MTAA WA TATU (40)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI
Kwa upande wa bibiye Vivian aliweza kutambuwa kipenzi chake kachukia kuhusu
lile swala akajaribu kumpigia simu ikajibiwa haipatikani akaona sio mbaya akiacha ujumbe wa kuomba
msamaha. Aliandika hivi “nafahamu ni kwakiasi gani umechukia kipenzi changu tafadhali baby nisamehe
niliingiwa na hofu kuhusu mwanetu wala sio mimi kama kweli umenisamehe ujibu ujumbe huu’’
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Ilikuwa siku ya Desember 1 siku hiyo kulikuwa na maadhimisho ya miaka 53 tokea Tanzania ipate uhuru wake
kutoka kwa wakoroni. Watu wengi sana kutoka mikoani na nnje ya nchi waliweza kufika ndani ya uwanja
wa taifa. Waweze kushuhudia maadhimisho hayo, muheshimiwa Raisi aliweza kufika akiwa kaongozana
na mkewe kipenzi , basi sherehe ikaanza kwa kupigwa ngoma za asiri kisha ngonjera wakaja wasanii wa
bongo fleva.
show ilikuwa babu kubwa kila mmoja akaenjoi vya kutosha kwenye jukwaa la wananchi tunamuona Hafidhi akishuka zile ngazi kwa kasi kisha akachumpa kulifata jukwaa ambalo Raisi alikuwa amekaa na mkewe,
Mzee J Ikram nae alikuwepo maeneo hayo kitendo cha kumuona mwanae akipiga hatua za haraka
kuelekea sehemu ambayo muheshimiwa Raisi amekaa na mkewe, kilimshtuwa sana, akakumbuka kauli ya mwanae kutaka
kumuuwa mke wa muheshimiwa akapaza sauti “walinzi!!! mlindeni mke wa muheshimiwa
sauti ilikuwa kali si yupo karibu na Mic basi vikosi vikajipanga kutaka kumzuia Hafidhi mwenzao akapiga
bomu la machozi na kupotea wakabaki kung’aa sharubu tu, na kujiuliza yuko wapi mwanaume
akatokezea kama nyau akiwa ameshachenji mavazi akaruka juu na kwenda kutuwa kwenye jukwaa
ambalo waheshimiwa wapo haikuchukuwa dakika nyingi kwake kuwafinya walinzi na kutupwa huku na
kule kisha akamuwekea jambiaa shingoni mke wa muheshimiwa bibiye Anna akabaki kutetemeka tu. Chezea kuchinjwa wewe utajamba,
“rudini nyuma yeyote atakaye thubutu kunisogelea basi kichwa cha huyu malaya ni halali yangu
kila mmoja akarudi nyuma kwa uwoga.
“skia nikwambie kitu wee nyau pusi naitaji uutangazie huu umati wote wewe ni nani kisha nitakuacha
mzima vinginevyo natowa kichwa chako’’ bibiye Anna huku akitetemeka ikabidi atii amri kwa kusema
“Ndugu Wananchi mimi sio mtu mzuri mimi ni muuwaji mtesaji muuza viungo vya watoto yatima kwa
matajili hata nnje ya nchi mimi ndio kabla hajaongea zaidi risasi ikatuwa kwenye paji la uso wake wake.
Hakika
alikuwa ni Snipe wa hatari sana kila mmoja akashtuka huku Hafidhi nae akipotea kwani ukatokea mkanyagano si kidogo
Vilema masikini ya Mungu wee mbona walijuta kwenda huko.
Kila mmoja alitaka kuiokowa nafsi yake baada kuona mke wa Raisi kapigwa risasi ya uso na kudondoka chini akiwa
chali,
Hafidhi kumbe hakuweza kwenda mbali na eneo hilo kwenye akili yake alikuwa akimtafuta huyo Shooter amejificha wapi yani akamsaka kila kona hakuweza kumuona wakati huo
Vikosi vinazidi kuongezeka sijui
Jwtz FBI yani kila kitengo vikafika muuwaji atafutwe popote alipo,
Hafidhi hakufanya mauwaji lakini nae atafutwe tu,
Nnje ya uwanja wa taifa kulikuwa hakupitika kabisa barabara zote zikafungwa huku
Raisi akipakizwa kwenye ndege ndogo na kuondoka zake,
“Copro William"
“naam mzee"
“naitaji yule kijana apatikane haraka sana, inaonekana ni jinsi gani anafahamu mambo mengi kuhusu watu kufanya mambo ya kishetani katika nchi him".....
Muheshimiwa Raisi aliongea hivyo huku akijifuta jasho.
Yani huku taifa kulikuwa na kivumbi jasho wenye kuweza kukimbia walikimbia wasioweza ndio hivyo tena wakaishia kukanyagwa tu,
Wakati huohuo 3Sisters wanaingia kwa mbwembwe zote kila mmoja akiwa na pikipiki yake,
Yani muuwaji alitafutwa kila kona magari yalikaguliwa polisi hawakuweza kuona mtu
“itakuwa muuwaji kajichanganya na huu umati wawatu kisha akatoroka
maana kila kona, kila nyanja hakuna kitu"
“itakuwa hivyo maana haiwezekani kumtafuta kote huku tusiweze kumuona"...
Basi wakatoka nnje ya jengo huku wakitowa tangazo kila mtu akamatwe na kuchunguzwa
3Sisters baada kufika eneo la tukio cha kwanza kukifanya ni
Kuichunguza maiti ya bi Anna
wakapima ile risasi ilipotokea na kuweza kupata kitu kuwa muuwaji alikuwa amekaa wapi Yusra akatoka mbio kumuwai ni akili tu
za kukisia hisia zikaja
Nnje kidogo ya uwanja huo kuna kijana mmoja mwenye asiri ya kutoka sijui America au wapi alionekana akitembea kwa kujiamini sana huku akiwa kabeba begi
jeusi akashtukia sauti yakike ikimwambia
“wee simama hapohapo"
Kijana akasimama na kugeuka.
“je unaweza kuniambia ndani ya begi lako kuna nini ndani yake?"
Kabla ya kujibiwa angalia jamaa mchezo alioucheza utaipenda hii yani akafanya kumrushia lile begi Yusra ile anajianda kulidaka tu akapokea mateke ya double kick na kutupwa kule,
Jamaa akajizungusha na kulivaa begi lake juu kwa juu
Hakika anatisha vibaya mno".......
Bibiye Yusra akaona wee usintanie kumbe unataka kuuwasha moto, wacha ukuwakie
Akamfata kwa kasi na kuanza kurusha makonde ya maana, wakati jamaa alikuwa akizitowa na kupanchi kwa dharau kama haitoshi akampa mgongo kabisa,
Basi bibiye kila akipiga zinatolewa na kupigwa yeye hakika
Agent alikutana na chuma cha puwa,
bibiye alipigwa teknick za chembe
Ghafla akakamata kichwa cha bibiye na na kumvunja shingo, yani kilikuwa kitendo cha faster
Bibiye kuanguka chini utasema mzigo wa kuni kisha jamaa akasema
“wasalimie kuzimu kitu chamoto kikapita karibu ya sikio lake ilikuwa risasi akatizama mbele kuna mabinti wawili wanakuja kwa kasi, akaona isiwe shida akaruka juu kwa kuchumpa na kupotea eneo hilo
“Yusra!!!
Vivian baada kufika hapo akafunga break huku akimuacha mariam akiendelea mbele zaidi
Akaita kwa sauti ya chini sana huku akiinama na kuushika mwili wa bibiye Yusra kwa wakati huo alikuwa tayari kaenda mbele ya haki.
“Yusra mpendwa wangu please inuka basi tuendelee na mapambano Yusra mdogo wangu huwezi kulala hapa
inuka!!! fumbuwa macho
Yusra utatuachaje katika kipindi hiki"...
Binafsi Vivian alilia si kidogo hata
Mariam aliporudi hakuweza kuamini nae akapiga goti chini wote walilia kwa pamoja hakika lilikuwa bonge la pigo kwa upande wao kumpoteza Commando mwenzao katika hatuwa za mwanzoni kabisa, polisi wakafika
mwili ukachukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili,
“Yasri kaka".....
“naam niambie ndugu yangu"...
“embu toka ndani njoo uwone matukio yaliyotokea uwanja wa taifa leo hii!"
Jackson alikuwa akimwambia Hafidhi aje kuangalia taarifa ya habari.
Nae akatoka chumbani kwake na kwenda kuangalia hiyo taarifa ijapokuwa anafahamu tukio zima jinsi lilivyo,
Akakodolea macho television ndogo yani nchi sijui kumi na nane,
Akapata mshtuko baada taarifa ya kifo cha bibiye Yusra kutangazwa hakika
akashindwa kuendelea kutizama akarudi chumbani kwake mchozi ukimtoka
“yani Yusra kauliwa
Hakutaka kupoteza muda akavaa nguo zake na kwenda kumuomba funguo ya pikipiki
Jackson,
“sema nini kaka chombo wese hamna kabisa kama vipi ukifika nayo pale Zakhiem nenda kaweke,
“usijali nipatie funguo"
Hafidhi hakuwa na raha tena kwenye akili yake aliwaza vitu tofauti kutokana na kifo cha Yusra baada kufika
Zakhiem na kujaza mafuta full tank akaendelea na safari mpaka ndani ya Hospitali ya Muhimbili hakupata shida kuulizia kwani ile anafika tu
akamuona Vivian akija mbio huku akilia na kumkumbatia,
sasa ilikuwa kazi ya kumbembeleza kipenzi chake,
Mariam nae alikuwa akibembelezwa na ndugu zake, binafsi ulikuwa msiba mzito wacha ule wamke wa Raisi
Hatimae siku ikafika Yusra Salimu wazazi wake na ndugu zake wakiwa wanaishi Ilala mtaa wa Lindi ndipo msiba ulipo fanyika hatimae akazikwa, huku baba yake
Marehemu akiwaomba kina Vivian kufanya kitu kizuri kwa ajili ya kulipa kisasi cha ndugu yao,
Hafidhi akiwa pembeni alikuwa makini kusikiliza maneno ya mzee
“Assalam alaykum kwa ndugu zangu Waislam
Na bwana Yesu asifiwe kwa wale wasiokuwa Waislam, kwanza kabisa nimesimama hapa kwa niaba ya mwanangu mpendwa binti yangu, ambaye leo hii hatuko nae,
Yusra ametutoka akiwa na umri mdogo sana ndio kwanza miaka ishillin na moja
Yusra siku zote ndoto yake ilikuwa aje kuwa
Commando mwenye kutumainiwa mwenye kutetea hali za wanyonge
Ndoto yake hii ikaweza kutimia baada kujiunga na chuo cha U.S.I kitengo ambacho kinajitegemea chenyewe hakifungamani na upande wowote si serikali wala nini
Leo hii akaweza kuchukuliwa na serikali mara ya mwisho alikuja nyumbani akiwa na furaha huku akisema kapata mchumba
siku si nyingi atamleta nimuone
Ndoto imekatika ghafla kama mshumaa
3Sisters haipo tena
Naomba kama huyo kijana ambaye ndio alitaka kutamburishwa na mwanangu
yupo hapa msibani basi asisite kujitokeza
niweze kumtambuwa mkwe wangu,
Yani mzee aliongea huku akilia,
Ajabu akajitokeza
Hafidhi na kwenda kumshika baba yake Yusra na kumwambia
“usijali mzee mkweo nipo hapa"
Vivian na Mariam wakabaki kushangaa inamaana hadi Yusra alikuwa mpenzi
wake.
Mmh! mbona balaa"....
Mariam akajiwazia hivyo,
“ohoo karibu sana kijana embu tuingie ndani, basi mtu na mkwewe wakaingia ndani sa sijui kweli au Hafidhi kazuga tu
maana hatukuwai kumuona
Akiwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu,
ilichukuwa kama nusu saa hivi
Mwanaume akatoka ndani ya nyumba hiyo akamsogelea Vivian na kumnong'oneza kitu akaenda kwa Mariam akafanya hivyo hivyo kisha akaondoka
safari yake ikampeleka hadi sehemu moja hivi kulikuwa na vijana wakicheza mpira wa basketball
Akapaki pikipiki yake na kupiga hatua kuingia ndani ya uwanja huo
akaingiza mkono wake kiunoni na kuchomoa kisu kidogo hivi, ilikuwa pande za
Don bosco mitaa ya Upanga
vijana nao walikuwa hawana hili wala lile wakiwa bize kucheza mpira ukarushwa juu
Mwanaume akaruka na kuudaka yeye kisha akautoboa kwa kisu
kitu puhuu ndio sauti iliyosikika baada mpira kupasuliwa,
Vijana wote wakabaki kutizamana pasipo kufahamu nini chanzo mpaka mshkaji kaupasusuwa mpira wao,
“wee kudadeki zako mtoto wa malaya umetumwa au? Ndio nini kutupasulia mpira wetu"...
mmoja kati ya vijana aliongea hivyo huku akimsogelea Hafidhi sema akasita na kusimama ghafla baada kuona mshkaji kashika kisu,
“Patrick vipi mbona unamchelewesha huyo pimbi?"
“njoo wewe jamaa kashika kisu sijui Zombie huyu au Vampire, mbona kasimama tu haongei kitu
Ghafla mwanaume anakuja,
Patrick akaanza kurudi nyuma kwa hofu sema alishachelewa
na kujikuta kisu kile kikituwa kifuani kwake, vijana wengine walianza kukimbizana huku na kule kwa kuruka senyenge
Maana sehemu ya mlango kulionekana hakutoshi
kumbe mwenzao shida yake ilikuwa ni Patrick si mtu mwingine baada kumkita kile kisu sehemu ya moyo
Patrick akabaki kupapatika tu huku damu nyingi zikimtoka,
Hafidhi akaushika mpini wakisu kile na kukichomoa akakifuta damu kupitia nguo za
Patrick kwa wakati huo roho yake
Ishaenda kwa Mungu baba baada kufanya mauwaji mwanaume bila kuwa na wasiwasi wowote akasogelea sehemu ya
Mabegi yalikuwa kama mabegi sita hivi
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni