Notifications
  • MY DIARY (9)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TISATULIPOISHIA...Basi Dj wangu aliendelea na mautundu yake akaniwekea mambo ya pwani na hapo ndipo uvumilivu ulipomshinda akaja kunibambia na mimi sikuona haja ya kumbania kwa kuwa ni mali zake mwenyewe. Nilizungusha nyonga na kiuno mpaka nikachoka nikajitupa kitandani ili nipumzike. Nafsi yake ilikuwa imeridhika kwani hakutka tena penzi bali alichukua lap top yake na kuanza kunionesha picha na vitu vingine ambavyo vilinipa raha.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (8)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Sijui hata haya maneno yalitoka wapi, fahamu zilinitoka na Ticha aliamua kuninyanyasa maana nilishajikojolea zaidi ya mara tano. Basi na yeye kwa kutafuta mbwembwe alianza yale mambo yao ya katerero, siunajua tena mwalimu John alitokea pande za Bukoba.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinichezea sana na baadaye nilishangaa kukuta jamaa ameshaingiza kunako. Sikujielewa kwa…
  • MY DIARY (7)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SABATULIPOISHIA...Kwaito zilivyonoga uzalendo ulinishinda nikajikuta na mimi nashuka ngazi kuelekea chini sehemu ya kuchezea.Nilizijua kwani shuleni tulikuwa tunazicheza sana hasa kwenye yale madisco yetu ya mwisho wa mwezi.John wangu alibaki juuu akiniangalia jinsi nilivyokuwa nikicheza vizuri.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Yeye alishindwa kushuka akiofika kile kitu kukaliwa na watu…
  • MY DIARY (6)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SITATULIPOISHIA...Akanambia kuwa wamemwambia wapo East Africa Pub na tayari wamaeshaagiza mkuu wa mbuzi. Mmmmhhhh kusikia mguu wa mbuzi mate yalinijaa mdomoni. Basi kwa harakaharaka nikamwambia naomba niende niende nyumbani nikachukue viwalo vya club kisha nitawakuta hapo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinambia mbona hizo nguo ulizofaa zipo poa tu wewe twende hivyo bhana si upo na…
  • MY DIARY (5)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TANOTULIPOISHIA...Akanisimamisha na kuanza kuiuliza maswali mengi yasiyo na maana huko akionekana kutojiamini. “samahani dada, sijui unaelekea wapi”? Nikamjibu dukani. Akavuta pumzi ndefu na kuniambia ok, nisaidie namba zako za simu. Nikamwangalia juu na chini nikwambaia nimezisahau na simu nimeiacha ndani nikirudi ndani nitakuletea..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Akaishiwa pozi akanambia,…
  • MY DIARY (4)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA NNETULIPOISHIA...Uchambuzi huu ulinigusa sana kwani hata mimi nilijihisi kuwa sikuwa na utando huo yaani bikira japo nilikuwa sijawahi kujamiana na mwanaume wa aina yeyote zaidi ya ile michezo ya utotoni ya kula mbakishie baba au ile ya kibabababa na kimamamama. Alianza kunishika mapajani na kunifanya nianze kusisimuka ajabu kwani japo alikuwa ni mwanaume mikono yake likuwa ni milani sana kama ya mtoto wa kike.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media…
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…

DHAMANA (11)

Jina: DHAMANA

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TULIPOISHIA...
"Baada ya yeye kuwapandisha majini wake kwenye kichwa chake niliamua kumkaba shingo yake hadi yakafa yote kisha nikampiga kofi moja yule mwenzake aliyetaka kuchochea kuharibika kwa kazi yako kwa kuleta udi unaowaka" Kainun alieleza kila kitu alichokifanya hadi Zalabain akatabasamu huku akitikisa kichwa kuashiria amependezwa na kazi yake.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"Vizuri sana kwa kumtandika kibao huyo Ally Buruhan maana anafuata mkumbo tu" Zalabain aliongea.

"Kainun napenda asipewe kazi nyingine hadi hali itulie maana majini aliowanyonga ni watoto wa mganga Sharkar aliyeuawa na kaka yangu Saliim miaka mia moja na ushee kupita baada ya kristo kuondoka, kwa mujibu wa maono yangu hao vifo hivyo tayari vishagundulika kwa ukoo wa Sharkar sasa huyu kumuachia kazi nyingine itakayomlazimu kutoka nje ya himaya hii ni sawa na kumkaribisha na vita na kifo chake" Salmin aliongea baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tena macho yake yakibadilika rangi yakawa yanawaka kama ya paka.

Zalabain aliposikia maelezo hayo akatulia akajifikiria kwani hakuwa na mwingine mwenye kuaminika na kutumwa katika kazi zake miongoni mwa majini wote wa himaya hiyo isipokuwa Kainun na ndiyo huyu ameambiwa asimtumie na jini mwenye nguvu zaidi na mwenye kuona yajayo. Himaya hiyo kuna baadhi ya watumishi walikuwa sio wa kuaminika kutokana na kuwa miongoni mwa wafuasi wa waziri kkuu aliyetaka kupata ufalme kwa hila sana, alipoambiwa asimtumie Kainun kwake lilikuwa ni jambo jingine gumu kwake.

"Hapo unanipa wakati mgumu sasa, watumishi hawa sio wa kuaminika huenda kuna wengine ni wafuasi wa aliyekuwa waziri mkuu aliyefungwa katika gereza la giza. Sina wa kuaminika atakayekuwa akisaidia kuzuia kazi yangu isiharibike zaidi ya huyu tu" Zalabain aliongea.

"Usisononeke Zalabain nadhani yupo jini mwingine mwenye msaada mkubwa kwako kama Kainun na naamini atakufaa kuzuia watu na viumbe wasiohusika wasiharibu kazi yako" Salmin alimuambia Zalabain kwa utulivu.

"unafikiri nani atakayeweza kuwa mbadala wa Kainun?" Zalabain aliuliza.

"Baada ya mimi na pacha wangu Saluim kuzaliwa katika kasri la mfalme Mukhatar wa bara Arabu kuna jini mmoja alinieleza kuhusu asili na chanzo cha kufanya mambo yasiyofanywa na binadamu wa kawaida. Jini huyu alinieleza kuhusu asili yangu mimi ni jini na niliyezaliwa na mwanamke wa kibinadamu ila baba yangu ni jini huyu Ibin Zultash na sio mfalme Mukhtar kama nilivyoelezwa wakati nikiwa mdogo na mama yangu ambaye alikuwa Malkia wa himaya baada kifo cha mfalme Mukhtar.

Jini huyu ndiye aliyemuelekeza kaka yangu akaenda kwa mganga wa kijini Sharkar akaongezewe nguvu, baada ya kaka yangu kuongezewa nguvu alikosea sharti akanywa damu aliyoambiwa asinywe na hapo akawa muangamizi akaangamiza himaya ya mama yetu na akataka kumuangamiza huyu jini ambaye aliamua kujisalimisha nyumbani kwao ambapo ndiyo hapa Majichungu. Nilipopambana na kaka yangu kwa msaada ya mganga Zaid wa bara Arabu nilifanikiwa kumshinda kaka yangu na nikamfungia kwenye sanduku nikaja kulifukia h Afrika kipindi hicho ni pori tu kwani ilikuwa imepita miaka 100 tu tangu Kristo aondoke duniani

Baada ya kazi hiyo niliwachukua Zaid na mama yangu tukaja kuishi huku na tukapokelewa na babu yako kipindi hicho bado ni kjana mdogo wa miaka arobaini hivi. Jini huyo alipokuja huku akifungiwa katika gereza la giza na hakuwahi kutoka hadi leo hii ninavyokusimulia habari hii, huyo ndiyo jini pekee kwa mujibu wa maono yangu anaweza akakaimu nafasi ya Kainun" Salmin alisimulia kisa cha MUANGAMIZI kisha akamtajia jini mwingine mwenye kuaminika.

****

"je naweza kulijua jina lake huyo kiumbe?" Zalabain aliuliza.

"usiseme unaweza bali ni wajibu wako kumjua anaitwa Maalun nadhani ukimpa uhuru atakaimu nafasi ya Kainun... Kainun utaendelea kuwa mkuu wa majeshi ya angani kama ilivyokuwa awali" Salmin aliongea kisha akamtazama Zalabain usoni, Zalabain alipotazamwa hivyo alipiga kofi mara na viumbe wa ajabu wakatokea mbele yake wakiwa na mavazi yanayofanana.

"Ndiyo mtukufu tumeitikia wito wako" Wale viumbe waliongea kwa utiifu wakipiga goti moja mbele ya Zalabain.

"nahitaji nimuone Maalun hapa akiwa ametolewa gereza la giza ndani ya sekunde tatu tu" Zalabain aliongea na wale viumbe walipotea kisha wakarejea wakiwa wamemkamata Maalun aliyeonekana kuwa mnyonge sana.

"muwekeni kwenye kiti na nyinyi muondoke haraka sana" Zalabain na wake viumbe wakakuweka Maalun kwenye kiti wakapotea.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Maalun kuwa huru baada ya kufungea gerezani kwa muda wa miaka takribani 2000 kutokana kuisaliti himaya hiyo na kwenda kuishi kwenye ardhi ya wanadamu, alipoona wale majini waliomleta wamepotea alianza kuwatazama wote waliobaki ambapo hakumtambua Zalabain wala Kainun. Yeye alimtambua Salmin tu na hapo akamuangukia miguuni akaanza kuonesha kuomba msamaha.

"Maalun yaliyopita na pia kuongelewa kwake kumepita, kosa ulilotenda milenia mbili zilizopita nishakusamehe cha msingi inabidi tuangalie liliopo hapa" Salmin aliongea na wote wakaafiki kwa kichwa, kauli hiyo ilimfanya Maalun atabasamu na apotee ghafla alipokuwa ameamuangukia na akatokea kwenye kiti kimojawapo kilichopo hapo walipo wenzake.

"Oooh! Namshukuru mungu kumbe nguvu bado zipo, haya nawasikiliza" Maalun aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu kisha macho yake yakaweka kituo kwa Zalabain halafu akamwambia " nakusikiliza ewe mtukufu"

Zalabain alianza kumueleza Maalun kila kitu hadi majukumu aliyotakiwa kuyafanya, maelezo yalipofikia mwisho wote walimtazama Maalun wakisubiri kusikia uamuzi wake.

"Kwa ajili ya kuokoa himaya hii isiteketee kwa kukosa mfalme anayestahiki nipo tayari kwa kazi yako ewe mtukufu na hata ungeniambia nikusaidie kuwaangamiza nipo tayari" Maalun alikubali na wote wakatabasamu.

"vizuri Maalun na anza kazi yako kuanzia sasa, yeyote atakayeingilia kazi ya mfalme mtarajiwa wewe mzuie ashindwe kuendelea kabisa na si kuua maana utamuharibia kazi Mfalme wetu mtarajiwa" Salmin aliongezea kisha akasimama akapotea na wote waliosalia wakatoka ndani ya chumba cha siri.

****

Upande wa ardhi ya binadamu kwa muda huo ndiyo muda ambao Shafii alifanikiwa kufika katika hospitali yake akapewa tiba ya majeraha yaliyompata na kushonwa usoni alipopasuka kutokana na kujigonga alipoona tukio la Mganga Sauti ya Radi akiuawa na Zalabain, alipomaliza kutibiwa ndipo alipopokea taarifa ya kulazwa kwa mdogo wake katika hospitali hiyohiyo upande wa wagonjwa mahututi.

Taarifa hiyo ilimfanya atoke sehemu aliyokuwa anatibiwa baada ya kumaliza tu kushonwa vidonda vyake akaelekea mahali zilipo wodi za wagonjwa mahututi wa hospitali hiyo iliyopo chini ya kampuni yake, alipokaribia katika mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi alimuona Hamisi akiwa amekaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akiwa amejiinamia. Shafii alimfuata upesi kisha akamuuliza. "Shemeji kuna nini kimemkuta Ally" Shafuu aliuliza huku akimtazama Hamisi ambaye naye aliishia kumshangaa kutokana na plasta alizonazo usoni pamoja na michubuko kadhaa.

"Aisee! Shemeji we acha tu. Hii ni vita kali na Ally amekumbwa na kadhia ya kupigwa na kiumbe kisichoonekana na mimi majini yangu yote yameuawa " Hamisi aliongea kwa masononeko.

"Vipi hali yake ipoje huko wodini?% Shafii aliuliza.

"bado madakatari wanafanya kazi yao, na wewe vipi mbona maplasta mengi usoni? Umepata ajali? Hamisi alimuekeza Shafii kisha akamuuliza kilichomsibu hadi akawa na plasta nyingi usoni.

"Yaani shemeji ni bora ingekuwa ajali ingekuwa afadhali kuhusu kisanga kilichonikuta huko kwa Sauti ya Radi, yeye mwenyewe ni mfu hadi muda huu" Shafii aliongea akioneksna anakaribia kukata tamaa kabisa

"hivi huyu anayeiangamiza familia yangu nimemfanya nini? Au uadui wa kibiashara, yaani Ally mdogo wangu hata kuoa hajaoa ndiyo kwanza anajijenga kimaisha yeye aje kumfanyia hivi kweli. Sikubali hata kidogo nitapambana kulipa kisasi cha hawa wadogo zangu" Shafii aliongea huku machozi yakimtoka kwa uchungu alionao.

"Shemeji nafikiri hii vita tutakuwa wote katika kukomboa familia zetu, waite Hassan, Yusuf na Halid waje watuongezee nguvu" Hamisi alimuambia Shafii, muda huohuo mlango wa wodi ulifunguliwa na daktari akatoka akiwa anaelekea ofisini kwake. Wote walipomuona walimkimbilia wakawa wanamuuliza ju ya hali ya Ally lakini dakari aliwasihi waende naye ofisi, wote walitii wakaelekea hadi katika ofisi ya Daktari huyo na walipofika wakaribishwa katika viti. Shafii na Hamis walikaa wakawa wanaamuangalia Daktari ili wapewe raarifa za Ally kimatibabu.

"Mgonjwa anaendelea vizuri kwa sasa ingawa bado hajarejewa na fahamu, tatizo kubwa alilolipata mgonjwa wenu ni kuvunjika kwa taya yake kwani inanekana alipigwa na kitu kizito shavuni na kupelekea damu zivuje sikioni pia ikionekana hata sikio lake limepatwa ingawa bado haijathibishwa na E.N.T surgery wa hapa hospitali. Kwa sasa tumempatia matibabu kwa ajili ya taya lake na baadaye mtaalam wa E.N.T atakuja kucheki sikio lake. Ni hayo tu bosi" Daktari aliongea kwa kirefu juu ya tatizo lililomkuta Ally, maelezo hayo yalimsikitisha sana Shafii na akajikuta anapandwa na hasira zaidi hadi machozi yakawa na yanamtoka.

"Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Na bado tu huo ni mwanzo tu ila kwa sasa naomba utambue binti yako wa pekee yupo katika himaya yangu" Mwangwi wa sauti ya Zalabain ulivuma katika masikio ya Shafii na kumfanya ashtuke sana hadi Hamisi na Daktari wakamshangaa.

"shemeji kuna nini?" Hamisi alimuuliza Shafii baada ya kumuona alivyoshtuka na sasa alikuwa anaangalia dari la ofisi hiyo ya Daktari kama ndiyo kwanza analiona kutokana na sauti hiyo iliyomjia masikioni mwake ikitokea huko darini.

"Ohoo! Zaina, Zaina mwanangu" Shafii aliropoka kisha akatoka mbio huko ofisini kwa daktari hadi Hamisi naye ustahimilivu ukamshinda ikabidi amkimbize shemeji yake, Daktari naye alijitahidi kukimbia kwa uwezo wake wote ili amuwahi Shafii. Wote kwa pamoja mbio zao hazikuzaa matunda katika kumkamata Shafii aliyeonekana amechanganyikiwa kwani aliingia kwenye gari yake aina ya Cadillac akaiwasha bila hata kumuambia dereva wake aliyekuwa yupo pembeni katika mti akiwa amepumzika

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
58 Dhamana Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni