TANGA RAHA (37)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
ILIPOISHIA...
“Ina maana huku hakuna watu wanaofika kwenye hii nyumba?”
“Hakuna kwa maana hapa ni katikati ya msitu isitoshe kuna ukuta kubwa umezunguka hili jumba upo mbali sana na hapa hadi kuufikia kwa kutumia miguu ni mwendo wa masaa matatu na nusu hadi mane”
SASA ENDELEA...
“Ehee kumbu ni kukubwa hivyoo?”
“Ahh wee acha tuu wezetu zamani walikuwa na akili sana na hata hii miti yote unayo iona asili-mia 90 ameipanda yeye mingine ni miti ya asili kama ulisha wahi kusoma kuwa kuna misitu ya kutengenezwa huu ni mmoja wapo”
“Ahaa kweli alijitahidi ndio maana nikawa ninashangaa ni kwanini hii miti imepandwa kwa mistari ila nikashindwa kukuuliza tuu”
“Ni yeye jamana alikuwa anaitwa Muller Shostaiger Manzuchuk”
“Ehee kweli hilo jina ni la kijerumani”
“Yaaa”
Tukaendelea kuzunguka maeno ya karibu na jumba lake na baada ya kumaliza tukarudi nyum-bani na kumkuta Rahma akiandaa kifungau kinywaa.
Kutokana na upendo nilio kuwa nao juu yake nikamsaidia kupika piaka anacho kipika,tukaandaa chakula mezani na sote tukajumuika kwa kula.
“Jamani mimi leo nitarudi mjini sasa nyinyi sijui mutakaa kwa kipindi gani huku?”
“Kama wiki hivi?”
“Eddy wiki…….baba yangu sisi tutakaa zaidi ya wiki sitamani kurudi mjini kwa maana ninajua ni lazima baba atakuwa ananitafuta”
“Sasa Sheila tutakaa kwa kipondi gani huku?”
“Kwa muda wowote hadi nichoke mwenyewe ndio nitarudi mjini?”
“Na shule jee?”
“Shule ya kazi gani?”
“Lakini Eddy wewe si mwalimu…..? Utakuwa unamfundisha huku huku mke wako”
“Ahaa jamani haya hapo sina ubishi mumeshinda nyinyi”
“Yeaa kila ninacho kifanya lazima nikishindee”
Raham alizungumza huku akinyanyuka na kuelekea jikoni
“Mmmm mwangu huyo mkwe wangu anavutia sana kwa maana mmmm hongera sana”
“Asante”
“Ila kitu ambacho ninapenda kukuambia usije ukaja kumuacha huyu msicha ua kumsaliyi kwa maana utakuja kupata matatizo makubwa sana utakayo yajutia kwenye maisha yako”
“Mmmm matatizo gani?”
“Hapa hakuna cha kuuliza ni matatizo gani ni wewe tuu kuwa makini na kumlindia penzi lake….Kindi ninamuoa mke wangu nilikuwa ninampenda sana tena sana ila hadi ikafikia hatua ya mimi kumuua ilinilazima kufanya hivyo ili kuondoa dukuduku nauchungu ulio kuwa moyoni mwangu”
“Alikufanyaje?”
“Ni historia ndefu tena sana”
Rahma akarudi na kukaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia na Mzee Ngoda akamtazama sana Rahma kisha akatabasamu na kumalizia na kicheko
“Baba mbona unacheka?”
“Ninacheka kutokana mke wangu alikuwa ni muarabu kama huyu mkwe wangu hapa na tabia za waarabu ninazijua vuzuri kwa maana wazazi wake nao hawakupenda sana mimi nimuoe na kipindi kile ndio ninatoka zangu depo bado kijana mbichi mbichi ninavutia ahaa basi mtoto alidata sana sema wazazi wake baada ya kugundua mimi ni mwanajeshi walipiga sana kelele nikaamua nimtoroshe kinguvu na kuja kumuweka huku msituni hadi alipo pata ujauzito na alipo karibia kuzaa ndio nikamrudisha mjini na akajifungua yule mwanangu wa kwanza na wapekee…..”
“Basi kadri miaka ilivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyozidi kumpenda mke wangu ila kuna kipindi nilichukuliwa na serikali nikapelekwa Cyuba nakumbuka ilikuwani mwaka 1999 na kule nilikaa miaka mitano mbali na yumbani kwangu.Ila nilipo rudi nikamkuta kijana mmoja ambaye alidai kuwa ni mhuhudumu wa ng’ombe…..aaah kuntokana sikuwa na mud asana sikuweza kumfwatilia sana mke wangu ila tabia yake ilianza kubadilika”
“Alibadilikaje?”
“Jamani mimi mwezenu wala sijui hta munazungumzia kitu gani?”
“Subiri nitakuaadisia wakati wa kulala”
“Mmmm jamani mbona munanitenga au mimi sistahili kuielewa story yenu”
“Lakini mpenzi wangu mbona unakatisha utamu hembu tulia kwanza baba amalizie”
“Mwaya mweke ni kwamba story ninayoizungumzia ni kuhusiana na mke wangu ambaye kaburi lake lipo nyuma yah ii nyumba”
“Ina maana baba wewe huna mke?”
“Ndio sina mke kwani alisha kufa siku nyingi sana”
“Ahaa masikini pole baba yangu”
“Asante”
“Alikuf a na nini?”
“Rahma unakatisha utamu wa story hembu nyamaza bwan”
“Kwani nimekuambia wewe Eddy.......hembu litazame lile komo leke”
“Ndilo ulilo nipendea”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha
“Kwa ufupi mke wangu nilimuua kwa kumpiga risasi”
“Haaaa....!!”
“Dawa ya meno hiyo si ulikuwa unataka kujua sasa unashangaa nini.....mwaya baba endelea na story”
“Kwa makelele yenu mumenifanya pia nimesahau ni wapi nilipo ishia?”
“Umeishia pale uliposeme tabia yake ilianza kubadilika”
“Eheee basi kila nilipokuwa nikimuomba chakula cha usiku basi akawa ananinyima kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi lakini kipindi cha nyuma yeye ndio alikuwa anakiomba tena kwamachozi pale nilipo kuwa nimechoka alikuwa akilia kama mtoto”
“Mmmm chakula cha usiku ndio nini baba?”
“Rahmaa ahaa utaniboa sasa”
“Mkwe wangu chakula cha usiku hata wewe jana ninaimani umekila”
“Rahma usijifanye hujui wakati kila kitu unakijua.....watu wamefunga bwana usiropoke mambo mengine si yakuyazungumza”
“Wewe umefunga wakati jikoni ulikuwa ukidokoa dokoa soseji”
Ikanilazimu nimzibe Rahma mdomo kwa kiganja ili mzee Ngoda aendelee na Stori ya ma ishayake
“Basi ile tabia mimi ikaanza kunipa mashaka na mbaya zaidi mwanangu alikuwa bord kwa maana nilimpeleka tangu akiwa chekeche”
“Eddy nikizaa mwangu swala la bord sitaki kulisikia”
“Haya nimekusikia nyamaza”
“Kuna siku nilimuaga mke wangu kuwa ninakwenda Congo kikazi na haikuwa hivyo nikachukua chumba hotelini na kukaa siku mbili bila kutoka njee na siku ya tatu usiku wa manane nikaelekea nyumbani kwangu nikaruka ukuta na kuingia......Sikuingia ndani kabisa ila nikazunguka kwenye chumba cha dirisha ninalo lala.....katika siku nilizo umia moyoni mwangu ni siku ile kwa maana nilimshuhudia mke wangu akishuhulikiwa na yule mtunza ng’ombe tena nilikuta kipindi anapigwa makofi ya makalio na yule mchunga ng’ombe huku akiamrishwa anitukane tusi ambalo hadi kesho naingia kaburini siwezi kulisahau ni lile alililokuwa anaalizungumza kwa sauti ya kejeli.....MUME WANGU NI FALA HAWEZI CHOCHOTE....iliniuma sana”
Rahama akaanza kucheka kichini chini na akashindwa kuvumilia na kuaanza kucheka kwa nguvu na kunifanya na mimi nijikaze kucheka huku nikimuliza Rahma
“Kinacho kuchekesha ni nini sasa....”
Nikajikuta na mimi nikicheka sana hadi nikahisi Mzee Ngoda anaweza akachukia ikanibidi niji-kaze japo sura yangu imejaa tabasamu la kucheka
“Wee acha tuu niliitwa Fala mimi na kuambiwa siwezi kabisa....hilo ni tusi dogo kuna mengine makubwa sana alinitukaa tungekuwa sisi wawili ningekuambia sema huyo mkwe wangu hapo ninalinda heshima yangu”
Rahma akainama chini ya meza kwani kila anapomuangalia Mzee Ngoda anashindwa kukizuia kicheko chake hadi machozi yanamwagika
“Niliondoka zungu huku nikiwa mnyonge sana ila nikaataka kumfanyia kitu kibaya mke wangu ila nikaona nimsamehe na kesho yake asubuhi nikarudi na kumuambia safari imehairish-wa......kutokana ninampenda mke wangu niliamua kumuambia tabia yake ila alikataa kata kata”
“Aaaah kweli hata kama ni mimi ningekuwa mwanaume huyo mwanamke ningemua kwa njia yoyote ile”
“Basi nilifunga kamera za ulinzi za siri siri nyumbani kwangu pasipo kumjulisha mke wangu cha kushangaza sasa wakawa wanaendelea kufanya vitu vyao kama kawaida.....nikaamua na mimi nianze kwenda nje ya ndoa na nikaanza kumfanyia kubuhu nikawa sirudi home nalala siku mbila tatu nje ya nyumba...kumbe na yeye akawa ananifwatilia na kunakitu nilimfanya yule mkata majani hadi kesho huko alipo kama yupo hai nahisi anajutia”
“Ulimfanya nini?”
“Nilimchoma sindano yenye dawa ambayo itamfaya mika yake yote hadi anakufa mashine yake isisimame hata kama anatumia dawa za namna gani haiwezi kusimama”
“Duuu”
“Tena ngoja nikawaonyeshe kaburi lamke wangu muda kidogo umekwenda”
Tukasimama na tukatoka nje na kuzunguka upande wa pili wa nyumba na gafla nikaanza kumuona Rahma akianza kubadilika sura yake baada ya kuiona picha iliyo wekwa juu ya kaburi la mke wa Mzee Ngoda
“Huyu ndio mke wangu ambaye alinifanyia mambo mengi ya ajabu sana”
Rahma akapiga magoti taratibu na kuitazama picha kwa kwa umakini huku akiifuta futa vumbi na mimi nikajikutana nikiikazia jicho kwani picha iliyo kuwepo pale inafanana sana na Olvia Hitler ambaye siku zote ninaamini ni shetani ambaye alikuwa akinifwatilia
“Baba huyu ni mke wako?”
“Ndio na nimezaa naye mtoto yule mmoja”
Nikataka kuuliza jina lake ni nani ila kwenye msalaba ulio tengenezwa ukanipa jina kamili am-balo ni Olvia Abdukarim,kajasho kembamba nikahisi kina nimwagika kwenye uso wangu huku kwa mabali mapigo ya moyo yakienda kasi kiasi
“Huyu dada mimi mbona kama ninamjua”
Rahma alizungumza na kutufanya sote tumtizame na mimi wasiwasi ukazidi kunijaa na kujikuta nikikishindwa hata kuzungumza
“Umemonea wapi?”
“Sikumbuki ni wapi nimemuona ila hata majuzi nilikuwa naye ila sikumbuki ni wapi?”
“Utakuwa umeota huyu mke wangu nilimuua miaka miine ya nyuma”
“Labda watu wanafanana na pia alinielezea mambo mengi sana ila ahaaa siyakumbuki”
Nikamtazama Rahma jinsi anavyo ishika shika picha iliyopo kwenye kaburi hata hamu ya kui-tazama ikaniishia
“Jamani mimi nipo ndani”
Nikaondoka taratibu huku nikiwaacha wakiendelea kuzungumza kuhusiana na maisha ya mke wa Mzee Ngoda,Amani yote ikatoweka moyoni mwangu ila nikaanza kujifariji kimya kimya ku-tokana nina pete mkononi ambayo alinipa Yudia.
Wakaingia na kunikuta nikiwa nimejilaza kwenye kochi na Rahma akajiusha na kunikalia kwenye mapaja yangu
“Tutaumizana bwana”
“Jamani eti baba mimi ninauzito gani?”
“Ahaa nyinyi malizaneni wenyewe.....mimi ngoja niwaache nirudi zangu mjini kati yenu si yupo mwenye simu”
“Yaa mimi ninasimu baba naomba namba yako”
Mzee ngoda na Rahma wakapeana namba kisha akatomba tumsindikize nje na akaingia ndani ya gari lake na kutuahidi atarudi baada ya siku tano kutuletea chakula kwa maanakilichopo kwenye mafriji makubwa yaliyomo ndani kinatutosha kwa siku zaidi ya tano
“Mkwe ukiwa na mhitaji ya chakula utanitumia meseji ni nini unahitaji ili nije nacho”
“Sawa baba wala usijali kwa hilo”
“Eddy mtunze mkwe wangu bwana si unajua nimewafungisha ndoa ya kijeshi”
“Ndio kwa hilo usijali baba yangu”
Nilimjibu mzee ngoda kwa unyonge na akawasha gari na kuondoka,tukarudi ndani huku moyoni nikijutia kwa nini nimekuja
“Eddy mbona huna raha mume wangu?”
“Mbona ninaraha tuu”
“Mmm unaonekana huna raha kabisa kuna kitu nimekuudhi?”
“Hapana baby”
“Ila mbona upo hivyo.....? mimi sipendi bwana”
Rahma akaanza kunitekenya huku akizungumza kwa sauti ya kudeka,nikajikuta nikicheka ila kusema ukweli moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo,kwa bahati mbaya katika kumi-nyana minyana na Rahma nikamkwaruza kwenye mkono
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni