DHAMANA (10)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Muda ambao Shafii alikuwa anaona vibweka vya kuuliwa mganga wake aliyeanza kumtumia miaka mingi iliyopita, ndiyo muda huohuo mdogo wake aliwasili nyumbani kwa shemeji yake Shafii yaani kaka wa Bi Farida mke wa Shafii anayeitwa Hamis.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Ally aliingia nyumbani kwa Hamis akiwa na huzuni kwa kuwapoteza kaka zake tena machozi yalikuwa yakitaka kumtoka kila akiwakumbuka kaka zake hao, alipokelewa na mfanyakazi wa ndani wa nyumba ya Hamis na akapelekwa hadi ukumbini ambapo alimkuta Hamis akiwa amekaa kwenye jamvi akinywa shurubati ya maembe.
"Ally vipi kwema?" Hamis alimuuliza Ally kutokana na hali ya huzuni aliyomuona nayo.
"si kwema shemeji" Ally alijibu na machozi yalianza kumtoka hapo hapo.
"heeh! Kunani hebu nieleze?" Hamis alimuuliza Ally.
"Kaka Hamid na Hussein hatunao" Ally akiongea na hapo machozi yakaanza kumtoka kama chemchem.
"Eti nini?" Hamis aliuliza kwa hasira na hapo akaanza kunguruma na mwili wake ukaanza kutetemeka kama kamwagiwa maji ya baridi, Ally alipoona hali hiyo aliacha kulia hapohapo akatoka mbio kufuata ukumbi mwembamba uliopo katika nyumba hiyo na alirejea akiwa ameshika udi unaowaka akamuwekea Hamis mbele yake jirani na pua zake.
"Kuna dhahama, kuna dhahama! Linataka kuikumba familia zetu nasema sikubali lazima nililizuie......nasema sikubali! Nasema sikubali! Nasema sikub...Aaaasrgh!" Hamis aliongea akionekana tayari ameshapandisha mashetani kichwani lakini alijikuta akikabwa shingoni hadi akashindwa kuongea akabaki akitoa ukelele wa maumivu huku akishika shingo yake hadi Ally akaanza kuogopa.
Hamis alianza kukoroma huku macho yakiwa yamemtoka kwa namna ya kutisha, Ally alipoona hivyo alinyanyuka akataka kukimbia lakini mtama mzito ulimkuta na yeye akaanguka chini huku mpigaji akiwa hamuoni. Alipoanguka alipigwa kofi la nguvu la kwenye shavu akatulia chini kama maji mtungini, baada ya Ally kuanguka ndipo Hamis alipohisi kuachiwa tangu aanze kukabwa. Alikohoa mfululizo akamkimbilia Ally akamtikisa Ally lakini hakuonesha dalili ya kuamka, Hamis alipagawa kabisa hasa alimpotazama Ally aliyetulia tu.
"Sijatumwa kuua bali nimetumwa kuzuia, Hamis umerithi majini kutoka kwa babu yako lakini ukataka kuyatumia kupambana na usichokiweza sasa nimeyakaba nikayaua na wewe utakiona. Huyo mwenzako pia kapata aliyostahiki kwa kiherehere chake" Sauti ilisikika ikitokea juu ya dari ikawa inavuma kama mwangwi ikapotea.
"Hamidaa!" Hamis aliita kwa nguvu huku akimnyanyua Ally.
"Abee Baba!" Sauti ya kike iliitika ikitokea chumbani.
"leta funguo za gari upesi" Hamis aliongea akielekea mlangoni, binti wa miaka takribani kumi na nane alimfuata kwa nyuma akiwa na ufunguo wa gari. Hamis alienda kwenye gari lake na yule binti akafungua mlango wa gari Ally akawekwa, geti kubwa lilifumguliwa na Hamis akaingia ndani akawasha akaliondoa kwa kasi.
Hali ya jiji la Dar es salaam ilikuwa tulivu na muda huo sehemu mbalimbali za jiji kulikuwa kuna watu wakiendelea na pilikapilika zao za kila siku, upande wa chuo kikuu cha Dates salaam wanafunzi walikuwa wakiendelea na masomo yao kama kawaida yao. Ilikuwa ni vipindi vya pili vya masomo baada ya vile vya asubuhi na wanafunzi wote wenye vipindi muda huo walikuwa wapo madarasani wakifundishwa.
Darasa la wanafunzi wanaosoma shahada ya sheria masomo yaliendelea kama kawaida na muda huo Professa wa chuo hicho alikuwa akifundisha darasani na wanafunzi walikuwa wapo makini sana kumsikiliza, katikati ya kipindi aliingia kaimu mkuu wa chuo darasani akiwa na mgeni ambaye hakufahamika ni nani hadi muda huo. Kaimu mkuu alimfuata Professa aliyekuwa anafundisha akamuuma sikio kwa sekunde kadhaa, Professa alimsikiliza kaimu mkuu wa chuo kisha akaafiki kwa kutikisa kichwa.
"Zaina Buruhan you are needed (Zaina Buruhan unahitajika)" Professa aliongea na wanafunzi wote wa humo darasani wakamtazama binti aliyenyanyuka katika viti vya katikati ya darasa.
"Take your things you are not return today, there is an emergence(Chukua vitu vyako hutarudi leo, kuna dharura)" Kaimu mkuu wa chuo aliongea na Zaina akachukua vitabu vyake akamfuata Kaimu mkuu wa chuo akiwa na yule mgeni kisha wakatoka nje.
Walipofika nje kaimu mkuu wa chuo alimtambulisha yule mgeni kwa Zaina na mgeni akaonesha kitambulisho chake akajieleza kwa Zaina dhumuni lake la kuja hapo chuoni.
"kuna dharura gani huko nyumbani?" Zaina alimuuliza yule mgeni
"nimetumwa tu kuja kukufuata mengine utayajulia huko huko nyumbani, Baba yako na mama yako wameniambia nisikueleze chochote" Yule mgeni alijibu, kwakuwa alikuwa ameshakamilisha taratibu zote za hapo chuoni Zaina na yule mgeni waliondoka kwa pamoja hadi kwenye gari la kifahari alilofika nalo yule mgeni wakaingia kwa pamoja na safari ikaaza, baada ya dakika thelathini walifika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakashuka wakaingia ndani ya majengo ya ndani ya uwanja sehemu ya ndege binafsi. Walipanda kwenye ndege ndogo ya kisasa ambayo ilikuwa ikiwasubiri wao na wakafunga mikanda, milango ya ndege ilipofungwa ndege ilianza kutembea taratibu ikielekea kwenye njia za kurukia na hatimaye ikaiacha ardhi ya jiji la Dar es salaam.
Baada ya dakika ishirini ndege hiyo ilianza kuinama kwa mbele kisha ikashuka chini taratibu, baada ya muda ndege hiyo iligusa ardhi kisha ikasimama papo bila kutembea ardhini kama ilivyozoeleka ndege ikigusa ardhi lazima itembee mitaa kadhaa ndiyo isimame.
"mbona ikitua hii ndege haitembei kama ndege zingine" Zaina alimuuliza yule mfanyakazi wa baba yake aliyemfuata chuoni.
"hii ni tofauti na ndege unazozijua, unaweza ukashuka sasa" Yule mgeni aliongea, Zaina alisogea mlangoni akafunguliwa na akakutana na ngazi ya kushuka kwenye ndege zenye rangi ya dhahabu tofauti na zile alizotumia kupanda. Aliposhuka chini kabisa alikutana na mandhari tofauti na ya uwanja wa ndege wa Majani mapana wa jijini Tanga, anga la eneo hilo lilikuwa jekundu kupitiliza na lisilo na wingu hata.
Mbele yake kulikuwa kuna kasri kubwa la kifahari lililotandazwa zulia jekundu kuanzia mlangoni hadi pale aliposimama, alipogeuka nyuma kuangalia ndege aliyoitumia ndipo aliposhtuka zaidi baada ya kubaini hakuwa amepanda ndege bali alikuwa yupo kwenye joka kubwa lenye miguu na masharubu kwenye mdomo na mgongoni alikuwa na kitu kama behewa la treni lilipambwa kwa vito mbalimbali na lilikuwa na ngazi ya dhahabu ambayo ndiyo ile aliyoshuka wakati anatoka.
Hadi kufika eneo hilo kumbe alikuwa amempanda mnyama anayejulikana kama dragon bila kutambua akijua ni ndege, alipoona yupo katika mazingira asiyoyaelewa aliachia ukelele wa uoga na kupelekea eneo zima pembeni ya zulia kuanzia kwenye ngazi alizoshukia hadi kwenye mlango wa kaari kuonekane kuna viumbe wenye sura za binadamu wakiwa wamekaa mstari mmoja.
"We mwanadamu hebu wacha kelele" Sauti ya yule mtu aliyemchukua chuoni ndiyo ilisikika ikitokea kisha yule aliyemdhania ametumwa na baba yake akatoka ndani ya behewa lililopo mgongoni mwa dragon akiwa ana mavazi sawa na viumbe waliojipakaza mstari.
"hapa ni wapi na wewe ni nani?" Zaina aliuliza kwa uoga.
"sina mamlaka ya kujibu maswali yako msubiri mwenye mamlaka akujibu maswali yako" Aliongea kisha akashuka akapiga hatua kumsogelea Zaina halafu akamwambia "angalia kule mlangoni kama ukijijua wewe ni mgeni, mkuu wa eneo hili mjukuu wa mfalme anaingia".
Alipomuambia hivyo alipiga goti la kiheshima na viumbe wote nao walipiga goti na mlio kama wa tarumbeta ulisikika na milango ya kwenye kasri ikafunguka, Zalabain alionekana akija hadi pale alipo Zaina huku akitabasamu akiwa na umbile lake la kibinadamu.
"Karibu sana Zaina nadhani majibu ya maswali yako yote utayapata" Zalabain aliongea akitabasamu.
"Wewe ni nani na hapa ni wapi?" Zaina aliuliza akiwa na hofu.
"Naitwa Zalabain mjukuu wa mfalme na hapa ni ndani ya makao ya himaya ya Majichungu" Zalabain alieleza
"Majichungu?! Ni wapi?" Zaina aliuliza kwa wasiwasi ingawa tabasamu la Zalabain lilimuonesha kwamba hakuna hofu yoyote.
"chini ya bahari" Zalabain alijibu.
"unasema?" Zain aliuliza akiwa na mshtuko kisha akaanza kurudi nyima kwa uoga. "Haina haja ya kurudia mara mbili Zaina utanijua zaidi ila inabidi ukae huku kwa ajili ya usalama wako tu na pia kwa ajili ya tahadhari, hutakiwi kuingizwa kwenye mtego wa panya bila kujijua wakati huna hatia, Hallain!" Zalabain alimueleza Zaina kisha akaita kwa sauti na kupelekea viumbe wengine wenye sura za wanawake warembo wenye asili ya bara la Asia wajitokeze mbele ya Zalabain.
"Kiongozi wetu tumeitika wito wako" Viumbe hao waliongea kwa utiifu wakiwa wamepiga goti moja kiheshima.
"Mchukueni huyu mmoja wa wanadamu wenye heshima huku kwetu.......Zayina utakaa hapa na usijaribu kuleta ubishi upate matatizo huku binadamu wanachukiwa kwani wao ndiyo chanzo cha kuwa na wingu jekundu kila muda humu kwenye himaya na mwanga wenye nuru haufiki kutokana na kuibiwa kito Dainun cha baba yangu Zaif" Zalabain aliongea na wale viumbe wakamchukua Zaina wakatoweka naye. Baada ya Zaina kuchukuliwa Zalabain aliingia ndani ya kasri akiwa ameongozana na yule kiumbe aliyemleta Zaina hadi katika chumba cha siri cha ndani ya Kasri hilo, huko ndani ya chumba hicho walikutana na Salmin akiwa amekaa kwenye kiti kimojawapo kilichonakshiwa na mapambo ya lulu. Zalabain na yule kiumbe waliketi kwenye viti vya aina hiyohiyo wakawa wanamtazama Salmin.
"je mmefanikiwa kuipata Dainun?" Salmin alimuuliza Zalabain
"hapana bado sijafanikiwa kuipata kwani kila anayetakiwa aende na maji nikimuuliza anasema hana" Zalabain alimueleza.
"Inabidi uipate hiyo ndiyo taji la kifalme litakaa kichwani mwako hata kama ukilipa visasi hadi ukamaliza bila ile hutakuwa mfalme na hata ukiipata hujalipa kisasi bado taji litakukataa vilevile" Salmin alimuambia Zalabain.
****
"Sawa nimekuelewa, enhe wewe Kainun niambie kazi niliyokuagiza imeendaje" Zalabain alimuuliza yule kiumbe aliyemchukua Zaina.
"Mtukufu mjukuu wa mfalme na mfalme wetu mtarajiwa kazi imeenda kama ulivyoniagiza kwa kumzuia yule mwanadamu anayeitwa Hamisi aliyepandisha vijini vyake akataka kuingilia kazi yako ya kurudisha nuru iliyopetea katika himaya yetu" Kainun alitoa maelezo kwa Zalabain.
"Vizuri kama umemzuia, je niambie ulimzuia vipi?" Zalabain alimpongeza kisha akahitaji kujua aliyoitumia kumzuia Hamisi asiingilie kazi yake.
"Baada ya yeye kuwapandisha majini wake kwenye kichwa chake niliamua kumkaba shingo yake hadi yakafa yote kisha nikampiga kofi moja yule mwenzake aliyetaka kuchochea kuharibika kwa kazi yako kwa kuleta udi unaowaka" Kainun alieleza kila kitu alichokifanya hadi Zalabain akatabasamu huku akitikisa kichwa kuashiria amependezwa na kazi yake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni