SUZAN WANGU (2)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA PILI
Baaada ya kumaliza kuongea na boss wake alirudi kitandani na kulala huku akiwa na mawazo sana, baadae alikata shauri na kuendelea na kazi ndogondogo za nyumbani huku akimsubiri Michael aje ili amueleze kilichomkuta….
**** **** ******
Siku zote katika maisha sio kila mtu atafurahi kuona mafanikio yako
SASA ENDELEA...
Wengine huchukia na kutamani ushuke na uwe masikine wa kutupwa, hivyo ndivyo ilivyokua kwa michael, sio kila mtu pale anapofanyia kazi alifurahia mafanikio yake japo ni wachache ambao hawakufurahishwa na mafanikio yake, wengi walimpenda hasa kutokana na ucheshi wake pamoja na upole wake, mbali na hilo pia michael alikua ni mshauri mzuri sana pale ofisini kwa wafanyakazi wenzake, endapo mfanyakazi yeyote alimfata na kumuomba ushauri, michael alimshauri vizuri na hata wakati mwingine kama mfanyakazi alikua anamatatizo, michael alidiriki kutoa pesa katika mshahara wake na kumsaidia huyo mfanyakazi ili atatue matatizo yako, havyo ndivyo jinsi michael alivyoishi na wafanyakazi wenzake.
Mbali na vyote hivyo vizuri ambavyo michael alikua akiwafanyia wafanyakazi wenzake, hali ilikua tofauti kwa Joel ambae alikua ni muhasibu msaidizi, alimchukia sana michael, tena alimchukia kupita kiasi, siku zote hakupenda mafanikio ya michael, alitamani mafanikio yale yawe kwake, siku zote aliweka tabasamu feki alipokua na michael, lakini moyoni mwake alimchukia kupita kiasi, uzuri ni kwamba michael alilitambua hilo na siku zote alijifanya kama haelewi kinachoendelea, alimpenda joel na alihuzunika pia kwanini joel alimchukia vile.
Siku hiyo walipomaliza kazi alimsubiria boss wake mr Alex ili amwambie kinachoendelea kati yake yeye na joel ili siku likija kutokea tatizo basi wajue pakuanzia. Alipomaliza maliza kupanga kazi zake alitoka na kwenda kwenye ofisi ya Mr Alex na kugonga mlango, aliruhusiwa kuingia….
“Ooo karibu mwanangu”
“Asante baba pole na kazi”
“Nashukuru pole na wewe”
“Aaaa baba nilikua na maongezi na wewe kidogo kama hutojali”
“Ebu keti kwanza hapo ngoja nimalizie hii kazi hapa halafu tuongee, kwani ni maongezi marefu sana?”
“Hapana ya kawaida tu na mafupi pia’
“Okay subiri kidogo”
Michael alisubiri na baada ya dakika kumi mr Alex alimaliza kazi zake…
“Sasa mwanangu tunaweza tukaongea”
“Baba ni kuhusu joel”…
“Joel yupi, yule muhasibu msaidizi?”
“Ndio baba”
“Enhe kafanyaje tena”
“Baba joel amekuwa akinichukia sana tangu mlivyonizawadia nyumba pamoja na magari, sasa nahofia siku ya siku anaweza akafanya jambo ambalo linaweza likaniweka mimi katika wakati mgumu au akaiweka ofisi katika wakati mgumu”
“Eeee kumbe kijana mbaya sana yule, kwanini akuchukie mwanangu, wewe umezawadiwa vile kutokana na utendaji wako mzuri wa kazi,sasa kwanini akuchukie, ngoja nitamfukuza kazi”
Hakika Mr Alex alichukia sana, hakupenda kuona mtu akimkwaza michael, kwani alimpenda kama mwanae…
“Hapana baba usimfukuze mwache tuu, jaribu kumuita na kumshauri itakua bora zaidi ya kumfukuza”
Mbali na yote mr alex alimsikiliza sana michael kwani alimuona pia ni mtu mwenye busara…
“Sawa nimekuelewa mwanangu, unaweza kwenda”
“Sawa baba jioni njema,msalimie mama”
“Usijali zimefika, kuwa muangalifu”
“Okay bye” Michael alimuaga bosi wake na kutoka nje kwakua muda wa kazi ulikua umeisha, alienda mpaka parking ya magari akaingia kwenye gari, akawasha gari lake na safari ya kuelekea nyumbani kwake ilianza…
******** ***** ********
Kutokana na foleni iliyokuwepo siku hiyo ya jumatatu, michael alifika nyumbani kwake mida ya saa moja na nusu, kama kawaida alitoa kirimoti kidogo katika mfuko wa suruali yake kasha akakibonyeza na geti lilifunguka, hapo alikanyaga mafuta taratibu na kuingiza gari lake aina ya prado, alibonyeza tena kirimoti na geti lilijifunga, alisogeza gari mpaka sehemu ya parking na kuliweka sehemu yake, na baada ya hapo alifunga vioo pamoja na milango ya gari na alipomaliza alielekea upande ambao ndiko ulipo mlango wa kuingilia ndani kwake, alifungua mlango na kuingia ndani lakini alishangazwa na ukimya uliokuwepo hapo ndani, alipita sebuleni na kukuta chakula kipo mezani lakini alipojaribu kumuita mpenzi wake suzan bado kuliendelea kuwa na hali ya utulivu, alitoka hapo sebuleni na kuelekea katika chumba chake, hapo alipigwa na butwaa baada ya kumuona suzan akiwa amelala na jinsi alivyoonekana ilionesha wazi kuwa hakutoka siku hiyo, michael alipatwa na wasiwasi na kudhani huenda kuwa mpenzi wake anaumwa, michael alisogea mpaka karibu na kitanda alicho lala mpenzi wake na kumuamsha kwa ustaarabu, suzan aliamka kivivu, alikutana na tabasamu murua la michael na bila kutarajia alijikuta akimrukia na kumkumbatia kwa nguvu, baada ya muda wa kama dakika moja huku suzan akiwa bado amemkumbatia michael, suzan alianza kudondosha machozi kuonesha kwamba kuna kitu kinamsumbua, michael aligundua kuwa suzan atakua analia baada ya kuhisi shati lake alilokuwa amelivaa limenza kupata hali ya ubichi, alijitoa katika kumbatio lile na hapo alikutana na uso wa suzan ukiwa umependezeshwa na machozi, michael alipagawa na asijue mpenzi wake amepatwa na nini, mambo mengi sana yalipita katika kichwa chake na kuhisi huenda tayari kuna vijidudu watu washaingia katika penzi lake na hapo tayari mpenzi wake ashapewa maneno ya uongo kuwa yeye kuna mtu anatembea nae, alitoka katika dimbwi hilo la mawazo baada ya suzan kuanza kulia kilio cha kwikwi, michael alimfuta machozo mpenzi wake na kumuuliza ni kitu gani kinamsibu, suzan hakuongea bali alitoa simu yake aina ya Samsung galax s6+ na kufungua sehemu ya ujumbe mfupi (message) hapo alitafuta ujumbe aliotumiwa na bosi wake na baada ya hapo alimkabidhi michael ile simu,michael aliipokea ile simu na kuanza kuusoma ule ujumbe mfupi, na hapo macho yalimtoka pima baada ya kuona ujumbe ule…
“Kuanzia leo sitaki kukuona katika ofisi yangu, nimekufukuza kazi kwasababu zangu binafsi, na wala usijisumbue kuja katika ofisi yangu kama unajipenda maana unaweza ukaozea mahabusu, ila kama utakua tayari kunivulia nguo yako ya ndani na kunipanulia mapaja yako unaweza ukapata kazi, kwa kifupi nalihitaji penzi lako ili uokoe kazi yako”
Michael alishusha pumzi ndefu baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo, alimtazama mpenzi wake ambae alikua akilia taratibu huku akivuta kamasi jembamba ambalo lilikua likitaka kutoka, michael alisikitika sana na alichukia kupita kiasi kwani hakupenda hata siku moja kumuona mpenzi wake akipata tatizo lolote kipindi ambcho yeye yu hai, alimpenda na alimthamini kuliko kitu chochote chini ya jua, licha ya suzan kuwa mpenzi wake pia alikua akimchukulia kama ndugu, licha ya suzan kuwa mpenzi alimchukulia kama mtu wa karibu kwake na pia alimchukulia kama mshauri wake mkubwa, alimtazama suzan ambae bado alikua akilia na hapo alipatwa na uchungu mkubwa moyoni mwake, alifikiria ni jinsi gani atamsaidia mpenzi wake, alifahamu fika kwamba suzan hana baba wala mama, hana kaka wala dada, hana mjomba wala shangazi, hana ndugu yeyote ambae alikua akimtegemea katika maisha yake, nguzo zake zote muhimu tayari alishazizika, na hapo michael ndipo alipogundua kuwa jukumu la kumsaidia suzan ni la kwake yeye mwenyewe, alitambua kuwa yeye ndiye nguzo pekee ambayo suzan anaitegemea, aliirudisha simu mahala pake na kisha alivua nguo zake na kupanda kitandani, alimvuta suzan karibu yake na kumlaza katika kifua chake….
“Suzan mpenzi wangu, yakupasa utambue kwamba katika maisha kuna changamoto nyingi sana ambazo binaadamu huwa tunakutana nazo, na ili ufanikiwe huna budi kupambana na changamoto hizo kwa nguvu zako zote ili ufanikishe malengo yako, kufukuzwa kazi wewe haimaanishi kwamba ndio mwisho wa maisha yako, yakupasa kukaa chini na kumshukuru mungu wako kwa kila jambo kwani huwezi jua mungu amekuepushia nini katika kampuni hiyo”
“Unayo yasema michael ni sawa sijakataa ila kwanini litokeee kwangu, mbona kila siku mimi ndo nakuwa napatwa na matatizo, nilipoteza wazazi wangu kipindi nimefikisha miaka miwili tuu, ndugu zangu siku bahatika kuwajua hata mmoja niliishi kama chokoraa mpaka nilipokuja kupata msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao walinipeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima ambao ndio walionigharamikia mpaka mimi kufikia hapa halafu leo mtu ananifukuza kazi kisa anataka afanye ngono na mimi, kwanini mimi? Eee mungu nimekukosea nini mpaka unanitenda haya, nibora uichukue roho yangu kuliko kuniacha hivi na kunipa mitihani kila siku”
“Paaaaa” ulisikika mlio wa kofi, naam ni kofi mwanana kabisa kutoka kwa michael lililotua vyema katika shavu la suzan, suzan hakuamini, tangu wajuane na michael na kukaa katika mahusiano kwa muda wa miaka mitatu hakuna hata siku moja ambayo michael aliwahi kumpiga hiyo ndo ilikua mara yake ya kwanza kupigwa na michael, alishika shavu lake na kukutana na sura ya michael ikiwa na makunyanzi huku macho yake yakiwa mekundu utadhani ametoka kuvuta bangi, hii ilitosha kabisa kumjulisha suzan kuwa michael alikuwa ana hasira kupita kiasi, licha ya suzan kupigwa kofi hilo hakuthubutu kuinua mdomo wake, alikaa kimya na kusubiri kusikia Michaela ataongea nini na ni kwasababu gani michael ampige kofi…
“Wakati mwingine uwe unalalamika lakini usivuke mipaka kiasi cha kumkufuru mungu namna hiyo, haijalishi nimangapi umeyapitia na mangapi utayapitia, kinachotakiwa ni wewe kumshukuru mungu kwa kila hatua unayopiga kwani huwezi jua mungu amekuandalia nini mpaka wewe upitie katika magumu hayo au huwezi kujua mungu amekuepusha na nini mpaka akaamua upitie hayo magumu, hivyo ni bora ukamshukuru mungu wako kwa kila hatua unayopiga katika maisha yako” michael aliunguruma kwa sauti nzito kiasi, suzan alikaa na kuyatafakari maneno hayo na kuona kwamba ni wazi atakua amemkosea bwana mungu wake, alifunga macho yake na kuanza kuomba kwa imani….
“Baba katika jina yesu, nakuja mbele za uso wako saa na wakati kama huu, tazama baba mimi ni mkosaji mbele zako, naomba unisamehe kwa niliyoyafanya na kutenda baba, tazama baba katika neno lako umesema samehe saba mara sabini na mimi ni mkosaji nahitaji msamaha wako, nakwenda kumfunga muovu shetani akae mbali katika maisha yangu, naomba unitakase kwa jina lako, unilinde kwa damu ya yesu, uniweke mkono wako wa kuume baba yako, nikatika jina la yesu mnazareti mwana wa mungu aliye hai nikiomba na kushukuru, aaamen”
Baada ya kumaliza maombi yale, suzan alishuka kitandani na kupiga magoti huku machozi yakimtoka..
“Michael mpenzi wangu, najua nimekosea, halikuwa kusudio langu kumkufuru mungu, nilikua najaribu tuu kuelezea hisia zangu na kuonyesha ni mambo mangapi mimi nimepitia”
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni