MTAA WA TATU (56)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
“Wee bwege mamayo zako ushatutafutia msala embu chukuwa hilo bagi ulirudishe fanya upesi kabla sijakutumbua macho malaya wee’’,,, mmoja kati ya vijana akang’aka kwa hasira kwa kumtaka mwenzake afanye haraka kulipeleka hilo bagi.NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Kijana huku mikono ikimtetemeka akafanikiwa kulibeba bagi na kupiga hatua za haraka kuondoka ndani ya mjumba huo, njia nzima alikuwa akijiuliza yule jamaa anaeishi kwenye chumba kile ni nani na itakuwaje akifika maeneo yale kisha watu wakamuona si watamuuwa maana wengi wao walimtambua wakati aliporuka ule ukuta na kuwatukana sema akajipa moyo.
“Baby’’ bibiye Saida akaita hivyo “Naamu niambie king’asti changu’’ “sijui kama utaweza kunielewa mpenzi wangu kwahiki nitakacho kisema sijui hata nianzie wapi’’,,, Saida akazungumza huku akimshikashika Hafidhi kifuani na kuvichezea vinyweleo sijui wanaita garden love “Wee niambie tu usihofie chochote kwani nini tatizo?’’ “Basi wakati unatoka ukaniambia nikusuuzie vyombo vyako nami nikafanya hivyo baada kumaliza nikaingia bafuni kujimwagia maji kidogo mlango niliusindika tu kumbe huku nyuma si akaingia mwizi na kuiba lile bagi kelele za mwizi zikanifanya nikurupuke na mapovu yangu kichwani hadi usoni kuja kuuliza mwizi yuko wapi sikuweza kupewa jibu, baby mwenzako nina wasiwasi mkubwa sana,
Mpaka hapo mwanaume akaweza kutambua kwanini wakati anataka kuufungua mlango wake kuna kitu kama mwanga wa taa uliweza kummulika kwenye paji lake la uso kumbe ilikuwa ishara ya kumjurisha kwamba ndani ya chumba chake kuna tatizo basi hakutaka kupoteza muda akanyanyuka kutoka kitandani na kuvaa nguo zake huku akiuliza huyo mwizi kakimbilia wapi. Saida akamjibu kwa kumwambia mbona yamepita masaa mengi sana tokea tukio hilo litokee haitokuwa jambo jepesi kuweza kumpata huyo mwizi, “wewe niambie kakimbilia wapi kuhusu masaa sijui dakika niachie mimi ndio ninaejuwa nitampata vipi’’ Hafidhi akawa mkali kidogo Saida nae hakuwa na jinsi zaidi ya kumtajia mwanaume akatoka kwe mwendo wa haraka lakini kabla ya kuingia vichochoro kadhaa akaweza kukutana na huyo kijana ajabu kila mmoja akampita mwenzie sijui hawakujuana au vipi “Shenzi zake ana bahati karudisha mwenyewe vinginevyo ningemtengua kiuno leo’’ Hafidhi akajisemea hivyo kumbe aliweza kumtambua basi kijana akaweza kufanikisha kulirudisha lile begi baada kufika maeneo hayo akalitupia mlangoni na kukimbia zake kumbe Hafidhi alikuwa yupo nyuma yake kile kitendo cha kulitupa tu mwanaume akaliokota huku akicheka na kuingia nalo ndani,
Saida hakuweza kuamini aisee kumuona Hafidhi akiwa na lile bagi akauliza “umelipatia wapi hilo bagi tena?’’ Hafidhi akabaki kumtazama pasipo kumjibu chochote na kuliweka kwanza lile begi kabatini kisha akasema “baby ujuwe mi noma sana yani nilipotoka hapa nikaruka ule ukuta na kutokezea kwenye mjumba fulani hivi kwa mwendo wa kunyata nikaweza kuwaona vijana kama sita hivi wote wakiwa arosto basi nikajongea na kulichukuwa hili bagi kulaini kabisa pasipo wao kuniona kisha nikasepa zangu, “mmh baby wee muongo yani unataka kusema uliweza kupanda kwenye ule ukuta kwanza ulijuwaje kama mwizi atakuwa maeneo yale?’’ “Si niliulizia hapo nnje ndipo nikaambiwa mwizi wakati anakimbia aliruka ukuta wa maji matitu’’ “Sawa hapo nimekukubali wewe noma yani sijawai kumuona mwanaume mjanja kama wewe’’ ghafla mtoto wakike akaguna baada kutekenywa kwenye chuchu yake ya kushoto kwa kusema “asssss,,,ohoooo,,,mi sitaki bwana akadakwa mdomo na kuanza kunyonyana denda hakika lilikuwa denda hatimae andunje akapenya kwenye kitumbua.
Baada kutimia kama wiki moja hivi ndani ya uwanja wa ndege uliopo maeneo ya Kipawa siku hiyo kulikuwa na ugeni ulikuwa ujio wa kijana matata sana kijana ambaye aliweza kuipa jambajamba nchi ya Marekani ijapokuwa sio wa kulipua ubarozi au nini “ohoo karibu sana kijana wangu hatimae umeweza kurudi nyumbani ukiwa salama salimini’’ Alikuwa baba yake Michael akimwambia mwanae na kumkumbatia hawakutaka kupoteza muda wakaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo, wakati huohuo ndani ya uwanja huo tunamuona mzee mzima akipandisha ngazi za ndege bila shaka safari yake ya kwenda nchini Marekani ilikuwa imewiva sijui anaenda kufanya nini sema ndio hivyo anaondoka. Yani ilikuwa kama vile wamepishana tu, “Baba unataka kusema ndani ya nchi hii kuna mpumbavu mmoja anawapa jambajamba’’ Michael akamuuliza swali baba yake. “Ndio mwanangu huyo kijana kwakifupi anatisha yani hivi tunavyoongea kauwa watu wengi sana polisi sijui FBI wanaangaika usiku na mchana kumsaka wanaishia kupigwa matobo tu hakika hakamatiki wala hashikiki’’
“mmh’’ Michael akaguna na kusema “Lakini baba tambua kitu kimoja hapa bongo hatuna vitengo vya maana kuweza kumshika kunguni kama huyo kitu kingine hii kesi ya panya huwezi kumpa mende ukitegemea mende atamkamata panya maadamu nimefika hii kazi niachie mimi nina hakika nitamshika siku si nyingi tena nitakuja kumuuwa mbele ya macho yako’’ Michael aliongea kwa ujasili sema mzee wake akaguna tu hakutaka kujipa matumaini ya aina yeyote kuhusu kijana wake kuja kumkamata Hafidhi j Ikram akajiseme moyoni mwake tusubiri na tuone asitukane mamba kabla ya kuvuka mto’’ Ndani ya hospitali ya Agakhani kulikuwa na pilika pilika za hapa juu ya bibiye Vivian baada kushikwa na uchungu wa kujifungua kwa mara ya kwanza tunaiona familia yake yani baba yake na mama yake na ndugu zake wengineo kama vile dada, kaka shangazi bibiye Mariam nae alikuwepo na kitumbo chake sijui yeye lini sema kuna kausemi fulani hivi ukimuona mwenzako akinyolewa naw tia kichwa chako maji sijui huu msemo unamaana gani “Mariam binti yangu yani mwenzako tokea arudi kutoka mafunzoni hakutaka kuja nyumbani kabisa yani hata kutupigia simu hakufanya hivyo tukaishia kumuona kwenye video tu. Sema nashukuru sana kwa kuweza kutujulisha hali yake’’ Alikuwa mama yake mzazi na Vivian akimwambia Mariam wakati wakiwa katika mazungumzo mlango wa wodini ukafunguliwa akatoka Daktari huku akiwaa na tabasamu mwanana akasema “ongereni sana hakika binti yenu ameweza kujifungua salama mtoto wakiume’’ kila mmoja akafurahi na kukumbatiana “vipi Daktari tunaweza kwenda kumuona?"
Mariam akauliza swali basi
Daktari akamjibu haina shida mnaweza kwenda kumuona basi wakaingia kwa pamoja binafsi ilikuwa bonge la furaha kwa bibiye Vivian kupata mtoto
Jamani huyu mtoto kafanana kila kitu na baba yake kuanzia unywele mpaka ukucha ni
Hafidhi mtupu sijui mwenyewe akirudi na kumuona mwanae atafurahi kwa namna gani"
Vivian alijisemea hivyo.
“Akirudi kutokea wapi tena?"
Mariam akauliza swali binafsi hakuweza kutambua kama kipenzi chake
Ameenda kwenye nchi za watu.
“Kwani wewe hajakuaga?"
Vivian nae akauliza swali
“Ndio hakuweza kuniaga kwani ameenda wapi?"
“Binafsi mimi kaniaga anaenda Marekani"
Mariam akashtuka nusra adondoke
sema akajizuia na kujishika kichwa palepale hali yake ikabadilika kwakuwa alikuwa yupo hospital ikawa rahisi kupatiwa msaada.
Hafidhi aliweza kupitia nchini Ufaransa na kutaka kuanzia upelelezi wake hapo katika jiji la Paris
Mwanaume akatafuta hotel yenye hadhi ya chini kidogo
Yote ilikuwa katika plan yake ya kutotaka kufahamika yeye ni nani kama ujuavyo nchi za barani ulaya kila kitu kinakwenda kutokana na tekenorajia. Akiwa ndani ya chumba chake alichoweza kukipata akawa akipanga ni jinsi gani ataweza kuwanasa wabaya wake kwa mara ya kwanza akafanya kitu cha ajabu baada kunyoosha kidole chake cha shahada kuelekezea ukutani ghafla kikatokea kitu kama zile tv za projekta akabaki kutabasamu huku akiikazia macho ile tv hakika uliweza kuonekana mji mzima wa jiji la Paris nchini ufaransa, akajiseme “yes! Wewe kenge nimeweza kukunasa na kuonyeshea picha ya baba mmoja hivi akiwa super markert, baada kuongea vile ile tv ikapotea na kubaki ukuta tu kama ilivyokuwa awali
Ni kesho yake asubuhi na mapema mwanaume akajihimu kuamka sema kulikuwa na baridi la maana akaingia kwenye mitaa na kujipatia jacket na kofia yake kisha akaingia kwenye mgahawa kwaajili ya kupata kifunguwa kinywa haikumchukuwa dakika nyingi akatoka na kujichanya na watu wa maeneo hayo watu wenye ngozi nyeusi walikuwa wanahisabika.
Kila hatua aliyokuwa akitembea akawa anajiangalia kwenye kiganja chake cha mkono unaweza kusema anacheki ramani safari yake ikampeleka mpaka kwenye hotel moja yenye hadhi ya nyota tatu kwanza maeneo hayo matajili pekee ndio wenye kuingia maeneo hayo mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi hugusi kwanza kulikuwa na ulinzi mkali utasema analindwa Rais kumbe vibopa, kutokea nchi mbalimbali walioweza kufikia kwenye hotel hiyo ya kifahari.
Hafidhi akachekecha akili na kuona kama atatumia njia ya kawaida kuingia ndani ya mjengo huo itakuwa vigumu kwake yeye kufanikisha lengo lake akaona njia pekee ni kuchenji uharisia kutoka ubinadamu na kuwa Jini, hakupoteza muda papo hapo akabadilika na kuwa kiumbe kisichoweza kuonekana kwa macho ya kawaida akaingia ndani ya hotel bila tatizo lolote, aliweza kuwaona watu wengi sana wakiwa wamejichanganya katika vikundi mbalimbali wapo ambao walikuwa wapo bize kwenye kucheza kamali wengine wakiwatazama wanadada fulani waliokuwa wakicheza nusu uchi yani ndani ya hotel hiyo kulikuwa na full burudani, yeye hakutaka kupoteza muda kaja hapo kwa nia moja tu kumpeleka mtu kuzimu.
Akapiga hatua za haraka huku akipigana vikumbo na baadhi ya watu sema wenyewe hawakuweza kutambua chochote kama wamepigwa vikumbo, kwenye kona moja hivi ya hotel kulikuwa na kikundi cha mabinti wamemzunguka mzee mmoja wa kiafrika , bila shaka mabinti wale walikuwa ni malaya wa jiji hilo,
Hafidhi akatabasamu baada kuweza kumuona huyo mzee akamsogelea kwa ukaribu zaidi na kujitoa kwenye umbile la kutoonekana na kuwa binadamu wa kawaida akamkazia macho yule mzee nae baada kumuona Hafidhi akashtuka na kudondosha glass chini mabinti wote wakashangaa imekuwaje tena buzi lao kawa vile yani kama mtu aliyeshikwa na degedege,
Walinzi wakawai kufika haraka baada kugundua kwa yule mzee kuna tatizo Hafidhi akatoa kauli moja tu tena kaongea kwa lugha ya kifaransa sema mimi natafsiri “Tafadhali nawaomba mtoke nnje haraka sana",,,,,Kila mmoja akashikwa na mshangao, wakati yule
Mzee akitafuta upenyo aweze kukimbia"
Kauli ya kuwaambia tokeni nnje basi watu wakapigana vikumbo katika kuugombea mlango, kila mmoja alitaka kuwa wakwanza kutoka. Walinzi wa ukumbi huo wenye asiri mchanganyiko yani kulikuwepo na Warusi, Wajapan, Wathailand hawakupoteza muda wakamvamia basi ulitembezwa mkono wa ajabu watu walitupwa huku na kule hakika Mwanaume hakutaka mchezo kabisa.
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni