SITOISAHAU FACEBOOK (8) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 1 Mei 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (8)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa


SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
“Yeah! Umejuaje kwani?.” Aliniuliza.“Ni yule alikuwa ndugu yako au sio..”“Ni yeye Michael ndio jina lake. Binamu yangu.” Alisema kwa masikitiko makubwa sana John kisha akainama. Hapakuwa na haja ya kuuliza kama alikuwa anajizuia kutoa machozi.“Pole John.”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Nilimwambia kwa sauti ya chinichini.“Wamemnyonga binamu yangu wameona kumuua Jesca haitoshi aaah!!.” Alilalamika mwisho akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa sauti ya juu. Nikawa katika hali mbili ghafla. Kwanza hofu kubwa kwani alichozungumza John sasa kilitaka kuwa kile ambacho nilikiota. Pili nikawa katika kumbembeleza Michael kwa juhudi zote. Huku nafsi ikiniambia ninambembeleza muuaji.Lakini muuaji gani huyu sasa asiyejitambua kuwa ameua? Nilijiuliza.Nikahisi kuchanganyikiwa.

“Isabela.” Aliniita.“Bee!!.”“Nitahakikisha namfahamu huyo muuaji…kitambulisho chake kilidondoka na polisi wamedai wanafanya upelelezi.” John alitoa kauli nyingine. Kauli ambayo ilinishtua upya. Niliona kitambulisho kwenye ndoto. Lakini mwenye hicho kitambulisho alikuwa ni John mwenyewe na muuaji ni John.Ina maana John anaapa kujitafuta mwenyewe ama!!Nilichanganyikiwa!!!Nilitamani kumweleza John juu ya ile ndoto lakini sasa hamu yote ilikuwa imetoweka. Sikuwa na haja ya kumweleza, ataniamini vipi. Kwamba ni yeye aliyemuua binamu yake kwa kumnyonga na kuwa hicho kitambulisho ni cha kwake.

Hapana hawezi kuniamini hata kidogo!! John ataniona mjinga na ataidharau ndoto yangu.Nikaghairi kumweleza. Siri hiyo ikajikita na kuanza kuutesa moyo wangu. Mateso makali.Baada ya maziko hayo. Sasa chuo kilikuwa kimesimamia kidete juu ya upelelezi juu ya vifo mfululizo vya wanafunzi katika chuo cha mtakatifu Augustino. Kitambulisho kilichookotwa eneo la tukio kilikuwa kimeamsha hamasa ya kumjua muuaji. Polisi walikuwa makini sana katika hili na walikuwa watulivu wakiendelea na upelelezi kimya kimya.Alipotoka msibani John alikuwa na jingine jipya. Alikuwa amepoteza kitambulisho cha chuo.

“Yaani sijui hata kimepoteaje. Maana kilikuwa kwenye Wallet yangu. Sasa ah!!” Alinieleza John. Sasa ndoto ikawa imekamilika kabisa.Ni John alikuwa muuaji. Lakini muuaji wa ndotoni.Ndani ya siku saba nilikuwa nimekonda sana. Uzito ulikuwa umepungua. Ni serikali ya ubongo wangu pekee iliyojua ni nini kinanisibu.Si John wala mtu mwingine aliyejua nini kinanisibu.Nilikuwa nawaza juu ya usalama wa John. Niliona kama anaenda kukutana na hatia kubwa sana ambayo hawezi kuikwepa. Lakini kosa lile alilifanya katika ndoto yangu mimi pekee!!!

Kivipi niwe na hofu!!Nilijifariji kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu lakini hapana bado nilikuwa hoi bin taabaniSuala la kupoteza kitambulisho chake lilinipagawisha.kimawazo.****Hakuna ambaye hakujua kuwa sikuwa na tabia ya kunywa pombe baada ya kuanza rasmi kuwa muelimishaji rika la vijana. Nilikuwa nahamasisha sana kuhusu jambo hili na kuipinga vikali pombe.Wataalamu wa mambo walikiri kuwa pombe husaidia kupunguza mawazo sana. Sasa Isabella mimi nilikuwa na mawazo. Tena mawazo makali yaliokuwa yakishambulia ubongo wangu.Kitambulisho!!!Hichi ndio kiliniua kabisa. Hamu ya kula, raha ya kuwa na pesa zote hazikuwa na maana tena.

Siku hii nikaamua kwenda kugida pombe. Lakini kwa siri kubwa kabisa nikaamua kwenda mbali na chuo. Mbali na John.Mbali ya kila jicho linalonifahamu kwa ukaribu.Mkolani!!!! Nikajichimbia huko. Nikatafuta baa safi kabisa, nikajiweka sehemu ambayo si rahisi kugonganisha macho na watu.Moja, mbili, tatu…nikaanza kuhesabu idadi ya chupa zinazokuwa tupu mbele yangu. Ni siku nyingi nilikuwa sijapata kinywaji hichi. Basi ilikuwa burudani.“Dada mna vyumba hapa?.”Nilimuuliza muhudumu mmoja. Akakiri kuwa vyumba vipo. Nikamwomba anifanyie Booking.“Standard, Suite ama Deluxe.” Aliniuliza. Swali hilo likanikumbusha wakati tunampeleka dokta Davis kuchagua hoteli ya kulala.Alijibu vipi vileeee.“Deluxe.” Nilimwambia kwa kujifan ya nimefikiria sana.

Sikuwa na muda wa kuulizia bei. Pesa ilikuwepo ya kutosha.Baada ya kusikia kichwa kinachemka sasa nikahamishia makazi chumbani. Elfu sabini ilinitoka kwa malipo ya chumba.Hata sikujuta!!Mashambulizi ya kunywa pombe yaliendelea kwa fujo. Kitanda cha sita kwa sita kikinisubiri iwapo nitapitiwa na usingizi.Chumba hakikuwa na mbu hata mmoja. Nani kakudanganya raha ni mpaka uende ulaya?Hata Mwanza kuna raha, sehemu yoyote kuna raha.Cha muhimu hizo raha jipe mwenyewe!!!Isabella nilikuwa najipa raha mwenyewe.

Muhudumu wa kike alikuwa bize kila mara kuja kunitazama kama nimemaliza pombe alete nyingine ama labda nahitaji kutafuna kuku akachome ama afanye lost ni mimi tu!!!. Na hiyo ndio ilikuwa kazi yake kwa ujira wa elfu ishirini niliyompa.Ni kweli nilikuwa nimelewa lakini bado nilikuwa ninao uwezo wa kuona. Safari hii mlango ulipofunguliwa aliingia mwanaume, huyu hakuwa na mavazi kama ya yule muhudumu.Alijitambulisha kwa jina sikuweza kusikia. Akataja wadhifa wake, ulikuwa wadhifa mkubwa lakini hata hivyo pia sikuweza kusikia vyema.

Macho yalikuwa yameanza kupoteza nuru. Nikaingia gizani.Saa nne asubuhi ndipo niliamka.“Dada mchemsho tuweke nini na nini?.” Aliniuliza yule dada niliyemlipa usiku uliopita. Hakika alifanya kazi yake ipasavyo.“Leta supu ya mbuzi..supu ya mbuzi unanielewa.” Nilimwambia. Akanielewa akaondoka.Hangover ilikuwa inacheza na kichwa changu. Na sikuwa na mawazo yoyote.Baada ya kunywa supu niliyoipenda kabisa nilijisafisha na kubadilisha nguo. Nikalipia bili zote, kisha yule dada nikamwongeza pesa nikaondoka.Nilipotoka nje niliangaza hapa na pale nikaona teksi, nikaipungia mkono.

“Nipeleke mjini.”“Elfu nane.”Akanitamkia sikumjibu. Nikaingia garini. Akaondoa.Hapakuwa na foleni. Dakika ishirini nikawa nimefika.Nikatoa pesa yake na kumpatia.Nikaanza kuondoka baada ya kuwa nimemweleza kuwa hiyo elfu mbili abaki nayo. Nilikuwa nimetoa noti ya shilingi elfu kumi.Sasa nilikuwa naondoka kabla hajaniita tena.“Umedondosha kikadi chako.” Aliniambia. Nilipogeuka. Nilitazama chini, ni kweli nilikuwa nimedondosha kitu. Nikajongea na kukiokota.“Asante!!” nilimshukuru. Sasa nilimtazama usoni kwa mara ya kwanza.

Nilitaka kumuita jina lake kwa sababu nilihisi ninalijua jina hilo. Hata sura mbona nilikuwa nimewahi kuiona hapo kabla? Lakini kabla sijajua anaitwa nani. Teksi ilipigiwa honi ikapisha njia ikaondoka zake.“Ah!! Huenda aliwahi kunibeba hapo kabla.” Nilijipa moyo.Nikafungua pochi yangu na kuhifadhi hicho nilichookota.“Mungu wangu!!!!” nilipiga kelele kwa nguvu sana. Nilikuwa nimesimama wima.Kwa kuwa halikuwa eneo la watu wengi nilipata sekunde kumi za kuhakikisha nilichokiona.

Hakika kilikuwa chenyewe.Kilikuwa kitambulisho cha chuo ni heri kingekuwa changu.Kitambulisho cha John mikononi mwangu. Kitambulisho kinachoaminika kupotea ,msibani huko Iringa , kitambulisho nilichokiona ndotoni.Kitambulisho cha muuaji!!!Ewe dunia funguka unimeze!!! Ni sala niliyoiomba kimyakimya. Nilikuwa nimezizima siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.Harufu ya kifo!!!!Nilisahau ni jambo gani lilikuwa limenipeleka huko mjini. Yale mawazo niliyoamini nimeyapunguza kwa kunywa pombe sasa yalikuwa yamerudi kikamilifu.

Tena mara mia zaidi.Hofu ikatanda. Nikachukua teksi nyingine nikarejea nyumbani kwangu.Nilikuwa natetemeka, na kila nilipoguswa na kitu nilishtuka. Hata nywele zangu za bandia kichwani ziliponigusa shingoni nilitetereka.Nilipohakikisha kuwa nimeifunga milango vyema kabisa na ndani nilikuwa peke yangu. Nilifungua mkoba wangu nikakitoa kitambulisho.Hapakuwa na mabadiliko. Kilikuwa kitambulisho rasmi cha chuo kikuu matakatifu Augustino. Mmiliki akiwa John Joseph.Mpenzi wangu.Nililazimisha akili yangu kutafuta kumbukumbu huenda siku moja aliwahi kunipatia kile kitambulisho. Hapana kitu kama hicho.

Au aliweka mwenyewe bahati mbaya akakisahau? Hilo swali walau kidogo liliamsha uhai na kunipunguzia hofu.Akija nitamuuliza!!! Nilimaliza hivyo. Nikautua mzigo wa mawazo.Nikaingia maliwatoni nikasafisha mwili wangu kijuu juu. Nikajitupa katika sofa iliyokuwa sebuleni. Ule uchovu wa ulevi jana usiku ukawa unanishawishi kusinzia.Nikajifikiria kwenda kulala chumbani. Mara mlango ukagongwa.Nikajikausha!! Ukagongwa tena.Nikaenda kufungua. Alikuwa ni John.Alilazimisha tabasamu!! Nami nikatabasamu. Hatukusalimiana.

Tayari kakereka jana sikulala nyumbani!!! Niliwaza, huku nikijiandaa kukabiliana na maswali atakayoniuliza kwa fujo. Wanaume wana mikwara!!!!Akafika hadi katika lile sofa nililokuwa nimejilaza awali. Akajitupa hapo. Akazishusha pumzi kwa nguvu sana. Kisha akajishika kichwa. Mimi yangu macho nikawa nasubiri lawama.“I hate this…..” Alisema huku akiwa kama anajisea mwenyewe.Yaleyale!!! Nikajisemea.“Uko ok!! John!!” Hatimaye nilimuuliza. Hakunijibu!!“John jamani….” Nilibembeleza. Bado hakunijibu kitu. Nikaamini kuwa John amekerwa sana na kitendo changu cha kulala nje biula taarifa.

Wazo!!! Wazo likanijia. Nikasimama tena bila kumuaga nikatoweka pale hadi chumbani. Nikazama katika mkoba. Nikachomoa kile kitambulisho.Nikakisokomeza katika sidiria niliyokuwa nimevaa. Kisha nikarejea sebuleni. Wanaume dawa yao ndogo tu!! Mfanyie kitu anachopenda kwa wakati!! Baaasi hakuna ujanja tena.John akishaona kitambulisho chake ndo basi tena anasahau kuhusu suala langu la kulala nje. Najua mada itageuka na yatazaliana maswali.

Umekitoa wapi? Ilikuwaje? Dah!! Siamini.Kwisha mchezo!! Nilijiaminisha.Sasa nilikuwa mbele ya John. Bado alikuwa kama anayefikiria kitu kabla ya kuzungumza. Nikamsubiri labda atasema kitu hakusema. Nikamuita akaitika kwa kichwa chake kutingishika.“I hate…my country (naichukia nchi yangu).” Alisema huku akitazama mbele. Nikaurudisha mkono uliokuwa umekama kile kitambulisho tayari kwa kumshangaza. Nikakirudisha katika sidiria ili nipishe kwanza anachotaka kusema John.

“Nini tena mpenzi wangu jamani.” Tayari nilikuwa ubavuni mwake wakati anayasema haya. Hakujibu upesi bali alicheka kwanza. Kicheko cha kujilazimisha.“Eti kile kitambulisho….kile kitambulisho kile.” Alianza kuzungumza, nikafarijika kusikia mada ni juu ya kitambulisho na sio wivu wowote wa kimapenzi. Kisha akamalizia, “kile kitambulisho eti kimeibiwa ama kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Serikali yetu bwana..haya sasa kuna haja gani ya kuipenda?” Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang’ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni