TANGA RAHA (42)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
“KWEENYE DUNIA,WANAKWENDA KUZUIA KUBADILISHWA KWA WEZAO,NA ENDAPO WEZAO WAKIBADILISHWA ZAIDI WATAWEZA KUKUANGAMIZA KWA MAANA WANAJUA SIRI ZAKO ZOTE”SASA ENDELEA...
“Sawa ila wewe sijajua ni nani?”
“MIMI UTANIJUA,NI KIONGOZI WAKO NILIYE AGIZWA KUFANYA KAZI HII”
“Asante”
Nikawatazama majini na kuona wakiendelea kusubiria kitu cha kuwaambia,Nikaaamrisha jinsi nilivyo ambiwa na nikapata majini kumi vijana wenye nguvu za kutosha na wenye miili mikub-wa.Mara moja wakaanza kazi niliyo wapa,wengine nikawaruhusu warudi nyumbani na nikabaki na wawili wa kunilinda.
Nikamuagiza jini mmoja kunishusha chini na akafanya hivyo.Nikaanza kukatiza maeneo ya Club Lakasa Chika na kukuta damu nyingi ikiwa imetawala sehemu nyingi za barabara.
“Mkuu,mimi ninaitwa Khadan huwa ukoo wangungu asili yetu kubwa ni ulinzi kwa binadamu wanao tuhitaji”
“Sawa”
Tukazunguka karibu mji mzima kuna maeneo yamesalimika kwa watu kutafun-wa.Wakanichukua hadi nyumbani,Na kumkua Rahma akiwa katika hali ya majonzi.Baada ya kuniona akanikumbatia huku akimwaga machozi
“Baby una nini?”
Nilimuuliza Rahma kwa wasiwasi huku nikiwa ninamashaka
“Eddy viumbe vyako vimeua ndugu zangu.”
Nikastuka kidogo sikujua ni vipi amezipata hizi habari
“Nani amekuambia?”
“Nimehisi tu mume wangu”
“Utahisi vipi wakati kitu haujakiona?”
Nikamtazama Rahma machoni,nikamvuta karibu na kumpiga busu la mdomoni na kuingia naye ndani.
Hadi inafika jioni majini ambao walikuwa wametekwa wakawa wamerudishwa kwenye himaya yangu.
Siku mbili zikapita nikiwa ninaendelea kupata kuwatamua majina na kazi zao wanazo zifanya majini ninao waongoza.
Siku ya tatu alfajiri na mapema nikaanza kuwaagiza kazi husika ambayo mimi ninahitaji waweze kuifanya
“Agizo la kwanza ninahitaji muwalete hapa viongozi wote wa dini ambao hawamchi MUNGU wanamtukuza BARBATOS na wezake”
Majini wapatao hamsini nilio wakabidhi kazi ninayo hitaji wakanisujudia na kuondoka zao.
“Eddy mume wangu hao viongozi watakao letwa utawafanyaje?”
“Nitajua ni nini cha kuwafanya”
“Ila kuwa makini katika maamuzi yako”
“Usijali kwa hilo”
Ndani ya masaa mawili wakaanza kuletwa watumishi mmoja baada ya mwengine na wengine nikabaki nikiwashangaa kwa maana ni maarufu sana nchini na duniani.
Idadi yao ikazidi kuon-gezeka hadi wakafikia watumishi zadi ya elfu moja.Nikamuomba Rahma kwenda ndani aniache niwashuhulikie hawa wapumbavu
“WAKATI WA HUKUMU UMEFIKA” Niliisikia sauti ikiniambia masikioni mwangu
“Niwafanye nini?”
“WAWEKE KATIKA MAKUNDI NA KILA MMOJA ATAPATA ADHABU YAKE KUTOKANA NA UDANYANYIFU ALIO UFANYA KWA WATU”
“Sasa makundi hayo yawe vipi?”
“NITAKUWEKEA KILA MWENYE KUSTAHILI ALAMA YA X NAWE UTAWEZA KUCHAGUA NI NINI CHA KUWAFANYA”
Ndani ya muda mchache watumishi wadanganyifu wengi wakawa wamewekewa alama ‘X’ kwenye mapaji ya nyuso zao.
Katika kupita pita na kuwachunguza macho yangu yakakuta na baba mchungaji ambaye anashirikiana na Olvia Hitler na nimiongoni mwa waliotaka kuniangamiza,akatabasamu huku akitingisha kwa dharau nikatamani nimzabe kofi ila askari wangu akanishika mkono na kuionya nisifanye hivyo.
Hakuweza kuzungumza chochote kwani nimewaamrisha majini wangu kuwafunga kauli,hii ni kuepuka kuomba misamaha isiyo na msingi wa aina yoyote.
Nikawatazama kwa umakini wakiwa katika mistari ya kunyooka kama wanajeshi wa Adolf Hitler.
Gafla nikaanza kuona madonge makubwa mawili ya moto yakija kwa kasi kubwa kutoka anga-ni,Majini baadhi yanayo nilinda yakapaa angani kwenda kuyazuia ila wakashindwa na kuun-guzwa miili yao
“NI WAKATI WAKO KUPAMBANA WEWE KAMA WEWE,HAO WANAO KUJA NI MAJINI WABAYA AMBAO UMEWACHUKULIA WATU WAO” Sauti iliniambia
“Nifanye nini?”
“TUMIA FIMBO KUYAZUIA”
Nikainyoosha fimbo ya dhahabu niliyo powa,Mwanga mkali ukatoka mbela ya fimbo na kusababisha madonge ya moto kujibadilisha na kuwa katika hali upepo unaokwenda kwa kasi midhili ya kimbunga cha Katrina.
Upepe ukaanza kunizunguka kwa kasi na kujikuta nikiaanza kunyanyuliwa kwenda juu
“USIOGOPE ENDELEA KUPAMBANA”
“Mbona nakwenda juu sasa?”
Niliiuliza sauti ninayo isikia ila haikunijibu kitu chochote,Nikazidi kwenda juu na jinsi ninavyo-zidi kwenda juu ndivyo nguvu za mwili wangu zilivyoaanza kuniishia.Kufumba na kufumbua nikajikuta nipo katikati ya usawa wa bahari.
Nikaanza kwenda chini kwa kasi kuelekea yalipo maji
Fimbo yangu ikatoweka mkononi mwangu,nikaanza kuchanganyikiwa.
Nikashtukia nikigeuwa kichwa chini miguu juu na kuingizwa kwenye maji kwa kasi ya ajabu,Nikaendelea kupelekwa chini hadi nikajikuta nipo katika mji ambao siuelewi na watu waliopo ndani ya mji huu wanasura za kutisha sana.
Gafla upepo ukaniachia na ukabadilika na kuwa watu wenye mikono miine mikubwa inayo tisha.Vichwa vyao vikiwa na mapembe yenye ncha kali sana
Ikaninyanyua juu na kunidumbukiza kwenye kisima chenye giza totoro,Nikaanza kushuka kwa kasi kwenye kisima hichi pasipo kufika chini.
Sikuweza kuona chochote kwenye kisima kutokana na giza kali.Nikastukia nikipigwa kikumbo kikali kilicho nipeleka chini zaidi.
Galfa nikaanguka kwenye ukumbi mkubwa ulio jaa watu wasio eleweka na wakaanza kushangilia,Chakushangaza sikuweza kuumia sehemyu yoyote
“KARIBU KUZIMU BWANA EDDY,NIMEFURAHI KUKUONA KWA MARA NYINGINE”
Sauti ya Olvia Hitler ilinifanya nigeuke nyuma yangu na kumkuta akiwa amekalia miili ya majo-ka mawili makubwa yanayotoa moto midomoni mwao.
Akasimama huku akipiga makofi kwa dharau
“EDDY,HUWEZI KUPAMBANA NA MIMI KAMWE.MIMI SASA CHAGUA MOJA KUACHIA WATU WANGU HURU AU MKE WAKO RAHMA NA KIUMBE CHAKO HICHI NIVIANGAMIZE”
Olvia alizungumza huku akiwa amemshika mtoto mchanga ambaye sikuweza kumuona vizuri sura yake.Olvia Hitler akanyoosha mkono wake kwenye moja ya lango kubwa,ukafunguka na yakatoka majitu mawili yakutisha yakiwa na vishoka vikubwa na kuwafanya watu waliopo hapa kuanza kushangilia
Nikabaki nikiwa nikiyatazama majamaa yanayo kuja kwa mwendo wa taratibu ulio jaa vishin-do.Nikatazama vishoka walivyo vishika na kujikuta mwili mzima ukiingiwa na hufu
“NIMERUDI”
Nikaisikia sauti ambayo mara kwa mara huwa inanielekeza nini cha kufanya,
“Muda wote ulikuwa wapi hadi umeniacha nimekuja huku chini?”
“NILIKUWA NINAMANA YANGU”
“Maana gani?”
“MANAA KUU NI KWAMBA UJE KUICHUKUA DAMU YAKO KABLA HAWAJAKUDHURU ZAIDI”
“Sasa nitamchukuaje?”
“USIJALI KWA HILO”
Sauti ninayo zungumza nayo kidogo ikanipa matumaini ya kuweza huku kizimu nili-po.Nikastukia kuona watu watu wapatao sita,walio valia mavazi meupe wakiwa wamenizunguka.Mwanga mkali mweupe ukaanza kumulika katika eneo zima lililo kaa watu wanaoshangulia.
Mwanga ukasababisha miili ya watu hao kuanza kupasuka vipande vipande.Majiu yaliyokuwa yakinifwata nayo yakaanza kupasuka vipande vipande.
Olvia Hitler akabaki akiwa amenitazama kwa macho makali.Sikuweza kujua ni kwanini mwanga haukuweza kumdhuru,
“Mbona yule msichana audhuriki na huu mwanga”
“TUNAUA KWANZA WATU WAKE”
Watu walio nizunguka,wakaanza kazi ya kukimbia huku wakinizunguka kwa kasi kub-wa,Nikajashangaa nikianza kupanda kwenda juu hadi nikafika sehemu alopo Olvia Hitler,
“USIMUOGOPE MSOGELEE”
Nikaanza kupiga hata za taratibu huku nikiwa ninajiamini sana,Olvia Hitler akabaki akinitazama kwa macho makila
“MCHUKUE HUYO MTOTO,HAWEZI KUKUZUIA TUMEMFUNGA MWILI WAKE”
Nikaupeleka mkono wangu wa kulia alipo mtoto,Olvia hakuweza kunifanya kitu chohote zaidi ya kubaki akinishanga,Nikamchukua mtoto wangu,Jambo ambalo linaniogopesha juu ya huyu mtoto ni jinsi alivyo.
Sura yake haijaendana kabisa na mimi hata mwili wake si wakawaida kama watoto wengine
“Hivi huyu ni mwanangu kweli?”
“WEWE MCHUKUE HUYO MTOTO TUONDOKE”
Sikuwa na lakuuliza zaidi ya kumchukua mtoto,Nikajistukia nikivutwa nyuma,watu walio nizingira kwakanishika na kuanza kwenda juu.Tukiwa katikati kuna sehemu nikaiona ikiwa na moto mwingi sana
“Pale ni wapi?”
“NI KWENYE ZIWA LA MOTO,WALE WOTE AMBAO WANAFANYA MAOVU WANAPELEKWA KULE.NA SIKU YA MWISHO WA DUNIA MOTO UTAONGEZEKA MARA DUFU”
“Mmmmm naweza kwenda kupaona?”
“UNA MOYO WA KUVUMILIA?”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“KUNA HALI YA KUTISHA JE UTAWEZA KUVUMILIA?”
“Ndio”
“NITAKUZUNGUSHA KWA DAKIKA KUMI NA TANO TUU”
“Sawa”
Wakanichukua na kunipelea sehemu yanye giza kuwba,Galfa nikasikia kelele za ajabu ambazo siwezi kuzifananisha na kiumbe cha aina yoyote duniani.
Kila tunavyozidi kwenda mbele ndivyo jinsi kelele zilivyo zidi kuongezeka.Gafla nikamuona mnyama mkubwa sana mwenye pembe kumi na vichwa saba na mfano wake kidogo anaendana na chui na mdomo ya vichwa vyake vimefanana na Simba.
Mwili kigogo ukaanza kunitetemeka,Pembeni ya mnyama huyu nikaliona jijoka likubwa lenye vichwa kumi na mbili.
Unene wa mwili wake sikuweza kuupatia mfano.Mkiwa wake unaendana na mkia wa Tai
“HILI JOKA NDILO LINALO TAWALA HUKU KUZIMU NA LINA MAMLAKA KUBWA SANA NA NDIO SHETANI MWENYEWE”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikatamani kuwaambia kuwa tuondoke
“Akituona itakuwaje?”
“HATUONI KWA MWAANA SISI NI TOFAUTI SANA NA WAO,ILA ITAFIKIA KIPINDI WATATUO-NA”
“Leo?”
“HAPANA”
“Na lile jinyama?”
“Na lile jinyama?”
“LILE NDIO MKE WA LILE JIJOKA NA PALE HUWA ANAPEWA MAMLAKA NA LILE JOKA”
Tukaipota sehemu na kutokea sehemu ambayo kuna eneo kubwa lenye moto mwingi.Watu wengi wakiwa wamo kwenye bwawa la moto.
Miili yao inatobolewa na funza wakubwa walio nenepa sana na wana midomo inayo fanana na nng’e,Nikabaki nikijaribu kutazama kama nita-weza kujaa baadhi ya watu ila sikuweza kuzitambua sura zao kutokana ni nyeusi sana,Vilio vili-tawala katika kila sehemu ya bwawa la moyo
“Hawa nao wamefanya nini?”
“HAWA NI WALE WOTE WANAO ENDENDA KINYUME NA TARATIBU ZA HUKU KUZIMU”
“Kivipi?”
“KUNA WATU AMBAO WANAMUABUDU SHETANI,SIKU AMBAYO WANAVUNJA MASARTI YA SHETANI BASI HULETWA HUKU,NA HUWA WANAKUFA KWA SIKU ZAO WAO WENYEWE ILA SI ZILE ALIZO ZIPANGA MUNGU”
“Mmmmm,sasa ikifika siku zao za kufa inakuwaje?”
“WANATOLEWA HUMU NA KUPELEKWA KATIKA SEHEMU AMBAYO YUTAIENDELEA”
Kila sehemu ya ziwa la moto kunamiminika uji uji wa moto kutoka juu sana,sehemu ambayo ukiitazama huoni mwisho wake.Uji unafanana sana na uji wa volcano inayo toka kwa wingi.
“UNAWAONA WELE”
Mmoja wa watu wangu walio nizunguka aliunyoosha mkono kwenye upande wa kushoto wa sehemu tuliyopo.
Nikaona kundi kubwa watu wakiwa wanalia kwa vilio vya ajabu sana na miili yao ikidonolewa na mandege makubwa mawili,yenye sura za kutisha sana.Midomo yao ikiwa ni mirefu sana na inafanana na misumeno mikubwa ya kukatia mbao
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni