DHAMANA (12)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Wote kwa pamoja mbio zao hazikuzaa matunda katika kumkamata Shafii aliyeonekana amechanganyikiwa kwani aliingia kwenye gari yake aina ya Cadillac akaiwasha bila hata kumuambia dereva wake aliyekuwa yupo pembeni katika mti akiwa amepumzika
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Shafii aliwaachia vumbi tu kwa mwendo bao aliondoka nao kama jambazi anayefukuzwa na polisi baada ya kupora benki.
"Beka daka ufunguo huo tumuwahi huyo asipatwe na matatizo" Hamisi alimwambia dereva wa Shafii kisha akamrushia funguo za gari halafu akakimbia kuelekea lilipo gari lake, Beka naye alimfuata akaingia upande wa dereva akawasha gari, Hamisi naye alishaingia kiti cha pembeni ya derwva akafunga mkanda.
Gari ya Hamisi nayo iliondoka kwa mwendo uleule alioondoka nao Shafii kuingia barabarani, baada ya kukimbiza gari sana waliona moshi mwingi ukiwa umetanda katika reli zilizopo katika njia iendayo Makorora tena kichwa cha treni kikiwa kimesimama mita kadhaa kutoka eneo la lenye moshi mzito.
Barabara nzima ilikuwa imefungwa na kundi hilo na ikawalizimu Hamisi na Beka wasimamishe gari lao wafunge milango vizuri waende kuangalja kuna nini kimetokea, waliposogea karibu zaidi ndipo walipoliona Cadillac la Shafii likiwa lipo matairi na wananchi walikuwa wakimtoa Shafii ndani ya gari hiyo baada ya kufanikiwa kuvunja kioo. Hawakutaka kupoteza muda nao walijichanganya katika kundi hilo la watu wakafanikiwa kufika mbele wakamtoa Shafii ndani ya gari hilo ambaye alikuwa hajitambui, walimpakiza kwenye gari wakishirikiana na wasamaria wema wakampeleka wakamkimbiza hospitali kwani alionekana bado anapumua.
****
Zaina alipelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa kina hadhi kubwa kuliko hata chumba alichokuwa akikitumia kule nyumbani kwao, alikuwa akipewa kila huduma aliyokuwa ya muhimu kwa wanadamu kutoka kwa vijakazi wa kasri la kifalme hadi akajihisi yupo ndani ya sehemu salama. Zilipita siku mbili akiwa ni mtu wa kukaa ndani na hana popote pa kwenda zaidi ya kukaa humo, hali hio ilianza kumchosha tu ndani ya siku hizo mbili tu kutokana na mazoea kutokaa ndani aliyokuwa nayo. Siku ya tatu ilipoingia alianza kulalamika kwa kufanywa mateka kwa watumishi hao waliomletea chakula, onyo alilopewa na Zalabain alilipuuzia na akawa anawatolea maneno mabovu vijakazi hao.
"Kelele wewe mwanadamu la sihivyo nitakiponda kichwa chako kwa ngumi moja tu ukasalimiane mababu zako waliotangulia" Sauti ya ukali ilisikika na kisha Kainun akatokea akiwa na hasira baada ya kusikia maneno ya Zaina.
"nirudisheni kwetu hamtaki!" Zain alizidi kuongea kwa ukali kama anaongea na binadamu wa kawaida.
"unasemaje wewe sasa nakutoa utumbo huku unajiona maana nyinyi wanadamu ndiyo chanzo cha matatizo kwenye himaya hii yote yaani nuru hatuijui tangu Mfalme wetu alipokufa kwa ajili ya ubaya wenu mlioufanya" Kainun aliongea kwa hasira akawa anamfuara Zaina kama Mbogo aliyejeruhiwa na sasa hivi akageuka na kuwa umbo la kutisha. Kuonekana kwa Kainun akiwa na umbile lake la kijini kulimfanya Zaina apatwe na mshtuko na azirai hapohapo, Zalabain naye alitokea hapohapo akiwa na hasira kupitiliza hadi macho yakawa mekundu. Alimpiga pigo la nguvu Kainun hadi akaenda chini kama gunia la udongo ulaya, alimuinua Kainun akamkunja akamuinua akamtazama usoni kwa hasira sana.
"unataka kufanya nini wewe?!" Zalabain alimuuliza halafu akampiga kichwa kizito.
"Ewe mtukufu hakika unatambua sisi tunavyowachukia binadamu kwa kutusababisha tusiwe na nuru, binti huyu wa kibinadamu ameanza kutoa maneno machafu katika kasri hili takatifu" Kainun aliongea kwa ghadhabu zaidi.
"hata kama afanye hivi unamjua ni nani huyu na kwanini nimempa hadhi sawa na familia ya kifalme?" Zalabain aliongea kwa hasira hadi mdomo wake ukawa unatoa cheche akamsukuma Kainun akaanguka chini.
"Mtukufu huyu si binti wa yule mmoja wa wabaya wako tu" Kainun aliongea akiwa amekaa kitako chini.
"Hata kama ni mtoto mtoto wa mbaya wangu lakini elewa mama yake ni mama yangu ila baba yake si baba yangu, huyu ni dada yangu mdogo Kainun. Unafikiri ukimuua nitakuacha wewe ukiwa hai" Zalabain aliongea kwa hasira zaidi hadi akawa anatetemeka, Kainun aliposikia hivyo alibaini kama ametenda kosa akaomba radhi hapohapo akiwa amepiga magoti.
"Inuka uende na usitie mguu chumba hichi ushamtisha Zaina" Zalabain alimuambia Kainun ambaye aliinuka na kuondoka.
****
SIKU ILIYOFUATA
Ndani ya nyumba mbovu yenye vumbi pamoja na samani za kizamani katikati ya jiji la Tanga, ndani ya nyumba hiyo Shafii alionekana akiwa amezungukwa na mke wake, mtoto wake na baba yake mzazi wakiwa wanamtazama kwa chuki huku yeye akionesha uso wa majuto akiwa amesimamia magongo mafupi kutokana na kushindwa kutembea.
"naomba kuanzia leo usiniite baba yako na mimi nasema sikuwahi na mtoto kama wewe!" Mzee Buruhan aliongea kwa hasira huku akimtazama Shafii ambaye alikuwa analia kama mtoto akiomba msamaha.
"Mke wangu, mwanangu nisameheni ili baba naye anisamehe" Shafii alipiga hadi magoti ingawa alikuwa anasikia maumivu kutokana na kutopona vizuri mguu.
"Baba yangu aliyepelekea uzao wangu hawezi akafanya hivi, nina wasiwasi nilikuwa nakuita baba kimakosa tu. Sina baba mshirikina na katili kama wewe" Zaina naye alitia msumari wa moto kwenye kidonda cha Shafii kwa maneno aliyoyaongea.
"We! We! We! Tena komaeh! Usiniite mkeo mimi, nafikiri nilioana na wewe kwasababu uliniloga lakini sikuridhia hivyo mimi siyo mkeo" Bi Farida aliongea kisha akamsindikiza na singi Shafii hadi akadondoka.
"Tena umuombe msamaha huyo hapo na siyo sisi" Mzee Buruhan aliongea huku akioneaha kidole kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya nyumba hiyo mbovu ya kizamani, Mtu mwenye joho jeusi alionekana akiingia akjwa ameahika sururu lenye mpini mweupe. Mtu huyo alipomkaribia Shafii, Mzee Buruhan, Bi Farida na Zaina walitoka nje wakimuacha Shafii na huyo mti aliyeingia.
"We shetani unakufa" Yule mtu alimuambia Shafii halaf akampiga sururu la kichwa kwa nguvu.
"Aaaaaaaaaaaargh!" Shafii aliachia ukelele wa maumivu lakini alipoangaza macho yake alijikuta yupo sehemu yenye kitanda cheupe na shuka jeupe, alipoona mazingira hayo alizidi kupiga kelele kwa nguvu akidhani labda yupo kuzimu.
"jamani atajitoa dripu yule, muwahini na sindano ya usingizi kabla hajajitonesha na ile shingo yake iliyovunjika" Ilisikika sauti ya kike ikitokea kushoto kwake.
****
Ilikuwa ni sauti ya muuguzi wa kike baada ya kuona dalili za purukushani anayotaka kuileta Shafii baada ya kuzinduka kutokana na ndoto mbaya aliyokuwa anaiota, mandhari ya eneo alilokuwepo ndiyo ilizidi kumchanganya kabisa akajiona ndiyo kama anaandaliwa kwa ajili ya kupigwa sururu na yule mtu aliyemuota ndotoni.
Wauguzi waliokuwa wapo ndani ya wodi aliyolazwa walimuwahi kwa sindano ya usingizi ili asije kusababisha madhara mengine zaidi kwa mwili wake. Hadi muda huo tayari mwili wake ulishapata madhara mengi kutokana na ajali ya gari na laiti kama angecheleweshwa basi ingekuwa ni mengine, Shafii tayari alikuwa kashavunjika shingo.na kiuno katika ajali ya gari aliyoipata kutokana na kuchanganyikiwa baada ya sauti kusikika akilini mwake ikimwambia mwanae kipenzi tayari yupo ndani ya mikono ya mtu asiyemjua tena mwenye nia mbaya na yeye.
****
RASKAZONE
TANGA
Siku iliyofuata katika jiji la Tanga ilikuwa ni siku nyingine iliyobeba tukio la ajabu jingine ambalo lilistahiki kuingia katika matukio ya ajabu yaliyowahi kutokea nchini Tanzania, ilikuwa ni siku ya pili imepita baada ya kutokea tukio la kuungua zile nyumba za kampuni Hamid kule Duga maforoni. Majira ya saa nne asubuhi wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya Matro ambao hawakumalizia kazi zao kutokana na tukio lililotokea hapo ofisini kwao la kuuawa kwa mmiliki wa kampuni hiyo walihitajika kufika mapema kumalizia viporo vya kazi yao ili waweze kwenda mapumzikoni kutokana na kifo cha mmiliki wa kampuni hiyo, ilipotimu saa tano asubuhi wafanyakazi wote walikuwa kwenye ukumbi wa mkutano wakimsikiliza msemaji wa kampuni hiyo baada ya kumaliza viporo vya kazi vilivyosalia siku iliyopita.
"Natumai wote ni wazima wa afya na mpo hapa kusikiliza jambo nililowaitia, kikubwa kilichonifanya niwaite hapa ni juu ya kutokea kwa msiba wa bosi wetu kipenzi na wote mnalitambua hili. Sasa basi kwa taarifa zilizonifikia ni kwamba kumetokea vifo viwili ndani ya siku moja ambacho kimoja ni cha bosi wetu kipenzi na kingine ni cha kaka yake mmiliki wa kampuni ya Extoplus nadhani wote mnamfahamu. Hivyo misiba hii yote miwili itafanyika nyumbani kwa baba yao mzazi mzee Buruhan maeneo ya Sahare jijini hapahapa, ikiwa sisi ni miongoni mwa wafanyakazi wake tuliyempenda inabidi wote twende tukamfariji mjane wa marehemu pamoja na familia nzima ya mzee Buruhan. Hakika sisi ni wa....."
Msemaji mkuu wa kampuni ya Matro alitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni aliyoyapata ambayo hayakuwa yamefika kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, alipokuwa anataka kuhitisha maelezo hayo alisikia mlango mmojawapo wa chumba cha mkutano ambao hautumiki ukifunguliwa kwa nguvu na ikaonekana aliyefungua ni mtu mwenye ubavu mkubwa kwa jinsi ulivyotoa kishindo hadi kitasa chake kikaanguka papo hapo.
Macho ya kila mmoja aliyepo eneo hilo yalielekea kwenye mlango huo na hapo ndipo wakapigwa na butwa baada ya kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye takribani miaka sita akiingia huku kabeba mdoli mdogo mwenye umbo la dubu mweupe, macho ya baadhi ya wafanyakazi yalionesha kumtambua huyo mtoto ila baadhi hawakumtambua hata kidogo. Mtoto huyo wa kike mzuri alizidi kumfanya Msemaji mkuu wa kampuni hiyo apagawe zaidi, mtoto huyo alipiga hatua hadi alipo Msemaji mkuu wa kampuni hiyo kisha akamuangalia usoni huku akitabasamu.
"Annet mwanangu umekuja na nani?" Msemaji mkuu alijikuta akiuliza huku akiwa ameduwaa na hata wengine waliduwa kwa jinsi mlango aliopitia huyo mtoto ulipotoa kishindo kizito sana hadi kitasa chake kikaanguka.
"nimekuja mwenyewe baba" Mtoto huyo anayeitwa Annet alijibu kwa lafudhi ya kitoto ambayo ilisikika na kila mmoja humo katika chumba cha mkutano.
Msemaji wa kampuni aliposikia hilo jibu la mtoto wake alichuchumaa chini akamshika mashavu huku akitabasamu kwa ishara ya upendo wote anaotakiwa kuuonesha baba kwa mtoto wake kisha akamuuliza, "ni nani aliyeufungua mlango kwa nguvu hadi kitasa kikaharibika?"
"Mimi hapa nimeugusa tu kwa mkono mmoja nikausukuma ukafunguka" Annet alijibu na akazidi kuwashangaza watu waliomo humo ndani hadi Msemaji mkuu wa kampuni naye akazidi kushangaa majibu anayoyatoa binti yake huyo mdogo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni