HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.
TUENDELEE...
Baada ya kikumbo hicho kilichomfanya ajibamize vibaya ukutani, alijikuta anaishiwa na nguvu na upanga wake asiuone mkononi mwake, haraka akautoa uta wake na kuchukua mshale ambao aliupachika na kuuvuta kwa kulenga shabaha kwa Yule farasi wa moto, alipouachia mshale ule ulikwenda moja kwa moja ukimuelekea Yule farasi wa moto ambaye sasa alikuwa sambasamba na Seidon. Seidon alimshuhudia aliyekuwa juu ya farasi huyo, akianguka udongoni kwa kishindo na kusababisha mlipuko mkubwa uliotetemesha pango lote hilo, mara vumbi na mchanga vilionekana kutokea katika nafasi zilizomo kati ya jiwe na jiwe. Amatagaimba aijinyanyua haraka na kukimbilia kule ambako Seidon naye al;ikuwa ameanguka baada ya mlipuko ule kumsukuma. Akamshika mkono na kumvutia kando.
Mchanga ulizidi kumwagika kutoka katika ile mipenyo na pango zima likawa linatetemeka, “Amatagaimba, tuondoke hapa si salama,” Seidon alimwambia Amatagaimba wakati huo yeye akiwa tayari ameanza kuondoka eneo lile, Amatagaimba naye akaanza kutimua mbio kumfuata Seidon, ule moto uliendelea kuwa mkubwa na ukaanza tena kuwafuata huku mbele yake ukitanguliwa na upepo mkali sana. Katika kimbia hiyo Seidon aliona katika ukuta kuna kitu kama kichwa cha farasi lakini kilichochongwa kawa kutumia jiwe kikiwa kimejitokeza katika moja ya mawe yale yaliyopangwa kwa ustadi kufanya lile pango kuonekana katika hali ile. Seidon alilishika kwa mikono miwili lile jiwe lenye umbo la kichwa cha farasi, akafanya kama anabembea, akitumia mikono yake na kuinyanyua miguu yake, uzito wake ulifanya lile jiwe kuinama na mara baadhi yam awe yakaaza kurudi kwa ndani na kutengenea uwazi mdogomdogo katika kuta hizo. Amatagaimba aliona mawe ya mbele yake yakifunguka na kufanya kitu kama mlango,
hakuuliza aliingia na kusimama ghafla kisha akageuka nyuma na kumchungulia Seidon ambae alikuwa tayari ameliachia lile jiwe na kukimbili kule aliko Amatagaimba wakati ule moto nao ulikuwa umemkaribia sana, kabla hajaufikia ule mlango tayari moto ulikuwa umemfikia, “Amataaaaaaaaaaaaaa!!!!!!” alipiga ukulele na kabla Amatagaimba hajafanya lolote mara ilipiga radi kali sana iliyofanya mistari ya mwanga wa kutisha ndani ya pango lile, na ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha, ajabu. Amatagaimba aliishuhudia mvua ile ikinyesha bila simile ikitoka tu juu ya pango lile ambalo lilikuwa limeezekwa kwa mawe kwa ufundi wa hali ya juu, akanyosha mkono wake na kuushika ule wa Seidon kisha akamvuta kule alikokuwa yeye, mara ile mvua ikaacha kunyesha ghafla, na ule moto ulikuwa umezimika wote, Amatagaimba alitazama na hakuona farasi wala mtu aliyekuwa na farasi, ‘Orion?!’ alijiuliza huku amejishika kifua, moyo ukimwenda mbio, akamtazama Seidon aliyekuwa kajilaza chini akitweta.
“Tuondoke,” Seidon alimwambia Amatagaimba huku akinyanyuka na kifuata njia hiyo inayopita chini kwa chini, sasa hawakuwa na kile kienge cha moto kwa ajili ya kuwaangazia, giaza liliwafunika kama kawaida, Amatagaimba akakumbuka kitu, akaufungua ule mfuko uliofungwa mgongoni mwa Seidon, mfuko wenye fuvu, akalitoa na kukuta liking’aa katika macho yake na kufanya mwanga mkali na mweupe kama wa jua la mchana. Mara baada ya kulito na kupata mwanga huo alianza kusikia kama kelele za vikaragosi vikishangilia na kukimbia huku na huko, “Nini hicho?” Seidon aliuliza. Amatagaimba akatega sikio kusikiliza akainua mkono wake na kuitazama pete yake ya ajabu, ndani ya pete hiyo aliona viumbe vya ajabu vikikimbia huku na huko, vingine havikuwa na vichwa, vungine vina mguu mmoja, vingine vilikuwa na shepu isiyoelezeka kimaandishi labda kimichoro.
Amatagaimba akashusha mkono wake chini, akamtazama Seidon, “Tupo kwenye roho chafu,” Amatagaimba alimwambia Seidon huku akimzuia kwa mkono wake maana Seidon alitaka kupita mbele yake, akamtazama Seidon na kumwambia, “Hapa lazima tupite kinyumenyume ili hizi roho chafu zisituone,” wakafanya hivyo, wakapita eneo lile kinyumenyume, bado waliendelea kusikia vishindo vya roho hizo zikimbia huku na huku huku zikipiga kelele kama za panya walionaswa katika mtego. Baada ya kuvuka eneo hilo wakajikuta wametokea eneo la wazi kisha kuna ngazi ndefu inayoshuka chini na huko chini kunafuko moshi kana kwamba kuna moto uliozimwa muda huohuo, wakasimama na kuangaza macho yao kule, “Hamunaptra,” Seidon aliongea kwa kunong’ona. Ni Amatagaimba tu aliyemsikia, kisha wote wawili wakaanza kutelemka zile ngazi kwenda kule chini, walipofika katikati ya waliikuta ile ngazi imeishia hapo na ule mji waliouona ukali mbali bado, wakasimama na kushangaa jambo hilo.
Walipokuwa kule juu waliiona ile ngazi imejichoma katika ule moshi, kumbe ilikuwa imeshia pale. Amatagaimba akabaki kuduwaa hajui afanye nini, alipogeuka nyuma alikuta hakuna ile ngazi ila yeye kasimama juu ya nguzo ndefu ambayo juu yake kulikuwa na eneo dogo sana la nusu mita ya mraba, alishindwa afanya nini, alipomtazama Seidon naye alikuwa katika nguzo nyingine kama hiyo. Amatagaimba aliangali chini ilikoanzia nguzo ile hakuona kutokana na kitu kama moshi kutanda eneo hilo, alichokiona ni urefu mfupi wa nguzo kama mita moja hivi zaidi ya hapo ni moshi uliokuwa ukipita kutoka sehemu moja kwenda nyingine ambao haukuwqaruhusu kuona chini kabisa zilikoanzia nguzo zile. Sauti za farasi na watu zilisikika mbali sana kutoka chini.
§§§§§§
“Aaaaaaaaaa ha ha ha ha ha ha ha ha …” ilikuwa sauti kali ya Sherhazad iliyosikika akiangua kicheko kikali ambacho kiliwatoa ndege kwenye matundu yao. Alivuta hatua chache kutoka kiti chake cha enzi kilichotengenezwa kwa dhahabu safi, akateremka vijingazi hivyo huku akifuatiwa na vazi lake refu lililokuwa likimetameta kwa jinsi lilivyoundwa, kwa maana halikushonwa.
Chini katika sakafu ya jumba hilo la kifahari kulikuwa na wazee wanne waliolala kifudifudi kuonesha heshima kwa Malkia huyo wa Soria. “Inukeni enyi wazee wangu,” aliwaamsha nao wakaamka. Akawatazama mmoja mmoja kisha akaangalia kule kwenye dirisha lake la kichawi na kuwaona Amatagaimba na Seido wakiwa bado katika zile nguzo, akacheka tena cheko lake la ajabu.
“Asanteni sana kwa kazi mliyoifanya ya kuwatega wale wajinga pale, sasa tunakwenda kuwamalizia palepale kwani hawana uwezo wa kukimbia,” aliposema hayo akatoa vazi lake alilojifunga shingoni na kuonesha jeraha lake kubwa, “Hapa ni upanga wa Amatagaimba umepita, lazima moyo wake niutafune nyama, twendeni,” Sharhazad akaamuru. “Sikiliza ee jirani sana na mwezi kwa sasa, hivyo mpaka yapite majua mawili,” alisema mmoja wa wale wazee, kisha mwingine naye akafungua kinywa chake akasema, “Tazama ee Malkia, Amatagaimba, shujaa wa msitu wa Solondo ana pete ya ajabu aliyopewa na Malkia Baghoza wa msitu wakati alipoweza kuurudisha utawala wake kwa kumuangamiza Kelume, akiwa na pete ile kamwe hatutaweza kumshinda, isipokuwa tunaweza kupotea sisi wote, na utwala wako ukaanguka vibaya,”
Yule mzee aliposema hayo Malikia Sherhazad alikunja sura yake na alionekana wazi hasira kumjaa kichwani mwake, radi kali zilipiga na kupasua anga, wale wazee wakaanguka kifudifudi, “Si hivyo ee Malkia, bali tahadhari ni muhimu kuliko hatari,” walisema wote kwa sauti moja. “Ninyi mnajua wazi kuwa tukilipata lile fuvu, sisi ndiyo tutakuwa na sauti juu ya ulimwengu wote wa majini, wale pale wameshafika Hamunaptra na tukiwakosa wakiingia katika pyramid kubwa, chini ya ardhi basi hatutawaweza tena,” Sherhazad aliwaeleza wale wazee, “Na sasa nataka niiteketeze hiyo pete ya Baghoza kwa moto wa ajabu kabla hatujaenda pale,” akaongeza kusema huku mikono yake ikiwa imeshikishwa kiunoni. Akautoa mkono wa ke wa kushoto na kuongea lugha ya ajabu lugha isiyoeleweka, macho yake yakageuka na kuwa mekundu kama makaa ya moto, ulimi wake ulikuwa kama muale wa moto unaowaka kwa nguvu, Sherhazad alipandisha sauti na kuwa makelele mengi ndani ya jumba lile kisha akatema donge kubwa la moto lililopita katika lile dirisha la ajabu na kupotelea milimani. Wale wazee waliinuka na kutazama pambano hilo litakalotokea huko katika mji wa Hamunaptra.
§§§§§
AMATAGAIMBA akiwa pale juu ya nguzo bado alikuwa hajui la kufanya kwa kuwa hakuwa anajua urefu kwenda chini, kila alipoangalia bado ni mawingu au ukungu ulimnyima uhuru wa kuona chini. Akiwa katika kutazama hilo alisikia sauti ya Seidon ikimpa tahadhari kuwa kuna kitu kama jiwe kikimjia kwa kasi, Amatagaimba aligeuka na kuona ile dhahama inayokuja, akashindwa afanye nini, alishangaa badala ya jiwe sasa liligeuka kuwa donge la moto, Amatagaimba akafikiri haraka na kujiweka tayari kuukinga moto ule, ulipofika akaepa ukapita pembeni lakini alishangaa moto ule ulikuwa ukija mkononi mwake, akagundua baadae kuwa ni pete inayotafutwa, akainua mkono akaibusu na kisha akanyoosha ule mkono wenye pete na kuusukuma kwa kasi ule moto kurudi ulikotoka, kitendo kile kilimfanya kuyumba na kudondoka kutoka pale aliposimama, alijitahidi asidondoke lakini haikuwa hivyo, alidondoka ila katika kujikinga akatanguliza mguu mmoja cha kushangaza hakudondoka badala yake mguu ule ulikanyaga ardhi umbali wa nusu mita tu kutoka pale aliposimama.
“Shiiit,” alitoa sauti hiyo na kumwambia Seidon ashuke kutoka pale alipo kuwa hakuna shimo eneo lile, Seidon akaruka na kutua chini kisha wakatimua mbio kushuka poromoko lile kuelekea chini, wakaingia kwenye pango kubwa. Amatagaimba alipogeuka nyuma hakuona ule moto, wakendelea kusonga mbele na walipoibuka upande wa pili, waliona mapyramid mengi sana yaliyojipanga katika mtindo mzuri.
“Sasa tupo Hamunaptra, inabidi tutafute pyramid la kale kuliko yote, humo ndimo tutapata Clakos,” Amatagaimba alisema hayo huku akiwa kasimama akiangalia yale mapiramidi, Seidon alikuwa nyuma yake tu nae akiuangalia mji huo. Akikumbuka jinsi alivyofika kwa mara ya kwanza kwa shida kuchukua fuvu lile. Wote wawili wakaendelea kutembea kwa kupita njia zinazowaficha ili watu wenye nia mbaya wasiwaone na kuwadhuru, lakini bado watu walikuwa wakiwakodolea macho kila hatua wanayopiga. Baada ya mwendo kidogo walikutana na mzee mmoja wa makamo, aliyevaa guo refu na kufunika kichwa chake, alionekana uso tu, uso wake ulikuwa ni kama wa kijivu hivi.
“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni