TANGA RAHA (40)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA...
Nikaanza kupiga hatua za kwenda nje gafla kwenye kona ya chumba akajitokeza bibi ambaye alinitibu kipindi nilipo okotwa msituni,sikustuka sana japo moyo ukanipasuka na kuyabadilisha utaratibu wa mapigo yangu ya moyoSASA ENDELEA...
“Shikamoo bibi”
“Marahaba......haikuwa ratiba yangu ya mimi kuja huku ila inanipasa kuja huku kukupa maagizo haya.”
“Mmmmm”
Niliguna huku nikimtazama bibi machoni mwake
“Kwenye lile shimo munalo lifungua mule kuna fugwa majini ambayo yakifuguliwa yatawadhuru walimwengu waliopo ndani ya huu mkoa hata nje ya mkoa kwa maana yanahasira na njaa kali na majini haya yanakula nyama za watu pasipo kuwa na huruma...”
“Ila kuna dhahabu nyingi ambayo ukiipata ni lazima uwe tajiri maisha yako yote wewe na kizazi chako ila sharti ni moja”
“Sharti gani?”
“Mupo wawili ila mmoja wenu ni lazima afa?”
“Nini wewe?”
“Ndio la sivyo mukifanikiwa kila kiumbe mutakacho kizaa au atakacho kibebe mke wako kitakufa tumboni mwake kwani hiyo ni kama sadaka ya majini hayo”
“Sasa bibi hakuna njia nyingine?”
“Njia nyingine ipo ila hiyo ni ngumu sana”
“Niambie tuu”
“Hiyo njia njingine ni kuweza kupata damu ya Ngamia mzee tena mwanamke.....sasa jiulize huyo Ngamia kwa hapa Tanzania utamtolea wapi?”
“Mmmmm sasa ni boara niachane na hio ishu”
“Huwezi kuacha kwa maana mumeshaanza ndio maana unazisikia kelele kama hizo huko nje hao ni watoto wa majini hayo ambao wanaweza kutoka kwenye lile shimo wakakupigia hiyo kelele ili ukawatoe wazazi wao”
“Sasa.....ahaaa bibi....”
“Na laiti ukiacha kuwafungulia matatizo ambaypo ulipia mwanzoni yataongezeka mara kumi zaidi ya ulivyo yapata”
“Ahaaa sasa bibi inakuwajee hapo”
“Ila usijali nitakupa dawa ambayo nitahitaji ujipake wewe na mwenzio usoni na mikononi pale mutakapo kwenda kukata ule mmnyororo”
“Je hao majini wakitoka itakuwaje?”
“Nitakupa fimbo ndogo yenye mamlaka ya kuwaamrisha kwa kila jambo utakalo wewe”
“Wapo wangapi hao majini?”
Bibi akakitazama kiganja chake cha mkono wa kulia sikujua anaangalia nini kisha akanitazama usoni
“Mmmmm wapo majini milioni moja,laki sina na hamsini”
Nikashusha pumzi kama nimetoka kukimbizana mbio ndefu
“Humo ndani walikuwa majini wachache ila kutokana na kuishi kwa muda mrefu wakazaliana na na kufikia hiyo idadi na kama wote hao ukishindwa kuwaongoza inakula kwako kwani watakutafuna wewe na uzao wako wote”
“Ohooo basi bwana bibi wewe nipe tuu dawa itakayo nisaidia kurudi zangu mjini na mke wangu ila si kuendelea na hiyo biashara mimi ni binadamu siwezi kuwaongoza viumbe wa ajabu kama hao”
“Mbona mfalme Suleima aliweza kuwaongoza majini na kuwaamrisha kwa kila kitu......Nahisi si mara ya kwanza kusikia neno hili kuwa nyota yako ni kubwa na inanguvu kubwa sana na inau-wezo mkubwa wa kuongoza chochote unacho kihitaji.........Pia majini hao watakusaidi kupamba-na na maadui zako ambao ukiwapa nafasi tuu ya kuiteka nyota yako huo ndio utakuwa mwisho wa maisha yako”
Nikatulia kama dakika tano nikimtazama bibi huku akilini mwangu nikiwaza ni jinsi gani nina-weza kufanya kazi hii ambayo tayari imesha nipa doa katika maisha yangu kwani sikuweza ku-tegemea kama ipo siku nitakuja kufikiria kumiliki jini
“Usiogope kwani kuna mambo mawili?”
“Kuifanya nchi na dunia kuendelea kuishi katika amani au kuifanya nchi kuingia kwenye matatizo makubwa na kila kiumbe aishie ndani ya nchi na nchi zote nazo zijua ndani ya ubongo wako watapata shida kubwa sana kwani ni lazima watafumwe”
“Mmmmm sasa mke wangu atakufa?”
“Hawezi kufa pale utakapo amua kuwaongoza hao majini ila ukikataa tuu atatafunwa”
“Bibi itakuwaje na hao majini wametokea wapi?”
“Wewe ndio utakuwa ni mridhi wa Mfalme Suleiman katika hilo hii ni baada ya karne nyingi kupita pasipo kupatikana kwa mridhi wake”
“Sasa bibi hawakuona mtu mwengine zaidi ya mimi kwa maana mimi kazi yangu ni ualimu”
Nilijitete nikimsikilizia jibu atakalo nipa bibi kwa maana ni hichi kikombe cha dhambi kilichopo mbele yangu ni zaidi ya kubebe sufuria lenye uji wa moto tena kwenye kichwa chenye upara
“Kuhusu ualimu wako weka pembeni....kilichopo hapa mbele yako ni kuangalia ni nini unapaswa kukifanya”
Nikasikia sauti ya kujinyoosha nyoosha kwa Rahma kitandani na kumfanya bibi kumtazama Rahma kisha akatabasamu
“Una kitoto kizuri ila usipo kiangalia kitatafunwa na hao majini ni kazi yako kukilinda”
“Daaaaa.....bibi inakuwaje sas?”
“Hapo hakuna ya itakukuwaje kazi ni kwako kulinda nchi,mke na kizazi chako”
“Nimekubali”
Bibi akatabasamu na kunipa kichupa kidogo chenye unga unaofana na poda nyeupe,Akanipa maelekezo yote yanayopaswa kufanywa kwenye dawa hiyo ambayo ni kuipaka usoni na miko-noni kwa kiasi kidogo,pia akanipatia kifimbo ambacho ni chakuongezea hao majini
“Kitu kingine nilitaka kusahau...usije kumuambia mke wako kuwa kwenye hilo shimo kuna ma-jini kwa maana kama unavyo wajua wanawake wenu wa kisasa walivyo waoga na ataaribu kazi yote namwisho wa siku katatafunwa mbele yako”
“Sawa bibi.....ila ngoja kwanza ile pete yangu imepotea”
Bibi akanigeukia na kunitazama kwa macho makali yaliyo jaa mshangao
“Umeipeleka wapi?”
“Anivua mke wangu”
“Utakufa kwa ujinga wako nisubirie”
Bibi akaondoka kwa njia aliyo jia na mimi nikarudi kitandani huku kelele za kengele zikinyama-za kimya.
Akili nzima ikawa imevurugika kila nilicho kiwaza hakuna ambacho nilikifikia maamuzi katika mawazo yangu.Baada ya muda bibi akarudi na nikanyanyuka kitandani na kumfwata alipo simama na akanionyesha pete yangu
“Umeipata wapi?”
“Si mulikuwa mumeitupa kwenye hizo bustani zenu kwa ujinga wenu”
Bibi alizungumza huku akinivalisa kwenye kidole ilipo kuwawepo
“Kumbuka hao majini hawaitaji kelele zozote za binadamu hadi ukiwaweka chini ya mamlaka yako ndio utakuwa huru kuwaongoza la sivyo watawatafuna”
Bibi akamaliza na kuondoka na kuniacha nikiwa na sinto fahamu hata kujilaza kitandani nilijilaza kama mgonjwa.Hadi kuna pambazuka sikupata usingizi wa aina yoyota.
Rahma akanigeukia na kunitazama kwa macho yaliyo jaa usingizi huku akipiga miyayo
“Mume wangu umeamkaje?”
“Nimeamka powa tuu”
Nilizungumza kinyonge kwani kazi niliyo nayo si ndogo,Rahma taratibu akajisogeza kifuani kwangu na kunikumbatia na kuanza uchokozi wa hapa na pale na kuufanya mwili wangu kunisisimka.
“Mume wangu naitaji tutafute mtiti wa asubuhi asubuhi”
Rahma alizungumza huku akiaendelea na uchokozi ambao moja kwa moja ninajua ni ugonjwa wangu,ndani ya dakika kadhaa tukawa ndani ya dimbwa zito la mapenzi hadi tunamaliza mechi yetu kidogo nikawa kwenye amani
“Alafu baby kuna kitu nilisahau kukuadisia?”
“Kitu gani?”
“Kipindi ambacho nilipigwa risasi na baba si nilikuwa nina ujauzoto japo mima ilikuwa ni chan-ga?”
“Ehee”
“Basi yule Olvier Hitler alikichukua kile kiumbe chenye changu na kukiingiza kwa msicha mwengine amabaye ni jini wakidai watanirudishia tumbo langu litakapo pona”
“Mamaa weee sasa ni kwanini na wewe ulikubwali?”
“Ahaa baby unadhani ningekataa vipi wakati watu wenyewe wale ni majini”
“Mmmmm sasa mke wangu aaahaa”
Ikawa ni taarifa nyingine mbaya kwangu kwa maana moja ya njia mbazo Olvia na majini wake wanataka kunifanyia ni kuipata kwanza damu yangu.
Na moja kwa moja endapo kiumbe changu kitazaliwa nilazima wataitumia damu ya mwanangu kuiangamiza dunia
“Sasaw wewe unadhani huyo mtoto atakuwa wetu kweli?”
“Hata mimi sijui mume wangu ila tumuachie MUNGU kwani si tutamzaa mwengine”
“Laiti ungejua kinacho endelea wala usinge zungumza hilo”
“Ni nini kinacho endelea”
“Utajua siku ila si kwa sasa cha msingi hapa ni kumtafuta mwangu kwa juhudi zangu zote”
“Mmmmm utampataje wakati wale ni majini na wewe ni mwanadamu?”
“Nitajua tuu jinsi ya kuwapata”
Nikanyanyuka kitandani na kuingia bafuni na Rahma akafwatia kwa nyuma na sote tukaofa ba-funi na kuvaa nguo zetu ambazo ni kauka nikuvae kwani hatuna nguo nyingine za kubadilisha zaidi ya makti tuliyo yakuta ndani ya hili jumba.
Tukashirikiana kupika kifungua kinywa na baada ya kumaliza kila mmoja akawa tayari kwa kazi.Nikakimbia chumbani na kuchukua kichupa chenye dawa pamoja na kifimbo changu na kurudi sebleni na kumkuta Rahma akiwa ameshika kishoka.
Nikatoa unga kidogo kwenye chupa na kujipaka usoni na mikononi kama alivyo niambia bibi
“Ni nini hiyo?”
“Wewe tulia nikupake”
Nikachuka tena unga kidogo na kumpaka Rahma kwenye uso na mikono yake na sote tukatoka nje.Tukafika kwenye sehemu lilipo shimo na kulikuta kama tulivyo liacha
“Hivi Eddy kwa mfano humu tunakuta mahela cha kwanza tuakwenda kuishi wapi?”
“Mbinguni”
“Jamani Eddy ndio jibu gani hilo mume wangu?”
“Niikuwa ninakutania mke wangu,tutaishi popote ambapo wewe utahisi panafaa”
“Mimi nataka tuishi kwetu Dubai”
“Hakuna shida mke wangu”
Rahma akakaa pembeni na mimi nikaanza kazi ya kuukata mnyororo kwa kutumia nguvu zangu na kila ninapo ukata ndivyo jinsi unavyo katika,nguvu nilizo nazo leo ni tofauti sana na nguvu nilizokuwa nazo jana kwani leo ninanguvu nyingi sana kupita maelezo.
Mnyororo ukakatika na kumfanya Rahma kuanza kupiga makofi akifurahia
“Baby leo unanguvu nyingi kama John Cena”
“Kwenda huko nyoo tusaidine kuufungua huu mfuniko”
Rahma akanifwata na tukaanza na kazi ya kuuvuta mfuniko huu ambao ni mzito sana na kuto-kana na kuwa na kutu nyingi ukasababisha kushikana kwenye maeneo ya pembezoni kwa mfu-niko huo.
Taratibu yukaanza kuufunua kwenda juu,tukiwa tumeufunua kwa kiasi fulani tukasikia sauti ya Mzee Ngoda ikutuita huku akija katika eneo tulilopo
“Munafungua nini wanangu”
“Njoo utusaidieee”
Nilizungumza kwa sauti ya kujiminya kwani mfuniko ulituzidi nguvu,Mzee ngoda akajiingiza katikati yetu na kutusaidia kuufungua mfuniko na kwa pamoja tukafanikiwa kuufungua.
Gafla tukastukia kumuona Mzee Ngoda akirushuwa juu kama kifaranga kilicho nyakukiliwa na Mwewe mwenye njaa kali na kitendo cha kutua chini hakuwa na kichwa na damu nyingi zikawa zinaruka kila sehemu na kumfanya Rahma kupiga ukulele mkali
Nikabaki nikiutazama mwili wa mzee Ngoda jinsi unavyo rusha rusha miguu,Sauti kali nikaisikia kwenye masikio yangu ikiniambia
“Mmoja wenu ni lazima afee”
Nikayakumbuka yalikuwa ni maneno ya bibi,kwa haraka nikamuwahi kumziba mdomo Rahma.
“Shiii nyamaza”
Nikaendelea kumziba mdomo Rahma kwa nguvu kwa kutumia kiganja cha mko-no.
Tukayashuhudia majini yakitoka na kulizunguka eneo tulilopo sisi huku wakiwa wanaelea elea angani.Nikakitoa kifimbo mfukoni na kuwanyooshea majini yaliyojaribu kwenda mbali,
“RUDINI HAPA”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali na majini hayo yakatii,hadi na mimi nikaanza kushan-gaa.Rahma akanikumbatia kwa nyuma,mwili mzima ukiwa unamtetemeka mithili kama ame-pigwa shoti ya umeme.
Eneoa la anga zima katika eneo tulilopo limefunikwa na majini haya am-bayo ni mengi sana na yana sura za kila aina
“Tunakushukuru sana kwa kututoa”
Niliisikia sauti kwenye masikio yangu ambayo ni tofauti sana usikiaji wake kama tulivyo sisi wanadamu,Kwani sauti niliisikia ndani ya masikio yangu na si kama ile inayo ingia kwenye ma-sikia yangu.
Nikawatazama kwa umakini na kuwashuhudia wakiwa akatika makindi tofauti to-fauti,Wazee sana,wazee kiasi,vijna na watoto
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni