DHAMANA (29)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alimlaza Jamadin juu ya jeneza kisha akatuamuru kila mmoja amchanje mara sita kwa kutumia kisu alichonacho mkononi, sote tulifanya ambapo Jamadin alitoa ukelele wa maumivu lakini hatukumjali hata kidogo mpaka tulipomaliza kumchanja ndipo tulipoanza kuona ajabu jingine lilitokea katika mwili wa Jamadin baada ya yeye kutanua mdomo apige kelele tulipomaliza kumchanja lakini kelele hazikutoka zaidi ya kutoka mwanga mweupe ulioingia ndani ya chupa.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Mganga aliifunga ile chupa kwa kukaza sana kifuniko halafu akaiweka ile chupa pembeni, alipomtazama Jamadin nasi tulimtazama ndipo tukaona ajabu jingine lililopo kwemye mwili wake ambalo awali hatukuliona. Shingoni mwa Jamadin tuliona amevaa mkufu wenye vito vyenye kuvutia ambavyo hatujawahi kuviona duniani na mpaka hii leo havijawahi kuonekana sehemu yoyote. Mganga aliniamuru niuvue ule mkufu shingoni mwa Jamadin niuvae mimi nami nikafanya hivyohivyo ambapo nilishuhudia maajabu mengine ambayo sikuwahi kuyashuhudia kwani ule mkufu nilipouvaa haukuonekana kifuani mwangu, kitendo cha kuvaa mkufu tu wenzangu wote vifuani mwao kulitokea mwangaza wa kung'aa kisha ukafifia papo hapo tukabaki tukishangaa lakini mganga aliishia kutabasamu tu kisha akatueleza sasa tupo miongoni mwa watu matajiri duniani kutokana na nguvu ya mkufu huo hivyo tujipongeze kwa hilo.
Kauli hiyo ulitufanya wote tufurahi sana kwani ndiyo ulikuwa mwisho wa kuteseka na kasumba iliyotukumba ghafla katika maisha yetu na sasa ni muda wa kufurahia maisha, baada ya hapo ule mwili wa Jamadin tuliuweka ndani ya lile jeneza jeusi na tuliliinfiza shimoni halafu zoezi la kufukia ndiyo lilifuata hadi likaisha. Mganga naye alifanya maajabu yake eneo lile likawa kama halijachimbwa awali wala halikuwa na muonekano wa eneo lililochimbuliwa, baada ya zoezi hilo ndipo tulirudi mjini haraka sana na tulienda hadi kwa minchi tukamuokota Ally kwanj tulijua ni eneo gani ametupwa.
Tulirudi naye nyumbani tukiwa hatuna Jamadin katika mikono yetu na hiyo ndiyo ilikuwa siku ya huzuni kwa Farida kwani alilia sana kutokana na hilo, kazi ya kumbembeleza ikawa kwetu sisi pamoja huku mioyoni mwetu tukitambua wazi tunafanya unafiki kwani tunatambua ni kila kitu. Siku iliyofuata wasamaria wema walileta mwili wa Jamadin uliokotwa Kisosora na walikuwa na asilimia mia kuwa yule ni Jamadin lakini hakuna aliyekuwa anatambua kuwa Jamadin tulishampoteza na tukamzika mpirani, mazishi ya mwili wa ulioletwa yalifanywa huku Farida akiwa na uchungu mwingi sana hadi nikawa namuonea huruma lakini ilishatokea.
Baada ya muda taarifa hiyo ilishasahaulika kidogo ndipo siku moja tukiwa tushaanza kuingia katika mafanikio Ally kwa bahati mbaya alitusikia tukizungumza kuhusu hilo suala tulilolifanya tukiwa na Salma, siku hiyo Ally alitufokea sana lakini niliweza kumdhibiti baada ya ule mkufu kutokea kimaajabu kifuani mwangu kisha ukaachia mionzi yake iliyoenda kumuingia na kuanzia hapo akawa anatusikiliza sisi tu na si mwingine".
Simulizi ya Shafii iliishia ambapo ndiyo simulizi iliyokuwa imemvua nguo zote mbele ya kila mtu hapo ndani kwani ubaya waliouficha sasa uliluwa umeshagundulika, Bi Farida alimtazama Shafii kwa chuki za wazi baada ya kubaini upande wake wa pili wa maisha yake aliouficha kwa kipindi. Hakuna mwingine ambaye aliyekuwa ametarajia kama Shafii angeweza kufanya vile kwa mtoto asiye na hatia kama Jamadin, ilikuwa ni huzuni iliyojaa chuki za wazi baada ya kila mmoja kubaini uovu uliokuwa ukifanywa na Shafii kwa takribani miaka ishirini na sita iliyopita. Baada ya simulizi hiyo hata Mzee Mahmud aliyekuwa akiitambua simulizi hiyo alisikitika pia kila akimtazama Shafii kwani alijua alikuwa amefanya janga kubwa tofauti na yeye alivyokuwa anadhani, alibaki akimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akajikohoza ili kusafisha koo lake apate kuongea bila sauti yake kukwaruza.
"Shafii hivi unajua ni kitu ulichokifanya mpaka dhahama hii inawakumba wenzako na hadi sasa mliousuka mpango huo mmebaki wewe na Salma tu kwani mliyemkosea tayari ameshawapoteza Falzal, Hassan na Hamis. Kwanini lakini unafanya mashindano na kiumbe usiyemjua Shafii?" Mzee Mahmud alilalamika kisha akamtupia jicho Zalabain halsfu akamnyooshea kidole akasema, "umemuona huyu aliyeingia na Farida na Zayina? Ulijua utamuua siyo mlipouchimbia mwili wake hapa tulipokaa? Huyo ndiye Jamadin mwenyewe na hakufa kama mnavyofikiria, na ile chupa iliyofungiwa kitu kilichokuwa kinatoka mdomoni mwake ilifunguliwa na huu mwili mliofukia ukatolewa akarudi kama awali.
Hivi we mtoto unamjua ni nani huyu uliyekuwa unamfanyia ubaya huo? Loh! Nakuonea huruma sana kwa ujinga wako ulioufanya mwanangu.... Jamani ngoja nimkaribishe mgeni mwingine ambaye sikuwaambia kama atakuwepo katika eneo hili aje awaeleze kuhusu asili ya Jamadin. Mzee Mubaraka karibu tafadhali" Mzee Mahmud alimlaumu sana Shafii kwa kitu alichokifanya na alitumia muda huo kumtambulisha Jamadin ambaye anajulikana alikufa mbele ya wote hapo ambapo wengine walishtuka sana walipolijua hilo, alitumia fursa hiyo kumkaribisha mgeni mwingine ambaye anajulikana hapo kama baba yake Faimu aliyekuwa lulu kwa warembo wa miaka mingi iliyopita ambao sasa hivi warembo hao walikuwa kina mama wanaoukimbilia uzee.
Ukaribisho wa Mzee Mahmud ulifafanya watu waangalie mlangoni ambapo walimuona mzee wa kiarabu mwenye ndevu nyingi aliyevalia kanzu safi ya rangi nyekundu na kofia akiingia ndani humo, alionekana ni mzee hasa lakini hapo alikuwa alitembea vizuri kama kijana wa kawaida tofauti na watu wengine waliomzoea. Mzee huyu hakuwa mwingine bali ni mzee Mubaraka ambaye baada tu ya kuingia alitoa salamu kwa wote na kupelekea kidevu chake kilichobeba ndevu nyrupe zilizosimama kama mwiba kicheze baada ya kinywa chake kufunguka. Salamu yake iliitikiwana watu wote na mzee huyu alienda moja kwa moja hadi kwa Zalabain akatoa salamu ya heshima kama wafanyavyo vijakazi wakifika kwa watukufu wa familia ya kifalme, salamu hiyo iliwashangaza sana watu wote kwani hawakuelewa kwanini mzee huyo alisalimia kwa salamu hiyo.
Iloonekana ni babu na mjukuu wake kwa jinsi walivyofanana lakini kusalimia kwa namna ile ndiyo kuliwapa swali jingine lisilo na libu katika vichwa vya watu wote waliopo eneo hilo, Mzee Mubaraka hakujali mishangao iliyowapata waliomo humo ndani yeye alienda kuketi jirani na mzee Mahmud.
"Naam mzee Mubaraka najua watambua suala lote uliloitiwa hapa sasa naomba ueleze asili yake jina lako na asili ya Faimu pamoja na Jamadin na vingine vyote" Mzee Mahmud aliongea huku akimtazama Mzee Mubaraka usoni ambaye alitikisa kichwa kuashiria amekubaliana naye.
Mzee Mubaraka alipopewa ruhusa hiyo aliwatazama wote waliopo humo ndani kisha akasema, "kwa jina naitwa Mubaraka bin Yaktwash ni jini niliyezaliwa katika himaya ya majini ya Majichungu". Alikatisha kidogo kusimulia kisha akawatazama waliopo mule ndani ambapo wengine walionesha kushtuka kusikia taarifa hiyo, hakuwajali mshtuko wao na aliendelea, "Nimezaliwa miaka elfu mbili iliyopita katika himaya hiyo na nilipoanza kuwa kijana nilianza kufanya kazi nikiwa kama mtumishi wa ndani ya kasri la mfalme Zulain, nikiwa nina miaka mia tano tangu nizaliwe katika alizaliwa mtoto wa pekee wa mfalme wetu mtukufu aliyeitwa Zaif.
Mtoto huyo nilikabidhiwa kuwa msaidizi wake hadi anakua mkubwa na alikuwa ni mtoto mwenye kupendwa sana na wanamajini wote wa himaya hiyo kwani alionekana aliwa mwerevu tangu yupo mdogo, Nilikuwa mlezi na msaidizi wake kwa muda wa miaka mingi sana hadi alipotimiza miaka elfu na mia tano mimi nikiwa nina miaka elfu mbili. Zaif kwa kipindi hicho alimuaga baba yake anakuja kufanya matembezi duniani na kukaa kwa muda kidogo ili aweze kuyaona maisha ya wanadamu yalivyo, alikubaliwa na baba yake kwa mikono miwili na akapewa angalizo la kuwa makini na wanadamu kwani siyo viumbe wazuri.
Alikabidhiwa watumishi wawili na mmojawapo akiwa ni mimi na mwingine ni jini wa kike mwenye taaluma ya upishi katika kasri la mfalme, wote kwa pamoja tuliingia duniani kama wasafiri na tulifikia kijiji cha Bwagamacho ambapo nilijitambulisha kama Mubaraka na yule jini wa kike nilimtambulisha kama mke wangu na mtoto wa mfalme wetu mtakatifu nilimtambulisha kwa jina la Faimu nikimtaja ni mtoto wangu wa kumzaa.
Tuliyaanza maisha yetu ya happ kijijini karibu kila mwanakijiji akidhani sisi ni wanadamu tena wa familia moja kasoro Mzee Mahmud hapa ndiye aliyeweza kubaini sisi ni majini ila hakuwa na neno na sisi baada ya kutubaini hatukuja kwa nia mbaya eneo hilo, maisha yetu yaliendele kwa amani hapo kijijini ambapo Faimu akiwa nje ya nyumba alikuwa akitupa heshima kama wazazi wake ila tulipokuwa ndani mbali na upeo wa mwanadamu yeyote tulikuwa tulimpa heshima kama mwana wa mfalme wetu mtukufu.
Hadi Faimu anaanza kupendwa na wasichana hapo kijijini tayari tulikuwa tumeshabaini hilo suala na walipokuja kujitolea kufanya kazi tulikuwa tukiwacheka sana wanadamu kwa jinsi walivyo na papara ya kupenda tu, kwa Faimu ilikuwa ni burudani tu kwani alikuwa anajifunza mengi jinsi binadamu alivyo ambavyo yeye alikuwa hawajui zaidi ya kuwasikia. Aliishi maisha ya kibinadamu tu na alikuwa akiona fahari sana kubadilishana mawazo na wanadamu ingawa wa rika lake wengi walikuwa wanamchukia, hata alipokuwa na urafiki wa pamoja kati yake na wanawadamu ambao ni Shafii na Hamis alikuwa akifurahi sana hata siri walizokuwa wakizificha aliluwa akizijua sana.
Kipindi hicho alishajua uwepo wa Farida kwa kutumia nguvu zake za kijini na alimpenda sana ingawa alitaka ajithibitishie kama anapendwa na hakuwa tayari kutumia uwezo wake kumuingilia na kumshawishi, alikuwa akitusimulia sisi watumishi wake ambao alitufanya kama washauri wake wakuu. Nasi tulimshauri asitumie nguvu bali ahakikishe anapendwa naye na kama hapendwi aache, ushauri huo alioufuata na akasubiria ziku ya kuonanana na Farida hadi ilipowadia. Hakumlazimisha Farida kuwa na mapenzi bali alikubali kwa hiyari na uhusiano ukaanza, huku huyu Ally akiwa mtu wa kwanza kubaini kwani ndiye aliyekuwa akipendwa hasa na Faimu kati ya wanadamu wote hapo kijijini.
Uhusiano wake ulipovurugwa alionekana ni jinsi gani ameuzwa lakini hakutaka kutumia nguvu zake kabisa na aliishia kumuomba penzi Farida kisimani akaambiwa anataka kubaka akapigwa sana akionekana hafai mwishowe akaondoka hapo kijijini baada ya kufukuzwa na hakuwa tayari kutumia nguvu zake na hata mtukufu mfalme aliposikia alitaka kuwaangamiza wanadamu hao lakini kwa huruma ya mwanae akawaacha.
Jambo ambalo wanadamu hawa hawakulitambua ni kwamba dawa waliyompa Farida kila siku usiku ilikuwa inapunguzwa na Faimu na hapo Farida hurudi katika akili na hukutana kimwili na Faimu kwa kipindi hicho chote huwa alikuwa anamjia kwa njia ya ndoto, hadi huyu bwana hapa anamposa Farida baada ya kumuweka chini yake kwa kutumia nguvu za kichawi tayari huo mchezo Faimu alikuwa anaendelea na ndiyo katika kipindi hicho akawa anamuona anaweweseka na hata alipokuja kuacha tayari Farida alikuwa ana ujauzito wa Faimu huyu bwana akidhani ni wake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni