HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (5)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Vernad alitua chini na kuuchomoa upanga wake, kabla hajaanza kuondo alipigwa ngwala moja na kujibwaga chini, wakati anapoanguka alijishika kwenye tofali moja wapo lililotokeza katika ukuta huo mara ardhi ikainamana na kufunguka Vernad alitumbukia katika shimo refu, alishuhudia radi kali zilizopiga huku na huku shimoni mle.
TUENDELEE...
Huku akiwa kajiziba masikio kutokana na upepo mkali uliyoyasumbua, upanga wake ukiwa haupo mikononi mwake, alijikuta akitua chini taratibu bila maumivu yoyote, alisimama wima na kushangaa eneo lile pana, uwanda mkubwa usio mawaa yoyote. Alijiuliza yuko wapi hakupata jibu, mbele yake aliona majengo mengi sana na watu wakiwa katika kazi nyingi, kazi mbalimbali. Aliinua mguu kuwafuata watu wale lakini nyuma yake alihisi kama anafuatwa alisimama na kugeuka, lo! Umati wa watu ulikuwa nyuma yake, alijaribu kuwahesabu harakaharaka lakini alishindwa kwa uwingi wao.
Watu wengi walionyamaza kimya hakuna aliyetikisika walimtolea macho Vernad mpaka akaogopa, aliporudi nyuma walimfuata alipojaribu kuwasemesha sauti haikutoka, walibaki kumtolea macho tu, watu waliovaa nguo kuukuu zinazoonekana kuoza, macho mekundu kwa meusi, wengine walikuwa na mkono mmoja wengine walikuwa hawana masikio ilimradi waliogopesha, wafu, lakini mikononi mwao walikuwa na visu, mapanga, miundu na kadhalika.
Vernad alijuwa wazi kuwa hapo hakuna msalie mtume, alianza kutimua mbio na watu wale wakaanza kumfuata, Vernad aliwaacha mbali kwa mbio zake lakini hakujua ni wapi anakoelekea, alipokuwa akiyapita yale majengo watu wengine walitoka katika yale majengo na kuanza kumfukuza, Vernad hakuchoka, aliongeza mwendo lakini ghafla alihisi kamba ikimfunga shingoni na kuanguka chini, haraka bila kuchelewa alijiinua na alipojaribu kuitoa kamba ile shingoni hakuweza kwani ilimfunga barabara, alihisi miale ya jua ikimchoma machoni kwa kubadilishana alijikinga kwa mkono wake wa kulia na kujaribu kuangalia, aliona kama kiumbe Fulani pale katikati ya mionzi ile. Mara miale ile ilianza kupungua nguvu,
Vernad alishusha mkono wake na kumuona mtu aliyevalia joo jeupe, kiunoni akiwa na upanga mkubwa, mkono wake wa kushoto kashika ngao na kulia ana kamba ambayo ndiyo hiyo upande wa pili imemfunga Vernad, mgongoni alikuwa na uta mkubwa na podo lililojaa mishale.
‘Orion’ Vernad alijiwazia, akasimama kwa miguu yake na kuinamisha kichwa kutoa heshima kwa kiumbe huyo, aliponamisha kichwa Orion aliufuta upanga wake na kukata shingo ya Vernad. Vernad hakuwa na kichwa tena, alibaki kiwiliwili tu, alianguka chini na roho yake ikauacha mwili.
seidon
…Hakufanikiwa kwa sababu Orion alimdhibiti na kumuua. Sasa mimi nilitumwa kuikamilisha kazi hiyo iliyoahirishwa vizazi na vizazi” Seidon alimaliza kumuelezea kisa hicho Amata ambaye alibaki mdomo wazi maana alijaribu kufikiri hatari aliyoikabili Vernad na sasa Seidon.
“Wewe umemshinda vipi Orion?” Amata alimuuliza Seidon
“Amata! Ni simulizi ndefu sana…” akashusha pumzi ndefu na kuendelea “Mimi nimepambana na Orion uso kwa uso, sikumshinda kwani yule ni kiumbe mwenye akili hata upiganaji wake hauna makosa shida yake niliisoma ni moja tu, si mjanja na wala si mwepesi, nilifanikiwa kulipata fuvu alipolificha na hapo ndipo kazi ngumu ilikuwa, Amata!…
…Sherhazad alimwangalia Seidon akipotea na farasi wake kwa kasi, akiwa pale katika dirisha lake la ajabu alitabasamu na kutikisa kichwa ‘wanaume wajinga sana! Ukilala nao kitandani tu watakupa kila kitu, ngoja alete hilo fuvu hakika kaburi lake litakuwa hapa hapa Soria’ alijisemea moyoni huku akitoka katika dirisha lake ambalo kwalo huweza kuona mambo yote yanayoendelea duniani na kusoma mawazo ya kila mtu anayemtaka.
Seidoni alipiga mbio bila kuchoka na farasi wake alitii yote aliyoambiwa na bwana wake, punde si punde alijikuta mbele ya jingo la ajabu, jingo kubwa lililoonesha kila dalili ya kutoishi mtu, alijitoma ndani akiwa na farasi wake huyo, ndani humo alipita kwenye njia ndefu iliyokuwa haionekeni mwisho wake, kwa kasi ileile alipita na farsi wake, akiwa katika kukimbia huko akasikia farasi mwingine nyuma yake akipiga kelele alipogeuka aliona akifuatwa kwa kasi na mtu aliyekuwa juu ya farasi aliyeoneaka si muda angemfikia.
Seidon aliongeza kasi lakini bado alijikuta umbali uleule na farasi yule wa nyuma. Hakuwa na jinsi kwa maana aligundua kuwa huyu wa nyuma yake angeweza kumdhuru muda wowote ukizingatia alikuwa karibu sana na yeye, alimkwepesha farasi wake upande na kusimama, yule wa nyuma alipitiliza na tayari upanga wa Seidon ulishapita katika ubavu wa mtu huyo, kwa kishindo alianguka chini, Seidon aliteremka na kumfuata pale alipo, damu ilikuwa ikitoka mdomoni, Seidon akapiga goti moja na kumtazama
“Wewe ni nani?” alimuuliza
“Mimi kiumbe wa Mashariki ya mbali” alijibu kwa taabu
“Kwa nini unanifuata?”
“Pepo zimenituma nikufuate nihakikishe hufiki uendako, na ukifika usifanikiwe lengo lako, na ukifanikiwe usitoke humu na ukitoka usifike mwisho wa safari yako…” kabla hajamaliza kuongea alikoroma na kukata roho. Seidon alipanda farasi wake na kuanza safari yake kwa mbio zilezile, lakini kamba iliyorushwa kwa ustadi iliifunga shingo ya Seidon na kuanguka vibaya, vumbi lilitimka mahali pale na lilipotulia hakukuwa na mtu zaidi ya farasi mweupe wa Seidon.
Orion alisimama kuangakli huku na huku hakumuona Seidon, kazidiwa ujanja. Aliiangalia kamba yake ambayo sasa ilionekana imemfunga farasi wa Seidon na sio Seidon mwenyewe. Orion alitereka kutoka katika farasi yule na kutua chini, kishindo cvhake cha kutua chini kiliwafanya popo kutimka na ardhi kutikisika kwa muda, kwa hatua fupi fupi alimuwendea farasi wa Seidon na kumuangalia kwa makini.
Orion ambaye daima sura yake haionekani kwa kuwa alikuwa akiifuanika kwa kinyago maalum huwa hashuki kwenye farasi, yeye hupigana akiwa juu ya farasi wake, lakini akikuona wewe ni mjanja zaidi yake hapo ndipo atashuka ili akukabili vizuri. Alimtazama yule farasi lakini hakuelewa kilichotokea, aliichukua kamba yake na kupanda farasi wake kisha kuondoka kuelekea uelekeo ule ule aliokuwa akielekea Seidon.
Seidon aliliachia jiwe alilokuwa amelidandia juu ya pango lile na kutua chini bila kufanya kishindo, ‘amenikosa’, alijiwazia kisha akapanda farasi wake na kuelekea kulekule alikoelekea Orion, baada ya mwendo wa kama dakika kumi katika pango lile alijikuta anafika njia panda, nji tatu zilikutana hapo, Seidon alifikiri ni ipi hasa anayopaswa kupita, kwenye njia moja alisikia mvumo wa maji kama mto upitao kasi lakini hakuyaona maji yenyewe, njia ya pili ambayo ilikuwa katikati alisikia mvumo wa moto uwakao mithili ya moto uchomao msitu na njia ya tatu alisikia kama watu wakinoa mapanga.
Seidon alitulia kimya akitafakari la kufanya, aligeuka na farasi wake tayari kwa kurudi akijua kuwa labda kuna njia nyingine lakini sivyo, alipogeuka alikutana na ukuta, hakuiona njia aliyojia, alitafakari na kuona kuwa hana ujanja zaidi ya kuchagua moja, alimgeuza tena farasi katika uelekeo wa kuendelea na safari na moja kwa moja moyo wake ulimtuma kupita njia ya moto, hakuwa na muda wa kufikiri alijitoma ndani ya ujia huo na kuendelea kupiga mbio, kadiri alivyouwa akienda alihisi sauti ile ya moto ikizidi kuwa karibu zaidi,kila alipotaka kupunguza mwendo alisikia sauti ikimwambia aendelee kwa kasi.
Seidon aligundua kuwa amepata kampan alipoona kuna farasi wawili na juu yake Malaika wa moto wenye upanga makali kuwili wakiwa katika kasi ileile, mmoja kushoto na mwingine kulia, Seidon alishindwa kujua afanyeje, akiongeza kasi nao walifanya vivyohivyo, mbele yake alishuhudia moto mkubwa sana ambao ulimtisha nafsi yake, afanye nini.
Aliamua, kama kufa wacha afe kwani tayari alikuwa kwenye mikono ya mauti, kwa mkono wake wa kulia aliufuta upanga wake na kwa pigo moja alimchoma yule Malaika wa moto wa upande wa kushoto lakini hakuhisi kama kachoma kitu alipogeuka kwa yule wa upande wa kulia alikutana uso kwa uso na joka kubwa lililoachama kinywa chake, Seidon bila kuogopa wala kufikiri alipiga pigo moja kwa upanga wake na kulichoma joka lile, alipouvuta upanga kuuchomoa alihisi kama damu ikimrukia usoni alichelewa kujikinga, alijikuta akipoteza uelekeo na kuanguka vibaya, alijiinua haraka na kusimama kidete, joka lile lilitema ndimi za moto, Seidon alijitupa chini na kujiviringa kuelekea kuelekea kule joka lile lilipo, alifanya pigo la upanga na kulikata joka lile kipande, kisha aliposimama alijikuta akipaishwa juu kwa ngwala maridadi iliyopigwa kwa mkia wa joka lile, alijigonga vibaya na lianguka kama mzigo, alijtahidi kunyayuka lakini alipoangalia alijikuta chini ya upanga wa moto, Malaika wa moto alisimama juu yake akiwa kamnyoshea upanga.
Seidon alitulia tuli, akijua sasa siku yake imefika, Malaika yule aliushusha upanga wake kwa kasi kwa nia ya kumkata Seidon, lakini kwa ustadi Seidon alipangua pigo lile kwa upanga wake na kumfanya Malaika yule apoteze shabaha ile, Seidon alinyanyuka kwa mtindo wa sarakasi na kusimama wima ardhini, alirusha teke kwa kujizungusha na kumtandika Malaika yule kichwani na kumfanya kuyumba kiasi lakini akajiweka sawa na kujibu shambulizi, aliuvuta upanga wake na kufanya pigo lingine ambalo almanusura liondoe kichwa cha Seidon endapo Seidon asingeinama. Seidon sasa alikuwa akitazamana na sehemu ya tumbo ya Malaika yule, bila kuchelewa aliuzungusha upanga wake na kukata tumbo hilo lakini alichokishuhudia ni kurushwa kwa nguvu na kutumbukia katika moto mkubwa uliokuwa ukizidi kusogea eneo hilo.
***
Anna Davis alitazama huku na huku, aliona sanduku kubwa kushoto kwake lililomkosakosa kumbonda na kumfanya aanguke tu kwa kishindo kile. Akiwa anatweta kwa nguvu alishindwa kujua ni nini hasa anatakiwa kufanya, alipotaka kupiga kelele za msaada alijikuta hana sauti ya kufanya hivyo, alipojiinua pale chini aligundua kuwa hakuwa peke yake bali pembeani yake kulikuwa na miili iliyokauka yaani iliyokufa miaka mingi nyuma, Anna aliogopa sana akaanza kutetemeka, taratibu aliinuka ili asisikiwe na miili hiyo. Alipoketi vizuri alitazama wapi pa kuelekea aliona ngazi ndefu zikishuka chini na pale alipo palikuwa na uwanda mkubwa kiasi uliozungukwa na kuta nene zenye michoro mbalimbali.
Sauti za watu wakisali katika lugha isiyoeleweka zilisikika, Anna alitazama vyema na kuona viumbe kama watu wapatao kama ishirini hivi wakiwa wamezunguka kitu kama kitanda na katikati yake kulikuwa kumelazwa mwili wa binadamu ambao Anna aliutambua vyema, mwili wa rafiki yake kipezi Nesta.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni