RANIA (2)
Zephiline F Ezekiel
3 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA MBILI
ILIPOISHIA...
Jao..kamata huyu twende nae kwenye jumba la kifalme akapate adhabu yake..hawezi kua na dharau kiasi hiki kwangu mimi...aliamuru fasha.SASA ENDELEA..
Jao alimkamata Rania na kumfunga kamba,lakini hata hivyo rania hakua na hofu yoyote.Wakiwa njiani wanaelekea kwenye kasri(jumba la kifalme),mara walikutana na omandi mlinzi mlinzi mkuu wa mfalme..
Fasha...aliita omandi baada ya kumwona fasha..
Fasha aligeuka na kumwangalia vibaya sana omandi kisha akasema:unaruhusiwa na nani wewe kuniita jina langu badala ya kuniita mwanamfalme?...alisema fasha.
Nisamehe sana mwanamfalme.....alisema Omandi akiwa ameinamisha kichwa chake.
Haya unashida gani?..aliulza mwanamfalme.
Mfalme ameniagiza kuja kukutafuta..alisema omandi.
Fasha alishtuka sana na kumuuliza omandi: nani amemwambia kua sipo kwenye kwenye kasri?
Hilo mimi sijui...alisema omandi
Haya twende...alisema fasha.
Mheshimiwa...na huyu binti ni nani?..aliulza omandi.
Fasha alimgeukia na kuwangalia jicho baya omandi..
Nisamehe kwa kuvuka mipaka mwanamfalme.. Alisema omandi akiwa ameinamisha kichwa..
Walipanda katika farasi na kuanza safari ya kuelekea kweye kasri(jumba la kifalme)..
Walipofika kwenye kasri hawakuingilia njia kuu..walipita chodo wasionekane...
Mfalme kwa kujua kua fasha hatapitia lango kuu la kasri,alikaa kwenye njia ile ya uchochoro kumsubiri fasha.
Fasha na wenzie waliingia ukulu bila kujua kua mfalme anawaona vizuri tu.
Fasha akiwa anatembea mule kwenye kasri mara alisikia sauti ya mfalme : hivi unazani unatoka wapi na unaelekea wapi na kwa ruhusa ya nani?.
Fasha alishtuka na kugeuka nyuma.. Alipokutanisha uso na mfalme aliona aibu na kusema : nisamehe sana baba.
Mfalme alimsogelea Fasha kisha akasema : hivi wewe kijana una akili gani?.. Unajua jinsi gani unaandamwa hapa ikulu kiasi gani!!...halafu unaleta upumbavu wako kila kukicha..unataka mimi nilaumiwe sio?...aliuliza mfalme.
Fasha aliangalia chini akiwa hajapata cha kujibu bado.
Na huyu binti ni nani na unakwenda nae wapi?..aliuliza mfalme.
Huyu amenitukana huko mtaani,nataka apate adhabu yake hapa ikulu ili iwe fundisho...alisema fasha.
Mfalme alimwangalia Rania ambae hakuonekana na wasiwasi yoyote ile..
Fasha... Wewe ni mpumbavu..alisema mfalme.
Eeeeh...aliuliza fasha kwa kimshituko kidogo.
Ndio wewe ni mpumbavu...kwahyo utamwadhibia wapi na ukiulizwa utajibu mmekutana wapi?.. Mbona unafanya mambo bila kufikiri?...aliuliza mfalme (vamani)
Lakini baba...alisema fasha kisha mfalme akamkatisha...
Lakini nini?...hebu mrudishe haraka sana ulikomtoa...?alisema mfalme na kuondoka kwa hasira.
Fasha alibaki amekasirika sana.Rania alipoona vile akafurahi na kuanza kumcheka Fasha kwa chini chini : hihihihihii
Fasha alizidi kukasirika baada ya kuona Rania anacheka..
Unacheka nini wewe? ..aliuliza fasha huku akiwa amemkaba Rania shingoni..
Hihihihihi...aliendelea kucheka Rania.
Jao...aliita Fasha kwa sauti yenye amri.
Ndio mwanamfalme...aliitika jao.
Mchukue huyu na ukamtelekeze msituni....alisema Fasha.
Ndio mwanamfalme... Alisema jao na kumkamata Rania.
Nini!!..msituni nimekuaje mimi?..nitatokaje?.. Aliuliza Rania.
Hayo hayanihusu...alisema Fasha.
We kweli mjinga kama nilivyosema..alisema Rania.
Fasha alimwangalia Rania vibaya sana wakati huo jao akitoka nae nje ya kasri (jumba la kifalme)
Wakati huo mfalme aliingia chumbani kwake akiwa amekasirika.
Akiwa amekaa sura ya Rania na matendo yake yalijirudia kichwa ni mwake.
Mmmh.. Huyu mtoto ni wa nani?..mbona tabia yake ya kutokuogopa kiasi hiki kama sio ngeni machoni kwangu?.. Alijiuliza mfalme.
Akiwa kwenye mawazo mengi mara mlango wa chumbani kwake uligongwa.
Ingia...aliamuru mfalme.
Mara aliingia mganga wa ikulu akiwa anahema sana sana na kusema: Mfalme....
Nini tatizo?.. Aliuliza mfalme kwa wasiwasi.
Nimeona ishara mbaya...alisema mganga.
Ishara gani hiyo?.. Aliuliza mfalme.
"NADISH" imeingia humu kwenye kasri muda sio mrefu.. Alisema mganga.
Nini?...nadish imeingiaaa?...saa ngapi?.. Aliuliza mfalme kwa mshtuko mkubwa
Sasa hivi tu... Tena umekutana nayo...na inaondoka sasa hivi... Alisema mganga.
Haaa....kumbe ni yule binti!!... Alisema mfalme.
Ni wa kike!!??..aliuliza mganga kwa mshangao.
Ndio...ni wa kike...alisema mfalme.
Kumbe ndio maana hakua na hofu yoyote mbele yangu na mbele ya mwanamfalme...
sasa nifanye nini?..aliuliza Mfalme.
Muue...ama sivyo utapoteza ufalme huu kama ilivyotabiriwa....alisema mganga.
Mfalme alimwita mlinzi wake omandi na kumweleza yote.
"NADISH"??...Aliuliza mlinzi wa mfalme kwa mshtuko.
Ndio...anatakiwa kuawa mara moja..tena sasa hivi kabla hajapotea..alisema mfalme.
Nitahakikisha anapatikana...acha nichukue walinzi niende kumsaka...alisema mlinzi wa mfalme..
Nitaenda na mimi maana nyinyi hamjamfahamu sura..alisema mfalme na kupanda farasi wake na kuanza safari ku wengine wakimfuata kwa nyuma.
Jao alipofika porini alimwambia Rania : tumefika sasa..naweza kukuacha hapa.
Sasa mimi nitatokaje hapa na njia siijui?..aliuliza Rania.
Jao hakutaka mazungumzo zaidi,alitoka na kuondoka zake.
Aaah...shenzi kabisa..shenzi sana..huyu Mpuuzi Fasha anapanga nife hapa kwa njaaa?..kwa taarifa yake sifi..nitakula Hata mchwa...alijisemea Rania kisha akaanza kutembea akiwa hajui anakoelekea.
Wakati huo Dom alikua kwenye shughuli zake za uwindaji kama kawaida yake..alikua mwindaji mzuri licha ya kua na umri mdogo.
Akiwa anatembea huku na huko mara aliona kundi la watu linakuja...wamevalia vinyago.
Akina nani hao?...alijiuliza dom huku anachungulia chungulia.
Watu wale waliendelea kusogea hadi wakakaribia alipokua Dom.
Dom aliamua kujificha.akiwa amejificha mara aliwasikia wakiongea.
Ni mtoto wa kike wa umri wa kama miaka kumi hivi... Ana nywele ndefu yeusi...alisema mmoja wa wale watu (mfalme)
Mmmh.. Nani huyo wanaemtafuta?...alijiuliza Dom.
Wakati anajiuliza mara alimwona Rania kwa mbali kupitia uwazi mdogo aliokua anatumia kuchungulia.
Rania alikua anachezea maua tu na kunusa harufu yake nzuri halafu anachekelea na kufurahi bila taabu yoyote.
Hawa mbona kama watakua wanamtafuta Rania?...au nakosea?..maana sifa wanazozitaja zote anazo Rania.
Mfalme na watu wake wakiwa wanamtafuta Rania, mlinzi mkuu wa mfalme aliuliza:
Mfalme, unahakika alikuja huku?..
Ndio..mganga ndo amesema amekuja huku...alisema mfalme.
Mmmh..sawa... Alisema omandi na wakaendelea kumtafuta.
Yule pale!!!....alisema mfalme baada ya kumwona Rania.
Bila kupoteza muda walianza kumfuata Rania kwa kasi.
Rania akiwa anaendelea na kazi yake ya kunusa maua mara alishukia amevutwa na mtu na kuingizwa uchochoroni..Nini kitafuata?
USIKOSE SEHEMU YA TATU
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni