Notifications
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…
  • MY DIARY (20)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINITULIPOISHIA...Nikamwambia kuhusu namba zangu za simu amuombe aliyemtuma anisaidie na kuhusu hilo la pili je hatuwezi kufanya kesho kwa sababu kuna mahali nilikuwa nikienda? Alifikiria kwa sekunde kadhaa na kuniambia kuwa hapana anaomba nimsaidie leo kama yeye alivyonisaidia mimi kwa sababu ningekuwa kwenye foleni nisingeweza kuondoka kirahisi hivyo kama ninavyofikiria.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (19)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya hapo niliendelea kumdadisi juu ya tukio lile lakini hakuwa tayari kufunguka zaidi ya kusema aliumia sana. Hapo nikaamua kuutafuta ukweli kwa kutumia mbinu za kike.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilimwekaa mikono begani na kumwambia pleaee dear naomba uniambie ukweli ili nijue nakusaidiaje? Basi Ramadhani akaanza kulalamika kuwa baba yake amekuwa akimwingilia…
  • MY DIARY (18)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...Halafu eti akawasha simu na kuonesha zile picha alizotupiga kweli huyu rafiki yangu alikuwa hamnazo sio picha tu alituchukua video kabisa na sauti. Akanambia ngoja ampigie paparazi mmoja hivi aje ili atengeneze habari tupate hela. Kauli hiyo ilinikosesha amani na kunikera sana akanmabia eti kuna namna ya kufanya ili sura yangu isitokee.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (17)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Nilijifikiria mara mbili nikajikuta namkubalia kwani alionekana ni mpole na mstaarabu sana.Basi tukaenda hadi kwake ambapo haikuwa mbali na hapo tulipokuwa na kweli alikuwa na chumba na sebule na sebuleni kwake niliona picha ya ukutani akiwe yeye na mke wake nahisi ilikuwa siku ya harusi yao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikasema huyu kijana atakuwa amefunga ndoa…
  • MY DIARY (16)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Mwanamke akaamua kuingia jikoni na kukarangiza viazi na nyama rosti na kilipoiva kililetwa mezani tukaendelea kujenga afya. Sikuaamini kama Joyce alikuwa anakumbuka hata kupika kwa sababu alibadilka sana na alikuwa akiishi maisha ya starehe.. Lakini aliniprovu wrong kwa kutoa rost ya hatari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kula alinambia kuwa alikuwa amechoka…
  • MY DIARY (15)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Hapo mzungu wa watu hakuweza kuvumilia tena aliichomeka yote.Mmmmmh mmmmmh ishiiiiiiiiiiii yeaaaaaahhhhhhhh yeaaaaaaah ni miguno niliyoitoa mara baada ya kusikia joto tamu la kiungo hicho.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ikabid nijivute kwa nyuma ili lengo likiwa ni kukaa vizuri ili kichwa cha nyoka kiwe juu juu ya pango langu ili niweze kukisugua sawa sawa na pia…
  • MY DIARY (14)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Nikamuuuuliza hivi wewe haugopi maradhi? Akanijibu kuwa angekuwa haogopi basi angeshakufa. Sikiliza Leah hapa nipo na vile vipimo vya ukimwi hivyo usiwe na wasiwasi tutapima wote wanne kama wapo fresh tutaingia kazini wewe si unatafuta hela ya kujiunga na chuo au?IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kabla sijajibu akanambia nitakupa na dawa ya kumeza ya kuzuia mimba na pia…
  • MY DIARY (13)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...Joyce akaanza kujimiminia mwenyewe, kweli dunia ina mambo wakati wenzake wakichanganya nay ale maji makubwa yeye alikuwa akinywa kavu kavu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kuaagiza ile bia yangu ambayo alinifundisha yaani savanna. Safari hii hakusubiri ili ifike mwisho ili anitambulishe bali tulivyoanza tu kunywa akawaambia wale…
  • MY DIARY (12)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...Niliamua kufanya ziara ili nijue pakoje na mwisho wa siku niliamini kuwa kutokana na umaarufu wa marehemu baba yangu isingekuwa kazi sana kulipata shamba lake..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilitembea kijiji hadi kijiji huku nikijaribu kuuliza kwa wenye viti wa mtaa kama walikuwa wakimjua marehemu Bura. Kwa kweli kazi ilikuwa ngumu sikuweza kuvimaliza vijiji…

DHAMANA (7)

Jina: DHAMANA

SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
"Hapo vipi utaniogopa tena?" Aliuliza huku akimtazama Hamid ambaye alizidi kuogopa na akawa anahangaika kufungua mlango ili ajitupe nje kuikimbia sura aliyoiona sasa hivi ikiwa ina macho mekundu, milango ya gari ilikuwa haifunguki na hata alipotoa kifunga mlango bado haikufunguka hata kidogo.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Hamid aliendelea kuhangaika na kukivuta kitasa cha ndani cha mlango akiwa haamini kama mlango umejifunga, alibaki akihangaika kuchezea kitasa kutokana na kuchanganywa na tukio hilo.

"ukimaliza uniambie" Yule mtoto alimuambia huku akikunja miguu yake ikatengeneza umbo la nne akimtazama akiwa na tabasamu lisiloashria furaha hata kidogo.

Hamid alikuwa ameshasahau kama alikuwa anaendesha gari na alipokuja kukumbuka aliona gari linaenda lenyewe kwa mwendo wa taratibu sana na lilikuwa likipitwa na magari yanayowahi. Alibaki akimtazama yule mtoto huku akitetemeka kiuoga na mikono akiwa ameweka ishara ya kuomba msamaha.

"halafu unataka kuruka nje huku umejifunga mkanda sasa ndiyo unafanya ujinga gani?" Yule mtoto alimuambia Hamid ambaye hakuwa anatambua hakuwa amefungua mkanda katika harakati za kutaka kuoko nafsi yake, alipotaka kuufungua mkanda yule Mtoto alinyoosha mkono wake na mkanda wa gari ukamzunguka Hamid shingoni mwake kama nyoka na ukaanza kumkaba kwa nguvu hadi mishipa ya damu ya kichwani ikawa inaonekana.

"Nipe" Yule mtoto alimuambia Hamid huku akimtazama kwa hasira.

"siii....sinaa" Hamid aliongea kwa tabu kutokana na jinsi mkanda ulivyomkaba.

"kimoja umenipatia, nataka unipe kilichobakia. Sasa nipe!" Yule mtoto aliongea kwa hasira huku akitokwa na cheche za moto mdomoni.

"sinaa!" Hamid aliongea kwa tabu huku macho yake yakibadilika rangi kutokana na kukabwa, mishipa ya kichwani ilikuwa imemtoka hasa.

"Ok haya fungua mlango ukimbie" Yule mtoto aliongea na muda huo mkanda ukaacha kumkaba Hamid na mlango ikawa ipo kawaida, Hamid alifungua mkanda akafungua mlango akajitupa nje bila hata kuangalia barabarani. Kitendo cha Hamid kujitupa nje ilsikika

honi ya gari ya mizigo iliyolia kwa nguvu pamoja na vyuma vya breki kutoa mlio mkali, vishindo viwili vizito vikafuata kwa kupishana sekunde mbili na hapo kila aliyekuwa yupo karibu na eneo hilo akashika kichwa kwa mshangao.

Gari aina ya Scania ya mizigo ndiyo ilikumbana na kishindo cha kwanza baada ya kumgonga Hamid na kupelekea kichwa chake kupasuka na kutengeneza taswira isiyofaa barabarani kuangaliwa na binadamu wa kawaida kwani haifai binadamu kuona kichwa cha binadamu mwenzako kikiwa kimepasuliwa kama puto liliingia katika kichaka chenye miiba. Kishindo kingine kilikuwa ni cha gari la Hamid baada ya kugonga mti wa mwembe uliopo katika makutano ya barabara inayotoka Kwa minchi, inayoelekea Amboni na hiyi inayopita Chumbageni.

Ndani dakika zisizopungua tatu tayari maaskari walishajaa kutokana na kituo cha polisi kutokuwa mbali na hapo ilipotokea tukio hilo, askari hao walikuwa mchanganyiko kati ya askari wa usalama barabarani na wa kawaida ambao walishiriakiana na kuifanya kazi hiyo kwa haraka. Uchunguzi wa magari yote yalipokaguliwa yalizidi kushangaza watu kwani katika gari aina ya Scania hakukuwa na dereva ingawa mashuhuda walisema dereva hakushuka na katika gari aina ya range rover sport aliyokuwa anaitumia Hamid hakukuwa na dereva vilevile. Maaskari wakiwa bado hata hawajasahau tukio la siku iliyopita tayari wanakutana na tukio jingine la kushangaza kama hilo.

"sasa haya magari yatajiendeshaje yenyewe hebu nyinyi kachunguze vizuri mazingira ya jirani na ule mwembe ilipogonga ile Range tena someni na stika zake tumjue mmiliki nilitaka kusahau hilo" Askari mwenye nyota tatu mabegani mwake aliongea, maaskari walipiga saluti kisha wakaenda kuchunguza walichoambiwa na mkubwa wao kwa haraka. Baada ya dakika moja tu tangu wale askari waondoka simu ya upepo ya yule Inspekta ambaye ndiye mwenye nyota tatu ikakoroma kisha ikasikika sauti ya yule askari mwingine ikimuita kule kwenye gari aina ya Range rover iliyogonga mti wa Mwembe, Inspekta huyu alienda haraka hadi pale kwenye kwenda kuona alichoitiwa. Alipofika alipigiwa saluti kisha akaongozwa na askari mwingine hadi kwenye kioo cha gari hiyo, yule askari aliyemuongoza alimuonesha yule Inspekta stika za gari ile ambazo ziliandikwa jina la mwenye gari.

"Hamid Buruhan, si mmiliki wa kampuni iliyokumbwa na kadhia isiyoeleweka jana" Inspekta aliongea

"ndiyo afande" Yule askari aliyemuita aliitikia.

"Sajenti Shehoza hebu licheki hili gari halafu..." Yule Inspekta aliongea lakinj akasitisha maneno yake baada ya kuona alama za kung'oka majani yaliyoonekana yametokana na kuburuzwa kitu kuelekea katika majani marefu yaliyopo jirani na Mwembe, aliamua kufuatilia alama hizo kuelekea kwenye majani marefu akiwa anatazama chini kwa umakini sana ambapo aliona vitu mbalimbali vya uganga vikiwa vimeanguka njiani kama vile hirizi na vibuyu pamoja na kitambaa chekundu cha kaniki. Inspekta huyo aliendelea kufuatilia hadi mwisho wake ambapo alikutana na mwili wa mzee wa makamo ukiwa umelazwa kwenye majani yaliyoonekana kupunguzwa kwa kitu chenye kali katika sehemu ulipolazwa mwili huo.

Mavazi yaliyokuwa yamevaliwa na maiti hiyo ambayo yalionakana aliyavaa mwenyewe kabla hajakumbwa na umauti yalikuwa ni ya kiganga kabisa, kaniki nyekundu aliyojifunga ilitosha kumtambulisha kama mganga ukiachilia mbali hirizi iliyopo begani kwake. Inspekta yule aliwaamrisha maaskari wale wachukua vipimo vyote juu ya mwili kisha wawaite wauguzi maaskari waliofika hapo baada ya kupigiwa simu waje wauchukue mwili ukahifadhiwe, Inspekta huyo aliondoka akarudi alipokuwa awali ambapo barabara ilikuwa inasafishwa baada ya uchukuaji wa vipimo kukamilika alisimamia taratibu zingine.

Gari la kuvuta magari mabovu maarufu kama Break down nalo liliitwa likaondoa magari yote yakaenda kuhifadhiwa katika kituo cha polisi cha Chumbageni. Maaskari waliokuwa kule kwenye majani marefu walirejea wakiwa na wauguzi maalum wa jeshi la polisi waliobeba machela yenye mwili wa yule mzee aliyekutwa kwenye majani, wakiwa wanaelekea kwenye gari la wagonjwa la hospitali kuu ya Tanga yaani Bombo. Mwanamke mmoja asiyejulikana ametokea wapi alikimbia hadi pale walipokuwa wale maaskari na wauguzi akaufungua ule mwili kisha akaanza kulia kwa uchungu huku akipiga kelele kwa uchungu.

"Jamani mume wangu mimi!" Aliropoka yule mwanamke huku akiishika machela iliyobeba mwili.

"we mama hebu tulia tufanye kazi yetu" Sajenti Shehoza aliongea huku akimzuia yule mwanamke na wale wauguzi wakaendelea na safari.

"Baba Hadija nilikumbia usisaidie usiowajua umeona sasa, Mayoooo mayooo" Yule mwanamke alizidi kuongea kwa nguvu huku akilia kama mtoto mdogo.

****

Wakati askari wakishughulika katika ajali ya kutatanisha iliyotokea Chumbageni, upende mwingine wa jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone hali ilikuwa shwari kuliko kawaida katika kampuni ya mafuta ya Matro inayosifika kwa kutoa huduma bora za mafuta jijini Tanga na kwingineko. Ndani ya makao makuu ya kampuni hii wafanyakazi walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida ili kuinua kampuni na pia kuendesha maisha yao. Siku hiyo mmiliki wa kampuni hiyo Hussein Buruhan ambaye ni mmojawapo wa matajiri wakubwa nchini alikuwa yupo ofisini kwake ghorofa ya kumi na mbili ya jengo la kampuni hiyo akiendelea na kazi kama kawaida.

Baada ya nusu saa za uchapaji kazi alianza kuhisi kubanwa na haja ndogo na ikambidi aende msalani kutokana na kushindwa kuvumilia kukaa katika hali hiyo, alifunga ofisi kisha akaingia katika maliwato ambayo ipo jirani na ofisi yako. Aliingia moja kwa moja msalani akajisaidia kisha akatoka akiwa anapiga uruzi wa nyimbo anayoipenda akiwa na tabasamu pana usoni mwake, kama ilivyo kawaida yake huwa akitoka maliwatoni lazima aende kwenye kioo kipana chenye masinki yenye koki kadhaa za maji kwa chini yake ili anawe mikono. Alienda kwenye sinki hilo akafungua maji akanawa mikono kisha akanawa uso akiwa anapiga uruzi wa wimbo anaupenda unaoitwa this i promise you ulioimbwa na kundi la wanamuziki wa kimarekani liitwalo N-sync, akiendelea kupiga uruzi huo ghafla taa za huko kwenye maliwato zikazima na kukawa giza kutokana na madirisha madogo yaliyomo humo kutopitisha mwanga vizuri.

*****

"shit! Yaani hawa Tanesco wanakera sana" Hussein alisema kutokana na umeme kuzimika humo maliwatoni, lawama zake zote alizielekeza kwenye kampuni ya usambazaji umeme nchini kutokana na kuzimika kwa taa ya humo ndani. Hakuwa ametambua kama alikuwa anawabebesha lawama kwa wasiohusika na tatizo hilo, hakika hakujua kama kuna ugeni uliokuwa umemfikia na dalili yake ndiyo hiyo ya kuzimika kwa taa humo maliwatoni. Akiwa na uso ulionekana kukerwa kabisa na tatizo hilo taa ziliwaka tena akajikuta akitukana tusi zito halafu akainama ili anawe uso ingawa alisita baada ya kuhisi hayupo peke yake blali kuna mtu mwingine, aligeuza uso pembeni akamuona kijana mwenye asili ys uchotara wa kiarabu na mbantu akiwa ananawa uso wake tararibu bila hata kushughulika kumuangalia Hussein na wala haikujikana aliingia muda gani hapo.

"wewe umeingia saa ngapi hapa?" Hussein alimuuliza yule kijana, yule kijana aliposikia swali la Hussein aliacha kunawa kisha akajifuta uso wake halafu akamtazama kwa sekunde kadhaa.

"nimeingia muda si mrefu" Yule kijana alijibu kisha akafungua tena koki ya maji akaendelea kunawa, jibu hilo lilimchanganya zaidi Hussein na akajikuta akimshangaa sana yule kijana hadi akaanza kumuogopa kwani mlango haukuwa umefunguliwa kuashiria kama kuna mtu aliingia.

"Kwanza wewe ni nani mpaka uingie kwenye sehemu ambayo staff wa kawaida hawafiki?" Hussein alimuuliza yule kijana.

"mimi ni Zalabain ndiyo maana nimeingia humu na cheo changu ni prince ndiyo maana nipo humu" Yule kijana aliongea huku akitabasamu.

"unasemaje mbona sikuelewi na sikujui?" Hussein aliongea kutokana na kuchanganywa na maelezo ya yule kijana.

"utanielewa na utanijua" Yule kijana aliongea na hapo ndani taa zikazimika tena na zikawaka, yule kijana sehemu aliyokuwepo awali hakuonekana kabisa na hapo ndipo Hussein alizidi kuingiwa na uoga. Alipoangalia kwenye kioo ambacho kilimuonesha upande wa nyuma yake ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kwa alichokiona, alitaka kusoma dua ya kujikinga na viumbe waovu lakini mdomo wake ulikuwa mziti na haukufunguka kabisa kama amelishwa mawe. Alipogeuka ili aone vizuri kwa kudhani labda anaona maruweruwe tu ndipo akajikuta akipokea kofi zito lililompeleka hadi chini, alipoinua uso wake alikutana uso kwa uso na yule mtoto ambaye aliwatokea Hisan na Hamid muda mfupi kabla hawajaiaga dunia.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
57 Dhamana Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni