SHETANI ALINIITA KUZIMU (2)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Shiwawa Binasalaan Al Jabry
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Baada ya kukaa kwenye kile chumba kwa muda mrefu niliona sikutendewa haki kutomzika mama mdogo, nilivunja mlango nikatoka mbio kwenda makaburini.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Nilipofika nilikuta ndiyo wanaingiza jeneza kaburini tayari kuzika, nililia sana hadi nikazimia. Siku ya pili baada ya mazishi, baba aliondoka Ngara kurudi nyumbani na
kuniacha nikiendelea kuombeleza msiba wa mama. Alasiri ya siku aliyoondoka baba nilihisi kuchoka niliingia kwenye chumba nilichokuwa nalala nikajipumzisha.
Kutokana na uchovu wa nilipitiwa na usingizi na kuota ndoto ya kutisha ndipo nilishtuka na kuanza kuangaza macho huku na huko huku nikihema. Jambo la
kushangaza mbele yangu nilimuona yule mtoto aliyenitokea wakati nakwenda kupanda gari kuelekea Ngara, aliyeniambia nitakuwa mchawi. Dogo huyo akiwa kanyoa
kipara na uchi wa mnyama aliniangalia kwa dakika kadhaa na kuniambia angenifuata usiku. Alipomaliza kuniambia hivyo alifungua mlango na kutoka mle ndani,
kutokana na kustaajabishwa na jambo hilo niliamua kumfuatilia ili nijue alielekea wapi,
Nilipotoka niliwaona watoto wakicheza ndipo niliwaulioza motto aliyetoka mle ndani alielekea wapi, wakanijibu kwamba hawakumuona. Kwa kuwa nilikuwa na imani
kwamba walimuona niliwauliza tena waniambie yule mtoto alikwenda wapi, wakasisitiza kwamba hawakumuona isipokuwa walimuona paka mweusi. Kufuatia kauli za
wale watoto, nilibaini yule mtoto alikuwa mchawi ndipo niliachana naye na kuendelea na mambo mengine.
Jioni ya siku hiyo niliwaaga wenyeji wangu kwamba asubuhi ningerudi nyumbani Lamadi, walinishukuru kwenda kuhudhuria msiba wa mama mdogo na kunitakia safari
njema. Kulipokucha walinisindikiza stendi ambapo nilipata usafiri na kuanza safari ya kurudi nyumbani, baada ya kusafiri kwa muda mrefu niliwasili salama
salimini. Nilipofika nilimkuta baba ambaye alinilaki kwa furaha na kuniuliza habari za Ngara, nikamfahamisha zilikuwa nzuri.
Kwa kuwa nilifika usiku, baada ya kula nilikwenda kulala ili niamke alfajiri tayari kwa kwenda shambani. Nikiwa nimelala saa nane usiku nilihisi kama kuna
kitu kimetua chumbani kwangu, nikaamka ndipo nilipigwa butwaa kumuona yule mtoto mchawi akiwa amekuja na wenzake watatu wakiwa uchi.
Yule mtoto na wenzake aliniuliza kwa vitisho "Wewe utakuwa mchawi mwenzetu"
Nikikataa kuwa mchawi nitauawa na nikikubali nitapewa nguvu na hakuna mtu atakayenisumbua duniani.
"Mimi sitaki kuwa mchawi"
Baada ya kutoa kauli hiyo, yule mtoto alikunja sura kuonesha alichukia kisha alimwita mzee mmoja na kumwambia amletee jambia lake ili anichinje kama kuku.
Alipoletewa jisu hilo kubwa lililokuwa na makali kila upande na kumeremeta, alinikamata na kuniuliza tena; “Utakubali kuwa mchawi au hutaki? Kama ukileta
ujuaji wako nakuchinja sasa hivi na kula nyama yako,” yule mtoto aliniambia.
Kwa hofu ya kuchinjwa, nilimwambia nilikubali kuwa mchawi ndipo wachawi waliokuwepo pale walishangilia na kuanza kupiga ngoma na vigelegele. Hawakuishia
hapo, walirukaruka huku na huko na wengine walinibeba juu kwa furaha hadi walipotulia baada ya yule mtoto kuwaonesha ishara ya kuacha kuimba. Baada ya wale
wachawi kutulia, yule dogo aliwauliza; “Hivi ninyi mnacheza tu, leo mtakula nini?” Kabla ya kujibiwa aliendelea kuwaambia kuwa; “Nawashangaa sana kwani
mnaelewa hatuna mboga na kawaida sherehe huwa ni kula na kunywa lakini mnaendelea kucheza tu.
Mtoto huyo ambaye niliamini alikuwa kiongozi wa wachawi aliyeheshimiwa aliongeza kuwaambia kuwa, kitendo cha mimi kukubali kuwa mchawi kilimfurahisha sana
hivyo lazima wanifanyie sherehe kubwa. Baada ya kutoa kauli hiyo, aliwaamuru baadhi ya wachawi waende wakatafute mboga na kurejea haraka na wengine waendelee
kucheza ngoma na kuimba. Alipotoa amri hiyo, wachawi wapatao kumi waliondoka na hazikupita dakika kumi walirejea wakiwa wamewabeba akina mama watatu, mmoja
waao na mimba kama ya miezi sita. Wakiwa na watu hao walioonekana walikuwa wafu, waliwalaza katikati ya wachawi ndipo yule dogo akawa anatikisa kichwa kwa
furaha. Akiwa anatazama miili ya wale akina mama, aliwaambia wachawi walioileta pale kwamba walifanya kazi nzuri sana hivyo atawapandisha vyeo na kuwaongezea nguvu.
“Kitendo cha kuleta mboga iliyonona kimenifurahisha sana, kila mmoja wenu nitampandisha cheo na kumuongezea nguvu za kichawi,’ yule mtoto aliwaambia wachawi wenzake.
Alipotoa kauli hiyo aliwaambia wachukue ile miili na kwenda kuandaa mboga kisha naye akawafuata ambapo hakukaa sana nikamuona akirejea huku mkononi kashika
kibuyu. Mtoto huyo alitembea na kuja kusimama mbele yangu na kunipa ishara nichungulie ndani ya kile kibuyu, nilipofanya hivyo niliona kimejaa damu. Tukio
hilo lilinisisimua sana na kugundua kwamba ile damu ilikuwa ya wale akina mama walioletwa wakiwa wameuawa tayari.
Baada ya kugundua hali niliyokuwanayo aliniambia nikibebe kwa mikono yote kile kibuyu kisha nimfuate, nikafanya hivyo. Aliniongoza hadi katikati ya lile
kundi la wachawi, nilishangaa kuona kuna majungu mawili ‘sufuria’ zilizoinjikwa kwenye moto. Moja kwa moja niligundua kilichokuwa kikipikwa zilikuwa nyama za
wale akina mama ndipo yule dogo aliwaamuru wote watulie. Alipotoa kauli hiyo alimuona mchawi mmoja akitafuna kitu ndipo alimwita na kumuuliza alikuwa akitafuna nini, akamwambia nyama.
Mtoto huyo alimuuliza nani alimpa kibali cha kula nyama kabla ya wakati muafaka, akamwambia alikuwa akionja ili kujua kama iliiva ili aipue isije ikalainika
sana. Mzee huyo aliendelea kujijitetea kwamba, nyama ya binadamu ilikuwa laini hivyo haikupendeza kuiva sana. Baada ya yule mzee kutoa maelezo hayo, yule
mtoto alifurahi na kumsifia kwamba alikuwa mpishi mahiri aliyeijua kazi yake.
Yule mzee ambaye awali alifikiria alifanya kosa, alimsujudia dogo kuonesha heshima kwake na kurejea sehemu aliyokuwa amesimama. Mtoto mchawi akiwa amesimama,
aliwaambia wale wachawi wenzake kwamba siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kufuatia mimi kujiunga na wao ndipo aliniambia nimpatie kile kibuyu, nikafanya hivyo.
Baada ya kumpatia kile kibuyu alikiweka kinywani kwake na kuanza kunywa ile damu kama vile maji, nikabaki nimeduwaa namuangalia. Alipotosheka alitoa kile
kibuyu kinywani na kuanza kulamba midogo kama afanyavyo mtu aliyekunywa kitu kitamu. Baada ya kujilamba alinipatia kile kibuyu na kuniambia nami ninywe ile
damu, kwa kuwa tangu nilipozaliwa sikuwahi kunywa damu, nikabaki nikimwangalia. “Kijana inabidi unywe hiyo damu kwa sababu wewe tayari umekuwa mwenzetu hivyo unalazimika kushirikiana nasi kwa kila jambo,”
Yule mtoto aliniambia kwamba nikinywa damu hiyo nitakuwa na nguvu nyingi za kichawi na kwamba hakuna mtu atakayenisumbua. Sijui ilikuwaje nikajikuta
nakipeleka kile kibuyu chenye damu mdomoni na kuanza kunywa, wakati nafanya hivyo yule dogo na wachawi wengine walikuwa wakiniangalia. Baada ya kunywa kiasi,
nilisitisha zoezi hilo ndipo yule mtoto mchawi akaniambia nimalize yote, nilitaka kugoma lakini nilipokumbuka kauli ya kwamba kama ningeleta ubishi wangeniua nikanywa yote.
Nilipomaliza nilishangaa kuwaona wale wachawi pamoja na yule mtoto wakicheka na baadhi walishangilia kwa furaha, nikajikuta nami nacheka kama wao. “Kijana
mbona ulipomaliza kunywa damu umekuwa na furaha tofauti na awali ambapo ulikuwa na huzuni?” mmoja wa wale wachawi aliniuliza.
Kufuatia swali hilo, nilimwambia kwamba nilikuwa na furaha kwa sababu nilikuwa nimepata nguvu za ajabu na watu wangenikoma. Nikiwa katika hali hiyo nilihisi
njaa, nikasogea kwenye sufuria moja ambalo wale wachawi walikuwa wakipika nyama za akina mama waliowaua, nikataka kuchukua mnofu mmoja lakini nikakumbuka ningekuwa nimefanya kosa.
Nilimfuata yule mtoto na kumsujudia na kumfahamisha kwamba nilisikia njaa kali sana hivyo aniruhusu nikachukue nyama, akatabasamu. Baada ya kumweleza hivyo,
alikwenda sehemu iliyokuwa na vyombo vya kulia chakula chao akachukua bakuli la dhahabu na kujongea kwenye sufuria ilimokuwa ikipikwa nyama. Alipofika
alichukua upawa na kuchota nyama na kujaza katika lile bakuli na kukaa pembeni kisha alituruhusu na sisi tuanze kuchota nyama, tukafanya hivyo.
Kama ilivyo kawaida ya Wakristo kuombea chakula, kabla hatujaanza kula zile nyama yule mtoto alituambia tuombe, nakumbuka tuliomba kwa kusema: “Tunakushukuru
ewe malkia kwa kutupatia nguvu na kuweza kutafuta chakula hiki, uwezo wako uendelee kudumu na kumalizia sala hiyo kwa kusema; “Asante malkia.” Baada ya
kuombea chakula hicho, tulianza kula nyama hiyo ambayo haikuwa na ladha nzuri kama nyama za kawaida.
Tulipomaliza kula, tulikusanya vyombo kisha mzee mmoja alipiga mbiu, wote tukakusanyika kama wafanyavyo wanajeshi wanaposikia tarumbeta la kuwaita. Tukiwa
tumetulia kimya, nilimuona yule mtoto akipita na kwenda kusimama mbele huku kashika mkoba mweusi. Aliponiona aliniita kwa kulitaja jina langu mara mbili,
moja kwa moja nilijua alikuwa akitaka kunikabidhi mkoba waliopewa na bibi yangu, moyo ukanipiga paa!
Nikiwa nimeduwaa, yule mtoto aliniita tena; ‘Kaloli, Kaloli, Kaloli! Nikaitika kwa kusema labeka mkuu. Baada ya kuitika alisema; “Nafurahi kukuambia kwamba
sasa umekuwa miongoni mwa jamii yetu, huu mkoba alikuwa akiutumia bibi yako upokee kwa mikono miwili.” Nilipoupokea aliendelea kusema; “Mkoba huu una nguvu
nyingi sana na utakuwezesha kufanya kila kitu utakachohitaji.”
Alipomaliza kutoa kauli hiyo, nilimuona akibadilika na kuanza kuongea lugha ambayo sikuifahamu lakini nilisikia akilitaja jina la malkia na kutamka herufi
zifuatavyo; “C.a,f,e,j,a,a,a,m, w,f,s,s,s,s,s,s,g,z,z,z,z,,f,f,f,f, naomba ujitokeze sasa.”
MANENO ya yule dogo yalinishangaza nikabaki nimeduwaa nikisubiri kitakachotokea ndipo ghafla kilitokea kimbunga, wachawi wote walitulia. Nikiwa nashangazwa
na mambo ya pale nilisikia kitu kikitua chini tii, nilipoangalia mbele yangu nilimuona mwanamke mmoja mrembo ambaye nashindwa namna ya kumuelezea akiwa
ameketi kwenye kiti. Kiti alichokalia kilikuwa cha kimalkia kwani kilitengenezwa kwa madini ya kung’aa ambayo nahisi ilikuwa dhahabu.
Mwanamke huyo ambaye nilijua ndiye malkia aliyeitwa na yule dogo, aliyekuwa na mkia mrefu alikuwa kazungukwa na nyoka kila upande.
Akiwa ametulia alisema; “Nimefika hapa baada ya kuitwa na nyinyi, naomba mniambie kinachowasibu ili niwasaidie kisha nirudi kwenye makazi yangu.”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni