MTAA WA TATU (54)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
Hafidhi baada kuwapiga chenga za mwili polisi na kikosi ca ma FBI safari hii tunamuona akiwa maeneo ya Mbagala sehemu ambayo alipanga chumba sema tokea rafiki yake wa karibu ambaye ni Jackson afariki dunia nae kuonekana kwenye mitaa hiyo imekuwa kwa nadra sana.NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
“Wee kaka mambo?’’ ilikuwa salamu kutoka kwa binti mmoja hivi akimsalimia Hafidhi
“Poa niambie dada yangu umzima weye?’’ Hafidhi akaitikia salamu sijui kwa kiswahili cha wapi na kuuliza swali. “mi mzima hofu kwako tu’’ binti nae akajibu, baada salamu kila mmoja akabaki kumtizama mwenzie kwa jicho la kiwiziwizi kabla ya simu ya Hafidhi kusikika ikiita ndani kwakuwa alikuwa akiosha vyombo akamuomba yule binti kwa kumwambia “Sister samahani kama hutojali je unaweza kwenda kuniletea simu yangu ipo mezani hapo’’ pasipo binti yule kuitikia akainuka na kuingia ndani kisha akatoka na kumkabidhi simu,
“Thank you my sister Hafidhi akashukuru kwa lugha ya kigeni binti akatabasamu tu “Halloo nani mwenzangu?’’ Hafidhi baada kupokea simu akauliza swali kwani number ilikuwa ngeni, sauti ikasikika ikicheka kwa dharau tena ilikuwa sauti ya kikebaada kucheka akakata simu pasipo kuongea chochote kile “halloo,,,halloo,,ohoo shit! Hivi duniani kuna watu wengine machizi ehee?’’ akasikika Hafidhi akiuliza hivyo, yule binti akamtazama na kuuliza “kwanini unasema hivyo?’’ “si huyu mtu kanipigia simu baada kuongea kaishia kucheka na kukata simu kama sio uchizi kitu gani’’,,,,”Mmh! Yani kacheka tu kakata simu kwani wakike au wakiume?’’ “Ni mwanamke kibaya zaidi nampigia hapa hapatikani sijui ndio nini’’
“Si ulimsevu jina lake?’’ “Hapana number yake ni ngeni’’ “basi usitake kuumiza kichwa sana chakufanya embu jaribu kucheki jina lake yani ufanye kama unamtumia pesa hivi iwe Tigo pesa au M-pesa utaliona jina lake’’ binti akatoa ushauri huo basi Hafidhi nae akafanya hivyo ghafla akashtuka na kuitupa simu chini sijui kaona nini “Vipi mbona umeshtuka kuna tatizo au, binti akauliza huku akiyokota simu na kuitazama “mmh! Kumbe mtu mwenyewe anaitwa Yusra Yasri yani double (Y) hakika lilikuwa jina la marehemu Hafidhi akabaki kujiuliza ni nani kasajili line kwa kutumia kitambulisho cha Yusra, hakutaka kujiuliza sana akaingia chumbani kwake sekunde si nyingi akatoka na kumwambia yule binti “nisuuzie vyombo vyangu mi natoka kidogo kisha akaondoka kwa mwendo wa haraka bila shaka kuna kengere ya hatari imeweza kugonga kichwani kwake isijekuwa kama yale mambo ya Chanduka Nusraty aliporudi kutoka kuzimu. Kumuachia chumba binti yule ilikuwa kama kumuachia marehemu Amina basi binti akaosha vyombo na kuingia zake chumbani mtoto wakike alikuwa akihishi nyumba ya jilani tu akavua dera lake na chupi kisha akajifunga upande wa kanga aliokuwa nao kisha akatoka kwenda kuoga waliomuona wakabaki kumshangaa tu.
“Huyu Saida kwa kujishauwa utasema mganga kaona jogoo yani kuambiwa asuuze vile vyombo ndio kaona ajiachie kabisa’’ mmoja kati ya wapangaji wa nyumba hiyo alimwambia mwenzake, “wee muache tu usikute jamaa kapigiwa simu na demu wake kuwa yupo stendi ndio kaenda kumfata hivyo mbona huyu mwehu atakoma, kila mmoja akaangua kicheko cha kishambenga, sauti zao ziliweza kumfikia vyema Saida ambaye alikuwa bafuni akijimwagia maji nae hakujali kama yuko chooni akaangua kicheko cha nguvu kwa kugonga gonga bati la choo “hahahaha,,,halloo,,,halloo ,,,,pyeee,,,nimepewa lift wacha nipige na honi kama limewauma kanyeni matikiti’’,,,, kauli ya Saida ikawafanya wale wamama wawe kimya siku zote Saida ni binti ambaye anajiamini sana kutokana na kaka zake wawili ni wacheza karate kwenye dojo la Mbagala kuu wakati kaka yake mwengine ni Mwanajeshi yani ikitokea siku ukampiga au kumchokoza mtu mmoja kutoka familia hiyo utajuta kuzaliwa yani kuanzia babu, bibi, baba, mama yani hadi virembwe wote watakuja mtapigwa nyumba nzima kwakifupi ni binti ambaye wanaume wengi wamemshindwa tabia, wakati Saida akiwa bado yupo chooni ghafla sauti ya kishindo ikaweza kusikika puhuu, zikifatiwa na kelele za mwiziii,,, jamani mwiziii sijui huyo mwizi kaingia muda gani chumbani kwa mzee wa nyapu yani wale wamama walishtukia mtu akitoka ndani mule kwa kuwaruka na kukimbia mbio mgongoni akiwa kabeba begi ndipo wakapaza sauti kwa kumuitia mwizi, bibiye Saida akatoka chooni mbio mbio akiwa na mapovu kichwani.
Sema akakuta watu washaingia vichochoroni kumkimbiza mwizi nae hakutaka kujiuliza akaingia ndani na kukuta mlango wa chumba alichoachiwa upo wazi binafsi hakuweza kufahamu mapema kama mwizi ndio kaingia ndani ya chumba hicho je kaiba kitu gani, akajipangusa mapovu na kuvaa nguo zake na kutoka kufika nnje akakutana na kikundi cha watu wakiwa wanarudi akauliza,
“Vipi jamani huyo mwizi kapatikana au?’’ hakuna aliye mjibu zaidi ya mwenye kubeba jiwe kutupa chini mwenye panga au sururu kuingia nalo chumbani kwake, “Yani Yule kijana anakimbia utasema kiberenge maana tumefika pale kwa mama Shego akaruka ule ukuta mrefu vijana kwa wazee tumeshindwa kuruka pale kwa dharau akatuonyeshea kidole cha kati na kupotelea upande wa pili’’ alisikika binti mmoja akisimulia hivyo mpaka hapo Saida akatambuwa kumbe mwizi kakosekana swali la kujiuliza kichwani kwake kaiba nini’’,,,,
“unataka kusema karuka ule ukuta wa pale!’’ “ndio maana yake sisi wakati tunamkimbiza tulipoona akikimbilia kule tukajuwa tunaweza kumshika tu kwasababu kule hakuna njia kumbe mwenzetu ndio anaenda kutuacha’’ “kwani kaiba nini?’’ Saida akauliza swali, “Hata sijui kaiba kitu gani sema mgongoni alikuwa kabeba begi bila shaka ndio mzigo aliouwiba,
Saida akavuta pumzi kwa ndani na kuzishusha hakika alitambuwa ni uzembe wa kuacha chumba cha mtu wazi ndio umepelekea kuibiwa je atamueleza kitu gani mwenyewe mpaka amuelewe sema akajipa moyo familia yake ipo, Hakuweza kufahamu kama familia yake si chochote si lolote mbele ya mwanaume huyo wa shoka.
Hafidhi nae baada kuondoka nyumbani kwake akapanda daladala mpaka Buguruni rozana na kushuka akavuka barabara na kuelekea maeneo ya kwa Madenge yani alikuwa anatembea haraka haraka sauti ya honi ndio ikamshtua na kumfanya akae pembeni kidogo
“Pisha njia mtoto wa malaya wewe yani unatembea njia nzima utafikili ya baba yako punga wee’’ alikuwa dereva bodaboda aina ya boxer akiongea hivyo na kumwita Hafidhi mtoto wa malaya yani bora wakati anaongea maneno hayo angeondoka si akasimama “Unasemaje wee jamaa mimi nani?’’ Hafidhi akauliza swali huku akimsogelea yule kijana ilikuwa kufumba na kufumbuwa kijana yule akirushwa hewani baada kutandikwa zinga la teke na kutupwa kule barabara kisha mwanaume akaondoka na pikipiki, yani kilikuwa kitendo cha haraka mno kijana akabaki kupiga kelele “jamani pikipiki yangu!’’
“pole sana kijana siku zote unaambiwa dawa ya kiburi jeuli hakika leo umeipata kiboko yako wewe ndio ulitaka kumgonga yule jamaa baada kumuomba samahani ndio kwanza ukamtusi sasa unaona kilichokutokea, kakupa teke moja tu kama vile Vann damme kwenye movie ya bloosport kamtandika Bolo younk pole ehee’’ Alikuwa mzee mmoja muuza kahawa na kashata katika maeneo hayo,
Unaweza kusema yupo kwenye mashindano au anafukuzwa na mapolisi kwajinsi alivyokuwa akiendesha ile pikipikki kwa kasi watu waliokuwepo maeneo ya sokoni wakabaki kutukana matusi na kulaani kitendo cha dereva yule kutokuwa mstaarabu yani watu walikoswa koswa kugongwa na pikipiki ile si akaingia nayo kwenye vichochoro vya Madenge mitaa ambayo kila wanaonyesha video show biashara za chipsi sambusa kachori ice cream zimejazana.
Mbele ya nyumba moja hivi ndipo akafunga bleak na kushuka akabisha hodi na kukaribishwa na mzee mmoja wa kiarabu kama tunamkumbuka ndio baba mzazi wa marehemu Yusra “Karibu sana mkwe bila shaka ujio wako ni wa neema kubwa sana kwetu’’
“Kwanza Assalam alaykum mzee wangu naona umeanza maneno kabla ya salamu’’
“Waaleykum ssalam kijana hivi unadhani hata salamu naweza kuikumbuka kweli maana kijana umetutenga kabisa yani sikuoni tena maana kile ambacho ulikuwa ukikifata hakipo tena’’ “Hapana mzee wangu si unajuwa mambo mengi kijana wako naangaika kila kukicha kumsaka muuwaji wa kipenzi changu’’
“ohoo basi vyema kijana kama bado unaendelea kufanya hizo harakati lakini naomba utambuwe kitu kimoja tu mpaka sasa muuwaji wa mwanangu nae yupo kuzimu. Ni kauli ambayo ilimshangaza sana Hafidhi na kujiuliza amejuwaje kama yule kijana kashauwawa tayari sema hakutaka kuonyesha mshangao wake wakaenda kukaa kwenye sofa dakika si nyingi kuna binti akaingia yani kitendo cha Hafidhi kumtia machoni tu moyo wake ukashtuka hakika binti alikuwa kafanana kila kitu na Yusra “Assalam alaykum ewe kaka yangu’’,,, yule binti akatoa salamu huku akimpatia kiganja cha mkono mwanaume akaitikia huku akiwa kashikana nae sema katikati yule binti aliweka kitambaa kama sheria ya dini ya kiislam inavyosema ni haramu kwa mwanamke na mwanaume kugusana nyama kwa nyama asiekuwa halali kwako,
“Waaleykum ssalam mzee wa nyapu akaitikia hivyo. Huku akikitumia kidole chake cha kati akimtekenya kwa style ya uchokozi bibiye akang’ata ripsi za midomo yake kuonyesha jinsi gani anajisikia msisimko wa ajabu yani kutekenywa kidole tu kwenye kiganja chake cha mkono mototo kapagawa
“Vipi mbona mmeshikana kwa muda mrefu hivyo?’’ Ikabidi baba aulize swali. “Ahaa hapana mzee unajuwa namfananisha huyu mwanao na Yusra hakika wanafanana sana’’ Hafidhi akazuga kwa kusema hivyo huku akimuachia mkono’’
“Ndio huyo ni mdogo wake anaitwa Sumaiya wamepishana mwaka mmoja na nusu tu,’’ “Duhuu yani wee mzee ni nom a sana mwaka mmoja na nusu ukawekeza kitu kipya hahahaha’’
Kila mmoja akacheka
“Sumaiya embu nenda kaandae chakula shemeji yako si unamuona ana maneno
Utasema yupo bungeni.
Sumaiya akaondoka mbavu hana kwa kicheko akaingia chumbani kwake na kujitazama mkononi na kujibusu
“kwa style hii siwezi kukukosa
Shemeji hakika wewe ni wangu, nichukuwe Mimi niwe kiburudisho chako kama alivyokuwa akikuburudisha Dada
Nami nitakufanyia hivyo hivyo".......
Wakati bibiye Sumaiya akimuwazia kumpata shemeji yake kama usemi unavyosema
Sijui hainaga ushemeji tunakulaga, huku
Sebuleni mazungumzo baina ya
Hafidhi na mkwewe yalikuwa yanaendelea.
“sasa mzee wangu mimi nimekuja kuna tatizo kidogo linanitatiza"
“Tatizo gani tena kijana?"
“Dahaa sijui hata niseme nini kwakifupi leo
Nikiwa nyumbani kwangu simu yangu ikaita kuitizama number ngeni basi nikafanya kuipokea ajabu
Aliyepiga simu ile akaanza kucheka yani akacheka sana mwishoe akakata simu,
Nikajalibu kuiangalia ile number kwa tigo pesa ajabu jina limetokea
Yusra Yasri"
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni