TANGA RAHA (25)
Zephiline F Ezekiel
7 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Hadi tunamaliza kupeana raha Yudia akaonekana kuridhika na akajizala kitandani huku akihema na jasho likimwagikaSASA ENDELEA...
“Eddy nikuambie kitu?”
“Niambie tu”
“Unajua kama baba na mama sio wachungaji kama watu wanavyo wadhania....Ila hii ni siri ninakuomba usimwambie mtu yoyote”
Nikajikuta mapigo ya moyo yakianza kuniende mbio kiasi kwamba nikajikuta nikinyanyuka kitandani na kukaa huku nikimtazama Yudia kwa macho makali kiasi huku nikiwa siamini manen anayo niambia
“Ikifika saa nane na nusu usiku nitakuonyesa ibada wanazo zifanya baba na mama na baadhi a watu kwenye kanisa lao”
“Unajua hadi sasa hivi sijakuelewa vizuri unamaanisha nini?”
“Ngoja ukajishuhudie na macho yako ndio utaelewa ninamaanisha nini kwani sasa hivi ni saa nane kasoro utaona tu kila kitu”
Tukakaa hadi mida ya saa nane usiku Yudia akaninong’oneza na kuniambia huu ndio wakati maalamu wa wazazi wake kwenda kwenye sala zao ambazo sikujua ni sala za aina gani wanazo zifanya wao.
Tukatoka ndani ya chumba huku tukinyata na Yudia akiwa amevaa gauni lake la kulalia na tukafika sebleni na taa zote tukakuta zimezimwa na Yudia akaniomba tuingie ndani ya
Chumba cha kusomea nikataka kumuuliza swali ila nikasita na kujikuta nikiingia ndani ya chumba hicho na Yudia akasimama kwenye moja ya ukuta wenye vitabu na kuusukuma na ikafunguka njia ya mlango mwembamba amabao unaruhusu mtu kuingia.
“Twende”
Yudia akaniambia na sote tukaingia ndani ya ya chuma hicho ambacho kinagiza totoro ila kwa mbali kuna taa za vibatari zinazo waka kwa kwa mwana makali na Yudia akaniomba nisipige kelele ya aina yoyote kwani watu wapo kwenye ibada na ikitokea nitafanya kitu kama hicho utakuwa ndio mwisho wa maisha yetu.
Katika chumba tulicho ingia kuna mabenchi kama ya kanisani ambayo kwa mbele yake kuna madhabahu ambayo wamesimama watu wachache walio valia mavazi meusi na mekundu ambayo yamewafunika vichwa vyao huku moshi mchache ukiwa umetawala kwenye madhabahu hiyo.
Tukajifichwa kwenye moja ya benchi na kuendelea kuwashuhudia watu wapatao theladhini wakiimba nyimbo amabazo sikuzielewa ni nyimbo za aina gani kwani hata tune yake si kama nilizo wahi kuzisikia
“Pale baba na mama yako ndio wapi hao?”
“Baba ni yule aliyeshika lile jitabu kubwa na mama yule akiyeshika msalaba wenye nyoka mbele”
Nikaendelea kutazama kwa umakini na kuanza kujiuliza kama dini yenyewe wanayo ifanya huyu mchungaji na baadhi ya waumini wake ipo hivi je nguvu za kuwaombea watu na wakatokwa na mapepo wameziotoa wapi
“Wanatumia lunga gani kuzungumza pale?”
“Kile ni kirusi kilicho changanyikana na kireno”
“Wewe unakifahamu?”
“Ndio naelewa wanacho kizungumza....Kaka pale baba anasema kwamba hali ya waumini inazidi kuongezeka kanisani na anatoa pongezi kwa kanzi nzuri waliyo ifanya katika kuongeza wafuasi wa kanisa lao ambalo ni jipya kwa hapa Tanga”
Tukaendelea kutazama mambo wanayo yafanya na baada ya muda nikamuona mchunaji akinyoosha mkono wake kwenye kioo kikubwa na gafla ikatokea picha yangu kipindi nikiwa nipo sebleni kwa mchungaji ninakula na nikaanza kujikuta nikitetemeka kiasi kwamba nikataka kunyanyuka na kuondoka ila Yudia akanizuia nisiondoke
“Wanasema kuwa wewe ni miongoni mwa watu wenye nyota zenye nguvu duniani na wanahitaji waichukue ili waweze kuongeza kasi kubwa ya ukuaji wa makanisa yao”
Maneno ya Yudia yakazidi kunichanganya kiasi kwamba nikatamani ardhi ipasuke na niingie na inimeze
“Na wanasema adhimio hilo watalifanya kesho saa sita kamili mchana watakapo kuja nyumbani kwako kukuombea.....Na wanataka damu yako ndio itakuwa ufunguo mkubwa wa nguvu zao ambazo wanazo hitaji kuzipata kutoka kwako”
Galfa hali ya hewa ikaanza kubadilika mbela ya madhabahu na upepo mkali ukatawala na radi vikaanza kutawalia kila pande ya madhabahu ila watu walio kuwepo wakabaki wakiwa wamesimama huku mikono yao wameinyoosha mbele kana kwamba wanapokea kitu kutoka juu.
Mwanga mkali ukatoka kwenye sehemu ya madhabahu yao na gafla wakatokea watu wawili walio valia nguo nyeupa na mmo akiwa ni mwanaume na mwingine akiwa ni Olvia Hitler na kunifanaya mwili mzima kunyong’onyea na kuishiwa nguvu kabisa
Olvia Hitler akasimama katikati ya mchungaji na muumini mwengine na akawawekea mikono kichwani mwao na kuanza kuzungumza maneno ambayo sikuwa ninayeelewa na kusababisha hali ya hewa kuzidi kutisha ndani ya kanisa lao la siri ambalo kusema
Kweli linatisha kupita maelezo.Upepo mkali mithili ya kimbunga ukaanza kuzunguka kwa kasi ndani ya kanisa huku kikiwa kama kinachungunza kitu fulani ndani ya chumba
“Eddy tuondoke ule upepo ni jini linaanalia usalama”
Tukaanza kutambaa chini mimi na Yudia na kabla hatujaufikia mlango tulio ingilia tukastukia watu wawili walio valia nguo nyeusi zilizo wafunika hadi vichwa vyao wakasimama mbele ye-tu.Yudia akasimama na kuwasukuma huku na yeye akiwa
Anazungumza manena ya ajabu kawa wafanyavyo watu waliomo ndani ya kanisa lao na kuwafanya watu hao kuangukia pembeni kisha na mimi nikanyanyuka na tukaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango mwengine ambao ni tofauti n mlango tulio ingilia.Katika mlango tulio ingili tukakuta vipande
vya miti vilivyo fungwa tambaa lenye mafuta ya taa vikiwaka huku vikiwa vimechomekwa kwenye sehemu za ukuta wa sehemu hii na kuufaanya mwanga wake kuwa hafifu tofauti namwanga wa taa,Yudia akachomoa kimoja na kutangulia mbele huku akiniomba nimfwate
Tukaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka huku kila wakati nikiwa nitazama nyuma kuangalia kama kuna watu wanao tufwata ila sikuona,Tukaendelea kwenda mbele urefu kidogo nikaanza kusikia kelele za watu wakilia na wasiwasi wangu ukaanza kunitawala
“Eddy usiogope hao ni miongoni mwa watu wanao sadikika kuwa duniani wamekufa ila wapo huku wamehifadhiwa na kila ifikapo mwisho wa wiki wawili huwa hutolewa sadaka ya kuteke-teza”
“Sadaka ya kuteketeza ndio sadaka gani?”
“Yaani wanapelekwa mbele ya Mungu wao ambeye ni yule mzee aliye kuja na yule mwanamke ndio malkia wao”
Tukafika sehemu ambayo tukakuta chumba kikubwa chenye giza kilicho fungwa na gati kubwa huku kukiwa na mnyororo ulio fungwa na kufuli kubwa kiasi kwamba si rahisi kwa mtu kutoka ndani ya chumba hichi.
Yudia akasogea huku akiwa ameshika kipande cha mti kinacho waka na kumulika kwa ndani ya chumba hicho na kujikuta nikiona watu wenye ngozi nyeusi mithili wamepakwa vumbi la mkaa huku wakiwa na nywele ndefu na chafu kiasi kwamba kinawafanya watishe tu kwamuonekano wao wakaanza kunyoosha mikono wakiomba msaada wa kutoka huku wengi wao wakiwa ni wamama na wanaume
“Eddy watu hawa wanateswa sana na laiti baba na mama wakikushika nao watakuleta huku”
“Hawa hawawezi kutoka?”
“Hawawezi kwani hawa huki duniani walipo kuwa walisha zikwa na watu walisha wasahau”
Tukazidi kwenda mbele huku nikijiuliza maswali ni jinsi gani Yudia amekuwa jasiri wa kuweza kuyatambua mambo ambyao ni yakuzimu japo kwa muonekano wake ni binti mdogo sana
“Yudia umeyajuaje haya mambo?”
“Baba na mama walinichagua mimi kuwa miongoni mwa waridhi wao katika kanisa lao kisheta-ni tangu mimi nikiwa mdogo,Kwa mara ya kwanza tulikuwa Marekani basi mama na baba wa-kawa wananifundisha mbinu zao zote ndio maana utaona siwaheshimu kwa maana wana roho mbaya na pele ulipo kuwa ukiona wanawekewa mikono kichwani walikuwa wanapewa nguvu na za ziada za kuweza kukukabili wewe”
“Mmmmm kwani mimi nina nguvu gani ya kuwafanya wao wapewe nguvu ya kunikabili mimi?”
“Eddy wewe kuna watu wanakulinda pasipo wewe mwenyewe kujua kama wanakulinda......Na watu hao ndio wanaokufanya wewe usiletwe huku na ikitokea watu hao wakauwawa basi wewe ndio utakuwa mwisho wa maisha yako kwa duniani na utaletwa huku kwenye shimo la giza na utakuwa ni miongoni mwa wale watu tulio wapiti pele wakiomba msaada”
“Yudia wale watu ulio wasukuma hawata weza kutufwatilia?”
“Wale hawawezi kutokana nimeyapoteza mawazo yao na kwanza walikuwa wamechelewa kwenye ibada na pale wamerudi majumbani mwao na afadhali nimekutana nao mimi na kama wangekutana na baba mwenye au kiongozi yoyote mule ndani ya kanisa leo wangesimulia”
Tuakafika kwenye sehemu yenye vichwa vingi vya watu walio wafiki duniani na mifupa ya miili yao imezagaa kila sehemu ya chumba hichi,Yudia akaokota fuvu moja na kunipa nikishike kipande cha mti kinacho waka moto
“Hili fuvu lilikuwa la msanii mmoja maarufu Tanzania na yeye nyota yake ilikuwa ni kubwa sana ila akishindwa kuiongoza na mwisho wa siku akajikuta akiletwa huku na kutolewa sadaka”
Kila kitu anacho nieleza Yudia kikazidi kunichanganya kiasi kwamba nikajikuta nikikaa kimya pasipo kumuuliza kitu cha aina yoyote.
Tukaondoka sehemu hii na kuzidi kwenda mbele na kutokea sehemu nyenye ngazi tukapanda na kutoka nje na tukatokea kwenye moja ya bustani zilizopo kwenye jumba la mchungaji.
“Eddy kuna pete nitakupa ambayo hawa watu hawata weza kukuona hata yule mkuu wao kwani hii pete ninayo mimi mwenyewe tu na nilipewa kipindi nipo mdogo na mzee ambaye alikuwa ni kiongozi wao kipindi cha nyuma na alitokea kunipenda na kunifundisha mambo mengi”
Tukaingia ndani na moja kwa moja tukapanda gorofani na kabla hatujaingia chumani kwake mlango wa chumba kimoja ukafungulia na akatoka mfanyakazi wa ndani na akaonekana kus-tushwa sana baada ya kutuona,akataka kurudi ndani ila Yudia akamuita na kumgandamiza ukutani kama mtu anayetaka kumpiga msichana wa watu
“Nisikilize wewe OLE WAKO.....OLE WAKO NISIKIE UMEMUAMBIA MTU YOYOTE KUHUSIANA NA HILI TUKIO LA KUINGIA NA EDDY CHUMBANI KWANGU.....UTANIJUA MIMI NI NANI”
Msichana wa kazi akatingisha kichwa akionekana kuelewa onyo hili kisha Yudia akamuachia na msichana wa kazi akarudi ndani kwake kwa haraka kisha mimi na yeye tukaingia ndani kwa Yudia.Chumba cha Yudia kimetawaliwa na mapicha makubwa ya makatuni huku kikiwa kimepangwa vizuri kwa umaridadi wa hali ya juu na kukifanya kiwe vizuri.
Akafungua kwenye droo ya kabati lake na kutoa kisanduku kidogo cha chuma kisha akakifungua kwa namba za siri anazo zijua yeye mwenyewe na kikafunguaka na akatoa pete moja nzuri ya kung’aa sana kisha akanisogelea na kuniomba nimpe mkono wangu wa kushoto kisha akanivisha kwenye kidole cha kati na kwauzuri ikakaa vizuri
“Eddy ninakuomba usiivue hii pete kwa maana siku ukiivua ndio utakuwa mwisho wa maisha yako....na kama unataka kujikinga na kitu kibaya wewe inyooshe mbele na kitu hicho hakita we-za kukudhuru hata wale wanao kutafuta pia hawata weza kukudhuru ikiwemo kina baba na majini wake”
Yudia akanibusu mdomoni kisha akanifungulia mlango wa chumbani kwangu na kuniomba ni-toke.
Nikaelekea chumbani kwangu na sikupata usingizi hadi kukapambazuka na mlango wangu ukagongwa na nikashuka kitandani na kuufungua mlango nikakutana na mama mchungaji akiwa amejifunga matenge yake akionekana ametoka kulala
“Eddy Bwana Yesu asifiwe”
“Amen”
“Umeamka salama?”
“Ndio mama sijui nyinyi mumeamkaje?”
“Salama tu....Chai ipo tayari karibu mezani”
“Asante mama”
Mama mwenye nyumba akaondoka na nikabaki nikimtazama kwa macho ya kujiuliza ni kwanini wanakuwa na roho za ajabu.
Nikafunga mlango wangu na kuingia bafuni na kusimama mbele yak ii kikubwa kilichopo ndani ya bafu hilo,nikafungua maji kwenye bomba na kuanza kunawa uso wangu gafla nyuma yangu kukasimama mtu mwenye sura ya
Kutisha na kunifanya nistuske ila nikaona kama anashangaa shangaa huku akinusa nusa kwenye sehemu niliyo simama na nikagundua hanioni ndio maana ana nusa nusa.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni