RANIA (31)
Zephiline F Ezekiel
4 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Kweli kaka Dom.. Angekufa huyu mapepe...alisema Fasha.Mmmh...kaka Dom?....alisema Rania kiumbea zaidi asijue kinachoendelea...
SASA ENDELEA..
Nini kwani..umbea tu...alisema Fasha.Kama wewe... alisema Rania.
Dom alicheka tu kusikia hivyo.
Walikaa pale kwa muda mrefu.
Huku Mfalme alikua ameshapata wasiwasi juu ya Fasha kwakua alikua hajarudu hadi muda huo...
Baada ya muda mrefu waliondoka na kwenda ikulu.
Mfalme alisubiri sana lakini Fasha hakua akija...ila baada ya kusubiri sana Mara Fasha alikuja.
Mfalme akiwa anamawazo mengi mara alikuja Fasha na kubisha hodi.
Aah..Fasha.. Umechelewa sana...haya niambie ulichokipata..alisema Mfalme baada ya Fasha kuingia.
Fasha alikaa na kusema... Baba ni mengi niliyokutana nayo huko...alisema Fasha.
Yapi hayo?...aliuliza Mfalme.
Fasha alihofia kumweleza yaliyotokea kipindi Rania anamfuatilia Mars maana Mfalme hakua akijua habari ya Rania na uhusiano wake na ufalme.. Ilibidi tu amweleze upande wa pili pekee.
Baba...yule mama niliyekua nimeenda anipe maelezo kuhusu wazazi wangu... Ndie mama yangu mzazi... Alisema Fasha.
Haaaa...mama yako mzazi?...aliuliza Mfalme kwa mshangao.
Ndio Mfalme...na yule mtoto wake ni kaka yangu.. Alizaliwa yeye kabla yangu... alisema Fasha.
Mmh... Hili nalo kubwa kuliko...yuko wapi kwa sasa huyo mama?..aliuliza Mfalme.
Yuko hapa ikulu nimekuja nae...alisema Fasha.
Unasubiri nini?...mlete hapa nimwone...alisema Mfalme.
Fasha alitoka na kwenda alipokua Dom, Rania na Rai.
Mfalme anahitaji kuwaona..wewe Rania kaa hapo ubaki unacheka na ndege....alisema Fasha
Ila siku nikikupiga utaniheshimu...alisema Rania hadi wote wakacheka.
Rai na watoto wake waliondoka na kwenda alipokua Mfalme.
Waliingia ndani na kukaa...
Mfalme alipomwona Rai alimkumbuka maana aliwahi kuishi ikulu.
Aaah...kumbe ni wewe...sasa nakukumbuka vizuri... Alisema mfalme huku akimwangalia Rai.
Ndio ni mimi mheshimiwa Mfalme... Alisema Rai.
Pole sana kwa kupoteza mtoto wako kwa muda mrefu sana..alisema mfalme.
Asante sana mtukufu Mfalme....alisema Mfalme.
Nimesikia unajua mengi hapa ikulu... Naweza kukuliza baadhi ya mambo?.. Aliuliza mfalme.
Ndio bila shaka mtukufu Mfalme... Alisema Rai.
Basi Fasha na mwenzio mwaweza kunipisha hapa kwanza... Alisema Mfalme.
Fasha na Dom waliondoka na kumwacha Rai na Mfalme.
Kwanza unaitwa nani?...aliuliza Mfalme.
Naitwa Rai....
Ni kweli wewe ulikua msaidizi wa Mganga aliekufa?..aliuliza Mfalme.
Ndio Mfalme.. Alisema Rai.
Swali langu muhimu ni hili...wewe ndie ulieachiwa kiini cha nguvu na Mganga aliepita?...au kuna mwingine.. Aliuliza Mfalme.
Rai alisita kidogo ila akakubali kua ni yeye.
Vizuri sana...nakuomba jambo moja... Alisema Mfalme.
Lipi hilo mfalme.. Aliuliza Rai.
Kua Mganga wa ikulu hii...Mganga wa hapa aliasi nikamwondoa..kwa sasa hakuna Mganga hapa...nahofia himaya hii kupata madhara... Alisema Mfalme.
Mtukufu Mfalme... Kabla ya kuendelea na lolote inabidi nikujulishe jambo moja... Alisema Rai.
Lipi hilo?.. Aliuliza Mfalme.
Mimi ni mtu wa ukoo wa kelkuni..mme wangu pia... Kwahiyo sizani kama kwangu itakua halali kuulinda ufalme huu..alisema Rai.
Mfalme alishituka sana kusikia hivyo... Ina maana hata Fasha ni mtoto wa ukoo wa kelkuni??!!!!!...alijiuliza Mfalme.
Daah..Mfalme alihisi kuchanganyikiwa... Hasa baada ya kujua kua Fasha ni ukoo wa kelkuni.
Nimeisha...sina mtoto yeyote..hata Fasha nae wa kelkuni!!???...hata nikisema arithi mdogo wangu bakanga nae ndio nitakua nimemuuzia nchi suya na ndugu yake.. Alijiuliza mfalme..
Haya kwa leo unaweza kwenda... Alisema Mfalme.
Rai aliondoka kiroho safi..
Huku Mfalme alibaki njia panda.. Alitafakari wosia ambao baba yake mzazi alimwachia kabla mauti haijamkuta..
Aliambiwa kwamba ahakikishe ufalme unakua wenye nguvu na asitokee wa kuupora..wala usitudi mikononi mqa wazawa wa kelkuni.
Kiukweli Mfalme alishindwa aseme nini.
Rai alipotoka tu ndani alikutana na vijakazi hapo nje wakimsubiri..walimwongoza hadi alipokua Fasha.
Mama...kwa sasa si salama kwako kurudi nyumbani wala kukaa ikulu..kuna sehemu salama nitakupeleka..alisema Fasha.
Sawa mwanangu... Nitakaa huko..alisema Rai.
Baada ya kumpeleka mama yake sehemu Salama alirudi hadi kwenye makazi ya mkewe Mars kuangalia kama amesharudi.
Huku Dom alikua akiongea na Rania.
Rania... Aliita Dom.
Abee..
Fasha ni mdogo wangu... Alisema Dom.
Unamaana gani kusema hivyo?.. Aliuliza Fasha.
Namaanisha hivi... Mimi na Fasha tumezaliwa na mama na baba mmoja...alisema Dom.
Rania alishangaa sana... Alibakia mdomo wazi...
Na Fasha analijua hili?...aliuliza Rania
Dom ilibidi amweleze yote mwanzo mwisho kilichotokea hadi wakafahamiana..
Haaaa....alishangaa Rania.. Alikaa katika mshangao kwa muda mrefu sana maana taarifa hazikua rahisi kuzikubali..
Baada ya muda Dom aliondoka na kumwacha Rania anashangaa..
Akiwa kwenye mshangao mara alikuja Namadi..
Namadi... Kulikoni?. Aliuliza Rania baad ya kumwona Namadi kama hayuko kawaida.
Namadi alisema kilichotomleta..
Rania alizidi kuchanganyikiwa... Aliashitushwa sana na taarifa zile.
Fasha alipofika kwenye makazi ya mars hakukumkuta Mars..alijiuliza sana.
Inamaana Mars hata sasa hajarudi?..atakua ameenda wapi?.. Alijiuliza Fasha.
Mahali pale akiwa na mawazo ya kutosha.. Akiwa anatembea mara alikuja Rania.
Mwanamfalme.. Aliita Rania.
Kuna shida gani mbona unahema kiasi hiki?.. Aliuliza Fasha.
Mwanamfalme... Namadi amekuja hapa...anadai amemwona mkeo sehemu... alisema Rania.
Fasha alishtuka sana..aliongozana na Rania hadi alipokua Namadi.
Namadi umesema umwemwona Mars wapi?.. Aliuliza Fasha.
Nilikua katika safari zangu mimi,hanna na yule mtoto Lau katika ziara yeye ya kutembelea misitu mbalimbali
Tukiwa bado tumepumzika majira ya asubuhi sana Mara tulimwona Mars na vijana wawili walinzi wakiwa pamoja nae.
Sina hakika ila walikua wameshika njia iliyokua ilkielekea Lazi..Mars alikua amejifunika kichwa asijulikane lakini kwakua tunamfahamu vyema tulimfahamu...alisema Namadi.
Lazi?..ameenda kufanya nini?..aliuliza Fasha..
Haya Namadi.. Nashukuru kwa taarifa.. Alisema Fasha.
Mwanamfalme.. Nitaondoka mimi na Namadi kwenda Lazi... Hakika tutarudi na suluhisho..alisema Rania.
Wewe na Namadi tu??...hapana... Unatakiwa kuweka ulinzi..alisema Fasha.
Hapana... Hili jambo si la kila mmoja..na kumbuka kua si kila mmoja anatakiwa kujua mimi ni nani na nilitoka wapi.. Alisema Rania.
Mmmh...sawa... Alisema Fasha.
Niagie kwa Dom.. Sitaki kukutana nae mwenyewe maana hatakubali m twende mimi na Namadi tu..alisema Rania.
Sawa... Nawatakieni safari njema... Alisema Fasha.
Mfalme bado alikua na mawazo sana..hakujua lipi liko sawa.
Baada ya mawazo ya muda mrefu alikata shauri..ingaqa hakutaka iwe hivyo ila hakua na jinsi
Kesho yake alimwomba Fasha amlete tena Rai waongee..Fasha alifanya kama Mfalme alivyotaka.
Mfalme.. Niko hapa..alisema Rai baada ya kufika.
Rai, naomba nikuulize maswali Machache.
Uliza mtukufu Mfalme.. Alisema Rai.
Hivi ni kweli kuna NADISH?.. Aliuliza mfalme.
Ni kweli Mfalme... Alisema Rai.
Yuko wapi kwa sasa?..aliulza Mfalme.
Ni wa kike au wa kiume?.. Aliuliza Mfalme.
Ni wa kike.. Alisema Mfalme.
Kwanini awe wa kike?....aliulza mfalme.
Kuna sababu kadhaa za kwanini awe wa kike..
Moja: aliletwa wa kike ili kuwapumbaza maadui..maadui wanaomshambulia hawawezi kuweka juhudi kubwa kumtafuta maana inasadikika wanawake ni watu ambao hawawezi mambo makubwa kamwe...alisema Rai.
Pili ndio mtu pekee alieonekana na hiyo nyota katika nchi nzima ya Lazi.. Alisema Rai.
Basi inatosha...mimi nitakubali kuuacha ufalme uende kwa wazawa wa kelkuni..najua nafanya makosa kwakua nilikula kiapo cha kutouachia ufalme huu kwa wazawa wa kelkuni.
Nafanya hivi kwa sababu sina mrithi mwingine tofauti na Fasha ambae pia ni wa kelkuni... Hata nikisema nimrithishe mdogo wangu ndo basi kabisa... Alisema mfalme kwa unyonge.
Sawa nimekuelewa Mfalme..haina jinsi maana kwa namna yoyote ile ufalme ulishatabiriwa kurudi kwa kelkuni... Haina haja ya kumwaga damu.. Alisema Rai.
Yuko wapi huyo mtoto?.. Aliuliza Mfalme.
Yuko hapahapa ikulu... Alisema Rai.
Mfalme alishtuka sana.. Hapa ikulu?!!!?....aliulza mfalme kww mshangao.
Ndio hapa ikulu... Alisema Rai.
Mfalme alibaki macho kodo.
Wakati huo Rania na Namadi walikua wako safarini wakielelea Lazi.
Mars alikua ameshafika Lazi na alikua ameshafika ikulu.
Walinzi wa ikulu walimpisha bila ubishi akaingia.
Mfalme alipopata taarifa za ujio wake alishangaa sana..
Mars?..amekuja hapa kwanini?..alijiuliza Mfalme.
Aliwahi na kwenda kukutana na Mars.
Walikaa na kuanza kuongea.
Mwanangu.. Mbona uko hapa bila taarifa?.. Bila walinzi?..aliuliza Mfalme.
Baba mwanao yamenikuta makubwa...nimenusurika kifo baba..Tharia ni watu wabaya sana..alisema Mars.
Wamekutenda nini?..aliuliza Mfalme kwa hamaki....NINI KINAFUATA?
MARS ATASEMA NINI?..
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni