SHETANI ALINIITA KUZIMU (3)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Shiwawa Binasalaan Al Jabry
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Akiwa ametulia alisema; “Nimefika hapa baada ya kuitwa na nyinyi, naomba mniambie kinachowasibu ili niwasaidie kisha nirudi kwenye makazi yangu.”
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Baada ya kutoa kauli hiyo, yule dogo alijongea mbele ya malkia na kumsujudia na kumwambia alimwita kwa sababu katika himaya yao walipata mgeni.
Kufuatia kuambiwa hivyo, malkia alitikisa kichwa na kuuliza; “Huyo mgeni yupo wapi?” Alipouliza hivyo, dogo alimuonesha kwa kidole nilipokuwa nimekaa ndipo
malkia alitikisa kichwa kuonesha alifurahi. “Kwahiyo mlitaka nimfahamu mgeni wetu?” alimwuliza yule mtoto mchawi. Dogo alimwambia licha ya kumfahamu
walihitaji nipewe nguvu ili nianze kufanya kazi ya kichawi kwa sababu tayari nilikwisha kabidhiwa mkoba wa bibi yangu.
Yule dogo alipotoa kauli hiyo, malkia aliinama sijui alifanyaje nikashangaa kuona mkia wake umenifikia, ukaanzaa kunipigapiga mwilini na kichwani. Wakati
nikipigwa na mkia huo, mwili ulinisisimka na kujikuta nimepata nguvu nyingi za kichawi, lakini kabla malkia hajaondoka aliniambia kuanzia siku hiyo niombe
kitu chochote nitapata. Baada ya kutoa kauli hiyo kilitokea kimbunga, kufumba na kufummbua, malkia alitoweka na kimbunga kikakoma.
Tukio hilo liliwafurahisha sana wachawi wenzangu ambao walirukaruka huku na huko na kuanza kuimba nyimbo hadi walipoamriwa kutulia na yule dogo. Kwa kuwa
nilikuwa nimechoka sana na niliambiwa nikitaka kitu chochote niombe kitakuwa, nikaomba utokee ungo ‘ndege’ya wachawi. Niliamua kuomba usafiri huo kwa sababu
nilikuwa nimechoka sana na nilihitaji kurudi nyumbani, nikasema: “Ungo tokea!”
Kwa mara ya kwanza niliamini kweli uchawi upo na ulikuwa na nguvu, ungo niliouomba ulitokea na kuja kutua mbele yangu. Wachawi wenzangu walinishangilia sana,
nilichokifanya kabla sijapanda na kuanza safari nilikwenda kuchukua mkoba wa kichawi wa marehemu bibi yangu.
Nikiwa na mkoba huo nilikaa ndani ya ungo na kutamka maneno haya: “We ungo naomba unirudishe nyumbani kwetu kwa sababu nimechoka sana.” Baada ya kutoa kauli
hiyo, kilitokea kimbunga kikauzoa ule ungo na kuupaisha juu, katika hali ya kushangaza nikauona ukitua juu ya nyumba yetu. Bila ya kuelekezwa na mtu,
niliteremka na kwenda kwenye pembe ya ukuta nikapitia na kuingia chumbani kwangu. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana, hakuna aliyenishtukia nikauchukua mkoba wa
bibi na kwenda kuuweka chini ya kitanda ambako ilikuwa vigumu kuonwa na watu wengine.
KWA kuwa ilikuwa usiku sana, baada ya kuuficha mkoba huo sehemu ambayo ilikuwa siyo rahisi mtu mwingine kuuona, nilipanda kitandani nikalala. Haukupita muda
mrefu nilipitiwa na usingizi mzito, kufuatia uchovu niliokuwanao nilala hadi saa nne asubuhi ambapo niliamka. Baada ya kunawa usoni, nilichukua jembe na
kuanza kuelekea shambani. Nikiwa sijafika mbali, nilimuona baba mdogo aliyekwenda shamabi alfajiri akirudi.
Nilipokutana naye hata bila ya salamu aliniuliza nilikuwa nakwenda wapi muda ule, nilimfahamisha shambani. Baada ya kumpa jibu hilo, aliniuliza muda ule
ilikuwa saa ngapi nikwambia saa nne, kwa hasira alisema; ‘mpumbavu sana wewe,huu ndiyo muda wa kwenda shambani? Haya rudi nyumbani.’ Nilipobaini baba
alichukia, nilirudi nyumbani nikaweka jembe. Kwa kuwa sikuwa na kazi nyingine niliingia chumbani ambapo nililala hadi saa sita na nusu mchana nikaamka ili nipike.
Kabla sijaanza mapishi niligundua ndani hakukuwa na maji ndipo nilikwenda kisimani ambako nilikuta kuna umati wa watu wakisubiri kuchota maji. Kufuatia shida
ya maji, nilikaa huko hadi saa kumi jioni nikarejea nyumbani. Baba mdogo alichukizwa sana na kitendo cha kuchelewa kurudi. Aliponiuliza nilichelewa wapi,
nilimfahamisha jinsi kisimani kulivyokuwa na watu wengi, hakunielewa akaanza kunifokea kwamba nilikuwa ninacheza. Kwa hasira alizokuwanazo alichukua fimbo na
kuanza kunitandika sehemu mbalimbali, nilipata maumivu maka sana,
Alipomaliza kunicharaza bakora aliniambia nikachukue mpunga ndani kisha niutwange kwa ajili ya mlo wa usiku. Kwa kuwa ndani hatukuwa na kinu, nilikwenda
kuazima kwa jirani yetu kisha nikaanza kufanya kazi hiyo. Kawaida unapotwanga mpunga lazima utamwagika chini, wakati nikiendelea na zoezi hilo kwa bahati
mbaya ulimwagika. Baba aliyekuwa ameketi alipoona mpunga umemwagika alikasirika ambapo alinifuata na kunizaba kibao ambacho kilinichanganya akili.
Kitendo hicho kilinikera, nilimwambia kwamba nilimvumilia sana na kufikia kikomo hivyo lazima nitamkomesha. “Wewe mtoto unasemaje… utanikomesha mimi… kweli wewe ni mwenda wazimu,”
Kutokana na hasira nilizokuwanazo, nilimwambia ile nyumba yake ataiona chungu na kukimbia kwani nilikuwa nimechoshwa na tabia yake ya kunipiga bila sababu.
Nilipomwambia hivyo alisema ataona kati yake na mimi nani mjanja na kuniambia nimuombe msamaha kwa kauli yangu, nikamwambia sitamuomba na kusisitiza lazima
ataikimbia nyumba yake. Baada ya kumwambia hivyo, niliacha kutwanga mpunga na kuingia chumbani kwangu, ile naingia nilishangaa kukuta chumba chote kikinuka
harufu ya bangi. Kule kwetu tunaziita "NJEMU"
Moja kwa moja nilijua aliyevuta bangi alikuwa ni yule ndugu yangu tuliyekuwa tukilala pamoja, nikachukia sana. Kukufafanulia ni kwamba hakuna kitu ambacho
akipatani na wachawi kama harufu ya bangi, nilifungua dirisha na mlango ili harufu itoke nje. Kwa hasira nilizokuwa nazo, nilipanga kumkomesha ndugu yangu huyo.
KWA hasira nilizokuwanazo, nilipanga kumkomesha ndugu yangu huyo ambaye sikuelewa alikuwa amekwenda wapi, nikaamua kumsaka kwa kutumia darubini ya kichawi.
Kukufafanulia hapo ni kwamba wachawi wana vifaa vyao maalumu vya kuwaangalia maadui zao walio mbali, baada ya kumwangalia nilimuona amekaa maskani akicheza
bao. Nilichokifanya nilichukua ule mkoba wangu wa kichawi nikachanganya ndumba kama nilivyofundishwa nikamuweka roho ya kupakimbia pale nyumbani, yaani tangu siku ile asirudi tena.
Baada ya kufanya uchawi huo, nilitoka na kuendelea kufanya mambo yangu huku nikiwa na hasira kufuatia baba mdogo kunipiga bila sababu. Hata hivyo, nilipanga
kumhamisha pale nyumbani baada ya kupita siku sita, kwa upande wa yule kijana ni kweli hakurudi nyumbani na tulipokutana njiani alinichangamkia kwa furaha
kuliko zamani. Nilipomwuliza kwa nini hakupenda kurudi nyumbani, akaishia kucheka na kunieleza kwamba aliamua tu mwenyewe.
Kumtega nilimwuliza kuhusu kuja kuchukua nguo zake, akaniambia alikuwa na zingine, nikajua uchawi wangu ulifanya kazi. Niliishi na baba mdogo kwa chuki hadi
ilipofika siku ya tano ndipo niliamua kumkimbiza pale nyumbani ili nipamiliki.
Usiku wa manane kukiwa kimya muda ambao wachawi huwa huru kufanya mambo yao, niliamka na kutengeneza ulosi kisha nilinuiza kwamba baba mdogo aondoke na
asirudi tena. Nilipomaliza, nilimfuata kiuchawi chumbani kwake na kumuwekea roho ya kuikimbia nyumba yake kisha nikarudi kulala chumbani kwangu. Kulipokucha
niliamka na kumkuta baba mdogo akiwa anaota jua la asubuhi, aliponiona alinichangamkia sana tofauti na siku nyingine tangu tulipokorofishana.
“Kaloli mwanangu umeamka salama?”
Aliponiuliza hivyo nilimwambia nilikuwa mzima wa afya ndipo alinieleza kwamba alihitaji kuzungumza na mimi, nikamwambia sawa. Baba mdogo aliniambia kwamba
nitakapomaliza kazi zangu ndipo tutaongea, nikamwambia hakukuwa na shida. Kama tulivyokubaliana, baada ya kumaliza kazi nilimfuata baba mdogo ambaye siku
hiyo hakwenda shambani ndipo alinifahamisha kwamba alikuwa anataka kuhamia kwao.
Alipotoa kauli hiyo nilifurahi sana kwani nilijua uchawi wangu ulifanya kazi, nikamwuliza kwa nini aliamua kurudi kwao na pale atapaacha na nani! Baba
aliniambia kwamba nyumba na kila kitu kilichokuwepo pale vitakuwa mali yangu, moyoni nikasema; ‘mimi si nilikuambia utaikimbia nyumba yako ukabisha…mimi
ndiyo Kaloli!’ Kumdhihaki nilimchimba anieleze sababu iliyomfanya aondoke, akaniambia alichoka tu kukaa pale hivyo aliamua kwenda kuishi na wazazi wake.
“Hivyo ndivyo nilivyoamua, nikiondoka sitarudi tena hapa…huu mji nimekuachia na hakuna mtu atakayekusumbua,”
Baada ya baba kuniambia hivyo, nilimuuliza alitarajia kuondoka lini, akasema siku iliyofuata asubuhi na mapema. Kauli hiyo ya baba ilinifurahisha sana kwani
nilijua muda wa kujitawala pale nyumbani uliwadia, jioni ilipofika baba aliniita na kuniambia kwamba ilitokea ghafla tu kupachukia sana pale alipokuwa akiishi.
Nilipomuuliza sababu za kupachukia alisema sijui anapaonaje ni heri arudi akaishi na wazazi wake, nikamwambia ulikuwa uamuzi wa busara.
Siku iliyofuata baba akiwa na furaha aliniaga ambapo nilimsindikiza akaondoka akiwa na begi la nguo tu, huku nyuma nikajisifu kwa kumkomesha. Kukufafanulia
hapo ni kwamba wachawi huwa hawana huruma wanapoamua kumroga mtu, huwa hawajali kama mtu husika ni mzazi au ndugu yake wa damu. Baba alipoondoka kwa furaha
niliyokuwa nayo, nilimchinja kuku kisha nilimchoma na kumla ikiwa ni kujipongeza kwa kumuondoa pale nyumbani kwa sababu ndiye alikuwa kikwazo.
Kwa kuwa nyumba ilikuwa kubwa, siku ya pili nilimtafuta dalali na kumwambia anitafutie wapangaji wanne, ambapo walipatikana watatu. Wapangaji hao wakiume
walikuwa na wake zao ambao walikuwa wazuri sana, baada ya kupita siku mbili yule dalali alimleta dada mmoja mzuri ambaye hakuwa na mume, nikampangisha chumba
kilichobaki. Nilipoishi na wapangaji hao kwa muda wa miezi minne ndipo niliamua nianze kuwawangia usiku, lengo langu lilikuwa ni kuwadhibiti kwa kila kitu.
Mpangaji wa kwanza kumchezea alikuwa wa chumba cha tatu kushoto kutoka nilichokuwa nalala aliyekuwa na mke mdogomdogo mzuri.
Nakumbuka siku hiyo usiku wa manane, niliamka kichawi yaani nikiwa sina nguo mwilini na kuingia katika chumba cha wapangaji hao. Baada ya kuingia niliwakuta
wakiwa wamelala, nilimtia roho ya usingizi yule mwanaume kisha nikambeba na kumlaza chini akiwa hajitambui. Akiwa amelala fofofo, nilipanda kitandani na
kuanza kufanya mapenzi na mkewe hadi niliporidhika ndipo nilimbeba yule mwanaume na kumlaza kitandani kisha nikamtoa ile roho ya usingizi.
Baada ya kufanya hivyo, nilirudi chumbani kwangu nikajilaza kitandani nikiwa mwenye furaha kufuatia kitendo nilichomfanyia yule mke wa mtu. Kwa kuwa usiku huo nilikuwa na hamu sana ya kula nyama, sikuweza kupata usingizi kabisa, nikaamua kuiita ndege ya kichawi (ungo). Baada ya kufanya hivyo, hazikupita dakika nyingi nikasikia kitu kimetua sakafuni tii, nilipoangalia niliuona ungo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni