KIJIJINI KWA BIBI (27)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"ile gari ya polisi wote wamekufa, ila yule bro kabebwa hajielewi, sijui hata kama atafika hospitali", Yule kijana alipigilia msumari wa mwisho katika maumivu ya mama kayoza na wanae, kisha akawaaga, ila hakujibiwa kutokana na hali iliyokuwepo.
"Mama sasa tunafanyaje?" Kayoza aliuliza kwa sauti tulivu,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Twendeni tu hospitali, hatuna muda wa kupoteza" Omary alijibu na kipindi chote mama Kayoza alikuwa amefumba macho anasali, hali aliyokuwa nayo ni dhahiri alikuwa amechanganyikiwa.
"Haya twendeni" Mama Kayoza aliongea huku akisimama,
"Sasa mama tunaenda hospitali gani?, au unajua hospitali aliyopelekwa?" Kayoza alimuuliza mama yake huku akimshangaa,
"Acha kuuliza maswali ya kijinga, wewe unadhani atapelekwa hospitali gani zaidi ya hospitali juu ya mkoa?" Mama Kayoza aliuliza huku akijitanda khanga,
"Mama tunapoteza muda bure, twendeni tuwahi" Omary aliongea huku akiwa amesimama mlangoni,
"Si huyu mpumbavu anauliza uliza vitu visivyokuwa na maana" Mama Kayoza aliongea kwa hasira huku akiuelekea mlango wa kutokea.
Majira ya saa sita mchana, mama Kayoza na wanae walikuwa wameshafika hospitali, moja kwa moja wakaenda kujitambulisha kwa madaktari, kisha wakaambiwa mgonjwa wao alipowekwa,
wakatoka tena hadi katika chumba cha wagonjawa mahututi(I.C.U), walizuiliwa mlangoni na manesi, wakaambiwa bado madaktari wako ndani wanapigania uhai wa mgonjwa.
Wakarudi kukaa katika benchi lililo jirani na kile chumba na wote wakakaa kimya huku kila mtu akiwaza jambo lake.
Mama Kayoza ndiye aliyeonekana amechanganyikiwa zaidi kuhusu hali aliyokuwa nayo Sajenti Minja.
Baada ya nusu saa, Daktari alitoka kutoka katika kile chumba alichokuwa amelazwa Sajenti Minja.
Mama kayoza na wanae wakamkimbilia, kisha wakajitambulisha, yule Daktari akawaangalia sekunde kadhaa, kisha akatingisha kichwa,
"Aya baba tuambie hali ya mgonjwa wetu ikoje?" Mama Kayoza aliuliza huku machozi yakianza kumtoka,
"Sasa mama unalilia nini, usilie bwana unakuwa unaleta uchuro" Kayoza alimwambia mama yake,
"Ebu ngojeni kwanza, wewe mama ni nani yake?" Daktari alimuuliza Mama Kayoza,
"Mimi ni dada yake, tumezaliwa baba mmoja na mama mmoja, baada ya kuzaliwa mimi ndio akafuata yeye" Mama Kayoza alijibu na kumfanya Daktari akili kuwa Mama Kayoza hayupo katika akili zake za kawaida,
"Na nyie vijana ni zake?" Daktari aliuliza huku akiwageukia Kayoza na Omary,
"Awa ni wanangu kabisa, yule ni mjomba wao" Mama Kayoza aliamua kuwajibia, maana aliona kama watachelewa vile kutoa jibu,
"Basi kama ni hivyo, mama nakuomba utusubiri nje, acha niongee na awa watoto wa kiume" Daktari aliongea huku akimtazama Mama Kayoza,
"Sasa utawaeleza nini awa watoto? Nieleze mimi mama yao, awa watoto wenyewe wananitegemea mimi" Mama Kayoza aliongea kwa hasira huku akianza kulia,
"Mama msikilize daktari, unapopayuka unakuwa unakosea mama" Kayoza alimwambia Mama Yake,
"Kaa kimya, tena funga mdomo wako, hujui uchungu ninaousikia hapa" Mama Kayoza alimkaripia mwanae huku akilia,
"Basi usilie, unalilia nini sasa?" Omary aliuliza baada ya kuona hakuna maelewano kutokana na kilio cha Mama kayoza,
"Muache alie, anastahili kulia kwa maana hata nyinyi mtalia muda mchache ujao" Daktari alimjibu Omary na kisha akawaambia habari mbaya ambayo ilipelekea mama Kayoza kupiga mueleka wa nguvu na kupoteza fahamu palepale…
…wakina Kayoza pamoja na manesi, wakambeba juu juu Mama Kayoza na kumkimbiza wodini haraka. Kayoza na Omari wakaambiwa watoke nje, mgonjwa anatakiwa kupewa huduma ya haraka.
Wakina kayoza ikawabidi waende nje wakasubiri.
"Aisee, mbona mitihani inaongezeka hivyo?" Kayoza alimuuliza Omary huku wakiwa wamesimama nje ya jengo la wodi aliyolazwa mama yake,
"Ila hatupaswi kukata tamaa, mjomba ataamka tu, Mimi nina imani hiyo" Omary aliongea kwa ujasiri,
"Ni ngumu sana, si umesikia daktari alivyosema?" Kayoza alimuuliza Omary,
"Kuna daktari, lakini kumbuka kuna Mungu pia" Omary alijibu,
"Sawa, ngoja tuone" Kayoza alijibu na kisha ukimya ukatawala huku wakiendelea kusubiri nje, ingawa hawakuwa wanachosubiri. Kila mmoja alikuwa kimya.
Baada ya robo saa wakarudi ndani ya eneo la hospitali, wakaruhusiwa kwenda kumuona mama yao, wakamkuta amekaa kitandani huku dripu ikiwa inahesabu matone yake,
"pole mama", Kayoza na Omari waliongea kwa pamoja,
"mh, mmeongea tena na daktari", Mama Kayoza badala ya kuitikia, akawauliza swali,
"hapana, nafikiri kama kuna mabadiliko yoyote yametokea atatuambia",Kayoza alimjibu mama yake,
"Atawaambiaje wakati hamjamtafuta?" Mama Kayoza aliuliza,
"Si angekuja hata hapa wodini ulipolazwa" Kayoza aliongea,
"Bado akili zako hazijakomaa, sasa hata kama angekuja unadhani angeongea nini na Mimi wakati Mimi ni mgonjwa?" Mama Kayoza aliuliza,
"Sasa hivi unajisikiaje mama?" Omary alimuuliza Mama Kayoza,
"mh, naisi mwili hauna nguvu kabisa",Mama Kayoza alimjibu Omary,
"mama nawe una presha ya ajabu, je ungeambiwa amekufa, si na wewe ungekufa!", Kayoza alimwambia mama yake,
"we Kayoza acha ujinga, sasa tumeambiwa uhakika wa kuishi ni asilimi 30, wa kufa asilimia 70, huoni ni jambo la kuogopa sana?",Mama Kayoza aliongea kwa ukali kidogo,
"mama wewe ni mlokole, ulichotakiwa kufanya ni kumuomba Mungu na si kukata tamaa", Kayoza alimwambia mama yake,
"Kwani mlokole sio binadamu? kuna hisia za kibinadam uwa zipo kwa kila mtu" Mama Kayoza aliongea,
"Hata kama, mbona sisi hatujapoteza fahamu baada ya kusikia hiyo habari?" Kayoza alimkazania mama yake kwa maswali,
"Kwanza nyie ni watoto wa kiume, alafu pia inawezekana upendo wenu kwa Minja sio mkubwa kama niliokuwa nao Mimi" Mama Kayoza alieleza,
"Kwa hiyo sisi hatumpendi mjomba?" Kayoza aliuliza,
"Sijui wenyewe, kwanza tuachane na hayo, kamtafute daktari aje kunipa ruhusa mimi", Mama Kayoza akamwambia mwanae.
Kayoza akaenda kumtafuta Daktari, baada ya muda kidogo, akarudi na daktari, daktari akampima pima mama Kayoza, kisha akamuuliza maswali mawili matatu, akamuandikia maelezo katika kikaratasi, alafu akamruhusu.
Walichofanya wakina Kayoza ni kumrudisha mama yao nyumbani, kisha wao wakarudi hospitali.Hata wenyewe hawakuelewa pale hospital wanasubiri nini, ilimradi walikuwa wanakaa tu ili kumridhisha mama yao ambae aliwataka wasiondoke eneo la hospitali.
Mkuu wa polisi kazi kubwa aliyokuwa anafanya ni kuwajulisha ndugu na jamaa wa marehemu juu ya ajali iliyotokea, na kuwapa taharifa za kifo, ila hakutaka kabisa kuwaambia askari wengine kuwa, yeye ndio aliwaagiza, maana angewaambia ni lazima angewajulisha kuwa aliwatuma kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya kunyonya damu na yeye hakutaka ijulikane, kwa sababu angetangazia uma, basi huyo muuaji angeshtuka na kuhama mkoa, ila alichoamua ni kufanya upepelezi wake wa kimya kimya. Alipekua makabrasha yake na kutoa gazeti ambalo lilionekana la siku nyingi, kisha akalikunjua, mbele kulikuwa na picha ya Omari, akaiangalia ile picha kwa muda mrefu sana, akajikuta anatabasamu mwenyewe,
"Yule mzee wa monchwari alimuona kweli muuaji, na kama alimuona alimjuaje, au lao lilikuwa moja?" Mkuu wa polisi alijiuliza huku akiwa bado anaitazama picha ya Omary iliyopo katika kipande cha gazeti.
"kama yupo hapa shinyanga, nitamkamata tu, huu mkoa ni mdogo sana", Mkuu wa polisi aliongea huku akiwa bado anaendelea kuitazama ile picha ya Omari.
Kisha akaikunja vizuri kama mwanzo, na kuirudishia katika droo ya meza yake ya pale ofisini, kisha akainuka na kwenda kabatini kisha akaitoa kofia yake na kuibandika kichwani.
Baada ya hapo, akamwita dereva wake na kumuamuru ampeleke hospitali.
Walipofika hospitali, Mkuu wa polisi alitelemka, kisha akaenda katika wodi alipokuwepo Sajenti Minja, ila alizuiliwa mlangoni na daktari,
"mimi nataka nimuone tu ili nijue hali yake", Mkuu wa polisi alimwambia daktari,
"hali yake sio nzuri kamanda", yule Daktari alimjibu mkuu wa polisi, alionekana kumfahamu haswa,
"kuna mtu yeyote aliyekuja kumuona?", Mkuu wa polisi alimuuliza daktari,
"ndio, kuna mwanamama mmoja, alikuja na vijana wawili, walijitambulisha ni ndugu zake", yule Daktari alimjibu Mkuu wa polisi,
"walikwambia wanapokaa?", Mkuu wa polisi alimuhoji Daktari,
"hapana, ila wameondoka mida hii hii, kwa sababu yule mwanamama alipoteza fahamu baada ya kumwambia hali ya mgonjwa",yule Daktari alijibu,
"kama mpaka alipoteza fahamu, basi anamuhusu",Mkuu wa polisi aliongea hivyo.
"Ila kiukweli inahitajika sala kweli ili huyu jamaa apone" Daktari alimwambia Mkuu wa polisi,
"Kwa maana hiyo nyie uwezo umefika mwisho?" Mkuu wa polisi alimtupia swali Daktari,
"Nikisema hapana, nitakuwa nadanganya, kwa hata ile tuliyofikia hakuna hata nyingine ambayo tunaweza kuipiga, sasa hapo ni uwezo wa Mungu tu ndio utamuweka hai" Daktari aliendelea kuongea anachokijua,
"Sasa kama ni hivyo si ni bora mmuandikie barua ya kumuhamishia hospitali nyingine zenye uwezo" Mkuu wa polisi alitoa maoni yake,
"Hata tuna uwezo, tungekuwa hatuna uwezo tungeshamuandikia barua hata ya kumpeleka india" Daktari alimjibu Mkuu wa polisi,
"Kwani tatizo ni hasa?" Mkuu wa polisi aliuliza,
"Uti wa mgongo umepata itilafu kidogo, kwa hiyo mawasiliano ya mwili hayapo na pia kichwa chake inaonesha kilipigizwa sana" Daktari alimjibu Mkuu wa Polisi,
"Tuweke imani tu atapona, tusiwe tunavunjika moyo kwa kitu ambacho kipo nje ya uwezo wetu" Mkuu wa polisi aliongea,
"Na hata akipona kuna mawili, anaweza kupata ulemavu wa maisha kutokana na tatizo la uti wa mgongo, au anaweza akapoteza kumbukumbu kwa muda mrefu au pia vyote vinaweza kumtokea" Daktari aliendelea kutoa Maelezo,
"Cha muhimu uzima, hayo mengine ni kuendelea kumuomba Mungu" Mkuu wa Polisi aliongea,
Wakiwa bado katika maongezi yao, mbele yao walikuja Kayoza na Omari,
"vipi Dokta?" Kayoza alimuuliza Daktari,
"vijana wenyewe ambao ni ndugu wa mgonjwa ni awa hapa",Daktari hakumjibu Kayoza, ila alimtaharifu mkuu wa polisi kuhusu wakina Kayoza, lakini Mkuu wa polisi hakuonekana kumsikiliza Daktari kabisaaa, badala yake, alimtumbulia macho Omary huku ile picha iliyopo katika kipande cha gazeti ikimjia….
aliendelea kumuangalia Omari kwa dakika nzima mpaka Omari akapata wasiwasi na lile jicho kali la Mkuu wa Polisi,
"we kijana unaitwa nani?",Mkuu wa polisi alimuuliza Omari, tena aliuliza kwa sauti ya ukali,
"remmy, naitwa Remmy", Omari akataja jina la uongo, alikuwa na wasiwasi ila alijitahidi kuficha hofu yake mbele ya Mkuu wa Polisi,
"Minja ni nani kwako?", Mkuu wa polisi akamuuliza tena Omari,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni