Notifications
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…

TANGA RAHA (22)

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Nikakohoa kidogo na kuwafanya mchungaji na mtu wake kunitazama kisha wakaendelea na mazungumzo yao
SASA ENDELEA...
“Basi nilimtumia tiketi ya boti nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa sita tarehe kama sita mwaka el-fu mbili na tisa(2009).Akaja hadi Dar baada ya ya kuipokea tiketi ambayo nilimkabihi rafiki yangu ambeye alijuwa ni mfanyakazi kweye boti za Baresa.Mchungaji nisiku danganye yule mtoto alikuwa ni mzuri na asili yake ni mwarabu....Ila kitu kilicho kuwa kikinishangaza mimi kila ilipokuwa ikifika saa sita usiku alikuwa anataka kwenda baharini kwa madai ya kwenda kuoga na kutokana tulikuwa tupo karibu na bahari nikawa ninamruhusu kama kawaida.Ile tabia ikaanza kunichosha ikanibidi siku nimfwatile hadi baharini na kukuta akabadilika na kuwa kama hawa NGUVA......Aisee ile siku Mchungaji niliogopa kupita maelezo na mbaya zaidi alikuwa na wezake wawili ambao nao walikuwa kwenye maumbo kama lake wakichezea maji.

Kilicho niingiza kwenye matatizo ni simu yangu kuita na enzi zile ile misimu yenye makelele ya kichina ndio yalikuwa yameingi.

Nikastukia kibao kimoja ambacho zikujua nimepigwa na nani na nikajikuta nimeangukia kwenya maji na wakanichukua hadi katikati ya kina kirefu na kutokana na uzoefu wangu wa bahari nilipajua kuwa pale ni Nungwi”

Nikajikuta nikishusha punzi kwa nguvu baada ya jamaa kupiga fumba la soda kwani story ya jamaa ilizidi kunisisimua mwili wangu na nikajiweka vizuri kwenye kiti huku nikiendelea kusikiliza stori ya jamaa kwani kwa mbali nilisha anza kusahau yaliyonikuta kwangu
“Basi baada ya wao kunichukua wakanizamisha kama mara mbili hivi nikanywa mafumba kad-haa ya maji nikajikuta nikiishiwa na nguvu za mwili wangu.......”
“Wakati wanakuchukua kwenye maji hadi mukafika nungwi mulikuwa munakimbia ua munafanyaje?”
“Mchungaji nilikuwa wala sielewi tunakimbia au tunakwenda taratibu kwa maana nilijikuta tu tumefika Nungwi na kufumba na kufumbua nikajikuta nipo kwenye mjia ambao sikuuelewa kama ni duniani au kuzimu kwani niliona watu wa ajabu sana kiasi kwamba mara kwa mara nikawa ninapoteza fahamu......Waliniingiza kwenye moja ya shimo ambalo kulikuwa na funza wa moto ambao hutoboa mwili kwa haraka kiasi kwamba nilipata maumivu makali”
“Pole Joseph....Unajua siku nilikuwa nimelala Mungu akaniletea maono kwamba kuna mwana-damu ambaye ni wewe upo kwenye hali ngumu sana na akanipa maagizo nifanye maombi juu yako na nifunge kwa siku 7 huku nikiomba na kula kipande cha mkate kwa siku na glasi ya ma-ziwa”

Nikaanza kujifikiria sijui nimshirikishe mchungangaji majanga niliyo nayo ila ikanibidi nikae kimya huku nikiwasikiliza

“Mchungaji sikuweza kuamini kama nitarudi tena duniani kwa maana walikuwa wakinileta hadi huku duniani kuangalia ndugu zangu wanavyo hangaika katika kunitafuta kiasi kwamba nikawa ninatamani niweze kuwasemesha ila nikawa ninashindwa......Nakumbuka mwaka 2010 wakaanza kunifundisha kazi ya kuua watu kwa kusababisha mambo yanayoweza kusababisha ajali.Hata ile ajali ya Nungwi ya kuzama kwa MV Speace mimi pia nilikuwa ni miongoni mwa vijakazi tuliokuwa tunaichukua miili ya watu waliokuwa wanakaribia kufa na kuwapeleka chini ya bahari kiasi kwamba wale watu tulikuwa tunawatumikisha katika kuwaleta wanadamu wengine amabao huku duniani wanakaa kihasara hasara”
“Ndio maana watu huwa ninawahubiria kila siku kuwa ndugu tubuni dhambi zenu mwisho wa dunia unakaribia ila bado wameiweka miiyo yao kuwa migumu”
“Kweli mchungaji unayo yasema.....Kule kuna mateso sana....Na usiombe ukatembea na jini lazi-ma ipo siku atakupeleka kuzimu”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbioa kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi baada ya kusikia kuna safari ya kwenda kuzimu
“Na kabla sijapata nafasi ya pekee ya kutoka kule kuna Malkia wao alitumwa kuja Tanga kuian-gamiza kupitia mwanaume mwenye nyota kubwa ambaye herufi yake inaanziwa na ‘E’ ila siku-jua hiyo ‘E’ ni nani?”

Mwili mzima ukaanza kunitetemeka kiasi kwamba nikaanza kujihisi haja ndogo ikitaka kunitoka kwa woga
“Huyo Malkia wao anaitwa nani?”
“Sisi kule tulikuwa tunamuita Mtukufu Malkia ila jina lake nililisikia siku akiitwa na baba yake ambaye anaitwa Hitler na mtoto wake anaitwa sijui Oli.. nini?”
“OLVIA”

Nikajikuta nikiropoka na kuwafanya wanitazame kwa mshangao na kumfanya jamaa kutingisha kichwa akiashiria jina nililo litaja ndilo jina halisi la Malkia wao na kunifanya nizidi kuogopa.

Mchungaji akanitazama kwa macho makali hadi nikajikuta nikitazama pembeni nikijifanya kama vile sielewi kitu kinacho endelea
“Kijana”
Mchungaji aliniita na kujikuta nikigeuka na kumtazama pasipo kuzungumza kitu chochote
“Unaweza kuja na kujumuika nasi hapa?”
“Ahhaa....Asanteni”
“Njoo tuu kijana wangu kwani kuna ujumbe wako nimeupata hapa nataka niseme nawe japo kwa ufupi tuu”
“Huo ujumbe umetoka kwa nani?”
“Wewe sogea Mungu atakonyooshea mkono wake na wala usiogope”

Nikanyanyuka na kukaa kweye kiti cha pembeni na mchungaji akaniomba nimpe mkono ka ishara ya kusalimiana.

Nikaanza kujihisi mkono ukinitetemeka kiasi kwamba nikajikuta niki-chomo kwa nguvu kuto kwenye viganja vya mchungaji.
“Kijana usiogope kijana....Mimi ninaona unamatatizo katika maisha yako ila jina la bwana wetu Yesu kristo litafanya maajabu juu ya maisha yako........”
“Umejuaje kuwa mimi ninamatatizo?”
“Nimekuona tuu jinsi unavyo teseka na majanga ya dunii hii na nafsi yako hivi sasa ipo kuzimu na wanaifanyia mpango wa kukufanya wewe kuwa kiongozi wa ambaye utaweza kuiteka hii Tanga na kuwa ndio Makao makuu ya kuzimu kwa Tanzania”

Nikabaki nikimtazama mchungaji huku mdomo ukiwa wazi na mwili mzima ukazidi kunitete-meka
“Mchungaji twende kwangu kuna tatizo?”
“Kwako ni mbali na hapa?”
“Hapna ni hapo juu tuu”
“Sawa...Joseph kama huto jali ywende tukaifanye kazi ya bwana”

Tukanyanyuka na kutoka nje ya bichi na kwauzuri wanagari lao walilo jia katika sehemu hiyo,Tukaingia na nikaanza kuwaelekeza hadi tukafika nyumbani kwangu na sikuwakuta Hilda na mwenzake ila geti tumekuta limejifunga vizuri.

Nikafunga geti na kuwakaribisha na kabla mchungaji hajaingia ndani nikaanza kumuona akizungumza zungumza mwenyewe maneno nisiyo yaelewa ila watu husema mtu akizungumza kwa mtindo huo ananena na roho.

Mchungaji akafungua mlango na huku akiendelea kuomba na Joseph naye akawa na kazi ya kuomba ila mimi nikawa na kazi ya kuwafwata kwa nyuma hadi sote tukaingia ndani na kwa bahati mbaya tukamkuta Mwajuma akiwa amelala chini huku akitoka damu za pua

Mchungaji akazidisha sauti ya kuomba na kila anvyozidi kuomba ndivyo jinsi hali ya hewa ikazidi kubadilika ndani ya nyumba hadi ikafikia hatua nikaanza kuogopa.

Upepo mkali unaokwenda mithili ya kimbuka kikali ukaanza kuzunguka sebleni na baadhi ya vitu vikaanza kuanguka chini ikiwemo vyomvo vilivyopo ndani ya kabati.

Nikastukia nikamuona Joseph akirushwa na kupiga ukutani na akatulia kimya na gafla nikamshugudia mchungaji akichmwa na kisu kilichoruka kutoka kabatini na kikatua kifuan kwake

Mchungaji akakishika kishu kilicho mchoma na kukichomoa na kuzidi kuomba huku akiiongeza sauti ya juu huku akiliitaja jina la Yesu kristo.

Miale ya radi na kurumo ikanza kupiga maeneo ya dari na kusababisa nilale chini kwa woga ila mchungaji hakulala chini na akazidi kuomba na taratibu na mimi nikajikuta nikiisema
“SHINDWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO”

Nikaendelea kurudia rudia maneno hao mara gafla nikajikuta nikinyamaza baada ya Olvia Hit-ler kusimama kwenye moja ya kona huku akiwa amevalia nguo nyekundu na sura yake ikiwa imejawa na hasira kali sana kiasi cha macho yake kutoa mwanga mkali
“Wewe pepo unayetaka kuchukua watu wa bwana leo hii ndio mwisho wako nakufunika na kukurudisha kuzimu katika jina la YESU KRISTO wa nadhareti TOOKKKKAAAAAAAAAAAAAAA”

Olvia Hitler akayumba kidogo akionekana kama ametetemeshwa kwa maneno hayo ila akanita-zama kwa macho makali na kuninyooshea mkono na kujikuta nikikabwa shingo na kitu nisicho kiona na taratibu nikaanza kunyanyuliwa kwenda juu.

Mchungaji akaunyoosha mkono wake mmoja kwangu huku akiomba kwa nguvu na kujikuta nikianguka chini na gafla Olvia akapotea na hali ya ndani ikaanza kutulia na baada ya muda ikarudi katika hali ya kawaida ila vitu vingi vimechanguka na kukaa katika sehemu tofauti na nilivyokuwa nimevipanga

Mchungaji akasogea taratibu na kukaa kwenye sofa huku jasho jingi likimwagika na nikaonda shati lake likilowana na damu
“Mchungaji umeumia hapo kwenye kifua”
“Hakuna tabu ni jeraa dogo ila tafuta maji na chumvi unilete hapa”

Nikatoka kiwoga woga na kwenda jikoni na kuanza kuitafuta chumvi na baada ya muda nikaipata kisha nikaweka maji kwenye kikombe na kurudi sembeni.

Mchungaji akavichanganya kwa pamoja maji na chumvi kiasi akaviombea na kujipaka kwenye jeraha lake na kuifanya damu kuacha kutoka.Akasimama na kumshika Joseph kichwani na kuanza kumuombea taratibu hadi Joseph akapia chafya na kunyanyuka.

Akamfwata Mwajuma na kumtazama kwa muda kisha akamnyooshea mkono na kuanza kumuombea na gafla Mwajuma akaanza kujikunja kunja mithili ya nyoka anaye tambaa.

Mchunagaji akazidi kuomba na baada ya muda Mwajuma akaanza kukoroma huku mapovu yakianza kumwagika mdomoni hadi ikafikia hatua akaanza kutoa vitu vyeusi mdomoni zikiwemo irizi mbili kubwa.

Nikabaki nikashangaa kwani kwenye maisha yangu sijawahi kuona kitu kama hicho kikitoka mdomoni mwa wa mtu.Mwajuma akatulia na baada ya muda akakaa kitako huku akihema akionekana amechoka sana
“Unajisikiaje binti?”
“Vizuri”
“Nyanyuka na ukae kwenye kiti”

Mwajuma akanyanyuka na kukaa kwenye kochi huku akiwa anashangaa shangaa
“Bnti unaitwa nani?”
“Anaitwa Mwajuma”
“Ahaa Mwajuma hali yako inaendeleaje?”
“Salama tu nipo wapi?”
“Mimi ni Eddy umenikumbuka?”
“Ndio nakukumbuka mbona nipo hivi baibui langu lipo wapi?”

Nikatizama tizama chini na kuliona baibui la Mwajuma nikaliokota na kumpa akalivaa na kisha mchungaji akamuoba aende bafuni akaoge.

Nikamuonyesha Mwajuma bafu la kuoga na nikamuonyesha na chumba changu kama atatoka bafuni aweze kuingia kupaka japo mafuna na nikampa na taulo langu kisha nikarudi sebleni na kukaa kwenye sofa moja wapo lililopo sebleni kwangu
“Kijana kwanza napenda kulijua jina loko?”
“Mimi ninaitwa Eddy Praygod”
“Unajina zuri..”
“Asante mchungaji”
“Amini Mungu yupo na shetani huwa hana nafasi katikati ya watu wa Mungu,Pale mwanzoni Shetani aliweza kuyateka maisha yako na kuyachukua na kuyafanya ni maisha ya ajabu....Ila kwa sasa ninakuomba umpokee Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

17 Simulizi Tanga Raha
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni