Notifications
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (11)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...“Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (10)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (9)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA TISATULIPOISHIA...“Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.“Usikate tamaa, hakikisha unafika…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (8)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Amata ga Imba alipoona giza hilo akajua kumekucha, akapiga mbinja kali na muda mfupi tu, farasi wale wawili walikuwa tayari wamefika, Seidon akarukia juu ya mmoja wapo na Amata vilevile kisha wakapiga mbio kuelekea upande wa kusini. Nyuma yao jeshi lilikuwa likija kwa kasi na farasi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amatagaimba! Wanatufuata….” Seidon alipiga…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (7)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA SABATULIPOISHIA...“Amata, nakualika katika hili, ufuatane nami tukakamilishe kazi hii, tuondoe laana katika jamii na baraka za Klakos zitumwagikie kama umande wa asubuhi” Seidon alimtupia ombi Amata kwa lugha ya kushawishi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Hamna shaka, ombi lako limefika panapostahili, bega kwa bega tutakamilisha hilo, mimi nitakusindikiza kwa jua na mvua, kwa…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (6)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA SITATULIPOISHIA...Sauti za watu wakisali katika lugha isiyoeleweka zilisikika, Anna alitazama vyema na kuona viumbe kama watu wapatao kama ishirini hivi wakiwa wamezunguka kitu kama kitanda na katikati yake kulikuwa kumelazwa mwili wa binadamu ambao Anna aliutambua vyema, mwili wa rafiki yake kipezi Nesta.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Anna alibaki kakodoa macho akiangalia tukio…

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (4)


SEHEMU YA NNE
TULIPOISHIA...
Mbele hapo kulikuwa na kitu kama jukwaa lenye ngazi ngazi na juu yake kulikuwa na skeleton ya kiumbe Fulani aliyekaa kwa kukunja miguu yake, pembeni kulikuwa na skeletoni zingine nne lakini zilikuwa na maumbo madogo kuliko ile ya katikati, zilionekana kuwa zimemuinamia kama ishara ya heshima kwake. Lakini ile skeleton kubwa haikuwa na kichwa! Cleopas.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“Wamechukua…” kiongozi wa wale wachawi aliwaeleza wenzake kwa lugha yao ya kichawi. Wengine walibaki midomo wazi. Walipanga kuingia kuchukua kichwa cha Cleopas ili kufanikishia mambo yao ya kichawi lakini hawakulikuta, walijiuliza nani mwenye nguvu za kulichukuwa fuvu hilo, hawakupata jibu kwa kuwa wao walijiona kuwa ndiyo wachawi bora duniani. Walibaki wameduwaa, hata wao walishangaa siku hiyo wakiingia kiulaini sana tofauti na karne za nyuma, walishawahi kufanya jaribio hilo mara kadhaa kizazi hata kizazi lakini hawakufanikiwa kufika hapo.

Siku chache baadae …

Wachawi na waganguzi wote wa Misri walikutana kwenye vikao vyao lengo ni kutaka kujua nani kachukua fuvu lile. Baada ya kikao kirefu, na kutumia mbinu zote za kichawi waligundua kuwa fuvu lile limechukuliwa na Waingereza miaka mingi nyuma.

“Haiwezekani!” Kiongozi wao alisema

“Watu wa Maghalibi hawawezi kutuzidi maarifa” mwingine aliongeza

“Haina haja kulumbana, tuangalie tunafanya nini kurejesha fuvu lile mahali pake”

Baada ya majadiliano marefu walifikia muafaka wa jinsi gani ya kurejesha fuvu lile. Walikubaliana kumtafuta muindaji maarufu wa Misri Orion, ambaye alikuwa ni shujaa katika mambo mengi, mpiga shabaha maarufu duniani mpaka sasa. Baada ya mapigano makali huko kusini mwa London alifanikiwa kulipata fuvu hilo akisaidiwa na uchawi wa Kimisri. Alipolirejesha fuvu hilo liliwekwa ndani ya piramidi kubwa kabisa huko katika mji wa Giza.

Watu wa makabila ya kiajemi waliijua habari hiyo, hapo ndipo ilipoanza vurugu ya kila kundi kufanya mbinu ya kulipata fuvu hilo. Tatizo lililowakabili ni ubinafsi, kila mmoja alitaka alipate ili ajinufaishe yeye na watu wake. Lakini Klakos ilitaka fuvu lile lilirejeshwe kwa Cleopas na huyo atakayelirejesha ndiye atakayepata neema za Klakos, yeye na watu wake.

Kazi haikuwa ndogo kwani Orion alidhibiti pande zote nne za dunia watu wasiweze kulipata fuvu hilo, kila aliyejaribu alitoka kapa.

Vernad alipokutana na Orion, haikuwa kazi ndogo kwake kufanikiwa kulipata fuvu hilo, mapigano yaliyoandamwa na nguvu za nyingi yalitawala katika mji wa chini ya ardhi. Si kwamba Orion alishinda bali alizidiwa maarifa na Vernad wa Relvesh. Wahamsud walifuatilia mapigano hayo toka mbali, wakitaraji kwa kwa vyovyote lazima mmoja ashindwe, hawakuamini waliposhuhudia Vernad akimshinda ujanja Orion na kutoroka na fuvu hilo. Relvesh ilijawa na furaha sana kwa kumpokea shujaa wao huyo akiwa na mkoba mweusi mkononi uliowekwa fuvu hilo la ajabu, walilihifadhi vizuri, wakiwa na nia njema tu ya kulitumia kwa manufaa yao. Lakini hawakujua kuwa pembeni yao kuna wanaowaangalia kwa jicho la husuda.

Ndipo walipojikuta usiku mmoja wamevamiwa na wapiganaji walio juu ya farasi, wenye mijeledi na majambia, kijiji kizima walipigwa na wengine kuchomwa moto, ilikuwa hali ya kutisha sana. Waajemi walifanikiwa kulichukuwa fuvu lile na kutokomea nalo.

Warelvesh waliapa kulirejesha fuvu hilo mikononi mwao wakati Wahamsud walilimezea mate, achana na Sherhazad ambaye yeye kama mwanamke asingeweza kulishika fuvu hilo. Tukio likawa historia, watu wakafa na wengine wakazaliwa, historia ikawa ni simulizi ya kuvutia, simulizi ikawa riwaya tamu unayoisoma sasa.

Rejea … Sasa

Upepo si upepo wala si mvumo wake, mara kwa mara Anna Davis alikuwa akisikia kitu hiko kikimsumbua, aligeukageuka mara kushoto na mara kulia, mara alizunguka kama pia, ilikuwa ngumu kwake kufuatia maelekezo yatolewayo na mtaalamu huyo.

“We una nini? Mbona hutulii?” mwenzake alimuuliza

“Hata sijui mwenzangu, naona kama vitu vinanipita hapa mara vinanizungukazunguka. Yaani mwili wote unanisisimka”

“Acha uoga wewe, mbona wenzako hatuvioni!” alijibiwa na mwanafunzi mwenzake, kisha wote wakaendelea kusikiliza maelekezo.

Kitu kama nyoka kilipita katikati ya wanafunzi wale na Anna lakini cha kushangaza wenzake hawakukiona ila yeye alishuhudia mchanga ukitimka mbele yake na mara nyuma yake, sauti kama mruzi mkali ulipenya masikio yake na kumfanya apige kelele. Muelezaji alinyamaza kwanza na kumwangalia Anna, ilionekana wazi hakufurahishwa na kitendo cha Anna.

“Msichana! Hutakiwi kupiga kelele ukiwa humu ndani, utaamsha waliolala” yule mzee alimkazia macho Anna na kumueleza hayo.

Macho ya Anna hayakuwa matulivu hata kidogo, kila alipoangalia michoro ya watu iliyochorwa katika kuta zile au wanyama yeye aliona kama zikimwambia kitu Fulani, aliona kama ni viumbe hai. Hali hii ilimfanya aogope sana, muda wote hakuwa na amani kabisa. Alitembea kwa hadhari kubwa huku akigeukageuka nyuma, maana alihisi kama kuna vitu vinamfuata na alipogeuka vilitulia. Katika moja ya kugeukageuka ndipo alipojigonga kwenye kigingi kikubwa cha jiwe, alianguka chali na kukosa pa kujishikia, bahati mbaya au nzuri mikono yake iligonga tofali mojawapo lililoshikia ukuta ule imara, mara juu yake aliona kukifunguka na kitu kama sanduku likianguka kuelekea alipo yeye, Anna alipiga kelele huku akiwa kafumba macho, hana la kujitetea.

Wanafunzi wenzake walishtushwa kwa kelele za mwenzao walipogeuka nyuma walishuhudia vumbi zito likitimka na kuweka kama ukuta kati yao na Anna, kwa mbali walianza kusikia kama watu wanaoswali, sauti nyinginyingi zilisikika humo ndani ya piramidi

“Tuondokeni haraka! Tutoke nje, nifuataeni mimi” yule mzee aliongea kwa kelele, wanafunzi wale walianza kukimbia kumfuata. Kipenzi cha Anna, alishindwa kumuacha shoga yake, alisimama na kugeuka nyuma huku akiwa amejishika mkono kujiziba mdomo.

“Annaaaaaa!!!!!” aliita kwa nguvu na kelele ile ililijaza piramidi lote, kabla hajatahamaki jiwe kubwa lilianguka na kumponda kichwani, alianguka na kuumia vibaya, hakuweza kujinasua kwani tofali lile ni kama kilo mia mbili, alipoteza maisha.

“Msisimame, twendeni!” yule mzee alizidi kuwahasa viajana wale ambao sasa walikuwa wakikimbia na kupoteana wengine wakitamani kubaki kuwasaidia wenzao. Piramidi lote lilianza kutikisika na kuta zake kuanza kuchezacheza kwa mtindo ule ule, vumbi likazidi kujaa ndani mle kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuona njia hasa zile za kupanda juu. Wanafunzi wale walipata shida kujiokoa lakini kwa maelekezo ya yule mzee walifanikiwa kutoka nje na kuliona jua waliloliaca likichomoza sasa lipo katyikati ya utosi.

“Nyie, yule mwenzenu ana matatizo gani?” yule mzee aliongea kwa ukali

“Matatizo kivipi?” kiongozi wa msafara alijibu kwa kuuliza.

“Hii hali yote kaisababisha yeye, unapoingia mle ndani hutakiwi kugusagusa vitu”

Vilio vilitawala kati ya wanafunzi waliobaki wakiwaomboleza wenzao waliosadikiwa kufa shimoni, hali ilikuwa tete.

Amata ga Imba, akiwa amelewa sana na pombe yake nyingine mkononi alisimama ghafla, akashuka kutoka katika farasi wake na kutua chini taratibu, aliliweka guo lake vizuri mwilini na kurudishia pama lake kichwani. Alifikicha macho yake kutazama kilichopo mbele yake; ‘huyu mtu au kitu gani?’, alijiuliza huku akijongea kwa hatua za taratibu mpaka pale, alichuchumaa na kuinua kichwa cha majeruhi yule taratibu, akaweka mkono wake kifuani kwa mtu yule, akagundua kuwa bado uhai upo kwa mbali sana, mtu yule hakuwa na fahamu. Akamnyanyua na kumlaza juu ya farasi wake, kwa pembeni alimuona farasi mweupe aliyelala nyasini, akampigia mruzi na farasi yule akainuka kutoka pale, kisha akaondoka na mtu yule pamoja na farasi wake mpaka katika kijiji alichokuwa akiishi.

Siku zote alikuwa akimpa tiba mtu huyu asiyemjua kwa muda wa takribani wiki moja mtu yule aliamka kutoka katika usingizi mzito, alikuwa akihema kwa nguvu na haraka haraka

“Likowapi, likowapi? Nipe, nipe haraka” Seidon aliamka na kupiga kelele za maweweseko. Amata alimtuliza na kumlaza taratibu pale katika tandiko lake.

“Tulia, tulia, usijitikise sana” Amata alimbembeleza Seidon ambaye alitii na kujilaza tandikoni.

“Hapa nipo wapi?” aliuliza

“Hapa ni kijiji cha Mshariki, kijiji cha wema kisicho na wabaya” Amata alimjibu Seidon kwa upole, akamtazama usoni na kuendelea “naitwa Amata ga Imba, nilikukuta porini karibu na jangwa la Sheba nikakubeba na kukuleta huku” akajikohoza kidogo kuweka koo lake vyema “pole sana! Hakika ungekufa lakini Mungu mkubwa nilikuwhi. Wewe ni nani?”

“Mimi ni Seidon kutoka Relvesh, nilikuwa safarini nikitokea Hamunaptra kupitia Mesopotamia, Wakalban walikuwa wakinikimbiza wakiwa kundi, walitaka nilichonacho, lakini nikiwa katika kasi kubwa niliona kitu kama kamba mbele yangu ambayo ilimnasa farasi wangu miguuni na mi kuanguka vibaya. Wahamsud walinifanyia hivyo na kuchuku fuvu la Cleopas wakatokomea nalo” Seidon alitokwa machozi na kamasi jembamba akendelea “Babu wa babu zangu Vernad alikuwa na mpango wa kulipata fuvu hilo kwa ajili ya kusaidia kijiji chetu cha Relvesh dhidi ya laana tulizonazo…

Rejea Vernad…

Vernad alitembea taratibu mpaka kwenye kilima kidogo, na alipofika juu yake alitazama chini na kuona mji mkongwe, gofu la mkji uliofunikwa kwa mchanga upande wa juu. Bia kuchelewa alitimua mbio kulielekea gofu lile, punde tu alikuwa mbele ya mlango mkubwa, bila kusita aliingia ndani, hakupiga hata hatua tano alijihisi kakabwa kwa nyuma, alihangaika kujinasua lakini ilikuwa vigumu, aliishika mikono ya kiumbe huyo sawia na kuinama hata kumdondosha kiumbe yule kwa mbele, kitendo bila kuchelewa aliuchomoa upanga wake na na kumshindilia kifuani, kiumbe yule alitoa sauti ya maumivu kama sauti ya nguruwe lakini hakutoka damu, Vernad aliuchomoa upanga wake na kumkata vipande vipande kisha akaingia mlango wa pili na kuchukua ngazi kuelekea chini ya gofu hilo, alijikuta kwenye ujia mrefu uendao asikokujua, kwa kasi ya ajabu alikimbia kuelekea ujia ule uendako akiwa na upanga wake mkononi.

Njiani alikutana mtu mmoja mbele yake ambaye alikuwa kafunga njia, Vernad bila kupunguza mwendo alijirusha na miguu yake kutangulia kifuani kwa mtu yule huku upanga ukifuata na kudidimia katika koromeo la mtu yule ambaye hakupata hata nukta ya kujitetea. Vernad alitua chini na kuuchomoa upanga wake, kabla hajaanza kuondo alipigwa ngwala moja na kujibwaga chini, wakati anapoanguka alijishika kwenye tofali moja wapo lililotokeza katika ukuta huo mara ardhi ikainamana na kufunguka Vernad alitumbukia katika shimo refu, alishuhudia radi kali zilizopiga huku na huku shimoni mle.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
66 Hamunaptra Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni