SITOISAHAU FACEBOOK (6) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 30 Aprili 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (6)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa


SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Nilivuta kumbukumbu ya sura ya Basu, nikamfananisha na yule mhanga wa kwenye ndoto.Hofu!!! Alikuwa mtu mmoja.Nikapiga ukelele wa hofu.“He Mungu wangu nimemuunguza dada wa watu.” Yule muhudumu alipiga kelele huku akizima mashine.Hakugundua kuwa nilikuwa dunia nyingine kabisa tofauti na hiyo aliyokuwa anadhania.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Alinimwagia maji akaniosha nywele. Sikujali ubora wa kazi, nilikuwa nimehamakinika. Akili ilimuwaza Basu.Kama amekufa kifo cha kufanana na kwenye ndoto maana yake nini?Au nataka kuwa mtakatifu??? Nilijiuliza. Huku nikiamini moja wapo ya dalili za kuwa mtakatifu ni kuyajua yanayokuja kupitia ndoto.Mh!! Utakatifu gani huu lakini hata kanisani penyewe siendi?? Nilitengua mawazo yangu.“Dada nakuita jamani!!.” Sauti ya yule muhudumu ilinishtua.

Inavyoonekana alikuwa ameniita mara nyingi sana.Nilikuwa sipo kawaida na niliombea sana wasiitambue hali hii.Simu yangu ikaita nikaitoa kuitazama alikuwa ni Dokta Davis.Nikapokea na kuiweka sikioni.“Samahani nipo saluni.” Nilimsihi.“Usijali nilikuwa nakutaarifu ukatazame salio katika akaunti yako.”“Hamna shida.” Nilimjibu na kukata simu.(Kovu la ajabu mgongoni)

Nilipotoka pale saluni nilitaka niende kwanza nyumbani kwangu lakini nikaona kwanza nipitie benki kutazama salio.“Laki sita elfu sitini na sita na mia sita sitini na sita.” Hiki ndio kiasi kilichokuwa kimeongezeka katika akaunti yangu. Sikushtuka sana safari hii, nilikuwa nimeanza kuizoea pesa hii kubwakubwa.Sikuwa na haja yoyote ya kutoa pesa kwani bado nilikuwa na pesa nyingi ndani. Niliingia katika bajaji iliyokuwa imenileta nikamuamuru anipeleke Kijiweni, huku ndipo nilikuwa naishi.Tulipoifikia kona ya kijiweni nilitelemka na kuliendea duka la madawa nikachukua dawa za kutuliza maumivu.

Nilipofika chumbani nikanywa na kujipumzisha kidogo kwa minajiri ya kuoga baada ya dakika kadhaa. Nilikuwa bado nawaza kuhusu kifo cha Basu kwa kung’atwa, lilikuwa jambo la kushangaza sana. Na kilikuwa kifo cha kustaajabisha, kivipi afe kama ndoto yangu ya usiku? Nilijiuliza sana. Sikupata jibu. Nikajitia imani kuwa hizo ni ndoto.Suala la kwamba ninaandaliwa kuwa mtakatifu lilinisaidia kupungaza hofu.Lakini utakatifu gani sasa huu wa kuupata bila kwenda kanisani??

Kwani watakatifu wote walikuwa wanaenda kanisani!! Nilijiuliza. Kisha nikaukatisha mgogoro huu wa nafsi kwa kumpigia simu John, nilizungumza naye kidogo akaniambia yupo njiani kuelekea Nyegezi kona kutazama maiti ya Basu.Aliposema jina hilo nikashtuka lakini hakugundua kwa sababu hakuonyesha wasiwasi na wala hakuuliza swali.“Basu…Basu amekufa?” Nilijifanya sijui lolote. John akanieleza stori ileile kama mama mnene wa kule saluni aliyosema.Nikaingia katika fumbo, sikumjua mfumbuzi!!!Nikapitiwa na usingizi!!!

Nilikuwa nautazama sasa umati wa watu ambao sikuelewa ni shughuli gani walikuwa wakiifanya. Sikuwatilia maanani sana na wala sikujuaeneo lile ni wapi. Mara nikamuona mtu ambaye ninamfahamu. Nilitamani kumuita lakini niliamini kwa zile hekaheka alizokuwa nazo wala asingeweza kunisikia. Nikapuuzia!!Sikujua nilikuwa nimejikita katika shughuli gani lakini kuna jambo nilikuwa nafanya.Mara nikamwona tena yule mtu ambaye nilionekana kumfahamu, sasa alikuwa katika mtafaruku. Wenzake wote walikuwa wakimpigia kelele katika namna ya kupingana. Alikuwa peke yake na hakuna aliyemuunga mkono. Mara wenzake wakaanza kumzonga sasa hayakuwa mabishano tena bali ugomvi. Mtu mmoja anachangiwa na watu zaidi ya kumi. Ugomvi ukawa ugomvi. Kuna jambo walikuwa wanalazimisha. Jambo hilo huyo mmoja hakuunga mkono kabisa.

Baada ya kuzidiwa mara yule mtu akawaponyoka. Akaanza kukimbia. Alikuwa anakimbia huku akiangalia nyuma. Nilikuwa natabasamu nikimtazama maana alionekana kuwa na hofu kuu.Alipogeuka mara ya kwanza lilikuwa kundi la watu watano wakimfukuza, akazidi kukimbia, alipogeuka tena walikuwa watatu, akajitahidi kujitetea kwa kuendelea kukimbia, wakabaki wawili. Safari hii hakugeuka.Alipokuja kugeuka sasa alikuwa amekaribia kukamatwa. Lakini cha kutia moyo alikuwa anakabiliwa na mtu mmoja tu. Japo alikuwa amechoka lakini hata huyu aliyekuwa anakabiliana naye alikuwa anahema juu juu. Walikuwa wanatazama kama majogoo yanayofanyiana ubabe.Mara jogoo lililokuwa linamkimbiza jogoo mwenzake likamrukia yule mkimbizwa. Wakaanguka chini, ugomvi ukazuka.

Wakagalagana hapo chini kwa namna ya kuchekesha. Nami nikawa nacheka.Mara yule mtu niliyekuwa namfahamu akaangushwa vibaya. Halafu yule aliyemuangusha akachomoa kisu kidogo, upesi akamchana nacho mgongoni. Akatoa ukelele wa uchungu na hofu.Kuchanwa huko kukawa kumemrejesha upya katika ugomvi. Sasa alikuwa na nguvu kamilifu. Yule aliyekuwa na kisu alipojaribu kumchana tena akawa amechelewa mkono wake ukadakwa, kisha kikafanyika kitendo cha sekunde kadhaa tu cha kuikamata shingo ya mwenye kisu na…na….na…“Mamaaaaa!!!” Nikakurupuka usingizi!!

Nilikuwa nimelala masaa sita. Niliyapikicha macho yangu huku na huko niweze kuangalia vyema mbele.Ukungu ulikuwa umetanda. Nikajipikicha zaidi nikaweza kuona, na sasa niliweza kusikia. Mlango ulikuwa unagongwa kwa nguvu. Fahamu zikanirejea vizuri, nikauendea bila hata kuulizia nikafungua. Alikuwa ni jirani yangu.“Kakasirika kweli John dah!! Amegonga mlango, kapiga simu yakohupokei.” Alinieleza huku na yeye akionekana kukasirika.Nilipiga mwayo mrefu kisha nikamuuliza kuwa alikuja saa ngapi. Akanijibu. Kisha akajieleza shida aliyokuwa nayo nikamsaidia . akaondoka!!!

*Sikuweza kuhudhuria msiba uliomuhusu Basu, akili yangu ilikuwa imechoka sana. Baada ya harakati za hapa na pale nilijipikia chakula kisha nilipomaliza nikalala tena.Mara hii mlango ulipogongwa nilisikia vyema kabisa. Nikasimama na kwenda kumfungulia. Alikuwa John na ilikuwa saa tatu usiku.John alikuwa amefanya mfano wa hasira usoni, nililitambua hilo na sikuwa na haja ya kumuuliza kwa nini amekasirika.Baada ya kuzungumza naye dakika kama kumi hivi huku nikijiweka karibu naye. Alilainika na uso wake ukaunda tabasamu.

Tulizungumza mengi na mpenzi wangu huyu wa zamani. Na kama vile tulikuwa tumeambiana kwa pamoja tukageukiana tukakumbatiana kwa nguvu. John alikuwa analia.Nilijua kuwa anamlilia Jesca, sikutaka kumuuliza najua angelia zaidi. Nilichofanya ni kuzidi kumkumbatia, viatu vikabaki sakafuni, sasa tukawa kitandani. Lugha iliyozungumzwa ilikuwa lugha ya mapenzi.John alikuwa mtulivu kama aliyesafiri kwenda ulimwengu wa mbali. Nikaitoa shati yake akawa amebakiwa na singlendi. Nikataka kuitoa na ile.“Ngoja nikaoge kwanza baby…” aliniambia kwa sauti nzito yenye kutamanisha.

Nikatulia nikamtazama naye akanitazama.“Twende wote pliiz.” Nilimsihi. Hakujibu chochote nikajua kuwa maana yake ni kwamba twende.Nikaziondoa nguo zangu, nikajivika upande wa kanga.“He!! Sa na hiyo singlendi waipeleka bafuni kufanyaje tena!!!” Nilimuuliza John baada ya kumuona akiingia na ile singlendi bafuni.“Si haujataka kunivua sa mi ntafanyaje?.” Aliniuliza kitoto. Nikatabasamu, nikamwendea, akakimbilia upande mwingine wa chumba nikamfata tukawa kama tunagombana. Japo hatukutumia nguvu sana!!!

“Ukiweza kunivua nakubeba mgongoni!!” Alinipa motisha nikazidisha juhudi. Nikaitoa nikawa mshindi.Mshindi kubebwa mgongoni!! Ikumbukwe hiyo.Mimi ndiye mshindi, mgongo mali yangu.John akachuchumaa nikawa nyuma yake.Ile nataka kupanda mgongoni nikaona kitu cha ajabu.Kovu!!! Kovu bichi!!! Kovu katika mgongo. Kovu la kuchanwa na kisu!!

“Mamaaaaa!!” nikapiga kelele. John akasimama. Tayari nilikuwa katika kona ya chumba nikiwa natetemeka sana!!!“Sabe sabe!! Umekuwaje…” aliniuliza huku akinisogelea. Nikawa namkimbia, lakini wakati huu haukuwa mchezo tena nilikuwa katika hofu ya ukweli. Nilikuwa namuogopa John.John alinisihi niache utani!!! Lakini sikuwa natania. Nilikuwa katika kumaanisha.Hali ilikuwa tete. John alikuwa ananitisha.Nikiwa katika kumkimbia John. Sasa aligundua kuwa kuna jambo limenisibu. Akanifuata kwa kasi. Akanivagaa. Nikajilazimisha kujitoa mikononi mwake huku nikipiga kelele. Ghafla akaninasa vibao viwili.

Sasa hapo ndio nikachanganyikiwa mwenzenu na kuamini kuwa dunia imefika mwisho. Nililia huku nikimtaja mwalimu Nchimbi.Lakini cha ajabu na kukera huyo mwalimu Nchimbi hata hakuwa akinisikia.Iliniuma. John akaniongeza vibao vingine viwili. Sasa yale maumivu akili ikasogeleana.“John una damu!! Una damu!!”“Damu??” aliniuliza.“Mgongoni umekuwaje wewe.”“Mgongoni pamekuwaje kwani…alilalamika huku akijipapasa”Maajabu mengine jamani!. Mkono wake haukuwa na damu. Akanigeukia.

Nikatamani kuiaga dunia niende likizo mbinguni. Hakuwa na kovu. Mgongo laini kabisa wa kiume ukatazama nami. Nikaruka mita kadhaa.Akapoteza uelekeo kuniona naruka vile nikataka kukimbia nje.Akanidaka kanga yangu. Kanga ikateleza ikauacha mwili.Shanga nane za rangi tofauti zilizokishika vyema kiuno changu ndio pekee zilizosalia katika mwili wangu. Sasa John alikuwa amebaki na kanga mkononi mimi nikiwa nina shanga kiunoni. Nusu nilikuwa nje na nusu nilikuwa ndani.Swali likavamia kichwa changu.

Nikimbie na shanga kiunoni kwenda nje ama nirudi chumbani kwa John huyu wa maajabu!!! John niliyemuhisi kuwa sasa ni Nikiwa katika kujiuliza iwapo nirejee ndani ama nikimbie hivyo hivyo uchi na shanga kiunoni, mara John akaanza kunisogelea huku akiniomba mkono wangu.Anakuita akuue!!! Sauti iliniambia.Hapohapo nikaamua kutimua mbio. Ilikuwa ni kama bahati kwenye kamba ya kuanikia nguo nikakutana na kanga nikaikwapua nikawa nakimbia huku naifunga.Ikawa kama ni muendelezo wa igizo. Wakati nadhani nipo peke yangu katika kukimbia mara nikashangaa tukiwa watatu. Wote wasichana. Mimi nilikuwa kimya. Wenzangu walikuwa wakipiga kelele za kuomba msaada

.John anatafuna watu!! Niliwaza. Nikaongeza mwendo zaidi. Sikuwa tayari kutafunwa. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwalimu Nchimbi. Anavyonitegemea!!! Atabaki na nani? Nikazidi kukaza mwendo. Kanga ikiwa imenikaa vizuri katika staili ya kupitia shingoni.Mara mmoja akaanguka huku akipiga kelele. Ni hapo ndipo niligeuka, kutazama kulikoni. Niliamini kabisa kuwa ni John anatafuna mtu pale lakini ghafla nikashuhudia mbwa mkubwa akimgalagaza msichana mwingine. Nikatoa ukelele wa hofu kuu.

He!! John kageuka mbwa!!! Nimekwisha mimi. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie. Sasa nilikumbuka kusali.Msikimbie nyie!!! Sauti kutoka nyuma ilitukanya. Haikuwa sauti ya John lakini ilikuwa sauti ya kiume.“Spider acha!! Spider shenzi acha!!! Acha!!!.” Sauti ile ilikuwa inakanya kwa ghadhabu. Waliposimama na mimi nikasimama. Lakini nikiwa nimejiweka tayari tayari kukimbia iwapo itabidi.Yule mbwa aliheshimu amri ile akaacha kumshambulia yule binti pale chini.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni