MTAA WA TATU (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
“Shika adabu yako mwenyewe kwanza ukumbuki wakati tunafika
pale
Hafidhi alitamka nini kumwambia yule bibi"
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Wakati wanaongea washafika nyumbani
kila mmoja akaingia ndani
kufika ukumbini
Hafidhi akaja kukumbatiwa na
Salma
“whaoo kaka yangu wanguvu huyoo"....
Leo tunaugeni my dear brother njoo uwone"
basi Hafidhi akajongea mpaka sebuleni
na kukutana na mabinti warembo sijui mamiss maana ni warembo balaa
Mwanaume moyo ukaanza kupwita
ameshatamani dodo.
"Assalam alaykum?
Hafidhi akaanza kusalimia hivyo huku akikaa kwenye sofa vizuri,
“waaleykum ssalam vipi umzima wewe"....
Mmoja tu ndio kaitikia na kuuliza hivyo.
Wakati mwingine alijifanya yuko
busy kuchart.
“wee Husna mbona uwitikii salamu kutoka kwa kaka?"
“ahaa poa niambie kaka binamu mambo vipi?
Baada kushtuliwa na Salma yule binti akajibalaguza na kuitikia, pamoja na kusalimia pia ni kweli alikuwa busy
akichart sijui whatsapp, au facebook,
Instagram,
Hafidhi akatabasamu na kusema
“hakika mi mzima sijui wewe Dada yangu mpendwa hofu kwako tu".....
Salma akaanza utamburisho kwa kusema
“kaka Hafidhi huyu ndio
Husna na yule mwenye miwani kama doctor wa kutoa mimba ndio Sada"...
Binti mwenye miwani kama ya macho au ya kisister duu iliyomkaa vyema,
akawa amenuna vibaya mno baada kuambiwa vile huku wenzake wakimcheka
“Salma ushaanza kunichokoza
ningejuwa ningeenda kukaa kwa bibi temeke.
Mpaka likizo iishe, ny**ko zako"....
Hafidhi akacheka tu, na kusema
“basi usikasirike mama watoto
na wewe mwite Salma mitako au sio".....
“mmh huko ni kumpaisha tu yani nimwite mitako, kwa kipi hasa embu cheki zigo langu hili"
Sada akainuka na kumpa mgongo kaka binamu huku akilitikisa bodi lake hakika kitu kilikuwa kitu kweli Salma mwenyewe akasome.
Mwanaume mate ya uchu yakamtoka maana dahaa, mbona binamu zake ni mtihani,
hatimae siku ikapita kesho yake
Asubuhi Hafidhi akatoka kwenda beach na kupitia uwanja wa mpira
ajabu siku hiyo uwanjani kulikuwa na sura ngeni machoni mwake.
Hajawai kuziona hata siku moja,
Hakutia shaka akaendelea na mazoezi tu wakati anapiga pushpu kuna sauti ikamshtua kwa kumwambia
“Hafiiiiiiiidhi"......kimbiaa!!!
Mwanaume kabla ajageuka kutizama sauti inapotokea kitu kizito kikatua kichwani kwake.
Kwanza akaanza kuona nyota nyota kizunguzungu Giza zito likatanda na kupoteza fahamu.
watu wale wakaanza kushangilia na kusema
wao ndio Gwanta kutoka
karibu na Lugalo basi wakambeba na kuondoka nae, safari yao ikawapeleka mpaka mtaa wa tatu.
Na kumkabidhi hapo,
“kweli nyie noma huyu kenge juzi tu kanivunja mkono kamuuwa Jimmy kule uwanjani kapiga sana watu
wengi wapo mahospitalini
kisa huyu malaya"....
Aliongea hivyo kaka yake Sharifa na kumpiga teke la tumbo,
“sikia nikwambie kitu Tizo kazi ya kukamata kenge wadogo kama hawa ni kitu kidogo sana kwetu.
Siku zote mnajiita sijui black sneak yani nyoka mweusi kumbe nyoka wa kibisa.
Mmeshindwa kumdhibiti huyu mjusi tu"...
Gwanta namo wakapewa pesa yao na kusepa huku
Hafidhi akipelekwa kufungiwa kwenye chumba kidogo hivi.
“kaka Tizo kwanini tusimuuwe kabisa kabla haja zinduka,
maana akirudiwa na fahamu zake itakuwa shida hapa"
“hawezi kufanya hivyo tunataka kumuuwa kidogo kidogo tena kwa maumivu makali subiri kina
Matiath warudi kutoka hospitalini"....
Kijana ambaye alipaza sauti kumwambia
Hafidhi akimbie baada kuona lile
tukio akatoka mbiombio mpaka nyumbani kwa kina
Hafidhi akiwa anahema kwa bahati nzuri
akakutana na
Ankor wake nae ndio anaingia ndani baada kurudi kutoka kazini.
huku akihema akaamkia
“shikamoo mzee"....
“marhabaa kijana vipi mbona unahema hivyo?"
Kijana hakutaka kujibu lile swali zaidi ya kusema
“Hafidhi kapigwa na kuchukuliwa amepelekwa kulee"...
“what?...unasemaje kijana, kapelekwa wapi embu twende, ndani ya nyumba
Akatoka kila mtu taarifa za kutekwa kwa Hafidhi zikasambaa kama umeme
Mtaa wa tatu kila mtu akatoka
Na siraha huku wakiimba
“tumechokaaa kuonewaaa awile munduu awile nakooo".....
twendeniii vitani tumechokaaa kuonewa awile mundu awile nakoo".....
Kamanda wa kikosi ni
Chollo akasimama mbele na kusema.
“siku zote usiogope kifo kwani kifo tumeumbiwa kwetu wanaadamu kifo ni lazima.
Ogofa kufa ukiwa na madhambi, maana huko kaburini kuna marungu kuna
Nyoka mwenye vichwa saba wadudu wenye sumu kali.
Sasa kila mmoja atubu madhambi yake, maana huku tunapokwenda ni kufa na kupona hao Gwanta tutawasaka popote tuanze msako mtaa wa pili.
Kisha twende mtaa wa tatu, kila mmoja aanze kusali kwa imani yake"....
Basi sala ikaanza yani hadi kina
Salma wapo humo hiyo vita haina cha mwanamke wala cha mzee wote ndani
“Ibnuwasi nakutuma nenda kamuokoe
Mwanao katika mikono ya watu wabaya please nakuomba usiuwe
Binaadamu yeyote yule
fanya kumtoa kijana wako kisha uje nae hapa. Tumpe kinga na nguvu za kupambana.
Mwanao hajitambui yeye ni
nani ndio maana anaishi kikawaida tu"
Alikuwa yule bibi akiongea na kiumbe cha kutisha yani ana jicho moja tu,
ndimi yake inawaka moto, hiyo minjino sasa kama Leki
Akawa kwa sauti nzito yenye kutetemesha hadi
Ardhi upepo ukavuma akaitikia kwa kusema
“sawa mkuu kiti wacha niende kunyonya damu zaoo".....
“hapana Ibnuwasi usinyonye damu kabisa nenda kamtoe mwanao unaona jinsi alivyolala pale"
Bibi akaonyesha ukutani kulikuwa na flat screen ya asiri.
Ibnuwasi akapotea.
Wakati mtaa wa tatu wakipanga kuvamia mtaa kwa mtaa wakati huohuo bibi katuma Jinni, kwa ajili ya kwenda kufanya kazi moja tu,
Ndani ya msitu mzito kulikuwa na kijana akikimbizwa na kikundi cha Maninja huku akikoswa koswa na mishare.
kijana alikimbia kwa speed zake zote kuwakwepa wale
Maninja siku zote unaambiwa kimbia wee
Utakuja kufika mwisho tu na kijana mwenyewe alikuwa ni
Hafidhi sijui kule mtaa wa kwanza katokaje.
Na huku msituni kafikaje.
Baada kuona sehemu aliyokuwa akikimbilia hakuna njia tena yani kuna mto mkuubwa
wenye mamba.
Basi akasimama na kugeuka nyuma maninja
nao hao ikawa sasa ni kuwekwa mtu kati.
Mwanaume akajipanga kujibu mapigo
maana ukizubaa utakufa kizembe.
Maninja wakachomoa majambia yao na kuitaji kumchana
chana ninja mmoja akaja kwa kasi kupiga
jambia
Hafidhi akadank na kurudi nyuma kidogo akaachia teke la nyuma inaitwa nenda huko
likatua moja kwa moja mgongoni mwa yule ninja
Akapepesuka na kudondokea mtoni
hapo sasa wakaja wote huku jambia zikilia kwa kugongana
ngwengwe".....tehaatahaa.... Hafidhi akazidi kuwapa kichapo kwa kupiga zile
fighting fish yani mapigo.ya samaki
mbona ilikuwa balaa
dakika si nyingi maninja wengine wakakimbia huku kawateketeza
Baadhi,
Pahaa pahaa sauti ya makofi ikasikika mbele yake kutizama ni Walimu wake
kama watano hivi wakimpigia makofi hapo yupo
William James mmoja kati ya walimu wa style za Taikondo kutoka nchini
Jamaica kuna Fung chu
mkari wa mapigo ya Wushu kutoka nchini china
kuna Tommy John kutoka nchini Thailand mkali wa merantau
bila kuwasahau bwana Dorms Son kutoka nchini
Urusi ni mkari wa mbinu za kivita
Jackson Wear kutoka
German nae ni mkali wa kivita wote ni walimu wake kumbuka tokea akiwa
na umri wa miaka 6 tu
akaanza kujifunza mbinu za mapambano
Kwahiyo kapitia kila nyanja ya mapambano.
Akiwa anashangaa kuwaona
walimu wake wapo pamoja
tena wote kwa pamoja wakamwambia
“kijana acha kulala hamka upambane
simama kijana
simamaa".......sauti ikawa kubwa akaja kushtuka amelala chini
Kumbe yote ilikuwa ni ndoto tu kitendo cha kushtuka akajikuta kalala chini kwenye chumba kimoja wapo kidogo hivi
kwa mbele kuna geti .
Kama vile yupo jera,
Mwanaume akasimama na kusogea mpaka kwenye nondo akapaza sauti kuita
“nifungulienii"......
Sauti yake ikamshitua kila mtu maana haikuwa ya kawaida vijana wa kiume kwa wanawake wakaja kumtizama na kumuona
Mwanaume kasimama
imara, nae baada kuona
watu wamemsimamia mbele yake akasema
“nifungulieni haraka sana nitoke vinginevyo nitauwa kila mtu"......
Kila mtu akacheka kwa dharau, ni kitu kisichowezekana
Kwa yeye kufanya vile,
“tulia bwana mdogo tulia, umeneng'eneka wee mwishoe umenasa nakuapia
Wallahi leo utoki jino moja, tena imekuwa vizuri umerudiwa na fahamu zako
tunataka tukutese
kisha tukule nyama huku unajiona"
Kaka yake
Sharifa akaongea hivyo kwa dharau ghafla bin vuu
Hafidhi akaanza kutikisa nondo si akang'oa geti.
Ni kitu kisichowezekana kwa binaadamu wa kawaida labda kina
John cena au Mark Henri wacheza mieleka
kidogo wanaweza.
Mwanaume akatoka sasa ikawa balaa si mchezo kila aliyejifanya kumvamia
alidakwa na kupigwa ngumi
za haraka haraka
na kutupwa kule, kuna mama mmoja mtu mzima hivi
akaja na chepe huku akipiga kelele
“nipisheni nauwaaa
ile anapiga tu kitu kikadakwa na kiumbe cha ajabu yeye peke yake ndio kamuona,
kiumbe kinawaka moto
yule mama presha sijui ilipanda au
ilishuka akadondoka chini
na kuwa kimya.
Hafidhi alikuwa yuko moto maana alimshika kaka yake
Sharifa na kumvunja mkono tena uleule
uliokuwa umefungwa Pop
kisha akambamiza kwenye ukuta
damu tu zikaruka
“Hafidhi hakutaka ujinga na mtu
“hallooo Gwanta tumezidiwa huku
msaada please tunakufaa"....
Kijana mmoja aliwapigia simu kikosi cha
Gwanta kuomba msaada.
Ibnuwasi akaingia mwilini mwa mwanae kimbembe hapo sasa
yani ikawa ukipigwa ngumi teke au kofi kichwa kama ujazima
utaona kama vile umeibeba dunia
Sharifa nae akajishauwa kuja na kisu kumtetea kaka yake.
Si unafahamu damu nzito kuliko maji
Sijui alijuwa ataonewa huruma kumbe wapi kitendo cha kusogea tu akadakwa,
yani ilikuwa kama jamaa ana macho mengi yani popote ukitokea kwa kunyata
anakuona.
Sharifa akadakwa na kupigwa kibao kimoja tu binti akayumba akataka kudondokea sijui jiwe.
Kwani kama angedondokea hapo
lazima apasuke Hafidhi akawai kumdaka
kuna muda kwenye akili yake akajiuliza mbona anapiga hadi
Watoto wakike akili nyingine ikamwambia
pambana kwenye vita hakuna cha mtoto wa
Mwanamke"......
Gwanta wakafika hawakuweza kuamini aisee
Jamaa kapige takribani watu ishillini na tano wapo chini
Vidume vikajipanga
Hafidhi akashtukia anapigwa teknik za ajabu akayumba na kwenda chini,
kumbe
Ibnuwasi kashatoka mwilini mwake na kuondoka si kaona kazi imeisha kumbe bado
Mwanaume akajipanga kwa kutumia
Style ya Merantau
fighting bounce yani vunja mifupa ni moja kati ya Style hatari sana
Akikamata hata shingo anavunja tu.
Gwanta nae sijui wamefundishwa wapi
Mastyle yao wenyewe wanaita
Black Eager yani mmoja anakuja kwa kasi
na kuinama huku mwingine akipanda juu
kwa kuruka ni
Style ya kipekee kabisa Hafidhi ilimpa wakati mgumu kuwasoma na kuishia
kuchapwa kama mtoto,
Gwanta ni kukundi cha vijana kama mia moja hamsini hapo wamekuja watano tu
Shida tupu baada kuona style ya
Merantau haifui dafu akachenji na kutumia
Style ya
Fighting fishi and bounce.
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni