Notifications
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (11)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...“Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (10)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (9)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA TISATULIPOISHIA...“Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.“Usikate tamaa, hakikisha unafika…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (8)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Amata ga Imba alipoona giza hilo akajua kumekucha, akapiga mbinja kali na muda mfupi tu, farasi wale wawili walikuwa tayari wamefika, Seidon akarukia juu ya mmoja wapo na Amata vilevile kisha wakapiga mbio kuelekea upande wa kusini. Nyuma yao jeshi lilikuwa likija kwa kasi na farasi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amatagaimba! Wanatufuata….” Seidon alipiga…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (7)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA SABATULIPOISHIA...“Amata, nakualika katika hili, ufuatane nami tukakamilishe kazi hii, tuondoe laana katika jamii na baraka za Klakos zitumwagikie kama umande wa asubuhi” Seidon alimtupia ombi Amata kwa lugha ya kushawishi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Hamna shaka, ombi lako limefika panapostahili, bega kwa bega tutakamilisha hilo, mimi nitakusindikiza kwa jua na mvua, kwa…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (6)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA SITATULIPOISHIA...Sauti za watu wakisali katika lugha isiyoeleweka zilisikika, Anna alitazama vyema na kuona viumbe kama watu wapatao kama ishirini hivi wakiwa wamezunguka kitu kama kitanda na katikati yake kulikuwa kumelazwa mwili wa binadamu ambao Anna aliutambua vyema, mwili wa rafiki yake kipezi Nesta.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Anna alibaki kakodoa macho akiangalia tukio…

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (9)


SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
“Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.

“Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho na unarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watu wako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.

“Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliuliza huku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amata ga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamiza chini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidole mahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,” alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na woga wa hali ya juu sana katika hilo. Akajiinamia kichwa kwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfuko mweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha macho yake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amata ga Imba, “Tunavuka?”

“Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imba akaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kisha akshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeee kwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika pale tayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu, najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishe safari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, haya twende,” Amata ga Imba alisema hayo na kumuamuru Seidoni kuendelea na safari.

Amata ga Imba na mwenzake Seidon walipewa ukarimu wa hali ya juu sana, huduma zote alizostahili kupata mwana wa Suiltan basi wao waliziopata pia. Seidon alihisi nguvu zimemrudia na mwili wote ulikuwa umekuwa katika hali yake ya kawaida.

“Unajisikiaje sasa?” mwanadada\mrembo aliyepiga magoti mbele ya Seidon alimtupia swali lile, Seidon alijikuta anashindwa kujibu, alibabaika kwa swali hilo hasa alipomwangalia msichana yule mbichi ambaye alivaa nguo ndefu lakini iliyoanzia kiunoni kurudi chini huku juu alibaki hivohivo, chuchu zilizochongoka na kusimama zilimfanya Seidon apagawe, midomo ilimchezacheza, kabla hajasema kitu alikabidhiwa ua zuri la manukato safi, akalipokea na kulinusa, ua la yugiyugi, Seidon akaongea maneno yasiyoeleweka katika lugha ya kwao na lile ua likachanua mkononi mwake, akatikisa kichwa kuashiria kuwa kuna kitu amegundua. Katika mila za Wavelvesh, ua la yugiyugi lilimaanisha bahati, hivyo msichana huyu kumletea ua hilo Seidon ilikuwa ni kama bahati.

“Unaitwa nani?” Seidon akamuuliza

“Teboria,” akajibiwa.

“Teboria, Teboria, Teboria!” Seidon alirudia kutamka jina hilo kwa mara kada kwa sauti ya chini, alihisi ameshawahi kulisikia sehemu lakini hakumbuki ni wapi.

Teboria akaketi jirani na Seidon, Seidon akahisi harufu nzuri ya manukato kutoka kwa binti yule, akasogeza kinywa chake jirani na yule binti, yule binti naye akafanya hivyo, ndimi zo zikapishana kwa ufundi mkubwa sana, Seidon alihisi raha ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata katika maisha yake, sauti za mahaba zikaanza kukijaza chumba kile. Seidon akachanganyikiwa, akaweka upanga wake pembeni na kutaka kumsaula yule binti, yule binti akajitoa kifuani mwa Seidon, Seidon alipomtazama usoni hakuwa Teboria, balisura ya msichana mwingine kabisa ambayo pia haikuwa ngeni usoni mwake.

“Ni nani wewe?” Seidon alimuuliza yule msichana huku akiwa kajirushia upande wa pili wa kichumba hicho.

“Ulinikimbia ee? Sasa nimekupata tena, na sintokuacha mpaka uitimize ile ahadi yangu, mimi ni Sherhazad, Malkia wa Soria, nimekuona tangu ukiwa Hamsud na nikafurahi kwa kuwa ulifanikiwa kuchukua lile fuvu, haya nikabidhi au la naitoa roho yako na fuvu nalichukua,” Sherhazad, sasa alichukua sura na umbo lake la kawaida. Chumba kikajaa manukato maradufu, Seidon akabaki anatetemeka mkononi akiwa ameshika ule mfuko mweusi ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu. Sherhazad alimfuata huku mikono yake ikiota kucha ndefu kupita kawaida, ilikuwa ni hali ya kuogofya, ulimi wake uligawanyika mara mbili, mara kichwa chake kikageuka na kuwa cha nyoka, Seidon alisimama na kuutwaa upanga wake, sasa Sherhazad akawa nyoka kamili, nyoka mkubwa, tuseme joka. Lile joka likaruka kumfata seidon pale aliposimama, Seidon akaepa na kuvurumisha ule upanga lakini akalikosa. Kishindo kile kikubwa cha lile joka kuangukia chini kiliwashtua wengi.

Amata ga Imba akiwa amejilaza chini ya mtende, alisikia kishindo hicho na mara akasimama na kukimbilia kwenye kile kinyumba alimokuwa Seidon, alipofika hakuamini macho yake, Seidon alikuwa amevirigwa na lile joka, Amata ga Imba akaufuta upanga wake na kukata sehemu ya mkia wa lile joka, mara akasikia sauti ya mwanamke ikicheka kwa kebehi, Amata ga Imba alitazama huku na kule hakuona kitu wala mtu ila sauti hiyo iliendelea kumcheka kwa kebehi. Amata ga Imba akatulia pale alipo huku upanga wake ukiwa juu hewani ameushika mpini kwa mikono yake miwili, alipoushusha alikata katikati mwa lile joka, lile joka likapiga ukelele wa ajabu na kumuachia Seidon, kisha likajizungusha pale chini na badala yake akasimama msichana mrembo, Teboria.

“Amata ga imba, majini haya, tuondoke,” Seidon, alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata, Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,” Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.

“Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imba alimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliuliza kwa kelele,

“Sikiliza Seidon nilishakwambia epukana sana na wanawake, hawa wataharibu mpango mzima, sio binadamu wale ni majini, sasa usirudie tena, Sherhazad keshajua unakoelekea na ameshakuona ukiwa na hilo fuvu sasa kazi ni nzito kufika Hamunaptra, na hii ni kwa sababu tu umekiuka masharti. Wewe mwenyewe ulinambia kuwa babu yako amekuonya hivyo hivyo juu ya wanawake, sasa kwa nini utaki kusikia? Kuwa mwangalifu,” alimaliza Amata ga Imba kisha akarudi na Seidon mpaka pale chini ya mtende.

Wakiwa katika kuketi pale mara akaja mmoja wa masuria wa yule mzee aliyewakaribisha akawapa ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo, wakaingia ndani na kuketi mbele yake.

“Sikilizeni vijana, hapa pameshaingia matatizo, inabidi muondoke mara moja, tayari pepo zinataka hilo fuvu kwa nguvu zote, pepo la Soria, mwanamke hatari tayari limeshakuja hapa kwa nguvu zote kabisa. Naomba watu wangu wasidhurike, muondoke, muende na safari yenu, lakini kwa kuwasaidi ili mfike salama, sikilizeni, msipande farasi kwani hana uwezo wa kuvumili shida na dhoruba za jangwani, maana sasa mtakatisha jangwa kubwa lenye vikwazo vingi lakini hamna budi kuvuka ili mfike haraka huko muendako na hiyo ndiyo njia fupi, piteni katikati, usiku, miifuata nyota ya kilimia itawaongoza mpaka katika bonde la Sham, ambapo amtalivuka na kutokea karibu na mto Frati kutoka hapo nafikiri mnaijua njia,” yule mzee mwnyeji wao aliwaekeza na kisha kuwapatia ngamia, masurufu ya njiani na kuwaruhusu waende zao, mara tu Maghalibi ikifika ili waondoa nuksi katika kijiji chao.

Safari ilianza jioni hiyo, Amata ga Imba akiwa mbele na Seidon akiwa nyuma yake, walilikata jangwa kwa taabu ya upepo na ghasia za vumbi lakini walivumilia ili lengo lao lipate kutimia. Usiku wa manane walijikuta wamefika mbali sana na mbele yao palionekana kitu kama korongo kubwa sana, mbala mwezi ilikuwa ikiwaongoza kwa mwanga wake mwanana, wakasimama kwa muda na kutazama mandari ile yakutisha kama si ya kuvutia, ‘Bonde la mauti’ Amata ga Imba alihisi sauti ikimnong’oneza, akageuka nyuma asione mtu, akaendelea kutazama kutazama lile korongo kubwa sana, kitu kama moshi kilikuwa kikifuka na kulijaza lile korongo, waliweza kuona vitu kama mawe si mawe ilimradi tu vilikuwepo vipo. “Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.

“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.

“Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho na unarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watu wako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.

“Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliuliza huku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amata ga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamiza chini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidole mahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,” alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na woga wa hali ya juu sana katika hilo. Akajiinamia kichwa kwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfuko mweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha macho yake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amata ga Imba, “Tunavuka?”

“Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imba akaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kisha akshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeee kwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika pale tayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu, najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishe safari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, haya twende,” Amata ga Imba alisema hayo na kumuamuru Seidoni kuendelea na safari.

Walishuka katika bonde lile wakiwa na wale ngamia taratibu, ukimya ulitawala kila kona giza likazidi kuwa kubwa, wakazidi kutokonmea gizani mpaka wakafika mahali hawaonani. Amata ga Imba akasimama, akapapasa na kumgusa Seidon, akamshika mkono, kisha taratibu akazidi kwenda nae ndani zaidi ya korongo lile. Kelele za watu waliokuwa sokoni zilisikika kwa mbali, mwanga hafifu ukaanza kujitokeza kwenye lile giza, Seidon alikuwa akiogopa sana, “Usioneshe unaogopa, jikaze, huu ni mji wa wafu, hawa wote utakaowaona ni wafu, waliokufa zamani huko duniani,” Amatagaimba akamwambia Seidon, wakaendelea kwenda, Seidon alianza kuona watu wengi kwa mbali na baada ya mwendo mrefu kidogo walifika kwa watu wale na kuwapita taratibu lakini baadae wakajikuta wamezingirwa na watu kama kumi na tano hivi, wao wakiwa katikati, Seidon na Amatagaimba wakapeana migongo na kuwatazama watu wale kwa zamu.

“Mnakwenda wapi?” mmoja wa wale watu ambaye alionekana ana rangi ya kijivu aliuliza, si Amatagaimba wala Seidon aliyejibu swali hilo, akaja mwingine wa kijani mwili wote mpaka mavazi aliyevaa, “Hamusikii? Au hamuelewi? Mbona hamjibu?” kabla hajamaliza kuuliza mwingine akapita katikati yao na kusimama uso kwa uso na Sedon, “Lete huo mzigo hapa haraka!” Amatagaimba alisikia sauti hiyo, akajua kuwa jamaa hao wamegundua kuwa wao wamebeba nini, akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
66 Hamunaptra Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni