MTAA WA TATU (57)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
Walinzi wa ukumbi huo wenye asiri mchanganyiko yani kulikuwepo na Warusi, Wajapan, Wathailand hawakupoteza muda wakamvamia basi ulitembezwa mkono wa ajabu watu walitupwa huku na kule hakika Mwanaume hakutaka mchezo kabisa.NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Basi vurugu mechi ikaendelea ndani ya hotel hiyo huku mrengwa yani aliefatwa akikimbia baada kupata upenyo sema mwanaume hakutaka kumuacha kizembe ijapokuwa walinzi walizidi kumzonga asiweze kumfikia huyo mzee “jamani mzuiyeni huyoo anataka kuniuwa,’’ mzee yule akapaza sauti kwa kupiga kelele akiwaomba walinzi waweze kumzuia Hafidhi sema ilikuwa kazi ngumu sana kwa walinzi hao kuweza kukizuia kiumbe hicho. Polisi wa jiji hilo nao wakafika mwanaume akawekwa chini ya ulinzi baada kuelekezewa bastola nae akatii amri kwa kunyoosha mikono yake juu lakini kabla ya polisi kumshika akapotea na kuacha hali ya mshangao kwa maafande wale mambo aliyokuwa akiwatendea maafande wa Tanzania sasa kahamishia Ufaransa.wakati maafande wakihaha kumtafuta ndipo zikasikika kelele za mtu “jamani nakufaa!!! Kelele zile zilisikika zikitokea gorofa ya pili kitendo bila kuchelewa wakapandisha ngazi haraka haraka kabla ya kufika kuna kitu kikatupwa chini kuja kuangalia ni mwili wa yule mzee akiwa na jina jipya marehemu, hakika polisi walidata si kidogo kwakuwa walijigawa wengine wakapandisha juu wengine wakabaki chini kivumbi jasho kiliwakuta wale waliopandisha juu wakakutana na kitu ambacho waliomba iwe movie au ndoto , Kwanza walifinywa na kunyongelewa mbali sauti zao tu ndizo zilizoweza kusikika mwishoe wakawa kimyaa hawakusikika tena, watu wakabaki katika hali kubwa ya sinto fahamu,
Wakati Hafidhi akifanya mauwaji ya kutisha katika nchi ya kigeni hali ilizidi kuwa tete ndani ya nchi hiyo kila kukicha watu wakazidi kuuwawa polisi wakazidi kumsaka muuwaji kila kona kulikuwa hola hatimae wiki miezi mitatu ikatimia huku takribani watu wapatao ishillini wakipoteza maisha kwenye matukio yenye kufanana “vizuri sana hakika kazi yangu imeweza kwenda vyema sasa wacha nirudi nyumbani,’’ ilikuwa kauli ya Hafidh,i tukirudi nchini Tanzania kijana Michael nae akaanza upelelezi wake wa kumsaka huyo kidudu mtu pasipo kutambua mwenzake hayupo nchini. “ohoo Mungu wangu yani huyu mshenzi kahamua kuwafungia safari ndugu zetu dahaa masikini bwana Sultan kauwawa,’’ alikuwa mzee Khatibu kama unamkumbuka ndio baba mzazi wa marehemu Habiba ni mtu ambaye amewekwa kama kiporo na Hafidhi kwanza hakuwa na haraka nae, hata yeye mwenyewe alitambuwa kitu kimoja ipo siku itafika zamu yake, wakati bibiye Vivian akijfungua mtoto wakiume mwenzake akajifungua mtoto wakike na kupewa jina la Yusra, wakiume akaitwa Ikram
Ilikuwa siku ya October 14 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa mwalimu Nyerere ndani ya uwanja wa taifa ndipo zilifanyika kumbukumbu hizo. Bibiye Mariam ukipenda muite Mama Yusra nae akapanga mipango yake ya kumuondoa hapa duniani muheshimiwa Rais hakika kumbukumbu ziliweza kupambwa kwa nyimbo za maomborezo kutoka kwa Kapten John Komba siku hiyo ulinzi ulikuwa taiti sana kila kona vikosi vya FBI vilitanda yote ilikuwa chochote kibaya kisitokee ukafika muda wa muheshimiwa Rais kupanda jukwaani kwaajili ya kuzungumza mawili matatu matarumbeta yakapulizwa kama kumkaribisha muheshimiwa nae akapanda jukwaani na kujiweka sawa, binafsi alikuwa ni Rais ambaye ni kipenzi cha wananchi yani tokea aingie madarakani kila kitu kiliweza kubadilika uchumi uliweza kupanda kwa asilimia tisini na tano. Ajila kwa vijana zilikuwa za kumwaga vitu viliweza kushuka bei sukari kilo shilling elfu moja unga kilo mia nane mchele bei ya juu kabisa mwisho kilo moja ni elfu moja na mia tatu, sasa wananchi watake nini tena ikiwa huduma mahospitalini ni sawa na bure. Baada kupanda jukwaani muheshimiwa akawapungia mkono wa salamu wananchi wake, nao wakasimama kwa kupiga vigeregere, ile anafungua mdomo tu aanze kuongea ghafla chuma cha moto kilikuja kwa kasi na kupenya kwenye paji lake la uso, kama alivyopigwa marehemu mkewe nae ikawa hivyohivyo akayumba na kudondoka chini puhuu, utasema mzigo wa kuni wananchi wakapigwa na butwaa wasiweze kuamini kwakile kilichoweza kutokea kwa mpendwa wao siku zote kuuwawa kwa Raisi inakuwa balaa walinzi wakatanda kila kona kwa kuuzunguka uwanja mzima ikiwemo na mijengo ya jilani yote ilikuwa katika kumsaka huyo mdunguaji wa masafa marefu siku ya sherehe za uhuru alimuuwa mke wa Rais leo hii kamuuwa mwenyewe hivi huyu muuwaji anania gani na nchi yetu. Ni maswali yaliojengeka kwenye vichwa vya watu wengi. Kwenye jengo moja hivi juu kabisa kama gorofa ya kumi na mbili hivi kuna kiumbe kimetinga mavazi meusi alikuwa akishuka kwa kamba kwa speed ya ajabu mmoja kati ya walinzi akaweza kumuona kitendo bila kuchelewa akawasiliana na wenzake kabla kile kiumbe hakijafika chini, vikosi vimetanda nae pasipo kutambua kama kaonekana akazidi kushuka.
Akiwa sijui gorofa ya tatu ile akashtuka baada kuangalia chini na kuona polisi wametanda kule chini wakimngojea yeye kwa hamu, kulekule juu kiumbe kikajibiduwa na kutaka kurudi alipotoka ghafla kamba aliyokuwa akishukia ikakatwa baada vua ya risasi kuanza kumiminiwa kule juu na kujikuta akidondoka kuja chini sema akatumia ujuzi aliokuwa nao. Asije kufa au kuumia kizembe akadank na kujiviringisha mpaka chini ile kutuwa chini tu akaanza kutembeza mkono kwa maafande binafsi alikuwa anapiga mapigo ya ajabu. Under cover agent bibiye Mona Risa nae akafika na kuwaomba polisi wakae pembeni hiyo ngoma hawaiwezi kabisa. Bila ubishi wakampisha bibiye hatari akaingia kwa mbwembwe za ajabu wote walikuwa wakali kwenye mapigo ya fighting wing chun, ikawa piga nikupige huku vikosi vya polisi wakizidi kuongezeka si akaingia bibiye Vivian sasa ikawa mtu mmoja kwa wawili sema muuwaji akasimama imara kwenye kupambana ikawa shida juu yake. Hakika akazidiwa uwezo na kujikuta akipigwa kama motto kibaya zaidi akaingia kiumbe mwingine anaekwenda kwa jina la Michael ghafla Vivian na bibiye Mona wakapigwa na butwaa baada muuwaji kuvuliwa mask sio wao tu hata baadhi ya polisi wakashtuka kumbe alikuwa bibiye Mariam kama tunakumbuka aliwai kumwambia kitu hiki Hafidhi kuwa ipo siku atakuja kumuuwa muheshimiwa Rais,
Mariam hakuwa na ujanja tena damu zikabaki kumtoka kichwani zingine mdomoni na puani hakika kitendo cha kumuuwa Rais ni kosa kubwa sana tena ukichukulia alikuwa ni kipenzi cha watu.
Utawaambia nini wananchi wakuelewe,
Michael akazidi kumtandika makofi
huku akimburuza kuingia nae ndani ya
Uwanja.
Vivian na Mona Risa roho zao ziliwauma Sema hawakuwa na chakufanya
“Mariam please nakuomba nisamehe kwa hiki nilichokutendea hakika sikuweza kufahamu kama ni
Wewe,
Vivian aliongea kimoyomoyo huku akishuhudia
Michael akichukuwa kipaza sauti na kusema
“ndugu Wananchi huyu ndio muuwaji mwenyewe tumefanikiwa kumnasa
sasa basi hukumu yake itolewe hapahapa,"
“ndioo nae auwawe!!! Auwawe"......
Wananchi wakapaza sauti kutaka bibiye auwawe
Undercover agent mmoja akachomoa jambia kwaajili ya kumchinja bibiye
Mariam akafumba macho kukingojea kifo chake,
Vivian nae akaangalia pembeni asiweze kuona jinsi mwenzake akifanyiwa kitendo hicho.
Wakati yule Undercover agent akiwa kainua jambia lake juu kabla ya kulishusha, ghafla kitu chenye ncha kali sijui kisu au nini
Kilirushwa na kwenda kukita mkononi mwake
Akalidondosha jambia chini
Upepo ukavuma aisee Ninja short huyo hapo mbele yao,
Vivian hakuweza kuamini, FBI wakafanya kumfata waweze kumdhibiti wakashindwa na kuishia kupokea maumivu,
Michael nae si alikuwa akimtafuta huyu kiumbe kwa muda sasa
Akachumpa kwa kupaa juu kabla ya kutua akajikuta akipokea mateke ya double double kulekule juu na kutupwa mbali na pale
Mwanaume alitumia dakika mbili tu kusafisha njia na kumsogelea kipenzi chake
Akambeba na kupotea nae,
Vivian na Mona wakabaki kucheka tu maana huyu kiumbe si wamchezo.
Michael akabaki kupiga kelele kwa maumivu ukichanganya na hasira imekuwaje yeye kapigwa kizembe vile.
Ikabidi nchi iwe mikononi mwa jeshi kwa muda mpaka pale
Madaraka atakapo kabidhiwa makamu wa Rais,
“ulimuona yule mshenzi jinsi alivyoweza kumtandika Michael?"
Mzee Khatibu akauliza swali wakiwa kwenye kikao chao cha siri.
“yani wee acha tu hakika yule kijana hawezekaniki kabisa
Itabidi Michael ajipange,"
“hapana yule bwege mimi hakunipiga kanibahatisha tu mbona alikimbia,"
Michael akapinga vikali kuwa yeye hakupigwa.
“Michael mwanangu usitake kutuona sisi hatuna akili
Yani tumeweza kukuona ukiruka kwa kumfata ukaishia kupigwa teknik za ajabu
Pole sana kijana wangu,"
“ohoo inamaana mnamsifia sana yule bwege sio subirini na muone,"
Michael akaongea hivyo na kuondoka zake.
Sijui anaenda wapi
Nchi ikaingiwa na simanzi watu walilia na kusaga meno hakika taifa liliingia kwenye msiba mzito sana ikafikia baadhi ya wananchi kupoteza maisha wengine kuzimia.
Hakika alikuwa Rais kipenzi cha wengi
Mikoa yote ikazizima,
Ni tukio ambalo haikutakiwa nchi zingine waweze kufahamu kuepusha nchi kuvamiwa kizembe ulinzi uliwekwa wa kutosha maeneo ya mpakani.
Nchi ikiwa mikononi mwa Jeshi kwa muda,
“Mona Risa imekuwaje mpaka nawe ukaletwa ndani ya nchi hii
wakati ulipelekwa Somalia kupambana na maharamia wa nchi hiyo?"
Lilikuwa swali kutoka kwa bibiye Vivian akimuuliza Mona.
“yani Dada wee acha tu wakati mimi napelekwa Somalia, nyie mkibaki kambini basi nikafika kule Somalia yani mambo niliyoweza kuyaona huko binafsi kuna
tisha si mchezo, watu wanauwana hovyo hovyo yani ukilala na kubahatika kuiyona kesho
Shukuru Mungu huko watu wanaishi kama kuku akija mgeni tu wanabaki roho juu.
Sema niliweza kuifanya kazi yangu vyema wakati nikiwa katika hatua za mwisho kumaliza mission ndipo nikapewa
Taarifa za kifo cha Yusra kwanza nilishtushwa na kuuliza alikuwa anaumwa au. Nikapewa maelezo ya kutosha nikaomba nije kuziba pengo lake.
lakini iwe kimya kimya uwongozi ukanikubalia basi nikaingia nchini kimya kimya na kuifanya kazi hii
Niliweza kumtwanga risasi yule muuwaji,"
Mona akamaliza kusimulia na kubaki kutizamana,
“vizuri sana mdogo wangu swali la kujiuliza kwanini Mariam katenda mauwaji haya nini tatizo nini shida,"
Vivian akasema hivyo.
“hata mimi najiuliza maswali hayo hayo sema kuna kitu nahisi ndani ya akili yangu lazima kunakitu kimeweza kutokea kabla ya mauwaji haya.
Lakini Dada mbona kile kiumbe ndio kaondoka na Mariam si ataenda kumdhuru?"
“hapana hawezi kufanya hivyo pale alipo
Yupo kwenye mikono salama kabisa,"
Hafidhi akiwa nchini Ufaransa
Aliweza kutambua kitu kimoja kama October 14 inakaribia basi
Bibiye Mariam anaweza kufanya kile ambacho aliwai kumueleza
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni