Notifications
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…

MUUZA CHIPS (84)

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA THEMANINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Aliuliza mama sarah huku akitoka nje ili aulize vizuri… Wakati huo miriam kimyaa

“si nakuuliza we mtoto, umefuata nini huku”

Mama sarah alikuwa anachimba mkwara lakini hata yeye alikuwa anaona aibu kukutwa ndani tena peke yake kwenye chumba cha kijana ambae hajaoa..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
“lakini mamdogo, kwani na wewe hapa umefikaje, mana mimi kuna pesa nimekuja kuichukuwa huyu kijana aliondoka nayo”

Miriam alivunja ukimya juu ya mama sarah na hata mama sarah kuskia hivyo ikabidi naye awe kimya, mana chidi ndio mpishi mkuu wa chipsi katika hoteli ya akina miriam MIRAS HOTEL,

“kwani hio pesa alishindwa kuileta kesho”

Mama sarah aliongea hivyo lakini chidi akaingilia kati,

“skia mamy,.. Hio pesa nilipewa mimi nikanunue maandalizi ya chipsi hivyo kutokana na kuchoka nikawa sijaenda, na kesho pia sidhani kama nitaenda na ndio maana katumwa aje kuchukuwa”

Aliongea chidi na kumaliza mzizi wa fitina.. Hata mama sarah mwenyewe katulia baada ya kuyaamini maneno ya chidi,

“na huyu mtoto ni nani”

“huyu ni mdogo wangu kabisa, anaitwa halima”

“ok sawa.. Vp si tayari umeshamaliza mizunguuko yako”

“ndio, tayari nimeshamaliza”

“ok.. Naondoka zangu”

“sawa boss, tutaonana kesho”

Mama sarah alishagunduwa kuwa hapa hapakuwa na la ziada mana kama ni kuachwa njiani kimapenzi keshaachwa na kwasasa kufanya mapenzi ndani ya hii nyumba kumeisha kwasababu kuna mtoto mdogo humo ndani hivyo itakuwa ngumu mama sarah kuja kufanyia humu labda wakutane gesti..

Basi chidi alimkaribisha miriam ndani lakini miriam alikasirika sana kwa kitendo cha kumkuta huyu mama humu ndani,

“yupo kama nani? Na kama kamseidia tu kumleta pale hotelini ndio sababu ya kuja mpaka nyumbani kwake?”

Miriam alijiuliza maswali kipeke yake peke yake,..

Basi walipoingia ndani miriam alikuwa kachoka sana lakini kama mwanamke alijitahidi tu kupanga chumba cha chidi, lakini chidi anashindwa kuelewa, kwanini miriam kaja huku anataka nini… Chidi alikuwa akijiuloza maswali mengi sana, lakini mara miriam kashindwa kuvumilia na kumuuliza chidi

“hivi omary, huyu mwanamke kaja kufanya nini huku chumbani kwako”

Aliuliza miriam huku akikaa kitandani ili kupata majibu

“lakini mamuu, si unajua kuwa huyu ndie alioniunganisha na kazi pale kwenu”

“sawa najua hilo, lakini swala lile sio lazima aje mpaka huku kwako, ilitakiwa atende wema aende zake, sasa anakuja kufanya nini huku jamani”

Chidi aliona miriam atagundua kitu hivyo akamsogelea kisha akaanza kumshika shika

“we omi kuna mtoto bwana”

Chidi akaacha kufanya hivyo baada ya kuambiwa kuna mtoto karibu..

“afu omi, huyu mtoto atalala wapi sasa”

Hilo nalo lilikuwa jambo la msingi kweli

“si tutalala nae hapa hapa”

“nyoooooooo kwenda uko… Ina maana usiku woote huo tutalala tukiwa tumetulia tu”

Miriam aliongea hivyo kumaanisha kuwa usiku atataka ahudumiwe, afu huezi amini miriam hajawahi kuguswa,… Kama unakumbuka sababu ya kutokuguswa walikuwa ni wasagaji na rafiki yake hivyo imewapelekea kutotamani mwanaume, lakini sarah yeye aliwahi kukutana na wanaume lakini miriam hajawahi hata siku moja yaani utamu wa uume yeye haujuagi..

Sasa hapo chidi ndio akapata jibu kuwa miriam kaja kwake ili amfanyie huduma ya upasuaji wa sehemu muhimu,

“sasa ngoja nikachukue kitanda fasta”

Aliongea kijana chidi huku akiamka..

“sasa ukichukuwa kitanda atalala wapi”

“si hapo kwenye korido”

Unajua nyumba ya chidi ni kubwa.. Yaani kapangisha dabo rumu, ambayo ina choo humo humo bafu humo humo, yaani ipo kama kaselfu flani hivi kakijanja,.. Hivyo kuna kachumba kengine kadogo ambako kamewekea masofa.. Hivyo chidi alitoka na kwenda mjini kununua kitanda kwa ajili ya mdogo wake, ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni…

Sasa tukija huku kwa akina sabra, jasmini alikuwa akimfokea sana mdogo wake kwa kumuhisi kuwa labda yeye ndio kamwambia chidi kuwa mdogo wake yupo hatarini na ndio maana kaja kumchukuwa

“sasa mimi nimemwambia saa ngapi na wakati tulikuwa wote”

Aliongea sabra huku akionyesha msistizo kwa kulia kabisa

“sasa kajuaje kama tutakuja kumchukuwa, au yeye ni nabii kaota… Acha ujinga wewe”

“lakini dada mimi sijamwambia mtu”

“kajuaje sasa”

“mi sijui”

“nina hofu na wewe sabra”

“wala usijali dada mimi nipo na wewe”

Aliongea sabra kana kwamba yeye hayupo tofauti na yeye,…

“unajua wewe hujui baba aliniambia nini na ndio maana unafanya ujinga mkubwa sana… Tutaishi kimaskini kama usipokuwa makini”

“lakini mimi sijui na hujaniambia, mana baba alipofariki alikuachia usia wewe”

Aliongea sabra huku akitamani kuijua hio siri alioambiwa na baba yake… Mana sabra yeye alikuwa shule hivyo usia hajaachiwa sabra bali aliachiwa jasmini,..

“sikiliza sasa… Leo nataka nikuambie ukweli juu ya baba alichoniambia mpaka kufika hatua hii ya leo”

Aliongea jasmini ili kumhakikishia mdogo wake….

Sasa tukija huku kwa akina chidi wakati chidi ndio karudi kutoka mjini kununua kitanda cha halima ambacho ni kidogo na ni spesho kwa watoto kama halima, kila kitu kiliwekwa sawa na mambo yakawa mazuri,… Wakati huo chidi akiandaa sehemu ya kulala ya halima, huku upande wa miriam alikuwa ndio kwanzaa mboga inaiva,… Kwa mara ya kwanza chidi anaona raha ya kuwa na mke ndani, mana nyumba leo imewashwa moto na chakula kinapikwa, hakuna raha kama kuoana watu mnaopendana kwa dhati,.. Binafsi chidi alijiskia raha sana kwa kuona miriam alivyoenea vizuri katika jiko.. Toka nyumba hio ihamiwe haijawahi kupikwa hata siku moja, chidi akirudi keshakula kwa mama ntilie hivyo hana muda wa kupika,.. Na uzuri ni kwamba chidi alikuwa na stoko ya chakula hivyo hata miriam hakuona tabu kupika,… Wakati huo halima alikuwa akisuuza vyombo mana vilikuwa ni vya kusuuza vumbi vumbi kwasababu havikuchafuka kwakuwa hakukuwa kukipikwa ila kila kitu kilikuwepo,… Chidi alitamani akamkumbatie pale jikoni lakini halima alikuwepo hivyo subira ilifanya kazi yake,

Sasa tukija huku kwa mama yake na miriam, ikiwa ni mida ya saa mbili za usiku… Mama alikuwa hata kula hali mana miriam hakuepo nyumbani,..

“uyu mtoto yupo wapi mama miri”

Aliuliza baba yake miriam huku akimuangalia sana mke wake…

“yaani hapa sina hata raha baba miri,.. Sijui mwanangu kapatwa na nini huko”

“lakini si ulikuwa nae kazini wewe”

“aliondoka na hakuniaga.. Na pia gari yake ipo kule kazini”

“sasa kaenda wapi…. Au yupo kwa rafiki yake yule nani yuleeeee….. Aahhh nani yule rafiki yake Mweupe Mweupe hivi ana kimwili hivi nani yuleeeee”

“Sarah”

“Enheeee sio atakuwa huko kweli”

“sidhani hebu ngoja nimpigie”

Yaani miriam kutofika nyumbani mapema kwao lilikuwa ni tatizo kubwa sana katika familia hio, afu ukizingatia ni huyo mmoja tu…

Miriam yeye hakuwa na tabia ya kuchelewa nyumbani, yaani akitoka kazini ile saa 11 au 12, moja kwa moja mpaka nyumbani na akitoka nyumbani moja kwa moja mpaka kazini.. Hivyo saa mbili hii wazazi wake wanaona kama vile ni saa 8 usiku, mana sio mazoea yake

“eeee mwanangu hujambo”

“sijambo mama shkamoo”

“marahaba… Ebu nipe niongee na miriam mara moja”

Mama alitumia akili ya kuto kuuliza kama yupo au hayupo badala yake alitaka aongee nae…

“mama mbona miriam hayupo huku… Hajaja tena nina muda sjamuona”

“jamani sarah, mwenzio hajarudi nyumbani mpaka saa hizi”

“lakini mama ukimpigia simu yake hapokei au”

“simu yake haipatikani kabisa”

“mmmhhh lakini huku sipo nae”

Mama miriam alikata simu kwa hasira huku akiwaza mtoto wake yupo wapi…

“au kazini atakuwa kakwazika nini”

Aliuliza baba yake miriam na kumfungua macho mama miriam

“aaaahhhhh ni kweli… Kuna kijana maskini anamnyemelea miri.. Sasa nataka nikatishe huo ujinga kwa kumwambia miri aende Uingereza kimasomo….. Nadhani ni hivyo”

Sasa mama ndio anapata picha kuwa huenda jambo hilo ndilo liliomfanya asije nyumbani…

“huyo kijana ni nani”

“ni mfanyakazi wetu”

“mmmhhhh bwana nyie mtajuwa wenyewe lakini nataka mtoto wangu arudi”

Baba hataki kujua kama kapendwa na maskini au tajiri lakini mtoto wake arudi,. Heeee chidi analo hilo… Sasa mama miri akavuta kumbukumbu ya chidi alikujaje pale kazini

“ooohhh yes, aliletwa na mama sarah… Ngoja nimpigie”

Oooohoooo na mama sarah ndio mtu wa kwanza kujua miriam alipo, mana walikutana kule ndani… Mama miri kavuta simu na kumpigia shostito wake kumuuliza kuhusu chidi

“haloo mama sarah habari yako”

“nzuri tu mama miri habari yako”

“sio salama sana”

“kwanini tena mama miri”

“nina shida na yule kijana, na naomba kesho unipeleke kwake, hawezi nitoroshea mwanangu kisa mapenzi”

“Whaaaaat??? Ina maana miriam na yule kijana ni wapenzi”

Mama sarah kaamshwa madudu yake, yaani mtu amhudumie mipesa kedekede nyumba analipia yeye, afu leo ana mpenzi mwingine, tena mbaya zaidi mpenzi mwenyewe ni mtoto wa rafiki yake

“ndio.. Wanaanza anza sasa ndio nataka niyakatishe miriam aendelee Uingereza… Hivyo nataka kesho nichukue jeshi la polisi tuende hapo anapoishi huyo kijana,… Mama sarah nitakupa kiasi chochote cha pesa lakini nijue alipo huyo kijana.. Sawa mama sarah”

Mama sarah kuskia kuna kiasi chochote cha pesa, weeeeeeeeeee alitokwa na macho kwa kuskia pesa…

“Mama sarah”

“Abeeeee”

“mbona kimya shosti wangu… Au kama kesho upo bize hebu nitajie namba ya nyumba anayoishi huyo kijana kesho niende,.. Atasema mtoto wangu yupo wapi”

Aliongea mama miriam huku akionekana kuwa na hasira na kijana chidi,… Sasa mama sarah kabla hajakubali aliwaza mengi sana kuhusiana na kijana chidi

“mbona huyu mtoto ana balaa hivi, na kila ishu inayomuhusu lazima nipewe pesa,.. Sasa hii itakuwaje”

Alijiuliza mama sarah katika moyo wake, lakini aliona potelea mbali

“lakini mama miri, yule kijana mimi aliniomba tu kazi wala sijui anapoishi”

“ooohhh shit, sasa mama sarah kwanini umpe kazi mtu ambae humjui,.. Sasa kama angeondoka na mabilioni ya fedha ingelikuwaje sasa… Ok sawa basi kesho”

Aliongea mama miriam huku akiwa na hasira juu ya kukosa njia ya kuanzia…

“mama miri, wewe ndio mwenye makosa lakini”

“jamani baba miri sasa mimi kosa langu ni lipi”

“kwanini umwambie aende Uingereza, kwani mimi nilivyokuoa kwenu ulikuwa tajiri wewe, au mimi nilikuwa tajiri?.. Si tumezipata tukiwa wote, sasa kwanini wataka matajiri ili iweje… Mimi nataka nimuone mtoto wangu”

Baba alikuja juu kuhusiana na swala hilo, lakini ghafla mama miriam anacheka huku akimsogelea mumewe baba miriam kisha akamnong’oneza kitu katika skio lake,.. Lakini maneno hayo yalionekana kuwa matamu mpaka baba miriam alicheka na kusema..

“kumbe una akili wewe”

Sasa je ni nini alikiongea mama miriam mpaka baba miriam kacheka na wakati alikuwa mbogo muda si mrefu,.. Usikose ili kujua huo mnong’ono wa mama miriam uliomfurahisha baba miriam..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
51 Muuza Chips Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni