DHAMANA (30)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA THELATHINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Jambo ambalo wanadamu hawa hawakulitambua ni kwamba dawa waliyompa Farida kila siku usiku ilikuwa inapunguzwa na Faimu na hapo Farida hurudi katika akili na hukutana kimwili na Faimu kwa kipindi hicho chote huwa alikuwa anamjia kwa njia ya ndoto, hadi huyu bwana hapa anamposa Farida baada ya kumuweka chini yake kwa kutumia nguvu za kichawi tayari huo mchezo Faimu alikuwa anaendelea na ndiyo katika kipindi hicho akawa anamuona anaweweseka na hata alipokuja kuacha tayari Farida alikuwa ana ujauzito wa Faimu huyu bwana akidhani ni wake.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Jamadin alipozaliwa Faimu alikuwa yupo makini sana katika kumlinda mwanae kuliko kitu kingine chochote pia alimpatia mkufu wenye kidani kinachoitwa Dainun ili umlinde na hadi hawa mabwana wanataka kumtoa kafara Jamadin kipindi hicho akiwa na miaka mitano hapa duniani na mmoja kwamujibu wa mila za kijini ambazo miaka mitano ya kwanza ya mtoto huhesabiwa ni mwaka mmoja . Faimu alishajua hilo na alifika eneo hili akiwa na jazba sana.
Alifanya hila ya kutengeneza upepo nje ili aharibu kazi yao kisha aliingia ndani akiwa yupo kama kimbunga ndipo alipojikuta amenasa kwa kuzungushiwa damu ya hedhi ya mwanamke akawa hawezi kutoka kwani ina madhara sana kwake kama akiisogelea, hapo ndipo mabwana hawa wakamchoma kwa pamoja visu vilivyochovya kwenye damu ya hedhi katika mwili wake na kumfanya apate jeraha kubwa.
Faimu aliishiwa nguvu na alizama chini ya ardhi mimi nikaja kumtoa nikampeleka kwa mtukufu mfalme ili apatiwe matibabu kwa jereha hilo, kuanzia siku hiyo Faimu alikuwa mtu wa kukaa kitandani kwani mkufu wenye Dainun ambao ni mali yake ndiyo ungeweza kumponya tu. Baada ya mwaka mmoja Faimu alifariki akitoa tamko mwanae ndiye aje kukaimu nafasi yake ya ufalme atapofariki baba yake, agizo jingine alilotoa ni kisasi chote kilipwe na mwanae tu. Kiongozi Zalabain au Faimu alipokuja kupatikana taji lilimkataa mpaka upatikane huu mkufu na kisasi kulipwe kwani hawa ndugu ndiyo chanzo kuzaliwa watoto waliodumaa katika himaya yetu kutokana na kutoonekana kwa usiku kwa muda mrefu".
Mzee Mubarak alimaliza simulizi yake iliyomliza sana Bi Farida baada ya kusikia kuwa Faimu kwa muda huo ni marehemu, mzee Buruhan aliposikia hiyo habari hasira zilimzidi maradufu na akasimama wima huku akihema kwa nguvu.
"Mzee mwenzangu tulia basi walsu kidogo tumalizie" Mzee Mahmud alimsihi rafiki yake.
"Sihitaji hata kuendelea kumuangalia huyu mwanaharamu na sina mtoto kama yeye ngoja niondoke nje mkimaliza mtanikuta" Mzee Buruhan alisema kwa jazna kisha akaanza kutembea kuelekea nje.
"Baba usifanye hivyo" Shafii alilalamika kumsihi baba yake.
"kelele wee! Shaytwani mkubwa usiniite baba yako na sina mtoto kama wewe mtoto wangu ni Ally tu" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali kisha akatoka nje akamuacha Shafii akilia kwa uchungu, muda huo huo Ally naye akainuka akamtazama Shafii kisha akamtazama na Salma halafu akamtazama Hamida kwa huruma sana.
"Salma naomba unipatie mwanangu niondoke naye" Ally aliongwa kwa ustarabu halafu akamuangalia Mzee Mahmud akamuambia, "Baba huyu mwanamke ni zaidi ya shetani yaani kanitumikisha kama mtumwa wa ngono kwa miaka mingi baada ya ule mkufu kunifanya niwapende na ushenzi wao, sijaoa wala kuwa na mke na umri huu matokeo yake napata mtoto kupitia huyu malaya tena mke wa mtu. Hebu muulizeni Hamida ni mtoto wa nani".
Ally alipoongea maneno hayo hadi Shafii aliweka mkono kinywani kwa ujinga alioufanya Salma ambaye aliishia kuona aibu tu, aliinamisha kichwa chini kutokana na fedheha iliyomkuta hadi wanae wakawa wanamuona ni binadamu wa ajabu.
"Salma huyo Hamida ni mtoto wa nani?" Mzee Mahmud aliuliza taratibu huku akimuangalia Salma kwa Macho ya ukali sana, Salma alishindwa kujibu na akakaa kimya akiwa ameinamisha macho chini hadi alipokaripiwa.
"wa A....A..Ally" Salma alijibu huku akitazama chini kwa aibu na kupelekea mwanae mkubwa Jamal asimame akawa anaenda alipo Ally ambapo ni jirani na mlango wa kutoka mje ili aondoke, Salma alimshikilia miguu mwanae lakini alijikuta akisukumwa kwa nguvu.
"Bora ningezaliwa na shetani kuliko wewe" Jamal aliongea kwa hasira halafu akatoka nje huku akilia kwa uchungu, Hamida naye alinyanyuka kisha akaanza kumtazama mama yake huku machozi yakimtoka kwa uchungu. Salma alipotaka kumkumbatia miguuni alimsukuma kwa nguvu halafu akaenda halipo Ally akawa anamtazama huku machozi yakimtoka, Hamida alimkumbatia baba yake kwa mara ya kwanza huku akilia na Ally naye alimpokea mwanae huku machozi yakimtoka kwa alichofanyiwa.
"Baba samahani naondoka humu nikiwa nina mwanangu, sina kaka humo" Ally alizungumza kwa hasira halafu akatoka nje akiwa na Hamida, Salma alipotaka kuwafuata alijikuta hawezi kuinuka kabisa.
"Shafii nadhani unakumbuka jana jioni nilikuambia leo ndiyo utapata nafuu ya tatizo lako, sasa basi napenda utambue kuwa sikumaanisha litatuliwa basi nafuu yenyewe ndiyo hii ya kuwaona Bi Farida na Zayina ila si kukusaidia zaidi kutokana na udhalimu mlioufanya. Niliwaonya msifanye hivyo tangu mnaenda kumuwekea dawa Farida lakini hukusikia kwa ubishi wako, sasa mwanangu donda la kujitakia halihitaji pole uguza bila msaada wala pole. Nadhani Zalabain Jamadin ana mengi ya kuongea na wewe mkiwa wewe na Salma sasa mtazungumza naye wawili, mimi sisaidii madhalimu kama nyinyi" Mzee Mahmud naye aliongea kisha akanyuka akasema, "lengo langu ilikuwa kumnasua Ally maana naye angekumbwa na balaa lisilomuhusu na nimefanikiwa sasa nawatakia mazungumzo mema na Zalabain".
Mzee Mahmud alitoka nje akazidisha machungu sana kwa Shafii ambaye alilia sana pia Salma naye alijuta kwa yote aliyokuwa akiyafanya kwani hakuwa na muda wa kurekebisha tayati alishachelewa kabisa.
Mzee Mubaraka, Bi Farida pamoja na Zayina nao walinyanyuka wakabakisha watu watatu tu waliobaki humo ndani na walianza kutembea kwataratibu kuufuata mlango ulipo.
"Mke wangu, mwanangu" Shafii aliita huku akinyoosha akiwa anazidi kulia sana kwani hakuwa anaweza hata kunyanyuka, maneno yake yalimfanya Bi Farida asimame kisha akamsonya kwa nguvu halafu akasema, "mkeo nani kwa ndoa ipi? Sina mume kama wewe".
Bi Farida alipimaliza kuongea hayo maneno alitoka nje kwa hasira akiwa amemshikilia Zayina aliyekuwa analia tu kutokana na kilio cha baba yake lakini alimuacha apate adhabu kwa uovu wake
Zalabain alipohakikisha mtumishi wake,mama na dada yake wametoka nje alimama wima akiwa na macho yaliyojaa ghadhabu sana akawasogelea Shafii na Salma, alimuangalia Salma kwa macho makali halafu akamsogelea karibu zaidi na kusababisha Salma atokwe na haja ndogo papo hapo.
"Wakati unatoa damu yako ya hedhi iliyosababisha baba yangu afe mbona hukujikojolea, ulijua na mimi itaniua wakati mnanichanja na visu vyenu nilikuwa nina Dainun shingoni mwangu. Sasa leo zamu yako" Zalabain aliongea kisha akaushika shingo ya Salma akaiminya kwa nguvu hadi mishipa ikapasuka damu zikaanza kuvuja, alishika na kichwa akakivuta akakichomoa kabisa halafu akamgeukia Shafii akamwambia "nipe".
Shafii kwa uoga aliokuwa nao aliposhuhudia Salma alivyouawa aliweka mkono kifuani mwanga ukatokea na hapo mkufu ukaonekana ukiwaka halafu ukazimika ghafla, kuzimika kwa mkufu kulimfanya Shafii ashangae sana akabaki akimuangalia Zalabain huku akitetemeka.
"He! Ulijua hiyo Dainun itatoa mwanga uniue nayo, kwa taarifa yako nguvu kubwa ya Mzee Mahmud inaizuia hiyo isifanye kazi. Nipe!" Zalabain aliongea huku akimsogelea Shafii akiwa na jazba, Shafii hakuwa na ujanja aliivua Dainun akampatia Zalabain huku akitetemeka.
Zalabain aliichukua Dainun akaivaa shingoni mwake na kusababisha Dainun ipige mwanga mkali ulioenda juu kisha ikaanza kung'aa, alitoa tabasamu kisha akanyooshea Shafii kidole akamuambia, "umenipatia kimoja bado kingine tumalizane kabisa".
"Kipi?" Shafii aliuliza huku akitetemeka
"roho yako" Zalabain alijibu na macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu tabasamu likawa limefutika usoni
"hapana" Shafii alisema huku aliweka mikono ishara ya kuomba msamaha lakini haikusaidia kitu kwani Zalabain alijigeuza kimbunga kikali kikamvaa Shafii kikawa kinamzungusha na kupelekea Shafii atoe mayowe ya maumivu yaliyosikika hadi nje, taswira mbaya ya kuruka kwa damu pembeni wakati akizungushwa ndiyo ilionekana na kisha vipande vya mifupa vvikaruka pembeni vikiwa na damu tupu. Muda huo tayari Shafii alikuwa ameaga dunia kutokana kupata mshahara kwa kile alichokifanya miaka mingi iliyopita.
****
Watu wote waliokuwa nje walisikia kelele za Shafii lakini hakuna hata oja aliyethubutu kumsaidia na makelele yalipotulia haukupita muda mrefu nyumba yote ikaanza kuporomoka yote kisha ardhi yake ikafunguka kifusi chote kikazama na huo ndiyo ukawa mwisho wa Shafii, watu waliona kitendo hicho walisikitika sana wengine walitokwa na machozi kwani ingawa kafanya mabaya bado alikuwa na nafasi kwa baba yake na mtoto wake.
Kulipotulia kabisa Zalabain alitokea akiwa ana Dainun shingoni mwake akamchukua mama yake na dada yake pamoja na mtumishi wake wakaondoka, waliobaki walitafita nyumba za kulala hapo Mpirani usiku huo baada ya kushuhudia mwisho wa dhahama ya kujitakia
****
Miale ya Dainun iliyopiga angani ilisababisha mwangaza wa kawaida kurejea katika himaya ya Majichungu, ndelemo na vifijo kutoka kwa majini wa aina mbalimbali ndiyo zilisikika na siku iliyofuata sherehe ilifanywa katika viwanja vya kasri la kifalme. Zalabain alivikwa rasmi taji la ufalme ambalo halikumkataa lilikaa kwenye kichwa chake vizuri kabisa, sherehe kubwa ilifanywa ilishuhudiwa na dada yake pamoja na mama yake wakiwa na furaha kama alivyokuwa yeye ana furaha.
MWISHO
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni