DHAMANA (14)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Salmin na Zalabain walipaa juu huku macho yao yakiwaka kama nuru ya nyota angani, walipofika juu walitanua midomo yao wakapuliza na ukatoka upepo mzito sana ambao uliliondoa giza lote kama unavyoondoka ukungu na mwanga ukarudi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Mbele yao walikuwa wakitazamana na viumbe wenye sura za ajabu tena wenye rangi nyeusi, miili ya viumbe hao haikuwa ikieleweka ilivyo ilikuwa na umbile kama tambara bovu jeusi. Viumbe hao walikuwa wamebeba silaha za aina mbalimbali za kijini wakiwa na hasira za dhahiri, viumbe hao wakihema walikuwa wanatoa moto mdomoni kwa jinsi hasira zilivyokuwa zimewazidi.
"Jisalimisheni kwa usalama wa jamii yenu yote hii" Mmoja wa wale viumbe aliongea.
"Ondokeni kwa amani kwa usalama wenu na si mpaka tutumie nguvu" Salmin aliongea kwa upole sana
"Naona jeuri sasa ngoja tuanze na wewe" Yule kiumbe alisema kisha akamnyooshea silaha yake Salmin iliamuangamize lakini alijikuta anaangamia yeye baada ya shoti kali zilizotoka kwenye macho ya Salmin kutua mwili mwake.
Wenzake waliosalia walijiandaa kuwashambulia Salmin na Zalabain lakini walichelewa kwani walijikuta wakizungushwa na upepo wa ghafla uliotengenezwa na Zalabain ambao uliwafunga kama wamefungwa na kamba ngumu kisha waliangamizwa wote kwa pamoja kwa kuunguzwa na moto uliotoka mdomoni kwa Salmin uliowaunguza wote wakawa majivu.
"Habari yao imekwisha funga kizuizi" Salmin aliongea kisha akashuka chini taratibu na Zalabain akaenda juu zaidi akanyoosha mkono mmoja uliotoa mwanga wa ajabu ulioelekea juu halafu akashuka chini taratibu baada ya kumaliza kazi yake.
"hakuna atakayeweza kuivamia himaya ya majichungu nikiwa mimi nipo na himaya hii itadumu mpaka mwisho" Salmin aliongea kumuambia Zalabain kisha akainama chini kiutiifu akapotea mbele ya macho ya Zalabain.
Baragumu la kuashiria hakuna hatari tena katika himaya hiyo lilipulizwa na raia wa himaya hiyo wakatoka majumbani mwao kuendelea na shughuli nyingine za kawaida na Zalabain akarudi ndani ya Kasri la ufalme.
****
Wakati majini waliotumwa kuleta maafa wanauawa upande mwingine kwenye chumba chenye watu waliovalia majoho meusi ambacho kilionekana kwa muonekano kilikuwa kipi chini ya ardhi. Kilikuwa kimetawaliwa na jazba miongoni mwa watu waliomo humo ndani, kiongozi wa watu ndiyo alionekana kuwa na jazba za wazi hadi akavua kofia ya joho lake akasema kwa hasira, "Haiwezekani! Haiwezekani! Hussein wamuue na majini yetu wayaue, lazima! Lazima! Tulipe kisasi kwa ajili ya Hussein mwanachama wetu".
Sauti ya kiongozi huyo ilisikika kwa nguvu na kusababisha tetemeko zito litokee kwa sekunde kadhaa na lilipotulia ilisikika sauti ikisema, "Dalipso Londo usiingie kwenye vita isiyokuhusu hata kidogo, Hussein alikuwa ana janga lake tofauti alilolichuma kabla hajaungana nanyi,nimetumwa na mkuu wa wakuu nikuonye ukae mbali na tukio hilo na uhakikishe unamtia nguvuni Qwanta Alfred Lumaki aliyetutia hasara".
Wote walikuwa wameinama kiutiufu na waliinua vichwa vyao baada ya sauti hiyo kuacha kuzungumza.
"ndiyo mkuu" Dalipsol Londo alitii.
"kazi ianze sasa hivi ili dunia iwe chini yetu tukiipata damu ya Alfred Lumaki na Qwanta wenzake,ndiyo furaha ya mkuu wa wakuu ni ushindi kuwa upande wetu na si vinginevyo" Sauti ile iliendelea kusikika kama mwangwi kisha ikapotea haraka sana, Dalipsol Londo aliwageukia wenzake akawaambia, "vita ya mamba kiboko haimtii wahka kwani amani hutawala hata bila kuingilia hiyo vita hivyo haina haja ya yeye kuingilia, ndiyo hivyohivyo vita ya Hussein na familia yake haitufai sisi kuingilia ile inawahusu yeye na familia yake na wala haivurugi hata kipengele cha kazi yetu".
Baada ya Dalipsol Londo kusema maneno hayo alipiga kofi mara moja na mlango wa eneo walilopo ukafunguliwa, aliingia mtu aliyevaa joho jeusi akiwa anavuta kitoroli kidogo kilichofungiwa kondoo mweusi na pembeni kulikuwa kuna kifaa chenye ncha kali. Toroli hilo lilivutwa hadi mbele ya Dalipsol Londo kisha yule mtu akamkabidhi kifaa chenye ncha kali huku akiwa ameinamisha kichwa kwa heshima, Dalipsol Londi alikipokea kifaa hicho kisha akasema, "ni muda kuanza ibada kuu zaidi ya zote kwa mkuu ambaye ndiye mungu yetu mkuu, hatuna Mungu mkuu zaidi yake mkuu wa wakuu".
Alipomaliza kutamka maneno hayo alimtoboa yule kondoo shingoni kisha chombo kikubwa kikakingwa chini, damu ya yule Kondoo iliingia ndani ya chombo hicho hadi kikajaa na Kondoo aliondolewa na yule mtu aliyemleta akiwa bado anatapatapa kutokana na jeraha lililotobolewa na Dalipsol Londo. Damu ile ya Kondoo ilitiwa kwenye kwenye bilauri zilizotengenezwa na madini ya fedha na zikasambazwa kwa watu waliokuwa wapo humo ndani, kila mmoja alikamata bilauri yake na wakazinyanyua juu kwa pamoja huku vichwa wakiviinamisha.
"Kwa jina la mkuu wa wakuu mwenye mamlaka kuu ya kutupa nguvu pamoja na pumzi kuu" Dalipsol alitamka maneno hayo huku bilauri akiwa ameinua juu kama wengine, alipomaliza kutamka maneno hayo aliinywa damu ile huku wenzake wakifanya hivyo hivyo.
Kakin ni jamii ya watu wanaoabudu nguvu za giza ambayo ilianzishwa miaka mingi iliyopita huko mashariki ya mbali na iliingia Afrika miaka mingi iliyopita kupitia waziri mkuu wa utawala wa Roma aliyetoroka katika himaya ya Roma kuepuka kuuawa na mtawala wa himaya hiyo aliyekuwa anaitwa Miltonus baada ya kubainika ni mwanajamii wa Kakin. Bwana huyu aliitwa Hilainus aliingia barani Afrika na akapokelewa kwa ukarimu sana kama ilivyo kawaida ya Waafrika kupokea wageni kwa ukarimu, aliingiza falsafa za jamii ya Kakin kwa siri sana hadi akajipatia wafuasi kutoka pande mbalimbali za Afrika. Hadi anafariki tayari alikuwa na familia yake na jamii hiyo ya siri ilikuwa imeshasambaa mhalimbali na ilikuwa inaendeshwa kwa siri mno kwani habari za uovu wa jamii zilikuwa zishasambaa barani kote ingawa haikujulikana ni nani aliyeileta Afrika.
Usiri wa ibada za jamii hii ulizidi sana pale mtawala wa himaya ya Soghai Sunni Ali alipowaua kwa kuwakata vichwa watu waliobainika ni watumishi wa jamii hiyo, asilimia kubwa ya himaya za kiafrika tayari zilikuwa zimeufuata uislamu baada ya kufanya biashara na waarabu kwa muda mrefu kipindi ambacho himaya ya roma bado inanyanyasa watumwa. Hadi imani za Kakin zinaingizwa barani hapa tayari Uislamu ulikuwa umeshasambaa sana, juhudi za upambanaji dhidi ya jamii haramu ziliwahusisha wanajamii wote wa Afrika bila kujali tofauti ya kiimani iliyokuwa ipo kati ya waislamu na ambao walikuwa wana imani za kizamani za kuabudu miti na mapango ambao walitofautiana sana kiimani na Kakin ingawa walitegemea majini walioiita mizimu. Wote kwa pamoja walipambana sana na udhalimu na Kakin na baadaye hatimaye waislamu walijitoa baada ya kuzaliwa mtoto aliye na mchanganyiko wa mashariki ya mbali na Habaishi waliokuwa wafuasi wa Waothodoksi, mtoto huyu alipewa jina cheo cha Qwanta ambaye katika uzao wake walishirikishwa majini weupe wanaojulikana kwa jina la majini wa nuru. Majini hao walikuwa wametengana na wale wa giza waliokuwa wako pamoja na Kakin, majini hawa walikuwa wapo tayari kuona jamii nzima ya Kakin inaangamia ili dunia iwe huru na walimpatia nguvu za ajabu mtoto huyo ili alete mapinduzi katika, kisa hicho kilichoelezewa na mwandishi wa mkasa huo aitwae Hassan Omar Mambosasa alichokipa jina la KUANGUKA KWA KAKIN kuanzia kitabu cha kwanza na hadi cha mwisho ndiyo kinaelezea kinagaubaga juu ya jamii hii na kuanguka kwake.
****
Baada ya siku kadhaa tangu mazishi ya Hamid na Hussein yafanyike Falzal alipanga arudi Marekani na alienda kukata tiketi katika ofisi za shirika la ndege la Ermirates za jijini Tanga lakini alijikuta akishindwa kuondoka baada ya kuambia kuwa hakuna ndege hata moja iliyokuwa ikiingia Marekani kutokana na hali ya ukungu iliyokuwa imetanda katika bahari ya Antalantiki, habari hiyo ilimnyong'onyesha sana na akajikuta akibakia kwenye jiji la Tanga na hata alipojaribu kwenda jiji la Dar es salaam ili akaendelee na starehe napo alijikuta akishindwa kutokana na kukosa gari linaloenda huko. Alipouliza juu ya chanzo cha kuvunjika kwa safari hiyo alijibiwa kuwa daraja la mto Wami lilikuwa limevunjika na hata alipojaribu kwenda uwanja wa ndege wa Majani mapana wa jijini Tanga kukata tikeri ya ndege alikosa vilevile akaambiwa ndege za mashirika mbalimbali zilizokuwa zinarusha ndege zake kuja Tanga zimevunja safari zao. Hali hiyo ilimfanya Falzal ajihisi ana mkosi baada tu ya kurejea nyumbani akiwa ili ahudhurie msiba wa kaka zake, maisha ya anasa aliyoyazoea kuishi kule marekani ndiyo yalimfanya ashindwe kukaa jijini Tanga kwani akiishi maisha hayo alikuwa anamtia aibu baba yake mzazi.
Heshima ya mzee Buruhan ndani ya jiji la Tanga kutokana na busara alizonazo kwa kuwaongoza wanae zilimfanya aheshimike kwani wanae ni watu maarufu sana ndani ya jiji hilo, hivyo laiti Falzal angeishi hivyo hapo Tanga angetia doa heshima ya baba yake. Falzal alijiona ni kama yu kifungpni kwa kukosa maisha anayoyapenda na aliyoyazoea, alivumilia kukaa hivyo kwa muda wa takribani siku mbili na hatimaye siku ya tatu akachukua mizigo yake akaiweka kwenye gari na akaazimia kuondoka mbali na jiji la Tanga ili akaishi atakavyo hadi pale atakapoondoka tena Marekani. Eneo alilofikiria kwenda ni Arusha tu kwani ndiyo ambapo hapakuwa na kikwazo chochote, aliamua kutumia usafiri binafsi ili awe huru zaidi.
Hakika hakutambua kama alikuwa anajaribu kukwepa jambo lisilokwepeka labda akukwepeshe muumba ndiyo linaweza kukwepeka lakini si kwa nguvu za kawaida kuweza kulikwepa, hakujua na alikuwa ameshasahau juu ya janga walilolifukia ambalo limejifukua bila ya wao kujijua. Hakutambua kama vikwazo vya safari vinatokana na jambo ambalo lisilokuwa na la kawaida.
Falzal aliwaaga ndugu zake pamoja na mzazi wake kisha akaingia kwenye gari binafsi anayoitumia aina ya toyota landcruiser, alianza safari vizuri huku akiwa na shauku kuu ya kuliacha jiji la Tanga ili aende kuendelea na maisha yake ya anasa aliyoyaacha hapo awali.
Aliendesha gari kwa mwendo wa wastani hadi alipoanza kukaribia Majani mapana ndipo alipozidi kuongeza mwendo wa gari ili aendane na mwendo unaotakiwa katika barabara aliyopo, alipokaribia eneo ambalo kuna njia iendayo kwenye mzani wa magari makubwa wa Majani mapana aliona mzee mwenye mizigo akumpungia mkono njiani ili amsimamishe lakini alimpita kwa mwendo mkali sana huku akisonya.
"Vizee vingine bhana vinadhani kila gari ni ya kubeba watu masikini kama wao, akapande basi huko asinisumbue mimi" Falzal aliongea kwa dharau kisha akaongeza mwendo zaidi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni