DHAMANA (9)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Shafii alipotangulia kushuka kamera mbalimbali za waandishi wa habari zilikuwa zikifanya kazi ya kumpiga picha tu, waandishi wa habari walikimbilia kumuuliza maswali mbalimbali lakini hawakupata ushirikiano.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Shafii aliingia ndani ya sehemu ya kuhifadhia maiti akiwa na Ally na alipita hadi ofisini ndani ya ofisi hiyo ya chumba cha kuhifadhia maiti alimkuta msimamizi wake akiwa amekaa kwenye kiti akipitia mafaili mbalimbali.
"karibu mzee" Msimamizi wa hicho chumba alimkaribisha.
"Asante" Shafii aliitikia huku akivua miwani ya jua akafuta machozi.
"pole sana mzee wangu kwa masaibu haya" Msimamizi alimpa pole.
"asante sana, nakusikiliza" Shafii alisema.
"Ok nifuateni" Msimamizi aliongea kisha akainuka akaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, Shafii na Ally nao walimfuata kwa nyuma. Yule msimamizi alielekea sehemu yenye mitoto mingi kama ya meza au kabati akiwa anatafuta namba maalum hadi akazifikia namba za mitoto ya makabati ya jokofu ya kuhifadhia maiti yanayofuatana, alifungua mojawapo kisha akafungua lailoni lenye zipu akamuonesha Shafii ambapo aliuona mwili wa mdogo Hussein ukiwa hauna koo. Shafii aliutazama mwili ule kwa umakini huku machozi yakimtoka kisha akamuamuru yule msimamizi afungue jingine, jingine lilipofunguliwa aliuona mwili wa mdogo wake Hamid ukiwa umeharibika kutokana na ajali aliyoipata.
"hapa kuna mkono wa mtu nasema sikubali" Shafii aliongea kwa hasira.
"ndiyo maana mzee nikakuita uje kujionea mwenyewe ili uwahi kwa babu kule" Msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti alimuambia.
"ok nashukuru ngoja niende kwa babu yako kabla mambo hayajawa mabaya" Shafii aliongea huku akimpa burunguru la pesa yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti halafu akaondoka huku Ally akiwa anamfuata, walipotoka nje Shafii alimuambia mdogo wake "Ally wewe nenda ukampe taarifa shemeji Hamisi na wengine juu ya vifo hivi, mimi naenda kwa Mtaalamu Sauti ya radi kule Amboni".
Shafii aliingia ndani ya gari na dereva akaondoa gari, Ally alichukua teksi naye akaondoka.
****
Safari ya Shafii iliishia Amboni kwa mganga wake ambaye ndiye babu yake yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Bombo, gari yake ilisimama kwenye umbali mrefu kutoka pale yalipo makazi ya mganga huyo kwenye pori dogo lililopo karibu sana na mto Zigi. Shafii alishuka akatembea kwa mguu hadi kwenye kibanda cha mganga Sauti ya Radi kisha akabisha hodi huku akivua viatu vyake, alipopewa ukaribisho aliingia ndani akaketi kwenye jamvi kuukuu mbele ya vibuyu vya mganga.
"Karibu Shafii mwana Buruhan" Mganga Sauti ya radi alimkaribisha Shafii kwa mara ya pili, Shafii aliitikia ukaribisho huo kisha akaeleza kila kitu kwa mganga.
"hakuna kinachoshindikana hapa mbele ya sauti ya radi nikinguruma natoa miale maadui wanashindwa wenyewe, kuna kiumbe anakuandama na leo ndiyo kiama chake" Mganga Sauti ya radi aliongea kwa msjigambo kisha akanyanyuka akatoka nje, alirejea akiwa na moto kidogo kwenye chombo kinachotumika kuwekea ubani. Alikiweka kile chombo mbele ya Shafii kisha akamwaga dawa zake kwenye moto uliomo kwenye chombo hicho, moshi mzito ulitanda humo ndani na mzee Sauti ya radi akawa anaimba nyimbo zisizoeleweka huku akimzunguka Shafii akicheza kama anacheza ngoma ya kikabila. Moshi huo ulipokuja kupungua Mganga akiendelea kucheza alihisi anashikwa kiuno wakati akicheza, moshi ulipoisha alihisi anashikwa makalio kwa kutomaswa. Alipogeula nyuma kumuangalia anayemshika alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa anatabasamu.
"Yaani ungekuwa mwanamke ungefaa kucheza Baikoko kwa jinsi inavyojua kukata kiuno" Zalabain aliongea akiwa bado hajatoa mikono kwenye makalio ya Mganga Sauti ya radi.
Zalabain alizidi kuonesha uso wa dharau kwa kuyaminya makalio ya mganga Sauti ya Radi na kusanabisha mganga huyo apandwe na hasira sana, Mzee Sauti ya Radi alinguruma kwa nguvu kama simba dume aliyejeruhiwa akiashiria mashetani yamempanda tayari kwa ajili ya kukabiliana na kiumbe aliyejitokeza muda huo ambaye hakuonekana na nia nzuri kwake wala kwa Shafii. Alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain aliambulia patupu kwani hakuonekana kabisa, Mganga alipoona anachezewa akili alizidi kupandwa na hasira mara dufu. Aligeuka kila pande za eneo alilopo lakini hakumuona Zalabain na alimuona Shafii akiwa amekaa pale alipokuwepo akionekana hajui chochote kinachoendelea, Mganga hapo alishusha pumzi kisha akasema "ana bahati sana yule".
"Nina bahati sana kwa kuweza kushika makalio yako sio, sasa nimeyashika tena ili nikujulishe kwamba bahati hiyo ni yangu tu" Sauti ya Zalabain ilisikika kwa mara ya pili na Mganga akahisi kushikwa makalio kwa mara nyingine tena safari hii alijiona kaingia katika mikono ya basha kwa jinsi alivyokuwa anatomaswa, mara hii hata Shafii alimshuhudia Zalabain akiwa yupo nyuma ya Mganga Sauti ya Radi akifanya udhalilishaji wake. Mganga alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain alipigwa kofi moja lenye uzito wa aina yake hadi shavu lake likachanika kabisa, Zalabain alipotea kwa mara ya pili na moshi mzito ukatanda kama ukungu ikifuatiwa na sauti ya Mganga akilia kama mtoto mdogo.
Sauti ya mtu akipigwa vibao ndiyo iliyokuwa imetawala ndani ya nyumba hiyo ya Mganga kwa muda wa dakika kadhaa, ilipokuja kuisha moshi uliotanda ghafla uliondoka papo hapo na Zalabain akaonekana amesimama akiwa ameukanyaga mwili ya Mganga ambao haukuwa hata na dalili ya kuwa na uhai. Alama za mikono zilionekana katika mwili wa Mganga zilizoweka kama mhuri karibu kila sehemu katika mwili wa Mganga huyo, Zalabain alikuwa kasimama akiwa na hasira tena akiwa anamtazama Shafii huku akihema kwa nguvu sana.
Shafii naye alijikuta akitokwa na upepo bila hata kutarajia na jasho lilikuwa likimvuja kama alikuwa amekaa jirani na moto mkali kwa muda mrefu, kila akitazama macho ya Zalabain yalivyo na hasira ndiyo alizidi kusota kwa kurudi nyuma hadi akafika ukutani kabisa akawa pa kwenda hana akabaki akimtazama Zalabain kwa uoga sana.
"Unafikiri unaweza kunizuia mimi kwa kutumia nguvu za huyu mzee?" Zalabain alimwambia Shafii huku akiukanyaga mwili wa Mganga Sauti ya Radi kwa nguvu hadi viungo vikawa vinavunjika na kuzidi kumtia uoga Shafii.
"Ujue kila mwizi na arobaini yake na siku ya arobaini yake ndiyo hukamatwa au kuuliwa, sasa wewe utabaki unapumua kwakuwa arobaini yako bado ila ikifika utakufa kifo cha huzuni kuliko hata hiki cha huyu" Zalabain aliongea huku akimtazama Shafii na akamaliza kauli kwa kuikanyaga shingo ya mganga hadi kichwa chake kikaruka upande aliopo Shafii na kupelekea yowe la uoga limtoke kwa uoga kutokana na kuogopa kichwa hicho kikiwa hakina uhai. Zalabain alipotea papo hapo baada ya kichwa kuruka upande aliopo Shafii na hapo ndipo akili ya kukimbia ilipomjia Shafii na akasimama na kuanza kukimbia bila hata kuangalia wala kuangalia mlango upo wapi, alijikuta akipigiza uso ukutani katika ukuta wa nyumba ya mganga baada ya kukimbilia ukutani akijua ni mlango ulipo kutokana na kuchanganyikiwa na balaa aliloliona.
"Oooow!" Aliachia ukelele wa maumivu kutokana na kuumia pua yake alipojibamiza ukutani hapo, Shafii alinyanyuka akawa anaona mawenge tu na asijue wapi mlango ulipo. Alipoamua kutimua tena mbio alikutana tena na ukuta ulimbamiza puani kisawasawa hadi zikaanza kumchuruzika damu puani, aliumia sana lakini alinyanyuka na kuanza kukimbia tena mbio akiwa amefumba macho kwa maumivu ya puani aliyonayo. Alifanikiwa kutoka nje na akatimua mbio moja kwa moja bila hata kuangalia mbele tena akiwa na mbio kuliko kawaida, laiti angeshindanishwa na mwanariadha Usain Bolt mwenye uwezo wa kukimbia mita 100 kwa sekunde tisa angekuwa mshindi yeye kwa jinsi alivyokuwa ana kasi ya ajabu kukimbia eneo ambalo alishuhudia mauzauza ya kifo cha Mganga wake wa toka siku nyingi.
Mbio za Shafii zote hakuwa ameangalia mbele na alikuja kufumbua macho na kurudiwa na akili zake za kawaida baada ya kuhisi amekumbwa kikumbo kikubwa na mtu mwenye mwili wenye ubavu kuliko yeye, alianguka chini moja kwa moja lakini alijiinua akiwa na wasiwasi sana moyoni mwake baada ya kumshuhudia mtu aliyechafuka kwa mchanga mweupe akiwa ameshika gunia.
"hivi we mzed una akili timamu kweli? Huoni kama ulikuwa unakimbilia mtoni tena kwenye Korongo ambalo chini kuna mamba wengi sana?" Yule mtu alimuuliza Shafii huku akimshangaa sana.
"hapa ni wapi?" Shafii naye alijikuta anamuuliza yule mtu.
"We mzee umechanganyikiwa nini hebu angalia kushoto kwako" Yule mtu alimuambia Shafii huku akimuonesha upande wa kushoto, Shafii alipogeuza macho upande wa kushoto aliona yupo mita takribani mbili kutoka mwisho wa Korongo refu ambalo chini yake mto Zigi unapita tena sehemu hiyo ya mto huo mkubwa Tanga nzima ulikuwa umejitanua sana na chini mamba walikuwa wanaonekana bila hata kificho wakiwa wapo pembeni.
"Hiii!" Shafii alisema kwa uoga akaanza kukimbia upande mwingine ili akae mbali na eneo hilo la korongo.
"Mzee wangu una matatizo sana, yaani isingekuwa mimi kukuona wakati naenda kuchimba mchanga mtoni basi ungekuwa kitoweo cha Mamba sasa hivi" Yule mtu alimuambia Shafii ambaye alikuwa ametulia tayari na akawa anamsikiliza.
"asante kijana, sasa utaendaje kuchimba mchanga mtoni wakati kuna mamba?" Shafii alimuuliza yule mtu kutokana na kushangazwa na mtu kwenda kuchimba kwenye mto huo wenye mamba wengi sana, yule mtu aliposikia swali la Shafii alimuonesha kamba nyeusi iliyofungwa begani mwake yenye hirizi pamoja na simbi kadhaa.
"hii ndiyo kinga yangu Mamba hanishiki ila kwa mgeni ukisogea hata pembeni umeisha, mzee umekumbwa na nini mbona una damu puani na usoni umechanika?" Yule mtu alimueleza Shafii kisha akamtazama kwa udadisi na akagundua ameumia, alimuuliza juu ya kilichomuumiza kwani alikuwa anavuja damu nyingi sana.
"Kijana ni habari nyingine kabisa usijali sana....asante sana hii ni zawadi yako ya kukomboa maisha yangu" Shafii aliongea kisha akatoa pochi yake mfukoni akamkabidhi noti kadhaa yule mtu halafu akamuaga akaondoka. Ilikuwa bahati kwa yule mtu kupata kitita kikubwa cha pesa kama hicho kwa kumuokoa mtu asiyemjua asiingie katika maskani ya mamba wengi wa mto Zigi ingawa kwa Shafii ilikuwa ni jambo dogo sana kutoa kitita kama hicho cha fedha kwani alikuwa ni tajiri sana. Shafii alirudi hadi alipoacha gari lake akaingia akamuamuru dereva aondoe gari kuelekea hospitali.
Muda ambao Shafii alikuwa anaona vibweka vya kuuliwa mganga wake aliyeanza kumtumia miaka mingi iliyopita, ndiyo muda huohuo mdogo wake aliwasili nyumbani kwa shemeji yake Shafii yaani kaka wa Bi Farida mke wa Shafii anayeitwa Hamis.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni