HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (3)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Msichana mrembo wa sura, mwenye rangi mororo ya kuvutia alikaribia eneo lile aliloketi Seidon, mwendo wake wa kunesa ulianza kuusumbua moyo wa Seidon, shujaa wa Relvesh ‘njiani usitamani mwanamke wala kulala nae’, kauli hii ya babu yake ilimkosesha raha kila alipoikumbuka.
TUENDELEE...
Aliendelea kumkodolea macho kiumbe yule ambaye sasa alikuwa kasimama umbali wa kurusha jiwe tu, alimtazama kuanzia macho mapaka miguu na kuridhika na uzuri wake, Seidon akajikuta hali yake inakuwa mbaya, mate ya utu uzima yakamtoka. Msichana yule alimsogelea Seidon na kumshika mkono akamuinua.
“Ewe mpiga mbio, mpanda farasi hodari, kwa nini wateseka hapa ilhali nyumba na wenyeji wa kukukarimu tupo?! Ondoa kongwa lako, njoo upumzike mahali salama” msichana yule alitumia lugha laini na nyepesi kumshawishi Seidon kwa hila hiyo. Seidon alisahau wosia wa babu yake aliinuka taratibu na kumfuata msichana yule.
Seidon alijikuta katika ukumbi mkubwa wenye harufu nzuri za kuvutia, udi uliozungushwa kila kona ya nyumba hiyo uliijaza kwa moshi, zuria lenye manyoya safi ya sufu, nakshi za kiajemi, matunda ya kila aina yalijaa mezani. Kwa hatua za kujivuta Seidon alitembea juu ya zuria lile akitanguliwa na msichana yule ambaye sasa alikuwa amezifungua nywele zake na urefu wake ulifika kiunoni, akiwa anatembea huku anawasha udi ambao ulikuwa bado kuwashwa, alikuwa akiongea maneno kwa lugha ya Kiajemi, Seidon hakuelewa chochote katika hayo.
“Unaitwa nani?” Seidon alivunja ukimya kwake baada ya kupaliwa na ule moshi wa udi
“Sherhazad binti Sahib” alijibu yule msichana.
“Nyumba hii yote unaishi peke yako?”
“Ooooh, mpiga mbio, niambie kwanza unaitwa nani.” Badala ya kumpa jibu lake; alimgeukia na kumshika mabegani kabla ya kumuuliza swali hilo.
“Sei…”
“Seidon!” yule msichana alimalizia jina hilo kala Seidon hajamaliza. Seidon alijiuliza imekuwa hata akajua jina lake na kulimalizia, “Umejuaje, hata ukamalizia jina langu?”
“Bwana wangu, Seidon!” Sherhazad alipiga magoti na kubusu kiganja cha Seidon, kisha akainua uso wake kumwangalia Seidon usoni ambapo Seidon, mono mmoja ukiwa kiunoni na mwingine umeshikwa na Sherhazad, “Nilikuona tangu ukitoka Relvesh kupitia njia ya maghalibi, watu wangu walikusindikiza kwa sababu tunajua nini unatakiwa kufanya.”
Seidon, alitafakari kwa sekunde kadhaa, akakumbuka kuwa alivyokuwa akija hakuona mtu yeyote kumfuata. Aliinua uso wake kutoka kwa Sherhazad na macho yake moja kwa moja yakaangukia ukutani, picha kubwa ya mtu aliyepanda farasi akiwa ameuvuta uta wake kana kwamba analenga mtu au kitu iliupamba ukuta huo na kuyavutia macho ya Seidon.
“Mimi ni Malkia wa Soria, nilikuwa nakusubiri hapa muda mrefu, nilijua kuwa siku moja utapita tu. Sikiliza, Seidon, nitakupa kila utakacho hata nusu ya tawala yangu iwe chini yako ukinitimizia jambo moja tu.”
“Jambo gani, Sherhazad?” Seidon aliuliza kwa shauku
“Nijibu kwanza kama utafanya hivyo nami nitakwambia ni jambo gani.”
Seidon alitafakari, hakupata jibu ‘majaribu’, alijiwazia, “Naahidi, ee Malkia uliyetukuka kutoka Soria”
Sherhazad, Malkia wa Soria alitembea taratibu akimuacha nyuma Seidon, moja kwa moja akaelekea kunako ile picha kubwa “Huyu anaitwa Orion, muindaji maarufu kutoka Misri, shabaha yake haina makosa, pigo lake halina huruma. Daima huonekana wazi majira ya mwisho wa mwaka, usiku wa giza nene, usio na mawingu. Kamwe huwezi kupambana nae, kwa maana wengi hata sasa wanasubiri, kwa kuwa wanashindwa kupambana nae. Wewe u peke yako, wenzako wapo jeshi lakini Orion amewadhibiti.
Bwana wangu, utakapolipata fuvu la Cleopas, niletee hapa nami nitakutimizia ahadi yangu kwani kwa Muungwana ahadi ni deni”, Sherhazad aligeuka na kumtazama Seidon. Seidon alitikisa kichwa kama ishara ya kutokubaliana na Sherhazad, alikumbuka wosia wa babu yake kuwa asitamani wala kulala na mwanamke katika safari yake hiyo. Sherhazad alimsogelea Seidon na kumuwekea mikono yake mabegani, sasa walikuwa wakitazamana, Seidon aliangali chini kwa aibu, Sherhazad akamvutia kwake na kukutanisha kifua chake na cha Seidon, Seidon alihisi kitu ambacho hakuwahi kukihisi kabla katika maisha yake, chuchu zilizochongoka za Sherhazad zilizojaa sawa sawa japo zilifunikwa kwa nguo ya hariri zilimchoma Seidon hata akaishiwa nguvu, alihisi kama ganzi kuanzia kifuani kwake mpaka katika nyayo za miguu yake.
Sherhazad alimuweka kichwa chake vizuri na kukutanisha midomo yake na ya Seidon, ulimi wa moto wa Sherhazad ulipenya kinywani mwa Seidon ukazungukazunguka ndani humo na kumpa Seidon ladha ya ajabu, alisahau kila kitu, alisahau kama ana safari ngumu inayomkabili mbele yake, alijikuta mikono yake ikikikamata kwa nguvu kiuno chembamba cha Sherhazad, ikikivuta karibu na chake.
“Subiri kidogo, mbona una haraka?” Sherhazad, alimwambia Seidon huku akijitoa katika himaya yake, akamuoneshea ishara ya kidole ya kumkatalia jambo hilo, huku akirudi nyuma. Seidon alibaki kumtazama, midomo yake bado ikiwa wazi kiasi, Punjabi alilovaa lilikuwa limetuna kwa mbele chini kidogo ya kitovu likiashiria shughuli, alivuta hatua chache kumfuata Sherhazad ambaye bado alikuwa akirudi kinyumenyume “Timiza nililokuomba utapata vyote” alimwambia Seidon.
“Nitakutimizia, nitakuletea fuvu hilo siku kama hii na muda kama huu” Seidon alimjibu Sherhazad.
“Nenda, kakamilishe kazi yako kisha urudi hapa na fuvu, nami nitakutimizia niliyokuahidi hapa hapa” Sherhazad sasa aliongea kwa amri kidogo. Seidon aliinamisha kichwa kama ishara ya heshima kwa msichana huyu ambaye sasa alikuwa ameketi juu ya kiti chake cha enzi, kiti kikubwa kilichowekwa nakshi za dhahabu na kufanya urembo mzuri wa kihindu na kiajemi.
“Sawa Malkia mtukufu wa Soria” Seidon alivaa kofia yake na kuuweka upanga wake vizuri kiunoni, alirudi kinyumenyume kama hatua saba na kuinamisha kichwa chake tena, akageuka na kuondoka.
“Seidon!” Sherhazad aliita, Seidon akasimama na kugeuka mzima mzima
“Malkia!” aliitika
“Ukikamilisha kazi yako huko Hamunaptra, rudi kwa kupitia njia ya kusini na si Mashariki kama ilivyo kawaida” Sherhazad alimwambia Seidon huku mkononi akiwa na zabibu kadhaa na kurushia kinywani.
Mwaka 2010
Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika kitengo cha mambo ya kale (ALCHEOLOGY) walikuwa kwenye lecture, katika ukumbi wa Nkurumah. Utulivu ulitawala ukumbini humo, mkufunzi professor Masati alikuwa akieleza juu ya chunguzi zilizowahi kufanya na mchunguzi maarufu wa Kiingereza Bw Paul Smith hasa ile ya Hamunaptra ambayo ilivuta masikio ya watu wengi duniani.
Maelezo yake kwa vijana hawa yalikuwa ya kina sana kwa akili yao, yaliwagusa kwa namna moja au nyingine hata wakavutiwa siku moja wafanye study tour huko. Wazo ambalo lilikubaliwa na wengi.
Hata lilipofika mezani kwa Pof. Mkandala, halikuwa na ubishi, liliandikiwa na kupelekwa wizara husika, siku si nyingi lilipitishwa na mipango ya safari hiyo ilianza.
Wanafunzi ishirini na wakufunzi watatu walikuwamo katika msafara ndani ya ndege kubwa ya Egypt Air, kuelekea Misri kisha kuchukua usafiri wa merikebu kupitia mto Nile mpaka mji wa Gosheni ambapo kwa usafiri wa ngamia wangefika Hamunaptra kwa mwendo wa masaa 6 jangwani.
Anna Davis, alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao, kila wakati alishtukashtuka hasa alipokumbuka kuwa wanakoelekea ndiko kunakosemekana kuwa kuna makaburi mengi ya kale yenye miujiza ya kutisha, makaburi ya mafarao wa Misri. Hata hamu ya kula ilimwishia kabisa katika safari hiyo.
Baada ya kukaa ndegeni kama masaa matano hivi, sauti nyororo ya msichana iliyoongea kwa lugha ya kiingereza na kiarabu iliwaashiria kuwa sasa wanapita juu ya anga ambalo chini yake kuna mapiramidi makubwa, mji wa Giza, ambayo duniani kote yanapatikana hapo tu na kuwa historia ya nchi ya Misri ilikuwa hapo katika mapiramidi hayo.
Anna aliangalia kwa makini majumba yale makubwa yaliyojengwa miaka na miaka yakiwa yamejipanga katika safu za kupendeza.
Punde si punde walikuwa katika ardhi ya Hosni Mubaraka, ardhi ya Misri, jiji la Cairo, jua liliwachoma kweli kweli lakini uvumilivu ulishika hatamu. Hamu ya kufika kujionea Hamunaptra ilikuwa imezidi mioyoni mwa vijana hawa, walionekana kuchangamka sana. Siku hiyo walipumzika Cairo na kesho yake walianza safari kuelekea mji wa Giza kupitia mto Nile.
“Hapa si Hamunaptra, lakini hamuwezi kuielewa historia ya Hamunaptra bila kupita hapa Giza” sauti ya kitetemeshi ya mmoja wa wazee waliokuwa wakifanya kazi ya kuongoza na kutembeza watalii katika hayo mapyiramid, alisafisha koo kidogo kwa kujikooza na kuendelea “Na lazima mjue kwamba Hamunaptra ni mji uliopotea miaka mingi iliyopita, ni mji wenye historia kubwa sana duniani, mji huu kiuhalisia upo India na si Misri, ila hapa Giza, kuna piramidi kubwa sana ambalo ndani yake, chini kabisa kuna pango kubwa sana, ukipita ndani yake utatokea Mesopotamia halafu linaendelea kutokea India katika eneo ambalo huo mji ulikuwa umefukiwa na mchaga kwa miaka mingi sana.” Walivuta hatua chache kidogo na kuanza kuyaona kwa karibu na hata kuyashika kwa mikono yao huku wakiuliza maswali mengi.
Hamunaptra
Hamunaptra (Mji wa wafu), uligundulika huko India mnamo mwaka 1850, wakati mainjiania wa kiingereza walipokuwa katika kujenga njia ya reli ndipo walipougundua. Mwaka wa 1920 ndipo wataalamu walipofanya kazi ngumu ya uchunguzi, chini ya ardhi walikuta mji mkubwa sana na wenye mambo mengi, ilisemekana kuwa kulikuwa viumbe walioishi huko miaka ya 1900-1700 kabla ya Kristu.
Mji uliotulia ardhini, ulijulikana hivyo kwa kuwa ulionekana huko, wachunguzi wengi waliojaribu kupita pango hilo walipoteza maisha, wengine kuwa vipofu na wengine walipatwa na hali za ajabu ajabu. Lakini ilisemekana kuwa miaka hii maajabu hayo hayakuwapo tena hivyo wengi waliingia ndani humo na kujionea yaliyokuwamo.
Karne kadhaa nyuma…
Wachawi kutoka Misri waliingia ndani ya piramidi hilo kubwa, lengo lao lilikuwa ni kwenda kuchukua fuvu la Cleopas. Walishuka mpaka chini kabisa ya piramidi hilo mpaka kwenye mdomo wa pango kubwa lililopo huko. Huku wakifanya matambiko kwa lugha zao za kichawi, walipita katika pango hilo na katikati yake wakaingia sehemu Fulani na kukuta chumba cha wastani kilichonakshiwa kwa maandishi ya kimisri na kihindu, michoro mbalimbali ilizunguka kuta zake zote.
Walisimama bila kutikisika na kutazama mbele kabisa ya chumba hicho cha chini. Mbele hapo kulikuwa na kitu kama jukwaa lenye ngazi ngazi na juu yake kulikuwa na skeleton ya kiumbe Fulani aliyekaa kwa kukunja miguu yake, pembeni kulikuwa na skeletoni zingine nne lakini zilikuwa na maumbo madogo kuliko ile ya katikati, zilionekana kuwa zimemuinamia kama ishara ya heshima kwake. Lakini ile skeleton kubwa haikuwa na kichwa! Cleopas.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni