SITOISAHAU FACEBOOK (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 1 Mei 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (9)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa


SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang’ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Nilikuwa wima!!! Mikono kichwani mara kiunoni, wakati mwingine najiziba uso. Mithili ya mwendawazimu.John alidhani nasikitika kwa jinsi alivyonitazama lakini sikuwa katika kusikitika, nilikuwa naogopa sana. Kitambulisho kilichoibiwa si ndio hichi katikati ya maziwa yangu ama!!! La haula!!Ndio hichi kitambulisho cha muuaji. Muuaji mwenyewe si ndio huyu mbele yangu. John ndiye muuaji anayejitafuta mwenyewe.

Mbiombio nikakimbilia chumbani. Sikujiamini tena kuwa mbele ya John. Sikuwa na uwezo wa kumueleza chochote juu ya kitambulisho chake. Kitambulisho kile kilikuwa na utata mkubwa.Nilipokuwa natimua mbio kwenda chumbani, John naye nyuma akanifuata. Muuaji nyuma yangu, lengo langu nifike chumbani niwahi kujifungia mlango. Maziwa yakaruka kwa fujo wakati nakimbia, kitambulisho kikazidiwa ujanja kikakosa pa kujificha. Upesi kikachoropoka.Kitambulisho haramu kikadondoka katika marumaru.Nikasita kuendelea mbele. Sikutaka John akione kile kitambulisho.

Niliweza kusimama nikageuka. John huyo anakuja mbiombio. Macho ya John kwangu. Macho yangu katika kitambulisho kilichokuwa katika marumaru. Kila mmoja na wazo lake.Kitambulisho sasa kikawa katikati yetu. John na mka zake modeli ya ‘wanchoma kumoyo’ akakikanyaga bila kutambua kile kitambulisho wakati ananikimbilia. Kitambulisho ni manira laini sana, kikaisikia kero ya kukanyagwa na bwana John. Zilikuwa zimebaki hatua moja na nusu niweze kukichukua ndipo nikakumbana na wakati mwingine matata ambao nisipousimulia utanilaumu mwisho wa simulizi.

Mi sitaki lawama!!!John akateleza, baada ya kukanyaga kile kitambulisho. Marumaru ikampokea kwa shangwe, kisogo kikatoa mlio kama chuma kilichogongana na chuma kingine. Kitambulisho kikaachana na kile kiatu kikawa mbele yangu.Shida yangu ilikuwa kukiwahi kitambulisho. Sasa kitambulisho kimetulia na John ametulia tuli sakafuni.Mamaaaa!!! Niliita tena, mama mwingine nani sasa zaidi ya mwalimu Nchimbi huko Makambako? Atanisikiaje sasa wakati nipo Mwanza. Ujinga!!

Nikimbie!!! Nilijiuliza huku nikitetemeka.Kwenda wapi sasa?? Ujinga mwingine.Mara damu nzito nyuma ya kisogo cha John. Macho yamefumbwa kistaarabu. Mdomo wazi.Nikahisi kuchanganyikiwa sasa. Damu ikazidi kusambaa katika marumaru ile nyeupe.“Atakufia huyu Isabella shtuka fanya kitu.” Sauti ikaniambia. Sasa hapo nikashtuka, nikainama nikakwapua kitambulisho chenye utata. Nikakimbia nje.

Taksiii!! Nikapiga kelele. Ikasimama, ikaanza kurudi nyuma. Macho ya dereva taksi badala ya kunitazama usoni na kunisikiliza shida yangu, yakawa yananitazama huku mapajani. Nilipojitazama, mbio nyingine mpya kurudi ndani. Nilikuwa nimevaa kinguo kifupi sana. Hakina tofauti na chupi. Kanga iliyokuwa inanisitiri ilikuwa imedondoka huko ndani.Dereva teksi alinisubiri. Nikarejea nikiwa nimeegesha kanga kiunoni.Nina mgonjwa!! Ni mume wangu. Ameanguka!!! Nilimsihi huku nikimvuta. Akanifuata. Tulipofika ndani bado John alikuwa ametulia tuli vilevile.

“Ameanguka!!.” Nilijibu bila kuulizwa. Dereva akafanya jitihada za kumnyanyua John. Wapi haikuwezekana. Kila aliposhikwa ili anyanyuliwe alilegea na kuangukia upande mwingine.Mimi nilikuwa mtazamaji na nilikuwa namuogopa sana John.“Hebu ngoja nakuja!!!.” Aliniaga dereva. Nikaamini anaenda kuleta msaada zaidi. Nikangoja kwa muda fulani dereva hakurudi!! Nilipotoka nje hapakuwa na dereva wala teksi.Nilitamani kupiga kelele. Nikahaha huku na huko. Baada ya robo saa nikaona teksi. Ilikuwa inakuja pale kwangu. Iliposimama alikuwa ni yule dereva. Nyuma yake ikafuatia Ambulance.Wakashuka wataalamu. Wakamtwaa John asiyejitambua.

Bahati nzuri walikuwa wananitambua. Ukarimu ukaongezeka maradufu.John akafikishwa hospitali. Agha Khan.Hakuwa amepasuka sana. Ulikuwa ni mpasuko wa kawaida. Akashonwa. Lakini akatakiwa kupumzika. Fahamu zilimrejea baadaye. Hakuwa msumbufu, alielewa upesi nini kinachoendelea.Siku iliyofuata ndio siku ambayo John alitakiwa kutoka.Nililazimika kurejea nyumbani kuchukua pesa kwa ajili ya malipo. Nikiwa katika teksi, niliwaza juu ya kile kitambulisho. Nikahisi kitaniletea matatizo iwapo nitaendelea kukishikilia, tayari kilitaka kuutwaa uhai wa John. Sasa kitazua mengine.

Sasa nimpatie ama vipi? Nilijiuliza. Sikupata majibu.Ile ndoto ya muuaji anadondosha kitambulisho ilikuwa inanikera maana haikutaka kufutika kabisa. Haikuwa ndoto kama ndoto nyingine maana sasa niliiona sura ya muuaji. Muuaji alikuwa John.Nguvu ya penzi lake ikanikwamisha kumwambia mtu yeyote ukweli huu. Hata yeye pia sikumwambia.“Hichi kitambulisho simpatii.” Niliamua kusimamia upande huo.Wazo la kukitia moto lilikuja baada ya kuwa nimefika nyumbani. Dereva teksi alibaki nje akinisubiri.

Nilikiendea kile kitambulisho nikatoka na mafuta ya taa na kiberiti.Dakika tano baadaye, moshi ulikuwa ukipepea juu, kitambulisho kilikuwa kinateketea. Sikuondoka hadi pale nilipohakikisha natazama na majivu mbele yangu.Hata hayo majivu, niliyakusanya nayo nikayafukia na mchanga.Rasmi nikawa nimekizika kitambulisho!!!Kitambulisho cha muuaji.Baada ya hapo nilifanya usafi kidogo kuondoa zile damu katika marumaru.

Nikiwa ndani ta gari kurudi hospitali walau nilijisikia kuwa nimeutua mzigo mkubwa uliokuwa unanielemea. Mzigo wa kitambulisho.Nilifanya malipo kisha teksi ileile ikaturudisha nyumbani. Mimi na John. Sasa alikuwa anajitambua kabisa. Alitakiwa kupumzika. Na hicho ndicho nilichofanya baada ya kufika nyumbani. Nikamwongoza hadi chumbani akaenda kulala.Mimi nikarejea katika usafi mkubwa sasa sehemu mbalimbali katika nyumba. Redio ilikuwa ikiniliwazana mziki mkubwa niliojaribu kuuimba kwa kukoseakosea.

Na ni redio hiyo hiyo iliyoniziba masikio nisiweze kumsikia mtu amliyeingia ndani bila mimi kujua. Alama za matope katika marumaru zilinishangaza na kujiuliza yametoka wapi.Hakungoja niumize akili yangu sana akanijibu.“Haujambo binti.”Sikumwambia chochote, nikawa namshangaa bado. Akatabasamu.“Haujambo!!!.” Akanisalimia tena, sasa alikuwa analazimisha nijibu.,“We ni nani katika nyumba yangu?.” Nilimuuliza.“Osmani kwani vipi.”Osmani!! Nikaliweka jina katika kumbukumbu kama niliwahi kukutana nalo hapo kabla. Yes!! Niliwahi kukutana nalo. Hata pale chuo tulisoma na akina Osman, wengi tu. Lakini huyu ni Osmani yupi. Nikaendelea kufikiria. Akatabasamu tena kama vile anaisoma akili yangu. Tabasamu lile likanisogeza kwenye jibu, niliwahi kuliona tabasamu hili. Ndotoni!! Hapana.Hoteli, na nilikuwa nimelewa!!! Ndio siku hiyo nililiona.

Si hapo tu, na siku nyingine tena. Lini?Huyu alikuwa ni dereva wa teksi aliyekuwa nami siku ya sakata la kitambulisho. Ni huyu aliyenikumbusha kuwa nimedondosha kitambulisho.“Unataka nini katika nyumba yangu?.” Nilimuuliza nikiwa na hofu.Akatabasamu tena.“Nina mazungumzo na wewe.”“Nitakupigia kelele za mwizi naomba utoke ndani ya nyumba yangu.” Sasa nilifoka. Nikiwa nimesimama wima. Lakini dhahiri nilikuwa katika kutetemeka.Akatabasamu kama kawaida yake. “Kweli unataka niondoke au unatania. Halafu nirudi saa ngapi. Au usiku ndio itakuwa vyema?.” Aliniuliza kwa utulivu kama vile nilikuwa nampa ushirikiano mkubwa kabisa.

Sikumjibu!! Midomo ilikuwa inatetemeka. Sasa wazo la imani za kishirikina likanitawala. Hapa kuna namna.Hapa kuna namna kweli mamaaa weeeee!!! Nilipiga kelele kubwa, kelele haswa. Yule aliyejiita Osman alikuwa amepotea mbele yangu. Alichoacha ni matope yale aliyoingia nayo.Riadha kubwa kuelekea chumbani. Mlango ulikuwa umeegeshwa nikasukuma. Nikamrukia John kitandani nikamkumbatia kama vile tunagombana. Naye akiwa katika usingizi wake akatoa yowe kubwa la hofu. Akanisukuma huko. Nikamrukia tena. Hadi alipokuwa sawa ndipo aliniuliza kulikoni.

Limtu John, limtu!! Nililia.John akanituliza akanishawishi kwamba zile ni ndoto za mchana. Wala sikupoteza muda kukubaliana naye. Ile haikuwa ndoto.Amesema anarudi baadaye John. Nilimkumbusha.“Atanikuta mimi hapa na atakoma kuingia katika nyumba hii usiogope.” Aliongea kiujasiri John. Mimi nimemkumbatia bado.Sikumueleza lolote juu ya huyo Osman. Kwamba niliwahi kukutana naye hotelini nikiwa nimelewa na pia aliwahi kunipatia kitambulisho ambacho kimepotea Iringa.Niliogopa sana kuzua mengine.Nikajikunyata na siri yangu.

Nilikuwa ninaenda na John kila hatua. Siku hiyo. Iwe jikoni, bafuni, na popote pale. Sikutaka kumwachia. Masaa yakahesabika na uoga ukaanza kukimbia.Usiku ukafika. Bado ni mimi na John. John mara nyingi alikuwa ananicheka. Alishangazwa na uoga wangu.Laiti kama angezijua baadhi ya ndoto nilizowahi kuota huenda naye angeogopa ten asana tu!!!.Hii sasa haikuwa ndoto. Nilitamani kubaki kumkumbatia John lakini. Nimuheshimu nani sasa John ambaye hata nyumbani sijamtambulisha kama mchumba ama mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi aliyeniagiza maji ya kunywa. Nikamtazama John nikatamani kumtukana kwa kusababisha nichelewe kuitikia wito. Nikamsukuma huko. Nikajitoa mikononi mwake.

Nikamsonya!! Nikavaa kanga yangu nikafungua mlango nikatoka.Nikaenda hadi lilipo jokofu, nikachukua maji yaliyokuwa katika kopo dogo. Nikachukua na kikombe nikajongea sebuleni.Hapo mama atagomba kweli!!! Nilijishauri.Sasa nilikuwa sebuleni. Mama hayupo.Mwalimu Nchimbi naye kwa kununa. Hapo keshanuna huyo.Nikataka kwenda kumuangaza nje. Lakini sikuona maana hiyo nikataka kumuita, mdomo ukawa mzito sana. Nikageuka huku na huko. Hola!! Nikageuka tena. Hakuna kitu.Nikajisonya!! Kisha nikaguna mwenyewe kuwa ninamtafuta mtu gizani.Mpuuzi kweli mimi!!! Nikasogea ukutani nikaanza kupapasa. Nikakipata kiwashio, nikabonyeza. Waaa!! Pakapendeza.

Nikageuka. Waaaa!!! Mdomo wazi, mtu anakula chakula.Pwaaaa!! Nikaachia kikopo na glasi.Osmani!!!Osmani anakula chakula nilichopika mimi.“Kaa hapo sahivi jamaa si amelala au.” Aliniambia kwa sauti isiyosikika vizuri, alikuwa na pande la nyama mdomoni.Puuuu!! Nikaanguka. Lakini fahamu zipo pamoja nami. Namtazama Osmani.

“John!!!! John!!!” Nilianza kuita kwa sauti ya juu sana. Osman alinitazama akacheka huku akijiziba mdomo. Nikaita tena. Hakuna John aliyetokea kunisaidia.“Amelala wewe acha kelele.” Alinionya Osman ambaye sasa alikuwa amemaliza kula na alikuwa anakunywa maji. Nikamshangaa.Alikuwa ananijibu bila wasiwasi wowote.“Unajua nini Isabela.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni