DHAMANA (13)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA KUMI NA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"Mimi hapa nimeugusa tu kwa mkono mmoja nikausukuma ukafunguka" Annet alijibu na akazidi kuwashangaza watu waliomo humo ndani hadi Msemaji mkuu wa kampuni naye akazidi kushangaa majibu anayoyatoa binti yake huyo mdogo.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Samahani kwa kuwavamia mkutano wenu na kuwakatisha, nimetumwa tu kuwaeleza ujumbe niliopewa ambao unawahusu nyinyi na ujumbe hamtakaa kuusambaza wala kusimulia kwa wengine kwani mlipewa nafasi mkaichezea. Ni hivi siku iliyopita baada ya kufa kwa bosi wenu nyinyi mlipoondoka hapa kwenye kampuni hii ilikuwa ndiyo salama yenu ila kwakuwa mmerudi, nimeambiwa niwaambie kuwa hili ndiyo kaburi lenu" Annet aliongea kwa sauti nzito tofauti na ile ya kitoto aliyokuwa anaongea tena akatoa maneno yaliyozidi kuwachanganya.
"We Annet unasemaj..?" Msemaji wa kampuni hiyo alishindwa kumalizia kauli yake baada ya Annet kupotea katika mazingira yasiyo ya kawaida, jengo zima lilianza kutingishika kama limekumbwa na tetemeko la ardhi vioo vya madirisha vikaanza kuvunjika na kuzidi kuwatia wafanyakazi wote hofu. Wafanyakazi walipojaribu kukimbilia mlangoni ili watoke walikuta milango ikiwa imejifunga, mtetemeko wa jengo hili ulizidi kuwatia hofu na wakajikuta wakitaja jina la muumba kwa mara ya kwanza baada ya kutaja majina ya mama zao kwa muda mrefu.
****
LAS VEGAS
MAREKANI
Wakati wafanyakazi wa kampuni ya Matro wakikumbana na janga lililotokea hapo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, upande mwingine wa bara la Amerika ya kaskazini katika mji wa Las Vegas nchini Marekani majira ya saa nne usiku kwa masaa ya huko ambapo yapo masaa kumi nyuma ya Tanzania. Kijana mwenye mavazi ya anasa zaidi alionekana akiingia ndani ya klabu maarufu ya usiku ya jijini humo, Falzal ndiyo jina lake huyu kijana mwenye kila aina ya majigambo na mwenye jeuri ya kuchezea pesa katika starehe. Ingawa bado ni kijana msomi na aliyekuja nchini humo kwa ajili ya masomo, aliishi mithili ya mtu maarufu wa jijini humo.
Alipoingia ndani ya klabu hiyo ilikuwa kama kawaida yake lazima aende kwenye meza ya wacheza kamari kama kawaida, hiyo ndiyo ilikuwa starehe yake nyingine ambayo ilimuingizia pesa nyingi na kumfanya aishi maisha ya kifahari sana jijini humo. Aliwasalimu watu anaocheza naoo kamari kila siku akiwemo Miliver mcheza kamari maarufu hapo La vegas kisha akaketi, alimuangalia Miliver akatabasamu kisha akasema, " naona leo umekuja kunikuzia mtaji kama kawaida yako"
"Ha! Ha! Ha! Leo unaliwa wewe ngoja utaona tu"Miliver aliongea huku akicheka.
Faiz alipotaka kuchukua kete alishtushwa na mlio wa simu kutoka kwenye suruali yake na ikamlazimu awaombe radhi wachezaji kamari wenzake halafu akasogea pembeni sehemu isiyo na sauti nyingi na akaipokea simu.
"Baba vipi mbona usiku hivi?" Falzal aliongea baada tu ya kumsalima aliyekuwa anaongea naye kwenye simu.
"kuna tatizo gani baba mpaka nirudi nyumbani si uniambie tu nielewe hapahapa"Falzal alizidi kulalamika akiona anaharibiwa starehe zake.
"Sawa baba nakuja kesho asubuhi" Falzal alikata simu kisha akionekana ni mwenye uso wa masononeko kisha akaondoka humo kwenye klabu ya usiku pasipo kumsemesha yeyote na uso wake ulikuwa unalengwa machozi, aliingia ndani ya gari na akaondoka hapo akionekana ni mwenye kuchanganyikiwa sana baada ya kupokea simu kutoka kwa baba yake.
****
RASKAZONE
TANGA
Wakati Faizal akiondoka kwenye klabu ya usiku majira ya saa nne usiku kwa saa za Marekani, huku Tanzania majira kama hayo ya saa nne ila asubuhi kuna kitu kingine kabisa kigeni ndani ya nchi hii kilikuwa kinaanza kutokea. Tukio la aina yake ndiyo lilianza kuonekana kwa watu waliopo karibu na jengo lenye ofisi za makao makuu ya kampuni ya mafuta ya Matro, jengo hilo lilianza kutetemeka na taratibu likaanza kuporomoka kuelekea chini likivunjika vioo pamoja na kuta zake zikiporomoka.
Lilikuwa ni tukio la kustajaabisha sana kwani eneo la chini ya ardhi lenye msingi wa jengo hilo lilipasuka kisha likafunguka na jengo zima likaingia chini ya ardhi huku eneo zima linalomilikiwa na kampuni ya Matro likiwa lunatetemeka kama kuna tetemeko la ardhi, tetemeko hilo lilipokuja kutulia eneo lenye msingi wa jengo la Matro lilibaki kama urefu wa kaburi lililojengewa. Jambo la namna hiyo halikuwahi kutokea nchini Tanzania ingawa huwa inakumbwa na matukio makubwa, tetemeko la ardhi lililoikumba eneo lenye ukubwa wa ekari moja ambalo ndani yake ndiyo zilipo ofisi kuu za kampuni ya Matro halijawahi kutokea hata katika nchi nyingine ndani ya dunia hii.
Baada ya muda mfupi kikosi cha uokoaji kilikuwa kimeshafika katika eneo hilo ambapo walibaki wakishangaa tu kwani hawakuwa na kifaa chenye uwezo wa kuchimba chini lilipodidimia ghorofa hilo wakati linavunjika, kikosi hicho kilichokuja kwa ajili ya uokoaji na chenye ari ya kufanya uokoaji kilijikuta kikishindwa kufanya uokoaji kutokana na ugumu walioukuta eneo hilo lililohitajika kufanyiwa uokoaji.
Wakiwa wamesimama hapo mlio wa mkoromo wa simu ys upepo ya kiongozi wao ilisikika na ikamlazimu kiongozi huyo atoe simu hiyo ya upepo na kuiweka mdomoni kisha akazungumza kwa kutaja eneo alipo halafu akajitambulisha, sauti yenye kukoroma ilisikika ikiongea ambapo ilisikika vyema kwa kiongozi ambaye alibaki akiwa amepigwa na butwa halafu akawaangalia wenzake huku akihema kwa kasi.
"Jamani sheli zote za Matro zinaungua sasa inahitajika timu kubwa ya msaada ya kusaidia uokoaji, sasa hatuwezi kukaa hapa mpaka mashine ya uokoaji kutoka Dar es salaam iletwe. Team twendeni tukasaidiane na wenzetu kwenye uwezekano wa kutoa msaada na sio kubaki" Kiongozi huyo aliongea kisha akaanza kukimbia yalipo magari yao na wenzake wakawa wanafuata nyuma, magari ya kikosi cha uokoaji yaliondoka eneo hilo la Raskazone kwa kasi yakiacha mamia ya raia kutojua sababu ya wao kuondoka eneo hilo
****
Siku iliyofuata nyumbani kwa Mzee Buruhan tayari turubai kubwa lilikuwa limeshafungwa katika eneo la wazi la nyumba hiyo pamoja na maeneo jirani na eneo hilo, hadi muda huo tayari watu walishajaa nyumbani hapo kutokana na umaarufu wa watoto wa mzee Buruhan waliofariki katika vifo vya kutatanisha. Upande wa kinamama kulisikika vilio kutoka kwa watu wa karibu ambao walikuwa na uchungu wq kuondokewa watu hao, ilikuwa ni siku ya kuhuzunisha kwa familia nzima ya Mzee Buruhan kutokana simanzi iliyowakumba.
Watoto wa mzee Buruhan waliosalia ambao ni ,Ally,Hassan na Falzal tayari walikuwa wapo msibani wakiwa na huzuni sana huku kaka yao mkubwa Shafii akiwa yupo hospitali kutokana na ajali aliyopata. Taratibu zote za mazishi ziliendelea kama zilivyopangwa na baada ya adhuhuri ndugu wawili wa damu walizikwa kwa wakati mmoja, baada ya mazishi watu walitawanyika na kuwaacha watu wa karibu wa marehemu wakiwa hapo msibani kuendelea na taratibu zingine zilizokuwa zimewekwa hapo awali katika ratiba ya msiba huo uliowagusa wengi kutokana na vifo vilivyowapata ndugu hao wawili wa damu.
****
HIMAYA YA MAJINI YA MAJI CHUNGU
Wakati mazishi ya Hamid na Hussein yakiwa yanaendelea yalikuwa yakishuhudiwa kwenye kioo kikubwa mithili ya sinema kilichopo katika chumba maalum ndani ya kasri la himaya ya Majichungu, Zalabain na Salmin walikuwa wakishuhudia kila kitu hadi maziko yanakamilika, baada ya kumaliza kuangalia tukio hilo waliangalia pia tukio la kuanguka kwa ghorofa la kampuni ya Matro na kuungua kwa sheli zote za kampuni hiyo.
"kazi nzuri ewe mjukuu wa mfalme nadhani bado magugu makuu manne ili kazi yetu ikamilike na hakikisha kila mmoja anaondolewa kwenye ardhi waliyokufanyia ubaya yaani Tanga na ukimmaliza yeyote nje ya Tanga utakuwa umefanya kazi bure tu" Salmin aliongea
"Nashukuru kwa kunifahamisha ewe jini mwenye nguvu uliyezaliwa milenia moja na robo tatu iliyopita, naishukuru sana nafsi yangu iliyonizuia kumuua yule mmoja wao anayesoma Marekani. Usiku kwa masaa ya Marekani tayari nilikuwa nimeshafika kwenye eneo maarufu analochezea kamari yule binadamu kwa lengo moja tu la kummaliza. Nilitumia njia ya kujigeuza Miliver ambaye ni mchezaji kamari maarufu jijini Las Vegas ambaye nilimlaza usingizi ili asije kucheza kamari siku hiyo. Nilikuwa na kila njia ya kumuangamiza lakini nafsi ilinizuia kufanya hivyo na mimi nikaacha, nafikiri nisingeisikiliza nafsi ningekuwa nimejipa hasara" Zalabain aliongea
"ungejipa hasara haswa kwani ufalme ungeupata kwa njia ya kafara ya ndugu yako wa damu kama ungefanya uzembe huo" Salmin alisisitiza kisha akaendelea kusema, "hakikisha yule binadamu harudi tena Marekani yaani kwa lugha rahisi ni kwamba anahitajika awafuate ndugu zake"
"Hilo ondoa shaka nitalifanyia kazi haraka iwezekanavyo na inabi......." Zalabain alimuambia Salmin na alipotaka kuendelea kuongea Salmin alimzuia huku macho yake yakibadilika rangi na kuwa mekundu yaliyokuwa yanawaka kisha yakarudi katika hali ya kawaida.
"vizuizi vya kuingia vya kuingia kwenye himaya hii vinavyozuia tusivamiwe vipo wazi" Salmin aliongea huku akisimama kwa haraka.
"Ndiyo ni kweli vimefunguliwa maana kuna mfalme wa himaya ya jirani ana ziara hapa kwenye himaya yetu" Zalabain aliongea
"Ni mtego huo hao ni watu wa jamii ya kishetani ya KAKIN wametuma majini yao kulipa kisasi, wale wabaya wako mmoja wao ni mwanachama wa jamii hiyo na hao majini wameshaingia inabidi tuwazuia kabla hawajaleta madhara sasa hivi" Salmin aliongea kisha akapotea hapohapo na Zalabain naye akapotea akatokea nje ya Kasri akamkuta Salmin akiangalia juu ya anga la himaya yao ambalo limebadilika rangi kutoka ile rangi nyekundu hadi nyeusi isiyopendeza kiasi cha kuleta giza.
"tangu Dainun iibiwe hatujawahi kupata giza sasa jiulize giza hili linatokana na nini kama sio kuvamiwa huku, agiza askari wa baragumu apulize baragumu la hatari ili raia wote waingie majumbani mwao na hii vita ni yetu wasihusike" Salmin aliongea huku akimtazama Zalabain ambaye alipiga kofi moja akatokea kiumbe wa ajabu mbele yake.
"Ndiyo mtukufu mfalme mtarajiwa" Yule kiumbe aliongea kwa utiifu.
"puliza baragumu la hatari haraka iwezekanavyo raia wote waingie majumbani mwao" Zalabain alitoaamri kwa kiumbe huyo, kiumbe huyo aliitikia kwa ishara kisha akapotea papo hapo na baragumu la hatari muda huo huo likaanza kulia.
Salmin na Zalabain walipaa juu huku macho yao yakiwaka kama nuru ya nyota angani, walipofika juu walitanua midomo yao wakapuliza na ukatoka upepo mzito sana ambao uliliondoa giza lote kama unavyoondoka ukungu na mwanga ukarudi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni