Notifications
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (10)


SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Amatagaimba na Seidon walipopata upenyo wakatimua mbio maana waliona wazi kuwadhibiti watu wale isingekuwa rahisi, nyuma yao bado kundi kubwa la watu lilikuwa likiwafuata kwa kasi wakiwa na silaha mbalimbali. Seidon na Amata walikaza mwendo kwa kukimbia wakifuata ujia mwembamba uliokuwa ukiongoza wasikokujua, baada yam bio za muda mrefu bila ya kusimama, wakafika eneo ambalo lilikuwa na miamba mingi sana wakasimama na kujificha, walikuwa wakihema sana, Seidon alijilaza chali chini katika vumbi, Amatagaimba akabaki kuchungulia kama hao jamaa wanakuja, hakuwaona. Akatoka katika lile jiwe na kujisjika kiuno, “Seidon! Hawapo,” akamwambia Seidon ambaye muda huo alikuwa amejilaza pale chini, akajinyanyua na kuketi, atulia kidogo na kuweka sawa ule mfuko wake ambao ndani yake kuna lile fuvu, alipoliufungua alibaki akishangaa, Amatagaimba akamtazama Seidon, “Vipi mbona umeduwaa?” akamuuliza Seidon.

“Amatagaimba, njoo uone maajabu haya!” Seidon akamwambia Amatagaimba, akajongea karibu na ule mfuko, alipotazama ndani alishangaa kuona lile fuvu liking’aa katika yale matundu ya macho, “Seidon,” Amatagaimba akaita kwa kunong’ona, Seidon akamtazama Amatagaimba usoni, “Klakos wameshapata harufu ya fuvu la Cleopas, sasa wao ndio watatuongoza katika hisia kulifikisha mahali pake, lakini bado mitihani mingi inatukabili, hatuna budi kuivuka, hasa hasa Serhazad, inabidi tumzunguke” Amatagaimba aliongea. Seidon akaufunga vyema ule mfuko na wote wawili wakaanza kutembea polepole kuendelea na safari yao, wakafika njia panda, sehemu hiyo ilikuwa ni njia nne zilizotoka kwenye njia moja, wakasimama. Amatagaimba akaziangalia kwa makini zile njia, Seidon alibaki amesimama akiwa hajui la kufanya. Kati ya zile nne, walipoiangalia njia ya kwanza mbele kabisa wakaona kuna msitu mkubwa ukali mbali, njia ya pili kulikuwa na maji mengi sana kama bahari kubwa ing’azwavyo kwa jua la adhuhuri, njia ya tatu kulikuwa na jangwa kubwa ambalo ukiangalia tu utaona kitu kama mvuke wa moto unaowaka juu ya mchanga ule, upepo nao uliuyumbisha huku na kule, njia ya nne ilikuwa na milima mikali ya mawe yabisi ambayo ilikuwa ni ngumu kwa mwanadamu wa kawaida kuyakwea. “Tunafanyaje?” Seidon akamuuliza Amatagaimba. Amatagaimba hakuwa na la kujibu kwa wakati ule, alilitazama jua linalochomoza kwa mbali likipendezeshwa kwa miale yake murua, akamtazama Seidon alieonekana kukata tama katika hali hiyo.

“Lete hilo fuvu ndilo litakalotuongoza njia,” akamwambia Seidon, akafanya hivyo, akatoa katika ule mfuko mweusi fuvu la Cleopas akamkabidhi Amatagaimba. Hatua chache katikati ya zile njia, Amatagaimba akalishika lile fuvu na kulitazamisha katika njia moja baada ya nyingine, njia ya tatu, njia ya jangwa, macho ya lile fuvu yakang’aa, wote wawili wakatazamana na kutabasamu. Seidon akalirudisha lile fuvu mfukoni, kisha wakaanza kutembea kuelekea ile njia ya tatu.

Jua lilizidi kupanda juu, mwendo ukazidi kuwa mgumu, mchanga ukaishika miguu yao na kuifanya mizito kama iliyofungwa mawe. Wakiwa katikati ya jangwa lile, Seidon aligeuka nyuma na kuwaona watu wane wakija kwa kasi farasi, wakielekea ule upande ambao wao walikuwepo. Amatagaimba aliwatazama watu wale akiwa amesimama bila kufanya lolote, nao wakizidi kukaribi pale walipokuwepo.

Amatagaimba alisikia mlio wa upanga ukifutwa kutoka katika ala yake, akamgeukia Seidon, akamuona ameushika upanga wa makali kuwili mkononi mwake. “Seidoni, yumkini watu hawa si wa shari, rudisha upanga wako mahali pake, tusije tukakosa Baraka za Klakos,” Amatagaimba alimwambia Seidon. Upanga ukarudishwa mahali pake na wote wawili wakasimama kwa heri. Wale watu wane wakawafikia Amatagaimba na Seidon, watu wale walikuwa wamevaa mavazi tofauti kwa rangi. Mmoja wao akashuka kutoka katika farasi, yeye alikuwa amevaa nguo nyeupe zinazometameta, sura yake haikuonekana sawasawa kutokana na kinyago alichovaa ambacho mbele badala ya sura kulionekana kama tundu kubwa jeusi. Akasogea na kumwasogelea Amatagaimba na Seidon, “Seidon, Amatagaimba,” aliwaita kwa kuwatazama kwa zamu kila mmoja kwa wakati wake, “Safari mnayokwenda ni ndefu sana ijapokuwa mmekaribia pale muendapo, sikilizeni kwa makini, sisi mnaotuona, tumetafuta hilo fuvu kwa karne na karne na hatukulipata ndio maana mwaona mvua hakuna, jua ni kali na kadhalika, ninyi wanadamu mnatutegemea sisi daima. Mimi ni Malaika wa Jua, huyo mwenye vazi la kijani ni Malaika wa Mvua, huyo mwenye vazi jekundu ni Malaika wa Vita na huyo mwingine mwenye vazi la kijivu ni Malaika wa ukame na shida, kila mmoja ana uwezo wa kuleta kile alichonacho na kukizuia.

Tulipata maono kuwa ninyi mnalo hilo fuvu na mko mbioni kulirudisha kwa Cleopas, maamuzi mazuri sana, sasa twaomba tuwasindikize mpaka katika mlango wa piramidi ambalo Klakos ipo ndani yake hapo sisi tutasubiri nje na kuwatakia heri kwa hilo lililo jema kwa wanadamu.”

Amatagaimba akamtazama Seidon na kumpa ishara ya kuwafuata, kufumba na kufumbua waliona farasi wao wakija pale walipo, wakashangaa kwa hilo, walipowafikia, wakawapanda na safari ikaanza, Amatagaimba na Seidon wakawa katikati na wale watu wakawa mbele wawili na nyuma wawili, safari ikaanza.

Baada ya mwendo mrefu juani walifika eneo pana lenye uwazi mkubwa mno, hakuna kilichoonekana zaidi ya mchanga na upepo unaovuma ambao unafanya vumbi la kutisha, “Sisi ni pepo nne za dunia, hapa tulipo sasa ni katikati ya dunia, nguvu ya uvutano inatawala eneo hili tulilosimama,” alisema Yule wa kijani.

“Nasikia vurugu kubwa huko katika dunia ya chini, ulimwengu unavutana na kuzimu, mbingu zimetulia,” akasema Yule mwenye guo jekundu. “Basi na tusisonge mbele, maana hapa tulipo ni mji wa wafu,” akamalizia Yule mwenye vazi la kijivu. Wakateremka kutoka juu ya farasi wao na kusimama chini, juu ya mchanga, wakakutanisha mikono yao pamoja na kufanya kitu kama mraba. Amatagaimba na Seidon hawakuelewa kinachofanyika, wale watu wakatulia kimywa wakiwa wameinamisha nyuso zao chini, mavazi yao yalikuwa yakipepezwa kwa upepo mkali uliofanya vumbi jingi. Mara tai mkubwa alipita kwa kasi katikati ya Seidon na Amatagaimba, kufumba na kufumbua Yule tai alikuwa amenyakuwa ule mfuko mweusi wa Seidon wenye fuvu, Amatagaimba bila kuchelea alichomoa mshale katika podo lake na kuuweka kwenye uta wake, akavuta huku akibana jicho moja na kumlenga Yule tai aliyekuwa akienda kasi sana, Amatagaimba alijuwa wazi kuwa kama tai Yule alitoka upande wa kusini basi lazima atarudi kusini aliufyatua uta wake na ule mshale ulichomoka kwa kasi ya ajabu, kila aliyeangalia kwa macho aliona mshale ule kuwa umepigwa upande tofauti.

“Usimuuuueeeeee!!!!!!” Yule Malaika wa jua alipiga ukulele na mara ule upepo ukakatika ghafla na vumbi lote likatulia ardhini kama mwanzo. Wote nyuso zao zikuwa zikitazama kule juu kwa Yule tai, mshale ule kama ulivyotumwa, wakati Yule tai akijigeuza kurudi upande wa kusini alikutana nao na ukampiga shingoni, miguu yake ikaliachia lile fuvu likawa likidondoka kwa kasi kurudi ardhini, Seidon alikwea farasi na kupiga mbio kuelekea kule fuvu linakodondokea, Amatagaimba alimtazama Yule tai na badala yake hakumuona tai bali aliona taswira ya mwanamke ikija kasi kutoka juu kuja kwake, mbele ya mikono yake kulikuwa na donge kubwa la moto.

“Tufaaaaaaannnnnnnnn” Yule Malaika wa rangi nyekundu, Malaika wa vita alipiga kelele na wengine wote wakalala chini katika mchanga, Amatagaimba aliuchomoa upanga wake na kuuweka barabara, Yule mwanamke akauzungusha ule moto na kuuwacha utangulie kabla ya yeye hajafika, Amatagaimba aliuepa kiufundi na kupiga upnga wake pigo la kifo lakini Yule mwanamke alipita na kutua akasimama chini. “Ni nani wewe mwanamke muovu?” Yule Malaika akauliza, “Sherhazad Malkia wa Soria,” Yule mwanamke alijtambulisha, kabla hajamaliza Yule Malaika wa vita akaizungusha mikono yake kwa namna ya ajabu na kutengeneza kitu kama moto uliokuwa ukiwaka mbele ya mkono yake na kuutuma kwa Sharhazad,

lakini kwa nguvu ya kichawi, Sharhazad nae aliuzuia moto huo katikati, ukawa ukiwaka hewani, Amatagaimba aliona ile vita haiwezi alisimama kando, alipowatazama wale wengine aliona bado wamelala kifudifudi huku vumbi kubwa likitimka upya eneo hilo, mapigano yalikuwa makali mpaka ardhi ya eneo lile ilikuwa ikitetemeka, Seidon alisimama kando ya Amatagaimba akiwa na ule mfuko mkononi baada ya kuudaka salama, wakati mapigano hayo yakiendelea asrdhi ilizidi kutetemeka, radi kali zikapiga na kuchora michoro ya kutisha angani, mara kipande cha ardhi kikamegeka na kudidimia, pakabaki uwazi mkubwa sana, Yule mwenye vazi la kijivu akawatazama na kuwaamuru kuingia kwa ishara ya mkono. Hakuna aliyesita, Seidon na Amatagaimba waliingia kwa kasi kwenye lile shimo wakiacha vumbi likitimka huko nje kwa jinsi ardhi ile ilivyokuwa ikizidi kutetemeka, hofu iliwajaa mara giza nene likatawala mbele yao,

Seidon alipogeuka nyuma hakuona mwanga wan je, ardhi imejifunga. Amatagaimba akapapasa ukutanai na kushika kitu kama mti kilichopachikwa katika kiango, akauchomo na kugundua kilikuwa ni kienge ambacho kingewasaidia kuona humo ndani, Amatagaimba akachukua kitu mfano wa kijiti katika pindo la vazi lake, akakisugua katika nywele zake kile kijiti kikashika moto, akawasha kile kienge na mwanga wakutosha ukatokea. Seidon alisikika akishusha pumzi ndefu, kisha wote wawili wakaongoza kwenye ujia mrefu ulioonekana ukielekea mbele zaidi. Huku wakisaidiwa na ule mwanga kutoka katika kile kienge walitembea kwa tahadhari kubwa, Seidon alikuwa mbele wakati Aamatagaimba alikuwa akifuata kwa nyuma.

Mchakato wa miguu ya farasi anayekimbia kwa kasi ilisikika, kwa jinsi ilivyosikika hakuna aliyejua ni upande gani ilitokea, mbele au nyuma. Mara ghafla upande wa nyuma waliona moto mkubwa ukija, wakaanza kutimua mbio kuelekea mbele, walikimbia na kukimbia lakini bado farasi Yule wa moto alikuwa akija kasi na akizidi kuwakaribia, “Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
66 Hamunaptra Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni