MUUZA CHIPS (99) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 25 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (99)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA TISA
ILIPOISHIA...
"nilijua bado upo na mawazo ya kuwa na sarah, binafsi pia sitaki uendelee kuwa na sarah"

"sio sarah tu, ni mtu yeyote yule kuanzia wewe"

"we mshenzi nini wewe… Unaongea ujinga gani uo"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"kwaio we watakaje… "

" nakwambia lazima umuache sarah lakini kwa mimi.. Hata uoe nitaibia tu iwe isiwe"

Mama sarah aliwasha gari na kurudi kule tulipotoka,

Lakini chidi akiwa ndani ya gari simu yake iliita ghafla, kucheki jina alikuwa ni boss, akajua enheee kimeshanuka sasa,

"haloo boss"

Aliipokea kijana chidi huku akiwa na hofu mana kaondoka bila kuaga

"uko wapi"

"nakuja boss, kuna mahali nilitoka kidogo"

"ok, ebu wahi huku nyumbani"

"nyumbani au kazini boss"

"nyumbani kwangu"

"sawa boss"

Chidi alishangaa kuitwa nyumbani kwa boss, hakujua kuna nini huko nyumbani,

Tukija huku kwa akina jasmini, tunamuona sabra anahangaika sana katika nyumba yao na hatujui alikuwa anatafuta nini,

"we umeanza kuwa chizi siku izi ee"

Aliingea jasmini ambaye ni dada yake, mana sabra alikuwa akizunguka nyumba nzima

"dada, musa yupo wapi"

Aliuliza sabra kwa dada yake,… Musa ndio yule mtoto wa chidi, anaitwa musa, sasa sabra toka asubuhi haoni mtoto akilia wala nini,..

"heeeeeeee ivi una akili wewe,.. Kwani hujui leo ni tarehe ngapi"

"najua leo ni tarehe 7 mwezi wa 7, lakini sasa mbona simuoni"

Lakini kabla jasmini hajasema mtoto yupo wapi, ghafla simu yake inaita, kucheki ilikuwa ni namba ambayo haijaseviwa lakini anaijua

"haloo boss"

Aliongea jasmini baada ya kuipokea simu hio

"mtoto wako kakataliwa na zachesi… Kwasababu kuna masharti umeyakosea, Anahitaji mtoto mwingine kwa kafala"

"mungu wangu weeeeee…. Kwahio nije kumchukuwa huyo"

"haiwezekeni tena, mtoto alishakufa siku nyingi sana, na zachesi kasema huyo ndio kafala juu ya masharti mliokosea"

"mungu wangu mimi nimekosea sharti gani jamani"

Jasmini alianza kulia mana mtoto hana na bado kafala halijafanikiwa

"kwa sasa hatakiwi kumiliki kampuni yeyote ile na nyumba unayoishi unatakiwa kuondoka haraka mpaka hapo utakapo pata mtoto mwingine, na zachesi anataka mtoto wako tu na siii damu nyingine, au ukikosa mtoto kama una ndugu uliozaliwa nae unaweza kumtoa zawadi"

"hapana siwezi tena… Lakini huezi ongea na Zachesi anipe muda"

Jasmini alitamani kupewa muda zaidi ili kuitafuta zawadi ya zachesi,..

"amri yake hua haigeuki mara mbili mbili"

"sa… Sa… Sawa… Lakini sisi tumeharibu sharti gani"

"mumetembea na mwanaume mmoja"

Jasmini kuskia hivyo hata simu ilimdondoka mpaka chini huku sabra akiwa katulia tu

Simu ilikata baada ya kudondoka chini

"we mpumbavu, ina mana ulishiriki mapenzi na mume wangu Ibrahim"

Aliongea jasmini huku akimsogele mdogo wake,…

"hapana dada, mimi sijatembea na Ibrahim,… Ni chidi"

"kumanina mshenzi wewe, kwanini usingesema sasa mbwa wewe, mpaka tumekiua kiumbe cha watu, kwanini lakini"

"lakini dada mimi sikujua na hukuniambia kabla"

Sasa kumbe sharti la tatu kama unakumbuka siku ile jasmini alimwambia sabra masharti matatu, lakini sharti la mwisho, sabra aliguna, alipoulizwa kwanini kaguna, sabra alikataa kuwa hakukuwa na kitu, sasa kumbe sharti lilikuwa ni hivi, hawaruhusiwi kutembea na mwanaume mmoja, awe ni mume au hata kijana yeyote yule,.. Na ndio mana kuna siku chidi alipewa milioni 50 na jasmini ili akae mbali na sabra, kumbe alikuwa akiepua sharti hilo, lakini sasa sabra alivyo hasikii na pia hakujua, alimtafuta chidi mpaka wakafanikiwa kufanya mapenzi, na ndio mana siku ile sabra aliguna, kwasababu kama ni sharti hilo tayari keshaliharibu, ila hakusema kama kaharibu…

"we mwana kumanina mbwa wewe, haya katafute mtoto sasa umlete hapa,.. Kwanini husikii sabra, sasa ona kiumbe cha watu kimekufa bila faida… Kafiri wewe, haya sasa hatuna kampuni wala nyumba na kila mtu ajue anapokwenda… Mbwa wewe"

"heeeeeeee dadaaaa, unasema hatuna kampuni"

"nitoleee ushenzi wako mimi… Toka apa"

Jasmini alikasirika mpaka macho yamekuwa mekundu mana kafeli kila kitu, we ulifikiri atatoa wapi mtoto kwa sasa hivi??….

Tukija huku kwa akina miriam chidi akiwa ndio anafika katika jumba hilo la kitajiri,… Lakini kabla hakuingia alikutana na mdogo wake halima akiwa na miriam, mana toka walipopatana halima alienda kuishi kwa akina miriam,..

"waaoooo jamani mume wangu"

Aliongea miriam baada ya kumuona chidi ndio anafika

"weeeeee mamuu tulia, mama yako akiona je"

"heheheeee…babuu ondoa shaka, sasa hivi mambo ni poa tu"

Aliongea miriam huku akimshika chidi na kuingia nae ndani

"shkamoo kakaa"

"marahaba ujambo mamii"

"sjambo"

Chidi aliingia mpaka ndani, lakini alishangaa kukutana na watu wengi sana hapo ndani, wamama wakiwepo wakutosha na baba yake miriam alikuwepo, chidi alisalimia mmoja baada ya mwingine kiheshima zaidi

"karibu sana kijana"

"ahsanteni sana mama zangu"

Chidi hakujua kinachoendelea hapo sebuleni,

"kijana… Kwanza naomba mnisamehe wewe na mwenzio miriam"

Aliongea mama Miriam tena kwa heshima kubwa tu,..

"hakuna shida mamy nilishasamehe muda tu"

"kiukweli kukuwakataza kwenu sio kuwa nilikuwa sipendi mahusiano yenu, bali nilikuwa nataka nijue mnapendana kweli au laa,.. Nakumbuka siku ile mtoto wangu katoroka sikujua kama yupo kwako, lakini nakumbuka kesho yake ulikuja na begi kazini,.. Nilikutuma ukanunue viazi ili nikague begi lile.. Nilifurahi sana kuona nguo zile zilikuwa ni za miriam na nilijua hilo kwasababu niliikuta kadi ya benki ya miriam… Na ndio mana sikutaka kufatilia sana mana nilijua upo nae,.. Na sikukueka sero kwa kukutesa, bali kuna hali nilikuwa naipima… Mpaka hapo nimegundua unampenda sana mtoto wangu na hujampendea kwa ajili ya mali zake… Mpaka sasa nimemaliza uchunguzi wangu.. Kilichobaki sasa hivi nataka tukaone mazingira ya nyumbani kwenu huko kijijini"

Mama Aliongea mengi na yupo tayari mtoto wake aolewe na chidi, na chidi kafurahi sana kuskia hivyo, lakini kichwa kilianza kumuuma baada ya kuambiwa waende kijijini kwao wakaangalie mazingira ya hapo nyumbani kwao.. Sasa chidi akifikiria nyumba yao ilivyo imetoboka toboka ukutani yaani kiufupi maisha ya kijijini kwao hayakuwa mazuri…

"chidi… Rashidi…. We kijana"

"Ennh,… Eehhn.. Sawa mama sawa"

Chidi alikuwa katika dimbwi la mawazo mazito sana kwasababu ya mazingira ya nyumbani kwao…

"wala usiwe na wasiwasi juu ya hilo, kikubwa tunataka familia yenye upendo… Na huko huko ndiko tunakwenda kuwafungisha ndoa,… Kazi kwenu na maandalizi yenu, nasi tunaanza kukusanya watu wa kwenda nao huko"

Chidi alipotoka hapo kwenye kikao cha ghafla, kichwa chake kilikuwa hakifanyi kazi… Kitu cha kwanza chidi alimpigia simu kaka yake

"haloo broo shkamoo"

"marahaba ujambo"

"sjambo… Sasa broo, ebwana kesho tunakwenda nyumbani, nakwenda kupata mke sasa"

"aahhh sasa mbona muda ule tuliongea hukuniambia"

"yaani broo hilo jambo ndio nimeambiwa sasa hivi na mama mkwe, mana mapenzi yetu na huyu mtoto wa kike yalikuwa ni ya kuiba iba, sasa leo ndio tumepewa ruksa kamili, na kesho tunakwenda tanga"

"aahhhh sasa mimi nitawahi vipi ili nijiandae"

"mnatakiwa mje sasa hivi huku arusha ili tuondokeni wote"

"sasa tutakuja na nini"

"pandeni ndege,.. Tumieni ule mtaji wenu afu nitakurudishia ukifika huku"

"sawa dogo tunakuja sasa hivi"

Basi Ibrahim nae kwenye mambo ya ndege, aahh anayafahamu sana mana si alikuwa boss katika kampuni za akina jasmini,..

Sasa miriam ndio alikuwa na furaha zaidi kuliko hata chidi,.. Miriam alitoa gari yake ili waende mjini kujiandaa na safari hio

Wakiwa wapo duka la wana harusi wakiwa wanachukuwa mavazi ya uwana harusi, lakini ghafla simu ya chidi inaita… Kuangalia anaepiga alikuwa ni sarah

"halooo"

"mume wa mtu sumuuu… Naskia unakwenda kuoa sasa"

Aliongea sarah tena yalikuwa ni maneno ya kejeli juu ya ndoa yao,..

"sarah naomba tueshimiane sawa"

"akuheshimu nani… Univishe pete mimi afu ukamuoe mwingine??.. Mi nasema hivi haiwezekani yaani lazima nihakikishe hufanikiwi"

"sawa tutaona sisi"

Sarah alikuwa akiwapiga mkwara akina chidi na miriam eti ndoa yao haitotimia

Wakati huo ndugu wa akina miriam nao wapo maandalizini, kumbe mama alishatoa taarifa muda mrefu kuhusiana na ndoa hio, ila sema alichobakiza ni kumalizia kwa chidi tu,.. Lakini hofu ya chidi ni kule kwao jinsi kulivyo kwa kimaskini, heeee anahisi anaenda kutia aibu kubwa sana, mana kajumbe chenyewe ni kajumba ka matofali alafu pia bati zenyewe zimechakaa…

BAADA YA LISAA LIMOJA KUPITA

Miriam na chidi wakiwa wapo geto kule wakiyafurahia mavazi walio yanunua ya bwana hatusi na bibi harusi, na mpaka hapo pesa inatumika ni pesa ya mama miriam mana alisema atagharamia kila kitu,.. Lakini wakiwa hapo geto, simu ya chidi iliita kuangalia jina alikuwa ni kaka yake,..

"haloo broo, vipi"

"aisee tumeshafika hapa lakini hatukuoni sjui upo wapi"

"mumefika Airport"

"ndio.. Nipo hapa mapokezi na shemeji yako"

"ok.. Ngoja nije sasa hivi"

Chidi alitoka hapo na miriam kuelekea kisongo ambako kuna Airport,

"kaka yako keshafika Airport"

"yes.. Kafika na mke wake"

"waaooooo natamani kuwaona yani we acha tu babuu"

Aliongea miriam huku akifurahi sana kwa kuiona familia ya chidi, tena ndio wamekuja wakati muafaka haswaaaa

Salma na mume wake mtarajiwa ambaye ni Ibrahim,…

"baby… Shem mbona anachelewa hivyo"

Aliingea salma huku akiwa na shauku ya kumuona shemeji yake ambae ni rashidi,..

"anakuja, sema atakuwa na furaha sana, kwasababu ndio anataka kufunga ndoa hivyo"

"wooooohhhh, sasa kwanini na yakwetu tusifunge hapo hapo"

"mmmhhhh kiukweli wacha aanze yeye japo mira zetu za kisambaa haziruhusu mdogo kuoa kabla ya mkubwa"

"eeeeeeeeee na nyie mna mambo"

Ghafla wanasikia sauti ya honi mbele yao, alikuwa ni chidi keshafika Airport ila alikuwa hajamuona salma vizuri mana alimuacha akiwa na mwili mdogo na sasa ana mwili mkubwa yaani ni mmama haswa.. Sasa chidi anashuka na mpenzi wake ili kwenda kuwapokea, na wakati huo salma alikuwa kavalia Kiislamu hivi, lakini haikusababisha chidi asimuone,

Lakini ghafla salma alisita kuja kumpa mkono chidi, na chidi alikuwa bado hajampiga macho vizuri salma mana alikua kajitanda kislamu.. Sasa kumbe salma keshamjua chidi na ndio maana kasita kuja,..

"vipi broo,… Afu shem yupo wapi.. Aahhh mbona yupo mbali hivi"

Sasa chidi kumuangalia vizuri huyo shemeji yake,.. Alishikwa na butwaa, lakini sasa hilo ni dogo, kumbe huku miriam na Ibrahim nao pia wanafahamiana, hivyo walikuwa nao wanashangaana, kwahio kila mmoja alikuwa akimshangaa mwenzie… Salma na chidi, afu miriam na Ibrahim.. Ukimya wa ghafla ulitawala eneo hilo,…

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni