja vya Tanganyika pale Pekasi,
akaisimamisha pikipiki kwa style ya pekee kabisa kwanza akachumpa kwa kwenda juu kisha
Akatuwa chini kama vile kizuka upepo ukavuma,
Makata nae akatuwa huku akicheka
“khakhakhakha! Hiyo sauti mbayaa kama vile mashine ya kuchana mbao,
Hafidhi hakuogopa kicheko chake wala sauti yake, ndio kwanza akazichomoa siraha zake na kuchumpa kuja kumfata
Makata lakini akakutana na kofi juu kwa juu na kutupwa mbali na pale.
Yani akadondokea nguzo moja ya goal lililopo Uwanjani hapo, kisha
Akanyanyuliwa na kuzungushwa juu kwa juu akatupwa tena,
Mwanaume alikuwa kapatikana, mbele ya kiumbe hicho hakuweza kufuwa dafu kabisa,
Akiwa chini amelala huku akiugulia maumivu, akajitahidi kujiinuwa akashindwa yani alihisi, kama miguu yake haiwezi
Kufanya kazi kwa wakati huo akashikwa kwa kukabwa na kuning'inizwa utasema kuku kishingo,
Makata akajiandaa kumtafuna
Ghafla bin vuu kijinga cha moto kikatupwa na kutuwa moja kwa moja mdomoni
Kwa Makata akayumba na kumuachia
Hafidhi akienda chini
Akatizama nani kampiga na moto,
Makata kwanza akashtuka baada kumuona
Ibnuwasi binafsi anamkumbuka vyema ni kiumbe hatari kushinda yeye
Akaona isiwe shida wacha asepe akakimbia
Ibnuwasi akamtizama mwanae pale chini
Akaonekana hajitambui kabisa,
Basi akamsogelea na kumbeba
na kuondoka nae.
Baada kupita siku kama tatu hivi tokea tukio la Hafidhi kupigwa na kiumbe cha kutisha
kinachoitwa
Makata, kwanza ilikuwa ni siku ya furaha kwa upande wa Steven kwani aliweza kupewa habari na mganga wake kuwa
yule muuwaji wa mdogo wake
ameshakuwa marehemu, hayupo tena duniani
“ni kweli Daktari au?"
“ndio ni ukweli mtupu uwamini au nikuitie
Makata aweze kudhibitishia"....
“hapana Mzee usimwite mimi nishaweza kuamini kwa asilimia mia moja
Hakika hapa nilipo nina furaha si kidogo, embu kamata hii,
Mganga au Daktari akapewa kiasi cha pesa sijui shilling ngapi.
Sema kilikuwa kibunda cha kutosha,
Wakati upande huu kukiwa na furaha upande mwingine kulikuwa na majonzi na vilio, haukuwa upande mwingine ni
Ujinini kikundi cha majini walikuwa wamekusanyika na kuombeleza sijui kulikuwa na msiba au vipi,
“sasa Ibnuwasi mwanangu kuanzia sasa unahitajika kupiga moyo konde
hutakiwi kulia tena kumbuka kila kitu kina mwanzo na mwisho,
Kila nafsi itaonja umauti muache mwanao apumzike kwa amani"....
Tobaa kumbe Hafidhi kafa mbona wanazungumzia msiba
mwanae gani huyo apumzike kwa amani.
“hapana mama kusema kweli yote umeyataka wewe laiti kama ningewai yote yasingetokea,
Hakika ulikuwa msiba mzito sana
“halloo baby mbona inapita wiki sasa hauji nyumbani kwani upo wapi?"
Vivian aliuliza baada kumpigia simu Hafidhi sasa sijui Hafidhi gani wakati inasemekana amekufa kule Ujinini,
“usijali my wife
nilisahau kukuaga kama nilipata safari ya ghafla sasa hivi nipo
Nchini Uganda muda si mrefu nitarudi my"
“mmh! Yani baby una safiri pasipo kuniaga kweli hunipendi"
“hapana mama watoto
Nakupenda sana tu sema ilikuwa ni safari ya kikazi tu kama ujuavyo kazi zenyewe za kuajiliwa Bosi akiamuwa kitu ndio hicho hicho ukisema ukatae utasikia
kazi hauna"...
“sawa my dear nimekuelewa ongea na mwanao"....Vivian akaweka simu tumboni kumsikilizishia mtoto kisha akairudisha sikioni na kumuuliza “si umemsikia ehee
Kasema anataka juice na Chocolate
Basi simu upande wapili ikasikika sauti ya Hafidhi akicheka na kusema Usijali
my dear vipi bi mdogo upo nae hapo?"
Vivian pasipo kujibu akampatia simu bibiye Mariam ambaye alikuwa bize kutizama television.
“halloo tumpase pahee chupke chumpke nyonga mkalia ini mambo vipi,
Mariam akabaki kutabasamu baada Hafidhi kuanza kuongea kihindi kwa kutaja majina ya Movie akijifanya ndio anaongea.
“nawe kujifanya ndio Sharkhan sijui
Ajey unachapia bwana"
“Ha!ha!ha!ha
Baby nachapia mimi huyo au wewe?"
“wewe ndio unachapia"..
Baada kuongea kwa kirefu kidogo simu ikakatwa kila mmoja akafarijika baada kupigiwa simu na kipenzi chao,
maana imepita takribani wiki moja
Hawakuweza kumtia machoni wala kuisikia sauti yake,
Tukija pande za Mbagala tunamuona
Hafidhi akiwa kavaa begi jeusi akifunguwa chumba chake na kuingia ndani
wakati tunaonyeshwa kule
Ujinini mwili wa Hafidhi ukiwa umelala kwenye moja kati ya sehemu za kuhifadhia miili ya Majini
pembeni akiwa kasimama
Ibnuwasi yani wiki nzima analia kumlilia mwanae
“Hafidhi kijana wangu umelala au?...kama umelala embu hamka basi
Mwanangu wa pekee,,,,inuka nikukabidhi nguvu simama upambane
Sauti ya Ibnuwasi ilikuwa kali na nzito,
Ghafla pasipo kutegemea hata
Ibnuwasi akashtuka baada
Hafidhi kupiga chafya akahisi labda masikio yake kasikia vibaya
Sema akajiaminisha baada kuona vidole vya
Hafidhi vikicheza akapaza sauti
Kuita “mwananguu!!!
Sauti ambayo iliwafanya baadhi ya Majini
waje mbiombio kutaka kufahamu kunani tena
Hakika kila mmoja akabaki kustaajabu baada kumkuta marehemu akiwa ni mzima amekaa kitako kwenye kitanda kile cha mauti.
“Hafidhi ni wewe kijana wangu? Yani siamini kabisa kama umeweza kurudi, tena duniani,
Hafidhi mwanangu"...
Ibnuwasi machozi ya damu yalimtoka
Na kwenda kumkumbatia
Hafidhi pale kitandani
“vipi Kaka ulikuwa wapi ndani ya siku mbili tatu hizi?"
Jackson akamuuliza swali
Hafidhi wakati huo alikuwa akiosha vyombo sema kimiujiza tu,
“nilienda kumtizama Bibi mzaa Baba huko kijijini, alikuwa anaumwa, sema sasa hivi kidogo ajambo,
“dahaa pole sana kaka
Juzi kati mwanangu mwenyewe yule demu mwenye kupiga mikelele si katia team
Mpaka magetoni kwangu
kushika kiuno tu mtoto akatoa sauti
Ayiiiiii,,,,,assssss,,,nikashika nido
Ndio nikammaliza kabisa, kitu ndembendembe"..
Basi wakacheka na kugongeana mikono
sema Jackson akahisi kama kupigwa short hivi baada kugusana na
Hafidhi ikabidi aulize
“wee jamaa mkononi mwako umeshika nini?"
Tukirudi Ujinini kulikuwa na shamrashamra juu ya kijana wao kurudi tena duniani
Kwa wakati huo alikuwa akifanyia tambiko la maana pamoja na kupewa nguvu zote
za Kijini
“Hafidhi mjukuu wangu ingia ndani ya chumba kile ukitoka humo hakika wewe ni mjeshi kamili
Hafidhi bila kusita akafanya hivyo
Akaingia
Vilio vya majini vikaweza kusikika ndani ya chumba hicho kisha Mwanaume akatoka akiwa katapakaa damu Minjino imetokeza utasema vile zombie
Au Vampire
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni